JE NI KIPI CHANZO CHA FURAHA HALISI KATIKA MAISHA?

NENO LA LEO (FEBRUARI 15, 2021): JE NI KIPI CHANZO CHA FURAHA HALISI KATIKA MAISHA?

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine ambapo ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuendeleza pale ulipoishia jana. Ikiwa ni siku ya kwanza ya juma natumaini kuwa umeainisha majukumu muhimu ambayo unatakiwa kuyatekeleza katika wiki hii. Hali hii inatokana na ukweli kwamba mafanikio hayapatikani nje ya majukumu yako ya kila siku ikiwa tu kila unachofanya kinatokana na lengo kuu la maisha yako.

 Kama bado hujajiunga na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI kwa ajili ya kupata neno la tafakari kila siku, tafadhali JIUNGE SASA.

Katika neno la tafakari ya leo nitakushirikisha chanzo cha furaha halisi katika maisha. Neno la leo limeandaliwa kutoka kwenye mafundisho ya Epicurus kuhusiana na jinsi mwanadamu anatakiwa kuwa na furaha katika maisha. Epicurus ni miongoni mwa Wanafalsafa kutoka Ugiriki aliyefundisha mafundisho ya Ustowa (Stoicism). Epicurus anachukuliwa kuwa mtu muhimu katika historia ya sayansi, falsafa na imani. Katika mafundisho yake alisisitiza umuhimu wa kulinganisha imani na ushahidi wa kimantiki na mantiki, na maoni ya kisayansi.

Kuhusiana na furaha alifundisha kuwa kuwa raha ndio thamani ya ndani kwa mtu na kupitia thamani hiyo mtu anapata sababu za kuendelea kuishi. Kwa Epicurus, maisha mazuri zaidi ni pale tunapoepuka tamaa zisizo za lazima na kufikia utulivu wa ndani kwa kuridhika na vitu rahisi, na kuchagua urafiki wa dhati na wa kudumu badala ya kutafuta raha za mwili kama chakula, kinywaji, mavazi na tamaa za mwili kama ngono.

Hivyo, kulingana na mafundisho ya Epicurus, “Furaha ni kuwa na raha katika kila unachofanya na kuendelea kuwa na raha kwenye matokeo ya kile unachofanya”; vitu vyote tunavyojihusisha navyo vinapaswa kufanywa kwa hisia za kupendezwa ambazo hupelekea furaha kwa mhusika.  Katika maisha ya kila siku kuna matakwa ya lazima na yasiyo ya lazima. Tamaa za lazima, kama kutamani kuwa huru kutoka kwenye maumivu ya mwili, husaidia kupata furaha, wakati tamaa zisizo za lazima, kama vile kutamani gari kubwa au chakula cha gharama kubwa, kawaida huleta kutokuwa na furaha katika maisha.

Kumbe, lengo siyo kutafuta mazuri ya raha katika maisha ya kila siku bali tunatakiwa kulenga kuondoa maumivu yanayotokana na tamaa umiliki wa vitu visivyo vya lazima.  Chanzo halisi cha furaha ni kuridhika na hali unayopitia ambayo mara nyingi hutafsiriwa kama "utulivu wa ndani." Hali hii inaweza kupatikana kupitia tafakari ya kifalsafa badala ya kutafuta raha za mwili. Na mwisho, Epicurus anatufundisha kuwa “Furaha” siyo jambo la kibinafsi: inaweza kupatikana kwa urahisi katika jamii ambayo watu wenye nia moja huungana pamoja katika kusaidia kuhamasishana kuishi maisha ya furaha bila kujali changamoto wanazopitia katika maisha.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI 

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza chanzo hali cha furaha kulingana na mafundisho ya Epicurus. Kupitia neno hili unatakiwa kutambua kuwa furaha haitokani na umiliki wa vitu au kuishi maisha ya kuridhisha matamanio ya mwili. Furaha halisi inatokana na kuridhika ndani mwako katika mazingira unayopitia. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(

Related Posts