NENO LA LEO (SEPTEMBA 13, 2020): FAHAMU SIFA MUHIMU ZA KUWA MUUZAJI BORA.
Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni wakati huu ambao tumepewa tena kibali cha kuendeleza bidii kwa ajili ya kubadilisha maisha yetu ili yawe na thamani kwa nafsi na roho zetu, jamii inayotuzunguka na mazingira tunayoishi kwa ujumla. Basi kila mmoja wetu aianze siku kwa kusema hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza mbinu muhimu za kufanikisha mauzo ya biashara yako. Katika neno la tafakari ya jana tulijifunza vitu muhimu vya kuzingatia wakati wa kuanzisha biashara. Wote kwa pamoja tunakubaliana kuwa ukuaji wa biashara yoyote unategemea uwezo wa mmiliki kufanikisha uuzaji wa bidhaa au huduma kwa wateja. Kwa ujumla ili ufanikiwe kuwa muuzaji mzuri ni lazima utambue kuwa wateja wanahitaji: “kukupenda, kukuamini, kuwa na tumaini na wewe na hatimaye wawe na uhakika na wewe” ili waendelee kununua biadhaa/huduma zako. Karibu tujifunze sifa muhimu:-
✍🏾 Sifa #1: Tambua kuwa wateja hawataki kuuzwa kwa maana ya kutapeliwa bali wanahitaji kununua. Hapa ndipo kila muuzaji ni lazima kwanza apate jibu la kwa nini watu wananunua kwake? Hili ni swali muhimu la kuzingatia kabla ya kuanza kuweka malengo ya mauzo japo wauzaji wengi huwa wanakosea na kujiuliza ni kwa jinsi gani nitauza? Hauwezi kufanikiwa katika jibu la swali la pili kwa maana ni kwa jinsi gani nitauza kama haujapata jibu la kwa nini watu wananunua.
✍🏾 Sifa #2: Jivike sifa za muuzaji bora. Kinachowatoutisha watu au taasisi katika viwango vya mauzo ni namna ambavyo wanatumia mbinu za mauzo. Mbinu za mauzo ni nyingi lakini ni vyema kila muuzaji akafahamu kuwa ili uwe muuzaji bora ni lazima uzingatie mbinu hizi hapa (a) Kwanza kabisa ujiamini kuwa unaweza (b) Andaa mazingira ya kukuwezesha kuwa muuzaji bora ikiwa ni pamoja na kuchagua kundi la marafiki wanaokufaha (c) Pata muda kujifunza (d) Kuwa na majibu ambayo unahisi wateja watakuuliza maswali (e) Toa thamani kwa wateja (f) Kuwa mtu wa vitendo na mara zote husiogope kushindwa (g) Chunga sana matumizi yako ikilinganishwa na uwekezaji au akiba yako (h) Jenga tabia njema na muda wote kuwa macho kwa ajili kuliteka soko; na (i) Wapuuze watu wanaokubeza.
✍🏾 Sifa #3: Andaa malengo ya mauzo na hakikisha kila siku unayapitia. Ili kujipima kama unasonga mbele kimauzo ni lazima uwe na malengo na kila siku unatenga muda kwa ajili ya kufanya tathimini namna ambavyo umefanikisha malengo ya siku husika. Hapa unatakiwa kuongozwa na nidhamu ya hali ya juu yenye chimbuko la hamasa kutoka ndani mwako pasipo kusubiria kusukumwa na mwajiri wako au mtu yeyote.
✍🏾 Sifa #4: Hakikisha upo tayari kuwajibika. Hautakiwi kulaumu mfumo au Serikali, mazingira au wafanyabiashara wengine wanaokuzunguka kutokana na kiwango duni cha mauzo. Watu wengi wanafikia hatua ya kulaumu waajiri wao, Serikali, watu wao wa karibu au hata pengine wateja kabla ya kujiuliza wao wanahusika vipi kwenye kiwango duni cha mauzo.
