HIZI NDIZO NJIA 3 ZA UHAKIKA WA KUPUNGUZA SIKU ZA KUISHI HAPA DUNIANI.

NENO LA LEO (NOVEMBA 01, 2020): HIZI NDIZO NJIA 3 ZA UHAKIKA WA KUPUNGUZA SIKU ZA KUISHI HAPA DUNIANI.

Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya kati ya siku 61 zilizobakia kuumaliza mwaka 2020. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutulinda na kutuweka salama kiasi ambacho tumefikia muda huu tukiwa na afya bora. Basi tuianze siku kwa kusema “hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani”.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache. 

Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza miongoni mwa tabia ambazo zinapunguza siku za mwanadamu kuishi hapa Duniani. Wote tunafahamu kuwa Dunia hii ni mapito kwa viumbe vyote vyenye uhai na kila kiumbe kina siku za kuishi ambazo kimeandikiwa. Tukisoma katika maandiko matakatifu tutaona kuwa wanadamu wa kale waliweza kuishi miaka mingi ikilinganishwa na binadamu wa sasa. Yapo mambo mengi ambayo kila kukicha yanapunguza siku za uhai wa mwanadamu na miongoni mwa sababu hizo zipo zinazosababishwa na mwanadamu mwenyewe na nyingine ni kutokana na mabadiliko ya asili ambayo hata hivyo undani wake ni mwandamu mwenyewe. Leo tutajifunza sababu tatu ambazo zinapunguza siku za siku kuishi kwa mwanadamu mmoja mmoja. Karibu tupitie sababu moja baada ya nyingine:-

Njia #1: Vuta sigara kila siku kwa kadri uwezavyo – Utapunguza miaka 10 kwenye siku za uhai wako hapa Duniani. Kila mtu anafahamu athari za uvutaji wa sigara ikiwa ni pamoja na hata wale ambao ni wavutaji athari za uvutaji kwa afya yao. Athari hizi zinaanzia kwenye kusababisha matatizo ya afya kwenye mfumo wa upumuaji hadi kupelekea kwenye magoja mengi kama kansa ya koo. Hata katika kipindi hiki ambacho Dunia inaendelea kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19, Shirika la Afya Duniani lilitoa angalizo kwa wavutaji wa sigara kuwa hatarini kudhulika na athari ya COVID 19 ikilinganishwa na wale ambao hawavuti. Pamoja na athari hizo kufahamika wazi bado watu wanaendelea kuvuta sigara wakijifariji kuwa hata wasipovuta watakufa tu kwa kuwa hakuna kiumbe ambaye ameandikiwa kuishi milele. Ni kweli kufa utakufa tu lakini kwa nini uwe sehemu ya kupunguza siku zako za kuishi hapa Duniani?

Njia #2: Kunywa pombe tena pombe kali kila siku – Una uhakika wa kupunguza miaka 30 kwenye siku ambazo umeandikiwa kuishi. Unywaji pombe wa kupindukia unaambatana na hatari nyingi ambazo zote kwa pamoja zinapelekea kuhatarisha afya ya mhusika. Unywaji wa pombe kali kila siku unaambatana na athari za afya kama vile kupungua uzito, kupungua kwa maji mwilini (dehyadration), magonjwa ya figo, moyo na ini, magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu (blood pressure). Hivyo, ikiwa unaendekeza unywaji wa pombe kali kwa kiwango kikubwa utambue kuwa unapunguza siku za kuishi hapa Duniani.

Njia #3: Penda mtu ambaye hakupendi – Utakufa kila siku. Mahusiano ya mapenzi au ndoa kwa ujumla ni miongoni mwa sababu kubwa ambazo zinasababisha vifo kwa watu wengi. Kupitia mahusiano ya ndoa, wapenzi wanaweza kuongeza au kupunguza siku za kuishi. Mwandishi John M. Gottman katika kitabu cha “The Seven Principles for Making Marriage Work” anatushirikisha kuwa tafiti zinaonyesha kuwa wanandoa ambao wameishi pamoja kwa muda wa maisha yao wanaishi zaidi umri wa kati ya miaka minne hadi nane ikilinganishwa na wale ambao wametalikiana. Hii ni kutokana na ukweli kwamba ndoa zenye msongo wa mawazo na kila aina ya misukosuko ni chanzo cha miili ya wanandoa kuwa na upungufu wa kinga za mwili dhidi ya maradhi mbalimbali.

Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa tunaweza kupunguza siku za kuishi kwa kuendekeza uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe kali kila siku na kupemba mwenza ambaye hakupendi. Wanadamu hatujaumbwa kwa ajili ya kufupisha siku za uhai wetu hila kutokana na kuendekeza tabia hatarishi kila siku tunapunguza siku za uhai wetu hapa Duniani. Amua sasa kuanza kuongeza siku za uhai wako kupitia kula/kunywa vyakula/vinywaji vinavyohitajika kujenga mwili, kufanya mazoezi ya viungo na kuchagua mwenza ambaye hatakuwa sehemu ya kukusababishia msongo wa mawazo. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(