NENO LA LEO (SEPTEMBA 18, 2020): WAKATI MWINGINE KATIKA MAISHA NI VIGUMU KURIDHISHA KILA MTU.
Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi mpya ambayo imejaa mategemeo makubwa kwa wale ambao wamedhamiria kuishi ndoto za maisha yao. Ni matumaini yangu kuwa tumeamka salama tukiwa na nguvu na hamasa ya kutosha kwa ajili ya kuendeleza yale yenye tija katika maisha yetu. Basi kila mmoja wetu aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍πΎ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza umuhimu wa kutambua kuwa zipo nyakati ambazo hauwezi kuridhisha kila mtu iwapo unahitaji kusonga mbele. Ukweli ni kwamba mafanikio katika maisha ni zao la maamuzi katika kutoa kipaumbele kwenye mambo ya msingi na kuachana na yale ambayo kwako yanaonekana hayana tija.
✍πΎ Tatizo huwa linaanzia hapo kutokana na ukweli kwamba yale yanayoonekana yenye tija kwako yanaweza kukufanya uonekane msaliti kwa wengine. Tunafahamu kuwa tunaishi katika familia tegemezi hasa katika bara la Afrika. Utegemezi huu ndiyo unafanya watu wengi washindwe kutimiza ndoto walizonazo kwa kuwa inafikia sehemu ambapo watu wanashindwa kufanya maamuzi sahihi. Yote hayo yanafanyika ili mradi tu kuridhisha wale wanaotuzunguka.
✍πΎ Hata hivyo, uzoefu unaonesha kuwa hakuna siku hata moja ambayo utaridhisha kila mtu. Kutokana na ukweli huu kuna kila sababu ya kuamua unataka nini katika maisha yako na kuamua kuziba masikio kwa kipindi cha muda maalumu ili kelele za watu zisikutoe kwenye mstari.
✍πΎ Suala la watu kutoridhika linaanzia kwenye ngazi ya familia mpaka kwenye ngazi ya makundi ya kijamii au uongozi wa juu. Mara nyingi tumeona katika ngazi ya taifa ambapo viongozi wengi huwa wanalamikiwa katika enzi za utawala wao lakini ghafla baada ya kutoka madarakani utashangaa watu wanaanza kusema bora flani.
✍πΎ Hii yote inadhihirisha kuwa binadamu ni kiumbe ambaye ni vigumu sana kukidhi matakwa yake. Ukifanya jambo moja utaambiwa mbona hili hukufanya? Ukifanya yote utaambiwa kulikuwa na ulazima gani wa kugusa yote kwa wakati mmoja. Hapa ndipo unatakiwa kuziba masikio na kutekeleza maamuzi sahihi na kuachana na kelele za watu.
✍πΎ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa utachelewa sana ikiwa unafanya mambo yako kwa ajili ya kumridhisha kila mtu. Tumeona kuwa ni vigumu sana kuridhisha matakwa ya watu kwa kuwa linaloonekana la msingi kwa mtu mmoja kwa mwingine linaonekana siyo kipaumbele. Ziba masikio, tekeleza maamuzi sahihi na hakika ipo siku watakuelewa. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.
ππΎππΎππΎππΎππΎ
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
ππΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(