✍🏾 Sifa #5: Fahamu kuwa mauzo ni matokeo ya mambo mengi yanayokuhusu wewe. Kiwango cha mauzo kinategemea na (a) Imani yako – Je unajiamini kuwa unaweza kuuza kwa kiwango kile unachokusudia? (b) Mazoea ya kazi yako – Je unaenda kazini ukiwa umechelewa na jioni unafunga mapema lakini bado unategemea kuwa na kiwango kikubwa cha mauzo? (c) Hisia mbaya juu yako – Je unahisia mbaya juu ya bidhaa/huduma au una wasiwasi wa bei zako? (d) Tabia mbaya kama ulevi/uvutaji wa sigara ukiwa kazini (e) Hautimizi ahadi kwa wateja au pengine unatimiza kinyume na makubaliano. Hizi baadhi ya sehemu muhimu ambazo unatakiwa kujitathimini kwa ajili ya kuboresha kiwango cha mauzo yako.
✍🏾 Sifa #6: Kuwa na falsafa zako kuhusu mauzo. Falsafa zinazaa mtazamo, mtazamo unaleta vitendo na vitendo vinaleta matokeo na hatimaye matokeo yanaleta mtindo wa maisha yako. Kama haupendi mtindo wa maisha yako ni lazima kwanza uangalie falsafa zinazokuongoza na hatimaye uzibadilishe falsafa hizo kwa ajili ya kufikia mtindo mpya wa maisha. Watu wa mauzo mara nyingi wanafanya kosa kubwa la kutazama sehemu ya vitendo kabla ya kuangalia kwanza falsafa zinazowaongoza. Kwa kifupi falsafa ni vile vitu ambavyo una imani juu yake na katika maisha yako na umevifanya kuwa mwongozo wako kwenye kila sekta ya maisha yako.
✍🏾 Sifa #7: Kuwa na mtazamo wa NDIYO. Mtazamo wa ndiyo ni nyenzo muhimu ya kukabiliana na kila aina ya mazingira au tukio kwa muuzaji yeyeto yule. Unapokua na mtazamo wa ndiyo moja kwa moja unakuwa tayari kufanya kazi kwenye mazingira ambayo wengine wanaona hayawezekani. Mtazamo huu unakufanya ujione kuwa kila kitu au tukio linaanza na NDIYO hata kama ni HAPANA hivyo kukujengea msingi imara wa kuona kuwa kila jambo linawezekana.
✍🏾 Sifa #8: Kuwa na utambulisho wako (self branding). Utambulisho ni nyenzo ambayo itakutambulisha kwa wateja wako pamoja na kukutofautisha na wapinzani wako katika soko. Kadri watu wanavyokufahamu zaidi ndivyo watavutiwa kufanya biashara na wewe. Kabla ya kutangaza bidhaa/huduma zako unahitaji kujitangaza mwenyewe. Katika kujitambulisha unahitaji kujipambanua kama mtu mwenye dhamira ya kupigania kutatua matatizo ya jamii inayokuzunguka. Katika tasnia ya mauzo ni lazima utambue kuwa “si yule unayemfahamu bali ni yupi anakufahamu” hivyo unahitaji kujitangaza kwa hali na mali.
✍🏾 Sifa #9: Tambua kuwa bei siyo kigezo cha kuongeza mauzo. Thamani ya bidhaa zako pamoja na mahusiano yako na wateja ni sifa mbili muhimu za kuongeza kiwango cha mauzo ikilinganishwa na bei ya bidhaa/huduma zako. Ukweli ni kwamba thamani kwa mteja ni vile vitu vinavyofanyika kwa mteja au mteja tarajiwa kwa ajili ya faida yake pasipokutegemea utafaidika na nini. Kwa maana hii ni lazima kwanza utangulize thamani kwa mteja na hatimaye faida itakufuata yenyewe. Mfano, unaweza elimu juu ya bidhaa au huduma yako kupitia makala, mitandao ya kijamii au semina za bure huku ukiacha namba zako za mawasiliano kwa ajili ya wateja tarajiwa
✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza sifa muhimu ambazo zitakuwezesha kuwa muuzaji bora. Ukuaji wa biashara ni mauzo hivyo hakuna namna nyingine zaidi ya kuweka mpango maalumu wa kujifunza mbinu za uuzaji. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika utaboresha mauzo ya biashara yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.
👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
👐🏾 Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(