ONDOKA 2020 LAKINI UMENIACHIA SOMO KUBWA KATIKA MAISHA YANGU.

Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Hongera kwa kila mmoja wetu kufanikiwa kufikia wakati kama huu ambao tumebakiza masaa machache kuhitimisha mwaka 2020 na kuunza mwaka mpaya 2021. Hakika tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kutokana na jinsi ambavyo mwaka huu ulikuwa na matukio mengi ambayo mengi yalikatisha tamaa kwa mtu mmoja mmoja au jamii kwa ujumla. Ni mwaka ambao ulitawaliwa na matukio ya majonzi katika kila kona ya Dunia. Hata hivyo, pamoja na yote hayo tuna kila sababu ya kusema ee Mungu umekuwa mwemwa kwangu katika kipindi hiki chote cha mwaka 2020 hivyo naomba wema wako uwe nuru ya kuniongoza katika kipindi chote cha mwaka 2021.

Karibu katika Makala maalumu ya siku ya leo ambapo nitakushirikisha namna ambavyo mwaka 2020 umeniachia somo kubwa la kujifunza katika kipindi chote cha maisha yangu. Katika kipindi hiki hasa katika wakati ambao Dunia ilikuwa imetawaliwa na changamoto ya COVID 19 nimejifunza kuwa HOFU ni moja ya hisia ambazo zinatawala maisha ya mwanadamu. Kupitia hisia hii mwanadamu amekuwa akijikadiria chini ya uwezo wake halisi na hivyo yapo mengi ambayo ameshindwa kuyatekeleza kwa kutawaliwa na hisia ya hofu.

Soma: [CHUKUA HATUA] HOFU NI ADUI NAMBA MOJA KATIKA SAFARI YAKO YA MAFANIKIO

Ni katika kipindi cha mwaka 2020 Tanzania imeishangaza Dunia nzima kwa jinsi ambavyo ilikabiliana na ugonjwa wa COVID 19. Mataifa yote yanayozunguka taifa letu yalionesha wazi kuwa Tanzania kama taifa tumeweka mzaa katika kukabiliana na ugonjwa huu hatari. Hata hivyo, pamoja na kusakamwa kila kona lakini Viongozi katika ngazi mbalimbali walisimamia misingi ambayo waliamini ni sahihi katika kupambana na ugonjwa wa COVID. Ni kupitia msimamo huo, taifa limeweza kupambana na ugonjwa wa COVID huku ukiendelea na mfumo wa maisha kama kawaida.

Kama taifa katika kila kona, ushindi dhidi COVID 19 ulipatikana mara baada ya hotuba ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli pale alipolihutubia wananchi wa taifa hili na kuwaaminisha kuwa ugonjwa wa Corona ni ugonjwa sawa yalivyo magonjwa mengine. Hapa nanukuu sehemu ya hotuba ambayo aliitoa tarehe 22 Aprili, 2020: “Tuwaondoe hofu wananchi, sio ugonjwa huu pekee unaosababisha vifo kwa wananchi, na sio kila anayepoteza maisha hivi sasa basi amekufa kwa Corona, COVID-19”.  Pia, katika hotuba yake alikataa kata kata kuweka “lock down” kwa nchi nzima au kulifunga jiji la Dar es Salaam kwa kigezo cha ugonjwa wa Corona kwani ilikuwa wazi kuwa kwa kufanya hivyo inafahamika kabisa kuwa jiji hilo ni kitovu cha uchumi wa taifa hili. Huu ulikuwa ni ushindi wa kwanza katika kupambana na ugonjwa huu hatari kutokana na ukweli kwamba hofu dhidi ya ugonjwa huu ilikuwa inasambaa na kuhatarisha maisha ya watu kuliko ugonjwa wenyewe.

Yapo mengi ya kujifunza kutokana na msimamo huu Tanzania katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona na hapa nitakushirikisha machache tu:-

Somo #1: Ni muhimu kumtanguliza Mungu katika kila jambo. Wakati Tanzania ilipotangaza siku tatu kwa ajili ya kufunga na kuomba Mungu kuliepusha taifa dhidi ya janga la virusi vya Corona pamoja na kutofunga sehemu za ibada, wengi waliona ni mzaa sawa na kuchezesha shilingi kwenye tundu la choo. Taratibu tulianza kushuhudia hata mataifa mengine yakifuata nyayo hizo hizo kwa ajili ya kujinyenyekeza na kuomba ili kuepushwa na janga hilo hatari. Somo la kujifunza: katika kila hali mtangulize Mungu hata katika nyakati ambazo kila mmoja anashangaa mbinu unazotumia.

Somo #2: Ishinde hofu pale ambapo maisha yako yamezungukwa na giza. Kupitia ugonjwa wa virusi vya Corona nimejifunza kuwa yapo mambo mengi ambayo tumeshindwa kutekeleza katika maisha yetu kutokana na kuendekeza hofu. Binafsi nilikuwa miongoni mwa watu ambao walihofia ugonjwa wa Corona kiasi cha kuanza kuogopa kuwa karibu na watu niliozoeana nao awali. Baada ya hotuba ya Mhe. Rais kuhusiana na umuhimu kuondoa hofu na kuwa tayari kuishi na virusi vya Corona kama ilivyo kwa magonjwa mengine nilijikuta katika hali ya kujiamini. Hali hiyo ilitokana na tumaini jipya dhidi ya ugonjwa huu hatari. Taratibu shughuli zote zilirejea kama kawaida huku majirani zetu katika mataifa mengine yakisubiria maiti za watu kuanza kutapakaa mitaani. Somo la kujifunza: kila mara pambana kuishinda hofu katika kila unalofanya kwenye maisha.  

