HII NDIYO THAMANI ILIYOPO KWA MAKUNDI YA WATU UNAOKUTANA NAO

NENO LA LEO (FEBRUARI 8, 2021): HII NDIYO THAMANI ILIYOPO KWA MAKUNDI YA WATU UNAOKUTANA NAO

Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya ambapo tunaanza juma jipya ambapo wote tunakaribishwa kuendeleza pale tulipoishia jana. Ni katika asubuhi hii tunakaribishwa kutafakari hatua tunazoweka katika kutimiza malengo tuliyojiwekea kwenye kila sekta ya maisha yetu. Hivyo, kipekee ufanye tafakari ya maisha yako na kisha kufanya maboresho sehemu unaona umekwama.

Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA 

Katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha umuhimu wa kuanza kugundua thamani iliyopo katika makundi mbalimbali ya watu unaokutana nao. Tunaishi katika makundi ya watu kwenye jamii na kila kundi lina thamani yake katika kuelekea kilele cha mafanikio ya ndoto zetu. Makundi haya yanaweza kuwa na idadi ya mtu mmoja au zaidi na wakati mwingine ni watu wa karibu yetu. Wanaweza kuwa marafiki, mwajiri, wafanyakazi wenzio, majirani, wafanyabiashara ambao unahusiana nao, wazazi au mwenza wako. Kila mtu katika makundi hayo ana thamani yake ambayo inaweza kuwa katika makundi yafuatayo:- 

Kundi #1: Watakaokujaribu. Kundi hili linahusisha watu ambao muda wote mnaokuwa pamoja wanakuweka kwenye majaribu ya kila aina. Majaribu hayo yanaweza kuwa chanzo cha kukukwamisha kufikia malengo binafsi katika kila sekta ya maisha yako. Wajibu wako katika kushinda watu hawa ni kutambua sehemu ambazo unajaribiwa na kusimama imara dhidi ya majaribu hayo. Hata hivyo, hupaswi kuwaona watu hawa kama maadui na badala yake unatakiwa kujua sehemu unazojaribiwa na sababu za kujaribiwa. Kama kuna sababu ambazo unataona wewe ni chanzo cha kujaribiwa huna budi kujirekebisha.

Kundi #2: Wanaokuchukia: Kundi hili linahusisha watu ambao inatokea kila unalofanya liwe jema au baya utaendelea kuonekana mbaya kwao. Hali hii ni kawaida kutokea maana huwa kuna kupishana mtazamo, fikra au upeo. Watu wengine katika kundi hili huwa wanafikia hatua ya kukuombea mabaya katika maisha yako. Mfano, mtu anaweza kukuombea ufukuzwe kazi, upate ajali, au lolote baya ambalo kwake atafurahi. Hawa ni watu ambao unatakiwa kuwaona kama maadui wako lakini katika hali ya kawaida husifanye uadui uwe wa pande mbili. Acha uadui ubakie upande wao kwa maana hautakiwi kulipiza ubaya kwa ubaya. Endelea kuwatendea mema au kuwaonesha kuwa wanachofanya siyo sahihi. Thamani iliyopo katika kundi hili la watu ni kutambua kuwa maisha siyo uadui, ikiwa hautaki kutendewa mabaya hautakiwi kuwatendea mabaya wengine.

Kundi #3: Watakaokufundisha. Hili ni kundi la watu ambao muda wote wapo upande wa mafanikio yako. Kundi hili linajumuisha watu ambao watakuhamasisha, watakuelimisha, watakukosoa na watakufungulia milango kwa ajili ya kupiga hatua za mafanikio zaidi. Watu hawa wanaweza kuwa wazazi, mwenza wako, walimu wako wa kitaaluma au kiroho au wasimamizi wako wa kazi. Hili ni kundi la watu muhimu katika mafanikio ya maisha yako hivyo ni watu ambao unatakiwa kuwatambua na kuwatumia kila mmoja kwa nafasi yake.  Wakati mwingine hauwezi kuona nafasi ya watu hawa katika maisha ya kila siku hila pindi unapowakosa ndipo unatambua umuhimu wao.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI 

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo nimekushirikisha makundi matatu ya watu ambao unatakiwa kutambua thamani yako katika maisha ya kila siku. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

 πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(