Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HAMASA. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HAMASA. Onyesha machapisho yote

NENA NA NAFSI YAKO KUHUSU UTAJIRI WA NDOTO YAKO: KAULI 20 ZITAKAZOBADILISHA MTAZAMO WAKO.


   NENO LA LEO (APRILI 20, 2021): NENA NA NAFSI YAKO KUHUSU UTAJIRI WA NDOTO YAKO: KAULI 20 ZITAKAZOBADILISHA MTAZAMO WAKO.

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi nyingine ambayo nafasi ya kukushirikisha neno la tafakari ya leo. Matumaini yangu ni kwamba umepata pumzi ya uzima na upo tayari kuendelea na majukumu yako siku ya leo. Katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza kauli 20 ambazo kila siku unatakiwa kuzinena dhidi ya nafsi yako kuhusu nguvu uliyonayo katika kuvuta utajiri unaohitaji. Tunafahamu kuwa maneno unayonena dhidi ya nafsi yako yana nafasi kubwa ya kuharibu au kujenga uwezo wako wa kujiamini katika kile unachoamini. Karibu tujifunze kwa pamoja:-

Je unahitaji kupata mafundisho ya aina hii kila siku? Jiunge kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, tafadhali BOFYA HAPA KUJIUNGA.

1. Mimi ni tajiri, mimi ni mwanaume/mwanamke tajiri, mimi ni sumaku nitavuta utajiri kwangu kutoka pande zote.

2. Mimi ni sehemu ya ulimwengu usio na mwisho na usio pungukiwa hivyo nimeunganishwa na kila kitu ninachohitaji katika kufikia utajiri wa ndoto yangu.

3. Nitawapa wengine thamani kubwa, kila mara nitakuwa mtu wa thamani kwa wengine, mimi ni mtu asiye na ukomo wa maoni na fikira za ubunifu. Natambua kuwa nitabarikiwa utajiri zaidi kadri ninavyotoa thamani kwa wengine.

4. Kuna zaidi ya kutosha kwa kila mtu. Wingi uko kila mahali ninapoangalia. Ninaona utajiri, wingi na ustawi kila mahali niendako.

5.   Nastahili kuwa tajiri. Utajiri ni haki yangu ya kuzaliwa. Utajiri ni sehemu ya maisha yangu. Ulimwengu upo tayari kunizawadia utajiri wa ndoto yangu.

SOMA: MAISHA YA UTAJIRI AU UMASIKINI: JE NI IPI HAKI YAKO YA KUZALIWA?

6.  Nimeumbwa kwa ajili ya kuishi maisha ya shibe, maisha ya kuwa na zaidi, maisha ya kujitosheleza. Hivyo, shibe ni haki yangu ya kuzaliwa. Sijaumbiwa maisha ya dhiki kwa kuwa Muumba anachukia dhiki kwa waja wake.

7. Ninawaombea watu wote maisha ya utajiri wa ndoto zao, maisha ya shibe. Ninanayo furaha kubwa kadri ninavyoona natumika kuwasaidia watu wengine kufikia utajiri wa ndoto zao. Upendo ni nyenzo kuu ambayo nitaendelea kuitumia kusaidia watu.

8. Mimi nimeumbwa na Mungu ambaye aliniweka katika Ulimwengu huu na kuinua nafsi yangu juu. Nimepewa mamlaka ya kutawala vitu vyote na kupitia kuumbwa kwa sura na mfano wake nimepewa mamlaka ya kuumba kila kitu ambacho nakiona katika fikra zangu.

9.   Kila siku, kwa kila njia, ninazidi kuwa tajiri. Najipima nakuona kuwa matendo yangu yananiwezesha kukua kiuchumi kila siku. Nitaendelea kuwa sehemu ya kukuza utajiri wangu kupitia matendo yangu.

10.  Hakuna ubaya wowote kuhusu pesa ikiwa pesa inapatikana na kutumika kwa njia halali. Mimi ndo nitaifanya pesa ionekane mbaya au nzuri kupitia matumizi ya pesa inayoingia mikononi mwangu.

11.  Matendo yangu yana thamani kwa wengine kiasi gani? Nitaendelea kutumia pesa kupima thamani ninayoitoa kwa wengine. Watu wapo tayari kulipia thamani ninayoitoa kwao kulingana na mahitaji ya soko.