Somo #3: Kama unahitaji kuwa kiongozi shupavu ni lazima ujifunze kusimamia misimamo yako. Kiongozi unatakiwa kuwa na fikra na maono pana zaidi ikilinganishwa na wafuasi wako. Hata katika nyakati ambazo kila mmoja anapinga njia unazotumia unatakiwa kuziba masikio na kusonga mbele. Wengi wataongea mengi kuhusiana na msimamo wako lakini husipokubali kurudi nyuma utafika wakati ambao wapinzani wako watakuelewa na wote mtaongea lugha moja. Hili lipo wazi kwa jinsi ambavyo Mhe. Rais alipingwa na watu wa kila aina ndani na nje ya nchi lakini mwisho wake wote walielewa msimamo wake na wengine wakaanza kuigiza mbinu zake pamoja na kwamba mwanzoni walizipinga. Somo la kujifunza: ikiwa unahitaji kuwa kiongozi shupavu ni lazima ujifunze kusimamia mawazo ambayo unaamini ni sahihi kwa maslahi mapana ya kundi unaloongoza.

Mwisho, ondoka mwaka 2020 lakini umenifundisha kutoendekeza hisia za hofu katika kila ninalofanya kwenye maisha yangu. Mwaka umeisha na naamini kuwa nitakuwa na mwaka mpya wenye mafanikio zaidi ya niliyofanikisha katika kipindi hiki matukio mengi yalitufanya tuone mwaka umekuwa mchungu. Karibu mwaka 2021 ili kwa pamoja tuendelee kuwa kama familia moja ya FIKRA ZA KITAJIRI. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

Nakutakia kila la kheri katika kipindi chote cha mwaka 2021.

 BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com 

KARIBU MWEZI DESEMBA, 2020: MWEZI WA USHUHUDA DHIDI YA NAFSI YANGU

NENO LA LEO (DESEMBA 1, 2020): KARIBU MWEZI DESEMBA, 2020: MWEZI WA USHUHUDA DHIDI YA NAFSI YANGU.

✍🏾 Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Hongera kwa asubuhi hii ambapo tunauanza mwezi wa mwisho katika mwaka 2020. Ni mwezi ambao tunahitimisha mwaka 2020 na kutazamia kuanza mwaka mpya 2021. Mambo ni mengi katika kipindi hiki kilichobakia hivyo una kila sababu ya kuwa macho muda wote. Basi tuianze siku kwa kusema “hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani”.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.  

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza jinsi ya kuutumia vyema mwezi Desemba, 2020. Wote tumebakiza siku 30 kwa ajili ya kumaliza mwaka 2020 na kuanza mwaka 2021. Siku hizi kwa hesabu siyo nyingi lakini kwa kuziishi zimejaa matukio mengi. Matukio hayo endapo hautakuwa makini yanaweza kukuharibia misingi ambayo umeiishi toka kipindi cha mwanzo wa mwaka. Hiki ni kipindi ambacho kinaambatana na mambo mengi yanayohusisha matumizi makubwa ya pesa sambamba na utapeli wa kila aina.

✍🏾 Tunapoendelea kumaliza siku zilizobakia, tunatakiwa kujiuliza tumefanikiwa kwa kiwango gani katika utekelezaji wa malengo tuliyojiwekea. Mwezi Desemba, ni mwezi wa mavuno, matumizi na mwezi wa kujipanga upya kwa ajili ya mwaka unaofuatia. Yamkini tulijiwekea malengo makubwa kiasi ambacho hadi sasa hatujafanikiwa kutekeleza hata robo yake, hiki ni kipindi cha kutafakari tulikwama wapi na tunatakiwa kurekebisha wapi ili makosa hayo yasijirudie katika kipindi cha mwaka unaofuata.

✍🏾 Mwaka 2020 kwangu mimi umekuwa ni somo kwa mambo mengi. Yapo mengi ambayo nimefanikisha kadri ya nilivyokuwa nimeweka lengo lakini yapo mengi pia ambayo nimetekeleza chini ya malengo. Moja ya mafanikio ambayo najivunia hadi sasa ni kufanikiwa kuandika kila siku asubuhi kupitia neno la tafakari ya siku. Nilianzisha kundi hili nikiwa na idadi ya wanafamilia wasiozidi 30 na lengo langu lilikuwa kuwafikia wanafamilia zaidi ya 100 katika kipindi cha mwaka mzima. Hili limefanikiwa kwa asilimia zote. 

✍🏾 Ndani ya kipindi hiki wapo wanafamilia ambao nimekuwa nao toka kundi hili lianzishwe na wapo ambao wamejiunga siku za karibuni. Katika kipindi ambacho tumefahamiana naamini kuna mengi ambayo umejifunza kutoka kwangu. Kwa moyo wa dhati naomba kusikia ushuhuda wako wa jinsi gani ambavyo nimegusa maisha yako. Katika ushuhuda huo naomba unieleze mafanikio ambayo umeyapata kutokana na uwepo wako ndani ya kundi hili. 

