PALE UNAPOGUNDUA KUWA WEWE NI CHANZO CHA MATATIZO


NENO LA LEO SEPTEMBA 1, 2020): PALE UNAPOGUNDUA KUWA WEWE NI CHANZO CHA MATATIZO.

πŸ‘‰πŸΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku ya kwanza katika mwezi mpya ambapo tunaelekea kwenye robo ya mwisho ya mwaka 2020. Ni wakati ambao tunatakiwa kukaa na kutafakari mwenendo wetu kwa kipindi chote cha robo tatu za mwaka 2020 ambazo tumemaliza. Basi kwa pamoja tuianze siku kwa kusema “hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii ili nipate yaliyo bora katika maisha”.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tujifunza umuhimu wa kuwa tayari kubadirika pale tunapogundua kuwa sisi chanzo cha matatizo. Bahati mbaya sana kwa asili hakuna mwanadamu ambaye yupo tayari kuwajibika kwa kukubali makosa pale mambo yanapoenda kinyume na matarajio. Kila mtu yuko radhi kutafuta sababu mbalimbali ambazo zinamuondoa kwenye uhusika wa tatizo ili aoneke mwema. Zipo nyakati ambazo kila mtu anakunyoshea mikono lakini kutokana uzito wa moyo bado unaendelea kupambana ili uonekane mwema.

✍🏾 Kukubali kosa ni moja ya ukomavu wa hekima na busara. Unapokubali kosa moja kwa moja unakuwa kwenye nafasi  ya kujifunza kutokana na kosa husika. Kadri unavyopambana kuonekana hausiki kwenye kosa husika ndivyo unajinyima nafasi ya kujifunza. Kila unapogundua umekosea unakuwa upo tayari kuwajibika kutokana na kosa husika na kwa kuwajibika huko haupo tayari kurudia kosa husika. 

✍🏾 Ni rahisi kulalamikia watu wengine, mfumo au mazingira ili mradi ionekane kosa lililopo mbele yako limetokana na sababu maalumu. Ikiwa haupo tayari kukubaliana na kosa moja kwa moja kuwa wewe ndo mhusika mkuu haipo siku ambayo utabadirika. Watu wengi mambo yanapoenda hovyo wapo radhi kutafuta visingizio ili wajinasue kwenye kosa. Ikiwa kila mara unalalamika hakuna siku ambayo utabadirika kutokana na makosa unayotenda. Katika kila kosa unatakiwa kujiuliza umehusika vipi kiasi cha kufikia hatua hiyo.

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza umuhimu wa kukubali kuwajibika kulingana na kosa lililopo mbele yetu. Uzoefu wa mtu unaundwa na makosa pamoja na yale aliyofanya kwa usahihi katika kipindi cha uhai wake. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika utaona mabadiliko katika maisha yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

onclick='window.open(