12.  Pesa ni nishati safi ya kuniwezesha kumiliki na kuitawala dunia. Pesa inaundwa katika mfumo wangu wa fikra. Pesa iko akilini mwangu. Nitaendelea kutumia akili yangu kuvuta pesa ninazohitaji siku baada ya siku.

13. Ninastahili kumiliki pesa. Ninastahili kuwa na pesa nyingi. Hivyo, nipo tayari kuvutia kiasi kikubwa cha pesa kwangu kupitia thamani ninayoitoa kwa wengine.

14. Kuwa tajiri kunanipa nguvu ya kusaidia watu wengine wenye mahitaji katika Ulimwengu huu kwa ajili ya kufanya mabadiliko makubwa katika maisha yao. Nitatumia sehemu ya kiasi cha pesa ninachopata kwa ajili ya kukusaidia na kuinua watu wengine.

15.  Mimi ni msimamizi mkuu wa pesa yangu. Sitakubali pesa itumike kuharibu maisha yangu. Nitasimamia maisha yangu ya kifedha kwa ajili ya utakaso wa nafsi yangu katika maisha haya na maisha yajayo.

16.  Pesa inaenda sehemu ambako inapendwa na kuthaminiwa zaidi. Nitahakikisha kila shilingi inayoingia mkononi mwangu inatumika kulingana na bajeti. Nitahakikisha natumia pesa ninayoipata kukuza uwezo wangu wa kifedha kwa kuhakikisha pesa inatumika kuzalisha pesa zaidi.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI

17.  Natambua kuwa kiwango cha pesa ninachopata kina uhusiano mkubwa na kiwango cha pesa ninachotoa kwa wengine. Kadiri ninavyotoa zaidi, ndivyo ninavyozidi kuwa tajiri. Kadiri ninavyotoa zaidi ndivyo nazidi kuunganishwa na watu ambao watanifungulia milango ya kukua zaidi kiuchumi.

18.  Watu wanaonizunguka wanabariki utajiri wangu kwa maana nimekuwa wa msaada kwao katika kila hali. Nimekuwa mtu wa kufunua fursa kwa wengine. Nimekuwa mtu wa kuendelea kuhamasisha wengine. Nimekuwa mtu wa kuonesha wengine kuwa kila jambo linawezekana.

19. Ninapumua kwa raha. Naendelea kuwa sehemu ya jamii inayolinda ubora wa hewa tunayovuta. Kila pumzi ninayovuta huongeza ufahamu wangu kuhusu wingi unaonizunguka.

20.  Nina fikra za kimilionea. Nina mawazo kimilionea. Natenda kama milionea, nahisi kama milionea, mimi ni milionea. Ninashinda vizuizi vyote ambavyo viko katika njia yangu ya mafanikio na uhuru wa kifedha.

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo nimekushirikisha kauli 20 kutoka kwenye vyanzo tofauti ambavyo vimeandika kuhusu utajiri. Hizi ni kauli chache ambazo unaweza kuzinena dhidi ya nafsi yako katika maisha yako ya kila siku. Unaweza kurekebisha au kuboresha kauli hizo ili ziendane na mazingira ya maisha yako. Kumbuka, mbegu ikidondoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganishi hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema OFA hii.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

MAFANIKIO NI WATU, FAHAMU MBINU AMBAZO UNAWEZA KUZITUMIA KUVUTA WATU CHANYA KWAKO.

NENO LA LEO (APRILI 14, 2021): MAFANIKIO NI WATU, FAHAMU MBINU AMBAZO UNAWEZA KUZITUMIA KUVUTA WATU CHANYA KWAKO.

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni wakati mwingine tumepata bahati ya kuwa hai huku tukiwa na deni la kuishi kulingana na ndoto kuu ya maisha yetu. Je umeshaitambua ndoto hiyo na tayari umeanza kuiishi katika maisha yako ya kila siku? Maisha yenye thamani yanakutaka uwe na ndoto ambayo kila siku kuna jambo unalifanya kupitia majukumu yako ya kila siku. Matendo yako katika kila siku ambayo umebahatika kuwa hai yanatakiwa kuwa sawa na uwekezaji unachangia ukamilisho wa ndoto kuu ya maisha yako.

 Je unahitaji kupata mafundisho ya aina hii kila siku? Jiunge kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, tafadhali BOFYA HAPA KUJIUNGA.

Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza jinsi ambavyo tunaweza kuvuta watu chanya katika maisha yetu. Ndoto yoyote ambayo umeichagua kuyatoa maisha yako kwa ajili ya ukamilisho wake inahitaji watu tena watu wenye mtazamo chanya. Hivyo, katika kila aina ya mafanikio unayoyataka kama matokeo ya ukamilisho wa ndoto ya maisha yako ni lazima utambue aina ya watu ambao wanatakiwa kukuzunguka sambamba na wale ambao unatakiwa kujitenga nao.

Soma: TABIA 10 AMBAZO ZITAONESHA KUWA UNAKIMBIZANA NA HELA MAISHA YAKO YOTE. 

Ikiwa unahitaji kuwa na mtazamo chanya ni lazima uzungukwe na watu wenye mtazamo chanya. Hata hivyo, kuzungukwa na watu wenye mtazamo chanya ni lazima ujue mbinu za kuwavuta watu aina hiyo. Kuvutia watu chanya kwako ni kunaanzia kwenye mtazamo wako. Kupitia mtazamo kuna vitu ambavyo utatakiwa kuvifanya kila mara na hatimaye vitu hivyo vitakuwa sehemu ya tabia zako. Karibu tujifunze mbinu ambazo unaweza kuzitumia kuwavuta watu chanya:-

Mbinu #1: Jisemee kauli chanya kabla ya kwenda kwenye matukio ya kijamii.

Mara zote sisi ni zao la kauli na imani tunazoamini dhidi ya nafsi zetu. Ili kuvuta watu chanya katika maisha yako ni lazima kwanza uwe na imani chanya juu ya nafsi yako. Kabla ya kukutana na makundi ya watu ni lazima uwe kauli zinazoifanya nafsi yako iaminiwe na watu. Pia, unatakiwa kuwa na kauli chanya kuhusu watu unaonenda kukutana nao. Kwa kufanya hivyo, utajisikia mwenye furaha na msisimko kukutana watu wengine kwa kuwa unajiamini kila katika kila hali. Hii itafungua akili yako na kukusaidia kuwa chanya na hatimaye kuvutia watu chanya kwa kuwa watu wanapenda watu wanajiamini na wacheshi.

Mbinu #2: Jitenge na watu wenye mtazamo hasi. Ikiwa umezungukwa na watu hasi katika maisha yako ni vigumu sana kwako kuwa na mtazamo chanya. Watu hasi mara zote watakufanya ujisikie uzembe wa kufanya kazi, mara zote utakuwa haujiamini katika maongezi yako au kila unalofanya, na utakuwa mtu wa kulalamika. Kuvuta watu chanya, ni lazima kwanza upunguze mawasiliano na ukaribu na watu wenye mtazamo hasi. Kwa kukimbia watu wa aina hii utaanza kushangaa uwezo wako kwa maana utaweza kufanya vitu ambavyo awali ulidhani haviwezekani.

Mbinu #3: Kuwa mtu Shukrani. Kwanza unatakiwa kwanza ujikubali na kushukuru jinsi ulivyo na kila ulichonacho. Kitendo cha kujikubali na kushukuru kwa kadri unavyotendewa, kitawafanya watu wavutiwe kuwa karibu nawe. Pia, mtu wa shukrani inajumuisha kuwa tayari kupokea mazingira mapya pamoja na watu wapya katika maisha yako.

Mbinu #4: Nenda kwenye matukio yaliyopo nje ya ukanda wako wa faraja. Kukutana na kuvutia watu wenye mtazamo chanya, ni lazima uondoke kwenye mazingira uliyozoe. Ni lazima ushiriki matukio ambayo haujazoe kushiriki. Ni lazima uwe tayari kushiriki mikusanyiko ambayo itakuongezea changamoto mpya za maisha. Ni lazima uwe tayari kushiriki matukio ambayo yanaongeza hali na msisimko wako dhidi ya watu na mazingira kwa ujumla. Hii haimaanishi kuwa kila mara unapaswa kwenda nje na kushiriki kila aina ya sherehe, badala yake inakukumbusha umuhimu wa kwenda kwenye hafla za kijamii ambazo ni mpya kwako na zinakukutanisha na watu wapya. Mfano, unaweza kushiriki semina mbalimbali, kujiunga na makundi mapya ya watu, kutoka nje kwa ajili ya chaku au kinywaji kwenye sehemu ya hadhi, au kwenda kwenye karamu ya chakula cha jioni na watu maalum.