Unaweza kujaza ushuhuda wako kupitia kiunganisho hiki [FOMU YA KUTOA MREJESHO WA JINSI AMBAVYO UMEFAIDIKA NA MTANDAO WA FIKRA ZA KITAJIRI] ili ushuhuda wako uendelee kuwa siri kati yako na Mimi.

✍🏾 Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa tupo mwishoni mwa mwaka 2020 japo siku zilizobakia zinabeba mambo mengi ambayo tunatakiwa kuwa macho muda wote. Hiki ni kipindi cha kutafakari mafanikio ambayo tumepata pamoja na sehemu ambazo tumeanguka. Iwe mafanikio au anguko, vyote ni kwa ajili ya kuboresha uzoefu wetu wa maisha hapa Dunuani. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

JINSI MFUMO WA ELIMU UNAVYOTUJAZA HOFU KULIKO MAFANIKIO

NENO LA LEO (NOVEMBA 12, 2020): JINSI MFUMO WA SASA WA ELIMU UNAVYOTUJAZA HOFU KULIKO MAFANIKIO

πŸ‘‰πŸΎHabari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine ambayo naamini tumeamka salama na zaidi ya yote tukiwa na hamasa ya kutosha kwa ajili ya kuendelea pale tulipoishia jana. Kutokana na hali kama hiyo hatuna budi kila mmoja kwa nafasi yake kusema kusema "hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana ninawajibika kumshukuru na kuitumia vyema siku hii ili nipate kuliishi kusudi kubwa la maisha yangu"

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.   

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutaona jinsi mfumo wa uliopo umekuwa chanzo cha kutujaza hofu ikilinganishwa na mafanikio tarajiwa. Wote tunakubaliana kuwa tumelelewa katika jamii ambayo inaamini wale wanaoganya vyema darasani ndiyo watafanikiwa kimaisha. Hali imetufanya katika ukuaji wetu kuamini kuwa wale wanaofanya vibaya darasani hawawezi kufanikisha maisha! Mbaya zaidi ni pale ambao wale wanaofanya vibaya wanapachikwa majina ya kila aina ambayo yanafifisha uwezo wa kufanikiwa kimaisha.

✍🏾 Je kufeli mitihani ni uthibitisho tosha kuwa mhusika atafeli maisha?. Siyo kweli kwamba ukifeli mitihani umefeli maisha. Mifano ipo mingi kwa watu ambao shuleni walionekana hawajui lolote lakini katika maisha ni mifano bora ya kuigwa. Mfano Bill Gates aliacha chuo na kujitosa kwenye sekta ya ujasiliamali. Pia, katika jamii tunayoishi wapo watu wengi ambao walishindwa kumudu maisha ya shule lakini kwa sasa wafanyabiashara wakubwa. Pia, wapo wanamochezo wengi ambao darasani hawakufanya vyema lakini kwa sasa wanaishi kupitia vipaji vyao.

✍🏾 Hali hii inatoa picha kuwa mfumo wa elimu wa sasa unaandaa wanafunzi kuwa waajiriwa badala ya kuandaliwa kwenye pande zote za ajira na ujasiliamali. Tafsiri yake ni kwamba unapofeli shule siyo kwamba umefeli maisha bali shule inakuwa imeshindwa kutambua kipaji chako. Baada ya kufeli mitihani unatakiwa kujiamini kuwa upande siyo sehemu yako na badala yake kuna upande ambao unakusubiria.

✍🏾 Asilimia kubwa ya watu ambao wamefanikiwa kufaulu mitihani na kuingia kwenye mfumo rasmi wa ajira wengi wao wanaishi kwa msongo wa mawazo. Hali hii inatokana na ukweli kwamba kiwango cha mshahara wanacholipwa pengine hakiendani na kiwango cha elimu waliyonayo au mshahara hautoshelezi mahitaji yao ya msingi. Mara nyingi katika kusoma wengi wanakuwa na mategemeo makubwa ya kufanikiwa kupitia elimu ikilinganishwa na uhalisia wa maisha. Na hapa ndipo hofu ya maisha inakoanzia.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limetufunulia jinsi ambayo mfumo wa elimu ulivyotuja hofu ikilinganishwa mafanikio tarajiwa. Kama mzazi una nafasi ya kutambua vipaji vya watoto wako zaidi ya kile wanachoonyesha darasani. Kauli hii ya mwanangu nenda shule ukasome kwa bidii ili uwe daktari bingwa imepitwa na wakati. Mpe mwanao kauli ambazo zitamfanya kuwa mdadisi na mtumiaji wa kalama alizojaliwa katika maisha ya kila siku.

 πŸ‘πŸΎNakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

πŸ—£πŸ—£ Mwalimu Augustine Mathias 

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

[UFUNUO] FAHAMU KUWA PESA HAINA THAMANI

NENO LA LEO (NOVEMBA 11, 2020): [UFUNUO] FAHAMU KUWA PESA HAINA THAMANI

πŸ‘‰πŸΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Hongera kwa siku nyingine mpya katika uhai wetu hapa Duniani. Ni siku ambayo tuna wajibu wa kuendelea kuwa bora ili maisha yetu yawe ya thamani kwa manufaa ya nafsi zetu na jamii inayotuzunguka. Basi kila mmoja wetu aseme "hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii ili nipate yaliyo bora katika maisha."

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.   

