KILA MTU ANATAMANI MADARAKA: ZINGATIA HAYA UPATE MADARAKA YA KWELI.

NENO LA LEO (FEBRUARI 20, 2021): KILA MTU ANATAMANI MADARAKA: ZINGATIA HAYA UPATE MADARAKA YA KWELI.

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine ambayo tunaendelea kupewa kibali cha uhai. Mara kadhaa nimekuwa nikiandika kuwa siku zetu hapa Duniani ni fupi. Katika siku hizo fupi kuna kipindi ambacho tunachanua kama maua, hiki ni kipindi ambacho tunatakiwa kujifunza kila mara sambamba na kuishi kwa vitendo yale tunayojifunza.

 Kama bado hujajiunga na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI kwa ajili ya kupata neno la tafakari kila siku, tafadhali JIUNGE SASA.

Miongoni mwa kiu ya binadamu katika siku chache za uhai wake ni kiu ya madara. Kwa maumbile kila mmoja wetu amezaliwa na nguvu ya madaraka ndani mwake na nguvu hii inaanza kutumika ipasavyo pale muhusika anapotambua yeye ni nani na ameumbwa ili atimize nini katika ulimwengu huu. Hata hivyo, kila mtu anatakiwa kutambua kuwa madaraka aliyonayo ni kwa ajili ya nafsi yake na watu wote wanaomzunguka. Pia, tunatakiwa kufahamu kuwa madaraka halisi kwa kila mtu chimbuko lake ni kuishi maisha yenye furaha kwa wakati uliopo, maisha yasiyo na hofu, ulevi, ubaguzi, hasira na upumbavu wa kila aina. Kwa maana furaha ni haki ya kuzaliwa ambayo kila mtu anastahili hata kama yeye mwenyewe hajatambua haki hiyo.

Ukweli ni kwamba tunaendelea kuishi katika nadharia ya uongo kuwa chanzo cha madaraka ni elimu, utajiri, mafanikio, ukubwa wa vyombo vya jeshi, umaarufu, kipaji na nguvu au nafasi ya kisiasa. Hii ni kinyume kabisa na chanzo cha madaraka halisi kutokana na ukweli kwamba madaraka yanatakiwa yaanzie kwenye mfumo wa fikra wa kila mtu pasipo kujali nafasi au elimu yake.

Madaraka ya kweli ni lazima yazingatie mambo yanayotokea ndani na nje ya mhusika. Kwa maana hii, madaraka ambayo kila mtu amerithishwa kupitia uumbaji ni lazima yazingatie mahitaji ya nafsi kupitia mfumo wa fikra lakini pia mahitaji ya watu wanaomzunguka. Madaraka ya namna hii yanajengwa katika msingi wa kufurahia kazi unayofanya ambayo pia ni lazima iwe inawasaidia watu wanaokuzunguka kutambua na kutumia vyema madaraka yao. Hii ni kwa mtu yeyote yule kuanzia kwa mfanyabiashara, mkulima, msanii, mwanasiasa au mfanyakazi. Kila mmoja katika makundi haya ni vyema kutanguliza lengo kubwa la kuwasaidia watu kupitia kazi yake na hatimaye mafanikio mengine yafuate.

Msingi wa madaraka tuliyonayo au tunayoyataka ni lazima uwe ni mapenzi ya dhati kwa familia zetu, wenza na watoto wetu, jamii inayotuzunguka. Ili kufanikiwa katika msingi huu ni lazima tusikubali kuruhusu maisha yetu yatawaliwe na yale tunayoyafanya kiasi cha kusahau kuwa karibu na wapendwa wetu. Daima tunakiwa kufahamu kuwa kuna furaha nje ya hayo tunayokimbizana nayo kila siku na furaha hiyo haipo sehemu nyingine zaidi ya kuwa na muda wa kufurahi na familia zetu.

Hata hivyo, ni lazima kutambua kuwa madaraka ya kweli yanatokana na mwendelezo wa bidii zako pasipo kurudi nyuma au kutafuta njia ya mkato. Njia rahisi ya kufanikiwa katika siri hii ni kujenga tabia ya utulivu wa akili katika kila jambo unalofanya na kuhakikisha unatenga muda wa kuongea na nafsi yako kila siku. Pia, mafanikio ya zoezi hili ni muhimu yapate baraka za wanafamilia. Hata hivyo, unaweza kufanikisha utulivu wa akili kwa kujenga tabia ya kufanya tajuhudi (meditation). Kupitia tajuhudi unapata utulivu wa akili sambamba na kuweza kuwasiliana na roho zenye mtazamo sawa na wako.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI 

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza mambo muhimu kuhusu madaraka ambayo ni kiu ya kila mwanadamu. Madaraka yanaambatana na uongozi katika kila ngazi ya makundi ya kijamii. Kutokana na hilo, madaraka uliyonayo yanatakiwa yawe kwa ajili ya watu ili uepuke kuumiza watu wa chini yako. Kiongozi bora ni yule anayetanguliza upendo, busara, huruma na hasiye na majivuno kwa watu wake. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(