NENO LA LEO SEPTEMBA 3, 2020): IKIWEZEKANA CHOMA MELI BAADA YA KUVUKA SEHEMU YENYE MAJI MWENGI.
ππΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi mpya ambapo tunaalikwa kuendelea kutoa thamani kwa jamii inayotuzunguka. Ni siku ambayo tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kutokana na baraka ambazo anazidi kutujalia katika kipindi cha maisha yetu. Basi kwa pamoja tuianze siku kwa kusema “hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii ili nipate yaliyo bora katika maisha”.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍πΎ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tujifunza umuhimu wa kuondoa visingizio vyote.ambavyo kila mara vimekuwa vikisababisha urudie maisha ya zamani ambayo hayakupeleki kwenye mafanikio unayotamani. Fikiria ni mara ngapi umekuwa ukitaka kujifunza tabia mpya lakini bila kupenda unajikuta umerudia tabia za zamani. Fikiria fursa ngapi umekosa kutokana na kuendekeza tabia ambazo ni hatarishi kwenye maisha yako. Fikiria ni watu wangapi wa muhimu ambao umewakosa au wamekukimbia kutokana na kukosa utayari wa kubadilika ili tabia zako zinaendane na hao watu wa muhimu.
✍πΎ Katika kitabu cha The Richest Man in Babylon tunatolewa mfano wa Kamanda wa Vita ambaye baada ya kuvusha askari wake kwenye eneo la maji mengi na kufika eneo la vita katika ardhi ya adui alichoma meli moto kisha akawaambia "tuna maamuzi mawili: Moja ni kupambana tushinde vita na la pili ni kukubali adui atuzidi nguvu na wote tufie kwenye ardhi ya adui." Jambo muhimu la kijifunza ni kwamba unapoamua kufanya jambo unahitaji kuondoa visingizio vyote na kujiambia sasa nina jambo moja nalo si jingine bali ni kuhakikisha nafanikisha jambo hili. Kama askari wapiganaji una maamuzi mawili kwa jambo lililopo mbele yako: Moja kupambana hadi unaikishe jambo hilo au kukubali visingizio vikutoe kwenye mapambano.
✍πΎ Katika kila jambo ambalo umeamua kulikamilisha ni lazima utambue kuwa ni "do or perish". Jiulize ni mara ngapi umeshindwa kuchoma meli ambayo kila unapoitazama imekufanya uendelee kurudi nyuma. Meli katika maisha ya mafanikio inahusisha marafiki wabaya au tabia mbaya. Jiulize ni meli zipi ambazo zimekuwa zikikurudisha nyuma na hakikisha upo tayari kuziteketeza zote ili usonge mbele kwenye mapambano. Kila mara jisemee sentensi hii "bila kujali ugumu uliopo au magumu yalipo mbele yangu sina namna zaidi ya kuhakikisha nayashinda magumu hayo."
✍πΎ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza umuhimu wa kuondoa visingizio vyote ili kufanikisha hitaji lililopo mbele yako. Maamuzi yaliyopo mbele yako ni mawili KUSHINDA au KUSHINDWA. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika utaona mabadiliko katika maisha yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.
ππΎππΎππΎππΎππΎ
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
ππΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(