ππΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine ambapo tunaamka tukiwa na afya na tupo tayari kuendelea kusukuma gurudumu la mafanikio. Ni asubuhi ambayo naendelea kukumbusha kuwa siku unayoisubiria ili mazingira yakae sawe ni leo maana hii ndiyo siku pekee ambayo kwa sasa una uhakika nayo. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍πΎ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza aina tatu za watu katika kufanikisha jambo lolote kwenye maisha. Binadamu wote ni wa baba na mama mmoja pale tunaporejea historia ya kuumbwa kwa mwanadamu. Hata hivyo kutokana na mazingira, malezi pamoja na elimu wanadamu wanatofautiana katika maamuzi na utekelezaji wa maamuzi yao. Kutokana na utofauti huo hebu tuangalie makundi matatu tofauti katika kufanikisha jambo:-
✍πΎ Kundi #1: Wale wanaoishia kutamani jambo litokee. Kundi hili katika jamii linahusisha watu ambao kila mara wanatamani jambo flani lifanyike katika maisha yao lakini hawachukui hatua yoyote ya kulifanikisha jambo hilo. Katika kundi hili watu hawana muda wa kujisumbua kujiuliza ni namna gani wanaweza kufanikisha jambo wanalotamani. Siku zinapita miaka inapita bila kuchukua hatua yoyote na hatimaye wanasahau kile walichotamani.
✍πΎ Kundi #2: Wale wanaojisikia au kuhisi kuwa wanaweza kufanikisha jambo lolote. Tofauti na kundi la kwanza watu katika kundi hili mara nyingi wanakuwa na uwezo wa kimbinu, maarifa/ujuzi na rasilimali kwa ajili ya kufanikisha jambo wanalotamani lakini huwa kila mara wanasogeza mbele kwa ajili ya kusubiria kesho iliyo bora. Na kuwa kesho haijawahi kufika, watu wanaendelea kukumbatia uwezo wao bila kuchukua hatua za kufanikisha jambo wanalotamani.
✍πΎ Kundi #3: Wale wanaochukua vitendo vya utekelezaji mara moja. Kundi hili linahusisha watu ambao bila kujali kama wana uwezo au hawana uwezo wapo tayari kufanikisha jambo lolote wanalotamani litokee maishani mwao. Kila wanapopata wazo jipya wanaanza kwa kujiuliza maswali muhimu ambayo yatapelekea kufanikisha jambo lililopo mbele yao. Hili ni kundi la watu wanaoishi kwa vitendo zaidi kuliko kulalamika au kuhairisha mambo.
✍πΎ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza makundi matatu ya watu katika kufanikisha jambo lililopo mbele yao. Amua sasa kuishi kwa vitendo badala ya kuendelea kusubiria kesho iliyobora. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.
ππΎππΎππΎππΎππΎ
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
ππΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(