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza ni kwa namna gani pesa haina thamani. Katika makundi ya kijamii kwa sasa ni vigumu kueleweka pale unaposema pesa haina thamani. Hali hii inatokana na ukweli kwamba toka pesa ilipogunduliwa imeendelea kutumika kama nyenzo ya kubadilishana kati ya huduma/bidhaa na kipimo cha pesa. Pesa imekuwa msingi wa watu katika jamii kufanikisha mahitaji yao.

✍🏾 Hata hivyo, ukweli unabakia kuwa "thamani ya pesa ni pale inapotumika kufanikisha upatikanaji wa vitu vyenye thamani". Vile vile, tunaweza kusema kwamba uthamani wa pesa ni pale pesa husika inapokuwa kwenye mzunguko. Tafsiri yake ni kwamba ikiwa pesa haitumiki kupata vitu vya thamani pesa hiyo haina thamani. Mfano, unaweza kupata milioni leo hii na katika hali ya kawaida ukaiona ni pesa nyingi, cha kushangaza milioni hiyo ukiiweka kwenye matumizi ghafla utajikuta inaisha ndani ya dakika chache tu.  

✍🏾 Ikiwa pesa haitumiki kununua vitu vyenye thamani au kuwekezwa sehemu ambapo thamani yake inaongezeka moja kwa moja pesa hiyo inayeyuka kana kwamba haikuwahi kuwepo mikononi mwako. Jiulize kiwango cha juu cha pesa ambacho umewahi kupata na jinsi ulivyotumia pesa hiyo. Ikiwa hauwezi kuiona pesa hiyo katika wakati wa sasa moja kwa moja ni dhahiri kuwa pesa hiyo uliitumia kwenye vitu ambavyo havina thamani.

✍🏾 Hapa ndipo wanafanya makosa kwa kuweka mipango ya kiwango cha pesa ambacho wanahitaji kupata badala ya kuweka mipango ya vitu vya thamani ambavyo wanahitaji kumiliki maishani mwao. Unatakiwa kuainisha mahitaji yako ya msingi katika maisha na kupitia mahitaji hayo ndipo unapata kiwango cha pesa ambacho unahitaji. 

✍🏾 Mwisho, neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa pesa haina thamani na badala yake thamani ya pesa ipo kwenye vitu unavyonunua kupitia pesa husika. Pia tumeona kuwa lengo kubwa katika safari ya pesa linatakiwa liwe kwenye mahitaji ya msingi ambayo unatamani kumiliki kama vile ardhi, viwanda, nyumba, biashara, umiliki hisa au uwekezaji kwenye mifuko ya uwekezaji wa pamoja na uwekezaji kwenye hati fungani za Serikali. Kumbuka, mbegu ikidondoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

FAHAMU SHERIA MBILI AMBAZO ZIMESHIKIRIA MAFANIKIO YAKO.

NENO LA LEO (NOVEMBA 8, 2020): FAHAMU SHERIA MBILI AMBAZO ZIMESHIKIRIA MAFANIKIO YAKO.

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine ambapo tunazawadiwa masaa 24 ambayo hatuna budi kuyatumia kutenda yaliyo mema ili maisha yawe na thamani. Ni katika asubuhi hii nakukumbusha kuwa maisha yako yanakuwa na thamani pale ambapo yanatumika kwa faida ya nafsi yako na jamii inayokuzunguka. Basi kila mmoja wetu aianze siku kwa “kusema hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani”.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.   

Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza kuhusiana sheria mbili ambazo zimeshikilia mafanikio yako kwenye kila sekta ya maisha yako. Kila siku tunawajibika kutii sheria mbalimbali ziwe za asili au sheria zilizowekwa na wanadamu. Sheria hizi ndizo zinaongoza maisha yetu na zinatuwezesha kuishi katika makundi ya kijamii. Katika neno la tafakari ya leo nitakufunulia sheria mbili ambazo pengine hukuwahi kuzisikia yamkini zimekuwa sehemu ya maisha yako ya kila siku. Karibu tujifunze:-

Sheria #1: Kanuni ya dhahabu (the Golden Rule). Sheria ya dhahabu ni moja ya sheria ambayo ina mchango kwenye safari ya mafanikio yako. Ni miongoni mwa sheria zinazopatikana katika dini na tamaduni nyingi. Sheria hii inasema “kila mmoja awatendee wenzake kama ambavyo angetamani wamtendee”. Misingi ya sheria hii ni kutoka katika mafundisho ya Yesu kwa wanafunzi wake kama ilivyonukuliwa hapa: “Basi yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii” (Mathayo 7:12, Luka 6:31 na Walawi 19:18).

Tafsiri yake katika safari ya fedha ni kwamba ikiwa unahitaji kufanikiwa katika maisha, unatakiwa kutenda mema kwa watu wengine kwa kuwa hakuna namna utaweza kufanikiwa kimaisha bila ya uwepo wa watu. Wafanyakazi wenzako ni watu, mwajiri wako ni mtu, wateja wa bidhaa zako ni watu na jamii inayokuzunguka kwa ujumla ni watu. Pia, sheria hii inaweza kutafsiriwa zaidi kuwa: katika ulimwengu wa biashara unatakiwa kutoa thamani kwa unaofanya nao biashara na thamani unayopokea. Husimuuzie mtu bidhaa au huduma ambayo wewe mwenyewe husingeweza kununua kama ungekuwa upande wa mteja.

