HUYU NDIYE ADUI WAKO NAMBA MOJA KATIKA KUISHI NDOTO YAKO.

NENO LA LEO (SEPTEMBA 10, 2020): HUYU NDIYE ADUI WAKO NAMBA MOJA KATIKA KUISHI NDOTO YAKO. 

πŸ‘‰πŸΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi mpya katika siku za uhai wetu ambayo tunakopeshwa kwa ajili ya kuitumia vyema ili mwisho wa uhai wetu tupate kutendewa kulingana na matendo yetu. Ni katika asubuhi hii naendelea kukumbusha umuhimu wa kuishi ndoto yako kwa vitendo bila kujali udogo wa vitendo hivyo. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza jinsi ambavyo unajichelewesha mwenyewe kutokana na uwepo wa matumaini kuwa siku zipo. Ni kawaida kwa mwanadamu kupanga ratiba ya matukio ambayo anatamani yakamilishwe katika kipindi cha siku zijazo. Kutokana na tabia hii wengi huwa wanasogeza mbele matukio ambayo kulikuwa na uwezekano wa kukamilishwa katika nyakati zilizopo.

✍🏾 Kwani nini watu wengi wana tabai hiyo? Hii ni tabia ambayo imezoeleka kwa kuwa wengi wanadangaywa na adui mkubwa aitwaye KESHO. Huyu ni adui ambaye kila mara anakudanganya kuwa kesho utakuwa na muda wa kutosha. Huyu anakuambia kesho nitakuwa sijachoka kama leo. Huyu ndiye anakuambia kesho mambo yako yatakaa sawa kiuchumi hivyo leo husijisumbue. Huyu ndiye adui anayekuambia kwa nini ujitese leo kwa kujinyima wakati kesho utapata pesa za kutosha. Huyu ndiye anayekuambia subiria kutekeleza wazo lako kwa kuwa kesho mazingira yatakaa sawa.

✍🏾 Baada ya kugundua adui yako mkubwa kwa pamoja tujiulize  ni lini kesho huwa anakuwa katika nyakati kamilifu?. Ukweli ni kwamba jibu ambalo tunapata kwa pamoja ni kukubaliana kuwa hakuna siku ambayo kesho atakuwa kamilifu. Hii ni kutokana na ukweli kuwa kila unaposema siku ya LEO kuna siku ya KESHO inafuatia. Tafsiri yake ni kwamba siku pekee ambayo ni kamilifu ni sasa. Wakati pekee ambao ni kamilifu ni huku ulionao sasa. Tunaweza kuweka mikakati kwa ajili ya wakati ujao lakini bila kujibidisha katika wakati uliopo hakuna siku hata moja mikakati hiyo itatekelezwa.

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa KESHO amekuwa adui wako namba moja katika kuishi ndoto ulizonazo.  Wakati wa kubadilika ni sasa, wakati wa kutembea ni sasa, wakati wa kuishi kwa vitendo ni sasa na wakati ulio bora zaidi ni sasa. Hakuna KESHO iliyo bora ikiwa LEO haijatumika vyema. Ishi sasa kwa ajili ya kesho. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

onclick='window.open(