Mbinu #5: Kuwa mnyumbulifu. Ili kuvuta watu chanya ni lazima uwe tayari kupokea mawazo na imani mpya zenye kukinzana na mawazo na imani ulizonazo. Ikiwa utafanikiwa kupokea mawazo na imani mpya bila bila kukasirika au mabishano yasiyo na tija, utavutia zaidi watu watu wenye mtazamo chanya upande wako.  Maisha yamejaa matukio yasiyotarajiwa, hivyo, watu wanapenda watu ambao wapo tayari kuendana na mabadiliko kwa urahisi. Ikiwa unaweza kuzoea hali yoyote kwa urahisi, itakuwa rahisi kuvutia watu chanya upande wako.

Mbinu #6: Kuwa mtu wa upendo na wasaidie wengine. Kusaidia wengine na kutoa upendo kwa wengine bila kutegemea mrejesho ni chambo cha kuvuta watu chanya bila kutarajia. Ishara za upendo na matendo ya kusaidia wengine wala siyo lazima zihusishe vitu vya gharama, vitu vya kawaida iwapo vimefanywa kwa upendo vinapelekea watu wakuamini na kukupenda. Kumbuka, toa kwa njia ya upendo wala sio kwa njia ambayo itakufaidisha kwa baadae. Haupaswi kutarajia malipo yoyote katika matendo ya upendo au msaada unaotoa kwa wengine.

Mbinu #7: Tumia mbinu za utulivu wa akili. Moja ya mbinu za kutuliza akili ni kupitia tajuhudi (meditation) ambayo inahusisha utulivu wa akili kwenye kufikiria juu mazingira na watu wanaokuzunguka. Utulivu wa fikra kwenye maisha yako kwa kuzingatia mawazo yako kwa wakati uliopo tu na jinsi unavyohisi wakati huo huo. Kupitia tajuhudi utakutana na mioyo ya watu wengine wenye mtazamo wako. Unaweza kufanya tajuhudi kwa kuifanya akili yako ijikite kuzingatia ulimwengu unaokuzunguka. Angalia vitu unavyogusa, unasikia nini, unaona nini au unanusa nini (tumia milango yako ya fahamu kuituliza akili yako). Mfano, ikiwa unakula, zingatia ladha na jinsi unavyohisi juu hiyo ladha. Zingatia kutuliza akili yako kwenye jambo unalojihusisha nalo kwa wakati husika.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI

Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza mbinu ambazo tunaweza kutumia kuvuta watu chanya katika maisha yetu ya kila siku. Mafanikio ni watu, hivyo tuna kila sababu ya kujifunza kuvuta watu sahihi katika maisha yetu ya kila siku. Kumbuka, mbegu ikidondoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganishi hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema OFA hii.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

TABIA 5 AMBAZO ZITAKUFANYA UJIAMINI ZAIDI

      NENO LA LEO (APRILI 5, 2021): [BURIANI JPM] TABIA 5 AMBAZO ZITAKUFANYA UJIAMINI ZAIDI

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya ambayo naamini tumeamka salama na tupo tayari kuendeleza jitihada za kuboresha maisha yetu. Leo hii tunaingia siku ya 19 kati ya siku 21 za maombolezo ya kifo cha mpendwa wetu, shujaa wa Afrika, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

 Kama bado hujajiunga na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI kwa ajili ya kupata neno la tafakari kila siku, tafadhali JIUNGE SASA. 

Katika neno la tafakari ya jana tujifunza kuhusu kauli ambazo watu sumu wanatumia kupunguza uwezo wa kujithamini kwa watu wengine. Pia, katika mafundisho yaliyopita tuliona kuwa watu wengi katika kipindi cha kukata roho wanajutia kuishi maisha ambayo hawakuweza kudhihirisha uwezo wao halisi katika kipindi ambacho walikuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Katika neno la tafakari ya leo tutajifunza tabia 5 ambazo zitakuongezea uwezo wa kujithamini ili kwa kufanya hivyo upate uwezo wa kujiamini zaidi (self confidence) katika kila unachofanya.  

