NENO LA LEO (SEPTEMBA 16, 2020): FAHAMU TABIA 5 AMBAZO ZITAKUWEZESHA KUJIFUNZA KWA HARAKA.
Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa wote tumeamka salama na tupo tayari kuendeleza pale tulipoishia jana. Ni asubuhi naendelea kuwakumbusha kuwa ili tufikie mafanikio makubwa tunayotamani hakuna namna zaidi ya kuhakikisha yale tunayofanya yanakuwa na muendelezo kila siku. Basi kila mmoja wetu aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍πΎ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza tabia 5 ambazo unatakiwa kuwa nazo ili kujifunza kwa haraka na hatimaye kufanikiwa kimaisha. Kujifunza ni moja ya misingi ambayo inaunda mafanikio ya watu waliofanikiwa. Ukiuliza siri ya mafanikio kwa kila aliyefanikiwa kwenye sekta yoyote ile moja ya majibu ambayo utapata ni kwamba anatumia muda mwingi kujifunza. Karibu tujifunze mbinu ambazo zinatumiwa na wenye mafanikio katika kujifunza maarifa na ujuzi mpya:-
✍πΎ Tabia #1: Jifunze kutoka kwa watangulizi wako. Katika jambo lolote ambalo unakusudia kufanikisha kuna watu ambao walishafanya jambo hilo. Katika hao ambao waloshafanya jambo hilo kuna ambao walifanikiwa na kuna wale ambao hawakufanikiwa. Ili uwe imara zaidi unatakiwa kujifunza kwa wale waliofanikiwa ni kwa nini walifanikiwa. Pia, unatakiwa kujifunza kwa wale ambao hawakifanikiwa ili kujua sababu zilizopelekea wakashindwa kufanikiwa.
✍πΎ Tabia #2: Epuka kufuata mkumbo. Tengeneza njia yako mwenyewe ili kuepuka kufanya yale ambayo kila mtu anafanya. Unatakiwa kuwa mbunifu zaidi ili ujitenganishe na msongamano wa watu kwenye njia unayosafiria. Zaidi unatakiwa kutambua kuwa njia ambayo unaifungua mwenyewe haina msongamano japo ina milima na mambonde kwa haijatumiwa na watu wengine. Wewe ndiyo wa kusawazisha mabonde na milima na wewe ndiyo wa kufyeka njia mpaka ufike kwenye kilele cha safari yako.
✍πΎ Tabia #3: Kuwa na maono mapana. Kupitia maono tunapata ndoto na kupitia ndoto tunapata malengo na tunapokuwa na malengo tunapata tumaini kwa maisha yajayo. Kubwa ni kwamba maisha yako ya baadae ni zao la maono uliyonayo sasa. Ikiwa hauna maono moja kwa moja hauna tumaini hai kwenye maisha yako ya baadae. Kwa ujumla unatakiwa kuishi kauli mbiu ya: "kesho inaandaliwa kutoka katika maisha ya sasa."
✍πΎ Tabia #4: Jifunze kusikiliza kuliko kuongea. Katika mkusanyiko wa watu lazima pawepo maongezi. Mara nyingi wengi wetu huwa tunapenda kuwa wazungumzaji kuliko kuwa wasikilizaji. Ni heri kuwa msikilizaji ili ujifunze kutoka kwa wengine. Hii ni kutokana na ukweli kuwa unapozungumza unatoa unachojua wewe ikilinganishwa na pale unaposikiliza kutoka wengine. Tuna masikio mawili ikilinganishwa na mdomo mmoja. Tafsiri ya viuongo hivyo vya mwili ni kwamba tunatakiwa kusikiliza mbali zaidi ya tuntunavyoongea.
✍πΎ Kundi #5: Tunajifunza kwa kufundisha. Ikiwa kuna maarifa au ujuzi husisite kushirikisha wengine maana kwa kufanya hivyo yapo mengi utajofunza zaidi. Jifunze kutoa maana kwa kadri unavyotoa ndivyo unaandaa mazingira ya kupokea.
✍πΎ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza tabia 5 ambazo zitakuwezesha kujifunza kwa haraka. Pia tumeona kuwa kujifunza ni miongoni mwa misingi muhimu katika kufikia hatua ya mafanikio unayotamani kwenye kila sekta ya maisha yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.
ππΎππΎππΎππΎππΎ
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
ππΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(