NENO LA LEO (SEPTEMBA 21, 2020): KIFO KINAOGOPESHA – FAHAMU JINSI YA KUKABILIANA NA HOFU YA KIFO.
ππΎHabari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi mpya ambayo tumezawadiwa katika siku za uhai wetu hapa Duniani. Ni siku ambayo tunaalikwa kuendelea kutoa thamani ili kuacha alama ya jina letu mara baada ya ukomo wa maisha yetu hapa Duniani. Basi kila mmoja na aseme hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate kilicho bora katika maisha.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍πΎ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza namna ya kukabiliana na hofu ya kifo. Kifo ni miongoni mwa hofu ambazo zinamwandama kila mwanadamu. Inafahamika wazi kuwa hatima ya maisha ya mwanadamu hapa Duniani ni kifo (human beings are destined to death). Hivyo, kifo hakina tiba kwa mwanadamu yoyote kwa kuwa mwisho wa uhai ni kifo. Ukweli huu kuhusu kifo ndiyo ambao umewafanya wanadamu kuandamwa na hofu ya kifo kipindi cha maisha yao yote.
✍πΎ Watalaamu wa kila aina wanazalishwa kwa ajili ya kupunguza vifo kupitia tiba mbalimbali pamoja na rishe bora. Yote hii ni kwa ajili ya kuhakikisha kizazi cha mwanadamu kinaendelea kuwepo vizazi na vizazi. Hivyo, tunaweza kuendeleza kizazi chetu lakini hatuwezi kukwepa kifo. Binadamu ni muunganiko wa mwili na roho, na ndiyo maana kuna dini kwa ajili ya kutuongoza ili pale tunapozama kwenye matendo ya mwili roho ipo kwa ajili ya kutukumbusha kujutia matendo hayo.
✍πΎ Kupitia dini wote tunaweza kukabiliana na hofu ya kifo kwa kutambua kuwa kifo ni mpango wa Muumba kwa waja wake baada ya kukamilisha kazi waliyotumwa hapa duniani. Hivyo, kifo katika umri mdogo tafsiri yake ni kwamba mhusika amekamilisha kazi aliyotumwa kulingana na mapenzi ya Muumba. Lakini pia kupitia dini tunaamini kuwa kifo ni njia ya kuhama kutoka maisha ya Ulimwengu na kuingia kwenye maisha mapya ya utakaso yasiyo kuwa na mwisho. Hivyo, kifo ni utenganisho wa maisha ya ulimwengu ambayo yanatawaliwa na matakwa ya kimwili na kuingia kwenye maisha mapya ya kiroho maisha mapya ambapo hakutakuwa na kuoneana wivu, njaa, magonjwa au mateso.
✍πΎ Si kweli kwamba watu wanaogopa kifo, ukweli ni kwamba katika nyakati ambazo watu wanaona kifo kipo karibu yao huwa kuna vitu vitatu ambavyo huwa wanaogopa ikilinganishwa na kifo chenyewe. Moja, katika nyakati za magonjwa hatari wahusika wanaogopa endapo wataendelea kupata msaada ipasavyo kutoka kwa watu wao wa karibu katika kipindi chote cha maumivu (kabla ya umauti kuwapata). Mbili, watu katika nyakati wa kukaribia kifo wanajutia kuwa huenda wamepoteza maisha yao kwa kufanya mambo ambayo hayakuwa na tija kwao na jamii iliyowategemea. Tatu, wanaogopa kuwa hawakutimiza wajibu ipasavyo kiasi ambacho hawajaacha alama ambayo ingekuwa ukumbusho wa maisha yao.
✍πΎ Sababu hizi zote zinapeleka wahusika wengi waliopo katika hali ya kungojea umauti kujiona kuwa kuna mambo mengi ambayo hawajayakamilisha katika enzi ambazo walikuwa na uwezo wa kuyakamilisha. Huu ndiyo uoga mkubwa wa binadamu kuelekea kwenye kifo hivyo ukiwa unahitaji kukabiliana na hofu ya kifo huna budi kuhakikisha unaishi maisha kwa ukamilisho wake kwenye kila siku unayobahatika kuishi.
✍πΎ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa kifo hakiondoi maana au thamani ya maisha yetu bali kifo kinasaidia kuelezea namna maisha yetu yalivyokuwa na thamani kwa siku hizo chache tulizobahatika kuishi. Tafsiri yake ni kwamba kutokana na hofu ya kifo tunatakiwa kuweka mipaka kwenye yapi tunaweza kufanya na yapi hatutakiwi kufanya katika enzi za uhai wetu. Fanyia kazi mafundisho haya ili maisha yako yawe na thamani kwako na jamii inayokuzunguka. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Neno la tafakari ya leo limeandaliwa kutoka kwenye uchambuzi wa Kitabu cha “Conquering Fear” kutoka kwa mwandishi Harold S. Kushner. Kujifunza zaidi kuhusiana na namna ya kukabiliana na hofu zinazomkabili mwanadamu hakikisha unapata nakata ya uchambuzi wa kitabu hiki kwa kulipia Tshs. 3,999/=. Hiki ni kitabu ambacho utajifunza mambo mengi hasa kwenye ulimwengu wa maendeleo ya kiroho. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.
ππΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(