SOMA: KAULI 6 AMBAZO WATU SUMU WANATUMIA KUKANDAMIZA UWEZO WAKO WA KUJITHAMINI

Kwa ujumla uwezo wa kujiamini unajumuisha mtazamo wako kuhusu ujuzi na uwezo wako. Inamaanisha unajikubali na unajiamini na unaweza kudhibiti hisia zako katika maisha ya kila siku. Unajua uwezo na madhaifu yako vizuri, na una mtazamo chanya juu ya nafsi yako. Kutaokana na tafsiri hii, kupitia ikiwa una kiwango cha juu cha kujiamini tunategemea unaweza kuwasiliana na wengine kwa ujasiri, unaishi matarajio na malengo yako halisi, kukosoa wengine na kuwa tayari kukosolewa au kujifunza na unachukulia madhaifu yako kama changamoto ya muda ambayo umedhamiria kuitatua. Karibu tujifunze kwa pamoja tabia ambazo zitaongeza uwezo wetu wa kujiamini:-

Tabia #1: Jifunze kutunza mwili wako. Ikiwa hauna tabia ya kutunza mwili wako ni vigumu kujiamini maana mwonekano wa mwili wako una nafsi kubwa katika kujiamini mbele za watu. Unapokuwa unautunza vyema mwili wako kwa kuzingatia kanuni za kulinda mwili wenye afya bora moja kwa moja akili, mwili na roho kwa pamoja vinajenga hali ya kujiamini zaidi. Unaweza kutunza mwili wako kwa kuzingatia ushauri huu:-

Zingatia mlo sahihi. Mlo sahihi una faida nyingi kwenye mwili sambamba na kuongeza viwango vya juu vya kujiamini na kujithamini. Unapoulisha mwili wako chakula kizuri unajihisi kuwa na mwili wenye afya, nguvu, na mwonekano mzuri hivyo kupelekea kila mara kujivunia mwili wako. Hali hiyo inakuongezea uwezo wa kujiamini.

Kufanya mazoezi ya viungo. Tafiti zinaonesha kuwa watu wanaofanya mazoezi ya viungo wanakuwa na ujasiri zaidi ikilinganishwa na watu ambao hawana mazoezi. Mazoezi ya viungo yanasaidi mwili wa mhusika kujengeka na kuimarisha vyema misuri hali inayopelekea wahusika wajiamini zaidi. Pia, mwili wenye mazoezi ya viungo ni nadra kushambuliwa na magonjwa ya mara kwa mara.

Kufanya tajuhudi (Meditation). Kama ambavyo tumeona kwenye umuhimu wa mazoezi ya viungo ndivyo ilivyo kwenye mazoezi yanayohusisha akili. Tajuhudi ni zoezi au tabia inayohusisha kiwango cha juu cha kutafakari kuhusu maisha yako kwa ujumla. Kupitia tabia hii unaweza kujitambua wewe ni nani, unatakiwa kuishi maisha yapi na kwa nini maisha hayo. Hali hii itakuongezea uwezo wa kujikubali na kujithamini zaidi. Pia, kupitia tajuhudi utafanikiwa kuachana na mitazamo hasi kuhusu wewe mwenyewe na mazingira yanayokuzunguka.

Kuwa na muda wa kutosha kwa ajili ya usingizi. Muda wa kutosha kwa ajili ya kupumzika ni tiba tosha kwa ajili ya mwili wenye afya. Usingizi unaweza kupelekea ushindwe kutimiza majuku yako kwa ufanisi, kutokana na kuwa na mwili uliosinyaa kila mara.

Tabia #2: Jifunze kujiongezea maarifa kupitia usomaji. Kujisomea maarifa mbalimbali ni tabia ambayo itakuwezesha akili yako isizeeke haraka. Kupitia tabia hiyo unaongeza uwezo wa kujiamini zaidi kwenye kila sekta ya maisha yako kwa kuwa unakuwa na taarifa, ujuzi na maarifa sahihi yanayoendana na wakati uliopo. Chochote unachosoma iwe hadithi za ukweli na uongo, historia, vitabu kuhusu viumbe, tamthilia, vitabu vya maarifa mbalimbali au mafundisho ya vitabu vya dini, una nafasi ya kujiimarisha zaidi kimwili, kiakili na kiroho. Kupitia usomaji unapata nafasi ya kutafakari, kupitia usomaji unatapa nafasi ya kuachana na mawazo hasi, na kupitia usomaji unajifunza kuhusu wewe mwenyewe, watu wanaokuzunguka na mazingira yanayokuzunguka kwa ujumla wake.

