NENO LA LEO (FEBRUARI 11, 2021): JE WEWE UPO KATIKA KUNDI LIPI KATI YA HAYA?
Habari
ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine
ambapo ni matumaini yangu kuwa umeamka salama ukiwa na hamasa ya kutekeleza
majuku yako ya leo. Kila siku mlango unafunguliwa kwetu ili tupate kubadilisha
mtazamo wetu kuhusu ulimwengu na vyote vilivyopo ndani yake. Siku ya leo
nakualika ubadili mtazamo wako kuhusu watu, badili mtazamo wako kuhusu pesa,
badili mtazamo kuhusu fursa, badili mtazamo wako kuhusu mwenza wako, badili
mtazamo wako kuhusu mazingira yanayokuzunguka na badili mtazamo wako kwenye
kila sekta ya maisha yako. Hatua hiyo itakuwezesha uione Dunia katika sura
tofauti na ulivyozoea.
Katika neno la tafakari ya leo nitakushirikisha makundi matatu ya watu katika jamii yetu. Neno hili ni mwendelezo wa neno la tafakari ya jana ambapo tuliona watu wengi wanachelewa au wanashindwa kupata hitaji la maisha yao kwa kuwa wanasita kuchukua hatua ya kwanza. Mafanikio ya aina yoyote yanaanzia kwenye hatua ya kutaka (want), inafuatia hatua ya kutamani (wish) na mwisho wake ni vitendo (action). Hatua ya kwanza inachochea hatua ya pili ambayo inapelekea kuingia kwenye hatua ya mwisho ikiwa mhusika amedhamiria kupata hitaji husika. Neno hili limeandaliwa kutoka kwenye nukuu ya mchezaji maarufu wa kipapu Michael Jordan kuwa "some people want it to happen, some people wish it to happen, others make it happen". Kutokana na hatua hizo tunapata makundi matatu ya watu katika jamii katika kuelekea kwenye mafanikio wanayotamani kama ilivyoelekezwa hapa chini:-
Kundi #1: Wale wanaoishia kwenye hatua ya kutaka mabadiliko yatokee. Kundi hili linahusisha watu wengi ambao huwa wanahamasika kubadilika lakini hawajibidishi kuchukua hatua za ziada kuelekea kwenye mafanikio husika. Katika jamii kundi hili lina watu wengi kwa kuwa wengi huwa wanataka mabadiliko lakini hawana mkakati wowote wa kufikia mabadiliko wanayotamani. Mfano, mtu anatamani kupungua uzito lakini hana mkakati wowote utakaopelekea apungue uzito. Kundi hili huwa linahusisha watua ambao wanaishia kushangaa matokeo ya wale wanaochukua hatua za kivitendo kufanikisha hitaji la maisha yao.
Kundi #2: Wale wanaoishia hatua ya kutamani mabadiliko. Kundi hili linahusisha watu ambao huwa wanaingia hatua ya pili katika kuelekea kwenye hitaji la maisha yao. Katika hatua ya kutamani mhusika anachukua hatua ambazo zinahusisha kujenga mazingira ya msingi katika kuelekea hatua ya mwisho ya vitendo. Hapa mhusika anafanya tafiti kuhusiana na hitaji lake ikiwa ni pamoja na kukusanya taarifa zinazohusiana na hitaji lake kwa wakati huo. Hata hivyo, wengi huwa wanaishia hatua hii kwa kuogopa kusonga mbele kutokana na kujiona hajawa tayari katika kuelekea kwenye hitaji husika. Kundi hili lina watu wengi ambao wanakuwa na maandalizi ya muda mrefu katika kuelekea kwenye hitaji la maisha yao.
Kundi #3: Wale wanaowezesha
mabadiliko yatokee. Kundi hili linahusisha watu ambao wanaongozwa na
vitendo zaidi kuliko maneno. Hawa ni watu ambao ni nuru ya katika jamii kutokana
na mafanikio wanayofikia katika maisha yao. Kundi hili linahusisha watu ambao
wanaenda hatua ya ziada ikilinganishwa na makundi mengine katika jamii. Kama ni
teknolojia mpya watu katika kundi hili huwa ndo wanakuwa wa kwanza kuitumia
wakati makundi mengine yakiwa hayana habari na teknolojia hiyo. Pia, watu wengi
katika kundi hili wanakuwa wabunifu katika maisha ya kila siku.
Mwisho, katika neno la tafakari ya leo nimekushirikisha makundi matatu ya watu kwenye jamii katika kuelekea kwenye mabadiliko wanayotamani. Kupitia neno hili unaweza kujipima upo kwenye kundi lipi kulingana na jinsi unavyopiga hatua kuelekea kwenye mabadiliko unayotamani katika maisha yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.
ππΎππΎππΎππΎππΎ
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu
Augustine Mathias
Mawasiliano:
0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua
pepe: fikrazakitajiri@gmail.com