Sheria #2: Sheria ya Platini (Platinum Rule). Madini ya Platini yana thamani ikilinganishwa na madini ya dhahabu. Hivyo, sheria ya Platini inathamani zaidi ikilinganishwa na sheria ya dhahabu. Sheria ya Platini inasema: “watendee wengine kadri ambavyo wanapenda kutendewa na siyo kadri unavyohitaji kutendewa”. Hii ni sheria nyingine muhimu katika kujumuika na watu wanaokuzunguka, kadri unavyowatendea watu kulingana na mapenzi yao ni rahisi kuaminika kwao. Ili ujenge uaminifu kwa wateja ni lazima uhakikishe unatimiza mahitaji yao kwenye bidhaa/huduma zako. Na kadri unavyotimiza mahitaji ya Wafanyakazi wako ndivyo wataendelea kuwa waaminifu kwako. Vitu vidogo ambavyo unawatendea wateja kulingana na mapenzi yao vina nafasi kubwa ya kukupatia wateja waaminifu kwenye bidhaa/huduma zako.

Mwisho, neno la tafakari ya leo tumejifunza sheria ambazo ni sheria ya Dhahabu na sheria ya Platini. Tumeona jinsi ambavyo tunaweza kutumia sheria hii katika maisha yetu ya kila siku katika kuelekea kwenye mafanikio tunayotamani. Tumia sheria hizi kuboresha mahusiano yako na watu katika jamii unayoishi kwa kuwa hakuna mafanikio bila watu. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

FAHAMU KANUNI YA 20:40:60 ILI UITUMIE KUEPUKA MAJUTO YA BAADAE KWENYE MAISHA

NENO LA LEO (NOVEMBA 4, 2020): FAHAMU KANUNI YA 20:40:60 ILI UITUMIE KUEPUKA MAJUTO YA BAADAE KWENYE MAISHA

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine ambapo tunazawadiwa masaa 24 kwa ajili ya kuendeleza bidii ya kuongeza thamani ya maisha yetu. Ni katika asubuhi tunakumbushwa kuwa maisha yanakuwa na thamani pale ambapo yanaleta mabadiliko kwa mhusika na jamii inayomzunguka au viumbe wengine kwa ujumla. Basi kila mmoja wetu aianze siku kwa kusema hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.  

Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza kuhusiana na kanuni ya 20:40:60 na jinsi tunavyoweza kuitumia kuepuka majuto au manung’uniko ya baada katika maisha yetu. Zipo sheria na kanuni muhimu ambazo katika safari yako ya kifedha unatakiwa kuzizingatia. Moja ya kanuni ambazo unatakiwa kuzitumia katika kuishi maisha yenye thamani ni kanuni ya 20:40:60 ambayo ilitolewa na mwanafalsafa Shirley MacLaine.

Kanuni ya 20:40:60 inasema“ukiwa katika umri wa miaka 20 (twenties) unajali sana mawazo na maoni ya watu kiasi ambacho unaruhusu yaamue au kuathiri mambo mengi ambayo unafanya; ukiwa katika umri wa miaka 40  (forties) unakuwa tayari umekomaa na wakati huo unajikuta unafanya kile ambacho unatakiwa kufanya bila kujali maoni au mawazo ya watu; na ukiwa katika umri wa miaka 60 (sixties) unakuja kugundua kuwa watu hawakuwa na muda na wewe kiasi hicho au kujali mambo yako kama ambavyo ulidhania hapo awali”.

Kutambua na kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni hii itakusaidia kuishi kimkakati mapema maishani mwako bila kufikiria watu wanahisi au kufikiria nini kuhusu yale unayofanya. Kanuni hii itakusaidia kuepuka kupoteza pesa na muda kwa ajili ya kuridhisha watu au kutafuta umaarufu ambao hata hivyo katika maisha yako ya baadae utagundua kuwa hakukuwa na tija katika yote hayo. Kubwa unatakia kutambua ukiwa katika umri mdogo kabisa kuwa hakuna mtu mwenye kukufikiria au kujali mambo yako hivyo unatakiwa kuendesha maisha yako kwa kuzingatia misingi na kanuni ambazo umejiwekea katika kufikia mafanikio unayotamani.

Mwisho, neno la tafakari ya leo tumejifunza kuhusu kanuni ya 20:40:60 ambavyo inaweza kutumika kuepusha majuto katika maisha yetu. Chochote unachofanya tekeleza kwa ajili ya ukamilifu wa malengo yako na siyo kwa ajili ya kuwaridhisha watu au kutafuta umaarufu kwa watu wanaokuzunguka. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

TUNAPOELEKEA MWISHO WA MWAKA 2020 JE UMESOMA VITABU VINGAPI?

NENO LA LEO (NOVEMBA 02, 2020): TUNAPOELEKEA MWISHO WA MWAKA 2020 JE UMESOMA VITABU VINGAPI?

Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya kati ya siku 60 zilizobakia kuumaliza mwaka 2020. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuendelea na majukumu yako ya leo. Basi tuianze siku kwa kusema “hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani”.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.  

Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza kwa pamoja tutafakari juu ya umuhimu wa kusoma vitabu. Nilianza kazi ya kuhamasisha jamii kuhusu usomaji vitabu kwa ajili ya kujiongezea maarifa mbalimbali tangu mwaka 2016. Katika kipindi hiki cha miaka minne kwenye usomaji wa vitabu nimegundua kuwa hatuwezi kujijua sisi ni akina nani na tumeumbwa kwa ajili ya kufanya nini hapa duniani ikiwa hatuna utamaduni wa kusoma vitabu.

