FAHAMU KANUNI YA 20:40:60 ILI UITUMIE KUEPUKA MAJUTO YA BAADAE KWENYE MAISHA

NENO LA LEO (NOVEMBA 4, 2020): FAHAMU KANUNI YA 20:40:60 ILI UITUMIE KUEPUKA MAJUTO YA BAADAE KWENYE MAISHA

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine ambapo tunazawadiwa masaa 24 kwa ajili ya kuendeleza bidii ya kuongeza thamani ya maisha yetu. Ni katika asubuhi tunakumbushwa kuwa maisha yanakuwa na thamani pale ambapo yanaleta mabadiliko kwa mhusika na jamii inayomzunguka au viumbe wengine kwa ujumla. Basi kila mmoja wetu aianze siku kwa kusema hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.  

Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza kuhusiana na kanuni ya 20:40:60 na jinsi tunavyoweza kuitumia kuepuka majuto au manung’uniko ya baada katika maisha yetu. Zipo sheria na kanuni muhimu ambazo katika safari yako ya kifedha unatakiwa kuzizingatia. Moja ya kanuni ambazo unatakiwa kuzitumia katika kuishi maisha yenye thamani ni kanuni ya 20:40:60 ambayo ilitolewa na mwanafalsafa Shirley MacLaine.

Kanuni ya 20:40:60 inasema“ukiwa katika umri wa miaka 20 (twenties) unajali sana mawazo na maoni ya watu kiasi ambacho unaruhusu yaamue au kuathiri mambo mengi ambayo unafanya; ukiwa katika umri wa miaka 40  (forties) unakuwa tayari umekomaa na wakati huo unajikuta unafanya kile ambacho unatakiwa kufanya bila kujali maoni au mawazo ya watu; na ukiwa katika umri wa miaka 60 (sixties) unakuja kugundua kuwa watu hawakuwa na muda na wewe kiasi hicho au kujali mambo yako kama ambavyo ulidhania hapo awali”.

Kutambua na kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni hii itakusaidia kuishi kimkakati mapema maishani mwako bila kufikiria watu wanahisi au kufikiria nini kuhusu yale unayofanya. Kanuni hii itakusaidia kuepuka kupoteza pesa na muda kwa ajili ya kuridhisha watu au kutafuta umaarufu ambao hata hivyo katika maisha yako ya baadae utagundua kuwa hakukuwa na tija katika yote hayo. Kubwa unatakia kutambua ukiwa katika umri mdogo kabisa kuwa hakuna mtu mwenye kukufikiria au kujali mambo yako hivyo unatakiwa kuendesha maisha yako kwa kuzingatia misingi na kanuni ambazo umejiwekea katika kufikia mafanikio unayotamani.

Mwisho, neno la tafakari ya leo tumejifunza kuhusu kanuni ya 20:40:60 ambavyo inaweza kutumika kuepusha majuto katika maisha yetu. Chochote unachofanya tekeleza kwa ajili ya ukamilifu wa malengo yako na siyo kwa ajili ya kuwaridhisha watu au kutafuta umaarufu kwa watu wanaokuzunguka. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(