Tabia #3: Hama kutoka kwenye ukanda wa faraja (Comfort zone). Inaweza kushangaza au kuwa ngumu, lakini unapoondoka kwenye mazoea ya awali inakuwezesha kutafuta changamoto mpya. Katika mazingira mapya na changamoto mpya unajifunza mambo mengi ambayo yatakuwezesha kujiimarisha zaidi kimaisha ikilinganishwa kama ungeendelea kuishi kwa mazoea. Hivyo, kila mara unatakiwa kujipa changamoto mpya kwa ajili ya kuongeza uzoefu wako kwenye kila sekta ya maisha. Kwa kufanya hivyo utafanikiwa: kuongeza ujuzi na kujifunza maarifa mapya; kutambua uwezo wako halisi katika kutatua changamoto za kimaisha; kupanua mtazamo na uelewa wako kuhusu maisha; na kuongeza ujasiri wako.

Tabia #4: Tumia nguvu ya mazungumzo chanya ndani ya nafsi. Mazungumzo chanya kuhusu nafsi yako yanakuwezesha kukuza matumaini, kukuza kiwango cha huruma, kuondoa shaka, kuchukua changamoto mpya, na kuepuka makosa. Kwa upande mwingine, mazungumzo hasi kuhusu nafsi yako yanaweza kupunguza uwezo wako wa kufanya kazi, au kupunguza ujasiri wako. Hali hii inatokana na ukweli kwamba mazungumzo hasi yana asili ya kushawishi ujione kuwa "hauwezi kushughulikia" au “kuona ugumu” katika kila kitu na kufifisha "ubunifu na morali ya kujaribu." Ukiwa katika kundi la watu kabla ya kuanza kuchangia mada iliyopo mezani anza kwa kuchangia mada husika ndani ya nafsi yako kwa kutazama ufahamu wako kuhusu mada husika. Tafakari kuhusu mifano hii michache: 

Badala ya kusema "Siwezi kushughulikia hili," au "Hii haiwezekani," jaribu kujikumbusha kwamba "Ninao uwezo wa kufanya…..," au "Ninachopaswa kufanya ni kujaribu kwanza kabla ya kuhitimisha kuwa siwezi.";

Badala ya kujisemea "siwezi kufanya chochote sahihi hasa baada ya kushindwa" kila mara unapokosea, jikumbushe kwa kujisemea "Kuanguka mara kwanza ni mwanzo wa kufungua nafasi za kufanya vizuri zaidi wakati ujao” au “pamoja na kutofanikiwa angalau sijapoteza muda, nguvu na rasilimali maana nimejifunza mengi”.

Tabia #5: Kubali na sherekea tofauti zako. Wakati mwingine, tofauti zako ukijilinganisha na wengine zinaweza kuwa ndio chanzo cha kutokujipenda, kujikubali au kujithamini mwenyewe. Unaweza kuwa unajilinganisha na wengine, lakini unajiona haufikii viwango vyao kutokana na nadharia ambazo umeweka kichwani mwako kuhusu watu hao. Tatizo ni kwamba kadri unavyoangalia mazuri ya wengine unasaha kunagalia mazuri uliyonayo badala yake unaishia kuangalia mabaya yako pekee. Wakati unafanya hivyo na kuishi kujidharau wapo watu wengine ambao wanatamani wangefanikiwa kupata mazuri yako. Fikra za namna hii ni sumu kwa maendeleo yako maana kila mara utaendelea kufifisha uwezo wako halisi. Kumbe, unatakiwa kutambua kuwa tofauti zetu ni jambo la kawaida maana wote hatuwezi kuwa sawa. Tofauti hizo ndizo zinachochea mafanikio kati yetu katika makundi ya kijamii tunayoishi. Udhaifu wako ni nguvu na tija kwa mtu mwingine, na mazuri yako pia ni tija kwako na watu wengine.  Sherekea tofauti zako na tofauti za wengine ukitambua kuwa Wewe ni wa kipekee, na wa aina yake na tofauti zako ni sehemu ya upekee wako katika kufanikisha kusudi kuu la Muumba wako.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI

Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo nimekushirikisha tabia 5 ambazo zitakuwezesha kuongeza uwezo wako wa kujithamini na kujiamini. Tumia tabia hizo kila mara na hakika utaona tofauti ndani ya muda mfupi. Kumbuka, mbegu ikidondoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

 