Kila mmoja wetu hapa duniani ameumbwa kwa ajili ya kukamilisha kusudi maalumu japo kusudi hilo halipo wazi kwenye maisha yetu ya kila siku. Kupitia usomaji wa vitabu tunaweza kujitambua sisi ni akina nani na tumeumbwa kwa ajili ya kukamilisha kusudi lipi hapa Duniani. Katika kuelezea neno la tafakari ya leo ningependa ninukuu maandiko matakatifu kutoka kwenye Biblia.

Kitabu cha Mithali 4: 13 ambayo yanasema “Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; mshike maana yeye ni uzima wako.”  Tafsiri yetu walio wengi tunadhania kuwa elimu inayoongelewa hapa ni elimu ya darasani na baada ya kumaliza elimu ya darasani tunakuwa tumehitimisha safari ya kujifunza. Pia, Mithali 1:29 nanukuu kwa kuwa walichukia maarifa, wala hawakuchagua kumcha Bwana”. Tafsiri yake ikiwa ni kwamba tunapokosa muda wa kujifunza maarifa mapya kupitia usomaji wa vitabu au semina mbalimbali moja kwa moja ni kwamba hatuwezi kumcha Bwana katika kweli na haki kwa kuwa hatuna maarifa ya kutosha kuhusu Mungu na maisha yetu kwa ujumla wake.

Katika kitabu cha Injili ya Yohana, Yohana 8: 32 “tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.”  Ukweli ni kwamba tumeshindwa kuwa huru kiroho, kimahusiano ya ndoa na familia, kwenye malezi ya Watoto, kiuchumi na kijamii kwa kuwa tumeshindwa kuijua kweli kupitia usomaji wa vitabu.

Katika kitabu cha Hosea 4:6 nanukuu: “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.Kila siku tunaangamia kupitia ndimi zetu, tunaangamia kupitia tabia zetu, tunaangamia kupitia uzembe wetu, tunaangamia kupitia upofu wa kutokuona fursa, na tunaangamia kupitia kutokujitambua sisi nani. Majibu ya namna ya kuepukana na maangamizo hayo yanapatikana kupitia usomaji vitabu.

Mwisho, neno la tafakari ya leo ni sehemu ya neno ambalo nililitoa jana katika hafla ya uzinduzi wa vitabu vitabu vitatu ambapo nilialikwa kama Mgeni rasmi wa hafla hiyo. Kubwa ambalo ningependa ujifunze katika neno la tafakari ya leo ni kujiuliza kuwa tunapoelekea mwishoni mwa mwaka 2020 Je umesoma vitabu vingapi? Ikiwa Dunia inabadilika na vyote vilivyomo ndani mwake vinabadilika kila mara, kitu pekee ambacho hakibadiliki ni kazi ya kalamu. Kazi hii inao uwezo wa kudumu vizazi na vizazi kuliko kazi nyinginezo. Hivyo, wajibu ulionao ni kuhakikisha unanufaika na kazi kalamu kutoka kwa waandishi ambao wametoa maisha yao kwa ajili ya kuielimisha jamii. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

HIZI NDIZO NJIA 3 ZA UHAKIKA WA KUPUNGUZA SIKU ZA KUISHI HAPA DUNIANI.

NENO LA LEO (NOVEMBA 01, 2020): HIZI NDIZO NJIA 3 ZA UHAKIKA WA KUPUNGUZA SIKU ZA KUISHI HAPA DUNIANI.

Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya kati ya siku 61 zilizobakia kuumaliza mwaka 2020. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutulinda na kutuweka salama kiasi ambacho tumefikia muda huu tukiwa na afya bora. Basi tuianze siku kwa kusema “hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani”.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache. 

Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza miongoni mwa tabia ambazo zinapunguza siku za mwanadamu kuishi hapa Duniani. Wote tunafahamu kuwa Dunia hii ni mapito kwa viumbe vyote vyenye uhai na kila kiumbe kina siku za kuishi ambazo kimeandikiwa. Tukisoma katika maandiko matakatifu tutaona kuwa wanadamu wa kale waliweza kuishi miaka mingi ikilinganishwa na binadamu wa sasa. Yapo mambo mengi ambayo kila kukicha yanapunguza siku za uhai wa mwanadamu na miongoni mwa sababu hizo zipo zinazosababishwa na mwanadamu mwenyewe na nyingine ni kutokana na mabadiliko ya asili ambayo hata hivyo undani wake ni mwandamu mwenyewe. Leo tutajifunza sababu tatu ambazo zinapunguza siku za siku kuishi kwa mwanadamu mmoja mmoja. Karibu tupitie sababu moja baada ya nyingine:-

Njia #1: Vuta sigara kila siku kwa kadri uwezavyo – Utapunguza miaka 10 kwenye siku za uhai wako hapa Duniani. Kila mtu anafahamu athari za uvutaji wa sigara ikiwa ni pamoja na hata wale ambao ni wavutaji athari za uvutaji kwa afya yao. Athari hizi zinaanzia kwenye kusababisha matatizo ya afya kwenye mfumo wa upumuaji hadi kupelekea kwenye magoja mengi kama kansa ya koo. Hata katika kipindi hiki ambacho Dunia inaendelea kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19, Shirika la Afya Duniani lilitoa angalizo kwa wavutaji wa sigara kuwa hatarini kudhulika na athari ya COVID 19 ikilinganishwa na wale ambao hawavuti. Pamoja na athari hizo kufahamika wazi bado watu wanaendelea kuvuta sigara wakijifariji kuwa hata wasipovuta watakufa tu kwa kuwa hakuna kiumbe ambaye ameandikiwa kuishi milele. Ni kweli kufa utakufa tu lakini kwa nini uwe sehemu ya kupunguza siku zako za kuishi hapa Duniani?

