NENO LA LEO SEPTEMBA 2, 2020): NITAFANYA, NITAFANYA...! SIKU ZINAPITA HAKUNA LINALOFANYIKA.
ππΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine tena katika siku za uhai wa maisha yetu. Ni siku ambayo tunaalikwa kuboresha maisha yetu kwa kuhakikisha kila siku tunatoa thamani kwa jamii inayotuzunguka. Ni siku ambayo tunakumbushwa kuwa ni kupitia kile tunachofanya kila siku tunapata kutengeneza mafanikio makubwa katika maisha yetu. Basi kwa pamoja tuianze siku kwa kusema “hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii ili nipate yaliyo bora katika maisha”.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍πΎ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tujifunza umuhimu wa kuwa mtu wa vitendo kliko na maneno yasiyotekelezeka. Ni mara nyingi tumekuwa watu wa kusogeza mbele mambo ambayo yanawezekana kutekelezeka leo. Mara nyingi tunaishi kana kwamba tuna uhakika wa matukio katika siku za maisha yetu ya baadae. Wakati mwingine tunaishi kana kwamba tuna agano na Muumba kuwa siku za maisha yetu zitadumu milele tena kwa afya na nguvu zile zile.
✍πΎ Siku zinakuja ambazo hatutaweza kutekeleza kile ambacho tuna uwezo wa kukitekeleza sasa. Siku zinakuja ambazo tutakuwa na majukumu mengi kuliko muda wa kuyatekeleza. Siku zinakuja ambazo hatutakuwa na nguvu tena ya kutekeleza yale ambayo tuna uwezo nayo kwa sasa. Siku zinakuja ambazo tutakumbuka fursa, nafasi, muda na rasilimali ambazo tumepoteza. Siku zinakuja ambapo tutawakumbuka watu muhimu ambao tulishindwa kuwatumia ipasavyo ili watusogeze hatua moja mbele katika safari yetu ya mafanikio.
✍πΎ Hakika wakati sahihi ni sasa, fursa muhimu ni hiyo ambayo kila mara unasema ngoja mazingira yakae sawa. Watu muhimu wa kutumia mabega yao kama ngazi ni hao ambao wanakuzunguka. Rasilimali ya kukuwezesha kupiga hatua ni hizo hizo unazomiliki kwa sasa. Mazingira sahihi si mengine ni hayo yanayokuzunguka. Umri sahihi ni huo ulionao maana kwenye kuishi ndoto ya maisha yako hakuna kuwahi wala kuchelewa. Unaweza kuanza ukiwa na umri mdogo ukatimiza ndoto zako lakini pia unaweza kuanza na umri ambao wengine wanasema umechelewa lakini ukawashangaza. Kumbuka, Colonel Sanders aliweza kuwa bilionea kupitia mapishi bora mara baada ya kustaafu akiwa na umri wa miaka 65!
✍πΎ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa wakati ulio sahihi ni sasa. Umri sahihi ni sasa. Mazingira sahihi ni sasa. Fursa muhimu ni hiyo ambayo kila mara unaisogeza mbele. Watu sahihi wa kuwatumia ni hao hao ambao unafahamiana nao. Anza sasa maana daima hakuna wakati ulio sahihi kuliko sasa. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika utaona mabadiliko katika maisha yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.
ππΎππΎππΎππΎππΎ
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
ππΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(