PS:  Ongeza maarifa yako kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

HII NDIYO NJIA SAHIHI YA KUKABILIANA NA ONGEZEKO LA MAHITAJI YA PESA

NENO LA LEO (JANUARI 14, 2021): HII NDIYO NJIA SAHIHI YA KUKABILIANA NA ONGEZEKO LA MAHITAJI YA PESA

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine ambapo tumepewa kibali cha kuwa hai. Kibali hiki in cha kuwa na uwezo wa kuvuta pumzi ya hewa safi na kutoa hewa chafu na katika kufanya hivyo tunapata nguvu ya kutafuta ridhiki kupitia majukumu yetu ya kila siku. Kila unapovuta hewa safi (Oxyjeni) na kutoa hewa chafu (Carbondiode) unatakiwa kutambua kuwa unazalisha nguvu kupitia mmeng'enyo wa chakula na nguvu hizo zinatakiwa   kutumika kwa faida.

Jiunge na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, kwa kujiunga utapata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, TAFADHALI JIUNGE SASA

Mwanadamu ni kiumbe ambacho kinategemea uwepo wa pesa kwa ajili ya kukamilisha mahitaji ya msingi. Toka pesa ilipogunduliwa katika historia ya maendeleo ya Mwanadamu imekuwa ni nyenzo muhimu ya upatikanaji wa mahitaji ya msingi kwa mtu mmoja mmoja, familia na hata taifa. Hata hivyo, katika maendeleo ya Mwanadamu kadri umri kuongezeka ndivyo mahitaji ya pesa yanavyoongezeka. Hali iko hivyo pia kwa familia na hata taifa. Mara zote ukuaji wa mtu, familia au taifa huwa unaambatana na ongezeko la mahitaji ya pesa.

Tutakubaliana kuwa katika kipindi cha utoto mahitaji ya pesa huwa ni kidogo sawa na ilivyo kwa familia changa ya watu wawili. Hila kadri umri unavyozidi kuongezeka au kadri familia inavyozidi kupanuka ndivyo na mahitaji ya pesa yanaongezeka. Katika jamii zetu tumezoea kuona mwezi Januari na Julai katika kila mwaka inakuwa ni miongoni mwa miezi ambayo huwa inahusisha mahitaji makubwa ya pesa kwa mtu mmoja mmoja au familia. Hali hii inatokana na ukweli kwamba miezi hii inahusisha ulipaji ada za wanafunzi pamoja kodi za pango la nyumba. Hata hivyo, mwezi Januari unakuwa na mwezi wenye vilio vikubwa vya upungufu wa pesa kwa kuwa wengi wanakuwa na matumizi makubwa nje ya bajeti katika sherehe za mwisho wa mwaka.

Je ni ipi tiba halisi ya kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya pesa? Katika jamii, watu wengi huwa wanatumia mbinu ya kubana matumizi kama tiba ya kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya pesa. Hata hivyo, mbinu hii huwa haimpi mhusika Uhuru wa kufurahia maisha kutokana na jinsi anavyojibana katika mfumo mpya wa maisha. Matokeo ya mbinu hiyo ni kuongezeka kwa msongo wa mawazo kadri mahitaji ya pesa yanavyoongezeka.

Kumbe, tiba halisi ya kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya pesa siyo kupunguza matumizi bali ni kuongeza mifereji mipya ya mapato. Wengi katika jamii wanaendelea kuteseka kwa kuwa wanaishi kwa kutegemea chanzo kimoja cha pesa bila kugundua kuwa chanzo hicho kinaelemewa kutokana na ongezeko la mahitaji ya pesa. Kama ni mshahara, ukweli ni kwamba kasi ya ongezeko la mahitaji ya pesa haiwezi kuendena na kasi ya ongezeko la mshahara toka kwa mwajiri wako. Hata kwenye biashara, tunashuhudia biashara nyingi zinakufa kutokana na kuzidiwa mahitaji ya pesa yanayowakabili wamiliki wa biashara hizo. Tafsiri yake ni kwamba kasi ya ongezeko la mahitaji ya pesa inakuwa kubwa ikilinganishwa na faida inayotengenezwa kwenye biashara.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI 

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo tumejifunza ni kawaida mahitaji ya pesa kuongezeka kadri umri unavyoongezeka. Baada ya kutoka kwenye maisha ya utegemezi wa wazazi, mahitaji ya pesa yanaongezeka kwa kasi sana ikiwa hakuna mkakati wa kuongeza vyanzo vipya vya mapato. Badala ya kupunguza matumizi kwa kujibana kama mbinu ya kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya pesa unatakiwa kuongeza mifereji ya kipato ili kuendana na ukuaji wa mahitaji ya pesa. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

JE UNAHITAJI MWAKA 2021 UWE WA TOFAUTI? MAMBO 10 KUZINGATIA.

