NENO LA LEO (DESEMBA 1, 2020): KARIBU MWEZI DESEMBA, 2020: MWEZI WA USHUHUDA DHIDI YA NAFSI YANGU.
✍πΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Hongera kwa asubuhi hii ambapo tunauanza mwezi wa mwisho katika mwaka 2020. Ni mwezi ambao tunahitimisha mwaka 2020 na kutazamia kuanza mwaka mpya 2021. Mambo ni mengi katika kipindi hiki kilichobakia hivyo una kila sababu ya kuwa macho muda wote. Basi tuianze siku kwa kusema “hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani”.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍πΎ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza jinsi ya kuutumia vyema mwezi Desemba, 2020. Wote tumebakiza siku 30 kwa ajili ya kumaliza mwaka 2020 na kuanza mwaka 2021. Siku hizi kwa hesabu siyo nyingi lakini kwa kuziishi zimejaa matukio mengi. Matukio hayo endapo hautakuwa makini yanaweza kukuharibia misingi ambayo umeiishi toka kipindi cha mwanzo wa mwaka. Hiki ni kipindi ambacho kinaambatana na mambo mengi yanayohusisha matumizi makubwa ya pesa sambamba na utapeli wa kila aina.
✍πΎ Tunapoendelea kumaliza siku zilizobakia, tunatakiwa kujiuliza tumefanikiwa kwa kiwango gani katika utekelezaji wa malengo tuliyojiwekea. Mwezi Desemba, ni mwezi wa mavuno, matumizi na mwezi wa kujipanga upya kwa ajili ya mwaka unaofuatia. Yamkini tulijiwekea malengo makubwa kiasi ambacho hadi sasa hatujafanikiwa kutekeleza hata robo yake, hiki ni kipindi cha kutafakari tulikwama wapi na tunatakiwa kurekebisha wapi ili makosa hayo yasijirudie katika kipindi cha mwaka unaofuata.
✍πΎ Mwaka 2020 kwangu mimi umekuwa ni somo kwa mambo mengi. Yapo mengi ambayo nimefanikisha kadri ya nilivyokuwa nimeweka lengo lakini yapo mengi pia ambayo nimetekeleza chini ya malengo. Moja ya mafanikio ambayo najivunia hadi sasa ni kufanikiwa kuandika kila siku asubuhi kupitia neno la tafakari ya siku. Nilianzisha kundi hili nikiwa na idadi ya wanafamilia wasiozidi 30 na lengo langu lilikuwa kuwafikia wanafamilia zaidi ya 100 katika kipindi cha mwaka mzima. Hili limefanikiwa kwa asilimia zote.
✍πΎ Ndani ya kipindi hiki wapo wanafamilia ambao nimekuwa nao toka kundi hili lianzishwe na wapo ambao wamejiunga siku za karibuni. Katika kipindi ambacho tumefahamiana naamini kuna mengi ambayo umejifunza kutoka kwangu. Kwa moyo wa dhati naomba kusikia ushuhuda wako wa jinsi gani ambavyo nimegusa maisha yako. Katika ushuhuda huo naomba unieleze mafanikio ambayo umeyapata kutokana na uwepo wako ndani ya kundi hili.
Unaweza kujaza ushuhuda wako kupitia kiunganisho hiki [FOMU YA KUTOA MREJESHO WA JINSI AMBAVYO UMEFAIDIKA NA MTANDAO WA FIKRA ZA KITAJIRI] ili ushuhuda wako uendelee kuwa siri kati yako na Mimi.
✍πΎ Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa tupo mwishoni mwa mwaka 2020 japo siku zilizobakia zinabeba mambo mengi ambayo tunatakiwa kuwa macho muda wote. Hiki ni kipindi cha kutafakari mafanikio ambayo tumepata pamoja na sehemu ambazo tumeanguka. Iwe mafanikio au anguko, vyote ni kwa ajili ya kuboresha uzoefu wetu wa maisha hapa Dunuani. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.
ππΎππΎππΎππΎππΎ
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
ππΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
onclick='window.open(