Njia #2: Kunywa pombe tena pombe kali kila siku – Una uhakika wa kupunguza miaka 30 kwenye siku ambazo umeandikiwa kuishi. Unywaji pombe wa kupindukia unaambatana na hatari nyingi ambazo zote kwa pamoja zinapelekea kuhatarisha afya ya mhusika. Unywaji wa pombe kali kila siku unaambatana na athari za afya kama vile kupungua uzito, kupungua kwa maji mwilini (dehyadration), magonjwa ya figo, moyo na ini, magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu (blood pressure). Hivyo, ikiwa unaendekeza unywaji wa pombe kali kwa kiwango kikubwa utambue kuwa unapunguza siku za kuishi hapa Duniani.

Njia #3: Penda mtu ambaye hakupendi – Utakufa kila siku. Mahusiano ya mapenzi au ndoa kwa ujumla ni miongoni mwa sababu kubwa ambazo zinasababisha vifo kwa watu wengi. Kupitia mahusiano ya ndoa, wapenzi wanaweza kuongeza au kupunguza siku za kuishi. Mwandishi John M. Gottman katika kitabu cha “The Seven Principles for Making Marriage Work” anatushirikisha kuwa tafiti zinaonyesha kuwa wanandoa ambao wameishi pamoja kwa muda wa maisha yao wanaishi zaidi umri wa kati ya miaka minne hadi nane ikilinganishwa na wale ambao wametalikiana. Hii ni kutokana na ukweli kwamba ndoa zenye msongo wa mawazo na kila aina ya misukosuko ni chanzo cha miili ya wanandoa kuwa na upungufu wa kinga za mwili dhidi ya maradhi mbalimbali.

Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa tunaweza kupunguza siku za kuishi kwa kuendekeza uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe kali kila siku na kupemba mwenza ambaye hakupendi. Wanadamu hatujaumbwa kwa ajili ya kufupisha siku za uhai wetu hila kutokana na kuendekeza tabia hatarishi kila siku tunapunguza siku za uhai wetu hapa Duniani. Amua sasa kuanza kuongeza siku za uhai wako kupitia kula/kunywa vyakula/vinywaji vinavyohitajika kujenga mwili, kufanya mazoezi ya viungo na kuchagua mwenza ambaye hatakuwa sehemu ya kukusababishia msongo wa mawazo. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

UKANDA WA FARAJA: KANDA TATU AMBAZO UNATAKIWA KUPITIA BAADA YA KUUKIMBIA UKANDA WA FARAJA.

NENO LA LEO (OKTOBA 31, 2020): UKANDA WA FARAJA: KANDA TATU AMBAZO UNATAKIWA KUPITIA BAADA YA KUUKIMBIA UKANDA WA FARAJA.

Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi mpya ambapo tunaendelea kuwa kwenye changamoto ya kufungwa kwa mitandao ya kijamii. Naamini kila mmoja wetu ameamka salama na yupo tayari kuendelea na majukumu yake ya siku ya leo. Basi tuianze siku kwa kusema “hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani”.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache. 

Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza kuhusu ukanda wa faraja (comfort zone) na kanda tatu ambazo unatakiwa kuzipitia baada ya kuukimbia ukanda wa faraja. Kwa asili tumeumbwa katika hali ambayo miili yetu haitaki kuumia hivyo inaridhika inapokuwa kwenye mazingira salama au tulivu (comfort). Mwili wa binadamu unaogopa mabadiliko kiasi kwamba inapotokea mabadiliko ya namna yoyote ile mwili unakuwa katika hali ya mshutuko. Ni kutokana na sababu hiyo, watu wengi wanaridhika kuwa kwenye mazingira ambayo yamezoeleka (comfort zone) kuliko kujaribu mazingira mapya.

Athari ya kuridhika na mazingira yaliyozoeleka ni kukosa ubunifu ni uthubutu wa mawazo mapya katika ukuaji wa mhusika kwenye kipindi cha uhai wake. Watu wanaofanikiwa kimaisha ni lazima wawe tayari kuukimbia ukanda wa faraja kwa ukanda huo unawafanya wengi kubweteka na hali inayowazunguka. Katika mzunguko wa ukuaji mhusika ni lazima apitie kwenye ukanda wa faraja (comfort zone), ukanda wa hofu (fear zone), ukanda wa kujifunza (learning zone) na ukanda wa ukuaji (growth zone). Karibu tuangalie sifa za kila ukanda.

Pia Soma: JE NI MARA NGAPI UNAJILAZIMISHA KUTOKA KWENYE UKANDA WA FARAJA?

Ukanda wa hofu – Huu ni ukanda unaofuatia baada ya ukanda wa faraja. Katika ukanda wa faraja mhusika anaridhika na kila hali inayomzunguka hila katika ukanda huu mhusika anakuwa hajiamini kwenye kila hatua anayokusudia kuchukua katika maisha yake. Katika ukanda huu mhusika anajiona mnyonge dhidi ya mawazo ya wengine (mawazo ya wengine ni bora kuliko yake); kila mara anatafuta visingizio vya kujifariji kulingana na hali yake; na hofu inamzuia kuchukua hatua zinazolenga kutekeleza kwa vitendo mawazo aliyonayo katika kuboresha maisha yake.

Ukanda wa kujifunza – Huu ni ukanda muhimu kwa mwanadamu yeyote anayelenga kuishi maisha ya thamani. Katika ukanda huu hakuna changamoto ambayo inamzuia mhusika kusonga mbele kwa kuwa katika kila changamoto mhusika anatafuta suluhisho. Pia, katika ukanda huu mhusika anajifunza mbinu na maarifa mapya yanayomuwezesha kuongeza uzoefu dhidi ya mazingira yanayomzunguka. Hata hivyo, kwenye ukanda huu mhusika anaweza kujikuta ameingia kwenye ukanda mpya wa faraja hali ambayo itapelekea hasiweze kukua zaidi katika yale anayofanya.

Ukanda wa ukuaji – Huu ni ukanda ambao mhusika anaishi kusudi la maisha yake kwa ukamilifu. Kwa kuliishi kusudi la maisha yake mhusika anaishi ndoto alizonazo kuhusu maisha kwa kuhakikisha kila mara anaweka malengo mapya mara baada ya kutekeleza malengo ya awali. Ilifanikiwe katika ukanda huu ni lazima ujifunze kuishi kwa hali ya uchanya (positive oriented) kwenye kila hali iliyopo mbele yako. Makwazo, madhaifu na changamoto siyo sababu ya kukuzuia kusonga mbele.

Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza kanda nne za ukuaji katika kuelekea kwenye mafanikio unayotamani. Watu wengi huwa wanajikuta wameishia kwenye ukanda wa faraja hali inayopelekea wasiweze kukua zaidi au kufanikisha ndoto walizonazo. Ikiwa unahitaji mafanikio ni lazima kila mara ukimbie ukanda wa faraja katika kila hatua unayopiga. Jiulize je hatua uliyonayo sasa siyo sehemu ya ukanda wa faraja? Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

KUMBE NDOA ULIYOIZOEA INAWEZA VUNJIKA NA MAISHA YAKAENDELEA.

NENO LA LEO (OKTOBA 30, 2020): KUMBE NDOA ULIYOIZOEA INAWEZA VUNJIKA NA MAISHA YAKAENDELEA.

πŸ‘‰πŸΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni nyingine ambayo tumeamka salama na tukiwa na nguvu na hamasa ya kutosha kuendeleza pale ulipoishia jana. Ikiwa ni siku ya pili tangu tumetimiza haki yetu ya msingi ya kuchagua viongozi wa kutuvusha salama katika kipindi cha miaka mitano ijayo tunaendelea kusikilizia maumivu ya kuzimwa kwa mawasiliano ya mitandao ya kijamii. Basi tuianze siku kwa kusema “hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani”.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza juu ya somo muhimu ambalo limetokana na hatua iliyochukuliwa na Serikali ya kuzima mitandao ya kijamii. Leo hii ni siku ya tatu tangu mitandao hii izimwe na maisha mengine yameendelea. Ukweli ni kwamba kizazi cha sasa ambacho kinamiliki simu janja kimeweka ushirika au kifunga ndoa na simu hizo. Kizazi hiki kinatumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii kuliko inavyokuwa kwenye majukumu mengine ya siku. 

✍🏾 Kuzimwa kwa mitandao hii ya kijamii ni ufunuo kwa wale waliofunga ndoa na simu janja kuwa wanaweza kuishi bila kufuatilia yanayojiri kwenye mitandao ya kijamii. Natambua kuwa zoezi la kuzima mitandao ya kijamii kuna ambao litakuwa limewaathiri kwa asilimia kubwa hasa kwa wale wanaotumia mitandao hii kama jukwaa la kutangaza biashara zao.

✍🏾 Ukweli unabakia kuwa asilimia kubwa ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanapoteza muda mwingi kufuatilia mambo yasiyo na tija. Katika kipindi hiki ambacho mitandao ya kijamii imezimwa unaweza kuamua kuanza maisha mapya ya kutokuendeshwa kwa rimoti na simu janja yako. 

✍🏾 Yanayojiri kwenye mitandao ya Facebook, WhatsApp au Instagram hayana tija sana ikilinganishwa na majukumu yako ya msingi ambayo umekuwa ukipiga dana dana (trade off) dhidi ya mitandao ya kijamii. Kipindi hiki ni muhimu kwako kupima ufanisi wa kutekeleza majukumu yako ya msingi ikilinganishwa na kipindi ambacho mitandao ya kijamii ilikuwa inaingilia utendaji kazi wako.

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza maisha yanaweza kuendelea hata bila ya uwepo wa mitandao ya kijamii. Mitandao ya kijamii imekuwa ni chanzo cha kupoteza muda na matokeo yake ni ufanisi mdogo katika kazi. Pia, mitandao hii imekuwa chanzo cha kuvunja mahusiano ya watu wengi, hivyo kuzimwa kwake kwa siku hizi ni fursa ya kutuonesha kuwa tunaweza kuiendesha mitandao hii badala ya mitandao hiyo kutuendesha. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com