NENO LA LEO (JANUARI 1, 2021): JE UNAHITAJI MWAKA 2021 UWE WA TOFAUTI? MAMBO 10 KUZINGATIA.

Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Hongera kwa kumaliza mwaka na kuunza mwaka ukiwa salama, hakika kwa wema wake Mungu tumehitimisha siku 365 na sasa tuna kibarua cha kuendeleza moto katika siku 365 zilizopo mbele yetu. Kila mwaka huwa unakuwa na matukio tofauti na matukio hayo huwa ndiyo yanauwafanya mwaka uonekane ulikuwa bora au mchungu kwa watu binafsi, jamii au taifa kwa ujumla wake. Mwaka 2020 kwa ujumla wake ulikuwa na matukio ya huzuni na majionzi zaidi kwa taifa na Dunia kutokana na kupoteza idadi kubwa ya watu waliopoteza maisha kwa ugonjwa wa virusi vya Corona.

Soma: ONDOKA 2020 LAKINI UMENIACHIA SOMO KUBWA KATIKA MAISHA YANGU.

Kama taifa tumeshuhudia huzuni kubwa ikitawala kutokana na kumpoteza Mhe. Benjamini Willium Mkapa ambaye alikuwa ni nguzo imara katika historia ya uongozi na mapinduzi ya uchumi wa nchi yetu. wakati mwingi Ni mwaka ambao ulitawaliwa na matukio ya majonzi katika kila kona ya Dunia. Hata hivyo, pamoja na yote hayo tuna kila sababu ya kusema ee Mungu umekuwa mwemwa kwangu katika kipindi hiki chote cha mwaka 2020 hivyo naomba wema wako uwe nuru ya kuniongoza katika kipindi chote cha mwaka 2021. Pia, itakumbukwa kuwa mwaka 2020 kama taifa ulikuwa ni mwaka wa uchaguzi ambao kawaida huwa unaambatana na matukio mengi katika kila kona nchi. Matukio yote haya yaliufanya mwaka uonekane kuwa mrefu zaidi ikilinganishwa na miaka mingine ambayo haikuwa na misukosuko mingi kiasi hiki. Pamoja na yote hayo, wewe na mimi na taifa zima la Tanzania tusiposema asante kwa Muumba tutakuwa hatuna fadhira.

Karibu katika Makala maalumu ya siku ya leo ambapo nitakushirikisha mambo kumi ya kuzingatia ili kipindi chote cha mwaka 2021 kiwe na mafanikio ya kila aina kwa kadri ya mahitaji yako kwenye kila sekta ya maisha yako. Naamini na wewe ni miongoni au umewahi katika kundi la watu ambao kila mwanzo wa mwaka huwa wanakuwa na kauli nyingi za kuonesha kuwa mwaka ujao utakuwa wa tofauti lakini mwishowe wanajikuta katika hali ile ile. Leo hii ukizunguka mitaani au kwenye kurasa za mitandao ya kijamii utasikia au kuona kauli nyingi kama vile: “mwaka mpya na mambo mapya, huu ni mwaka mabadiliko, mwaka wa urejesho, mwaka wa upendo,” na kauli nyingine nyingi.

Hata hivyo, kauli hizo huwa zinayeyuka taratibu kadri siku na miezi inavyosogea na mwisho wake watu wanajikuta kwenye sehemu au tabia zile zile ambazo mwanzoni mwa mwaka waliweka mikakati ya kuachana nazo. Huo ndiyo ukweli kwa asilimia kubwa ya watu katika jamii kwa maana wanaishi katika tabia ambazo hawaridhishwi nazo.

Je mwaka 2021 nifanye nini ili mwaka huu uwe wa tofauti katika historia ya maisha yangu?

Ushauri #1: Je umeweka vipaumbele kwa mwaka 2021? Kinachogharimu watu wengi wasifikie malengo kama wanavyodhamiria mwanzoni mwa mwaka ni kutokuwa na vipaumbele. Wengi hawana mpango unaowaongoza n ahata kama wana mpango hawazingatii mpango huo na matokeo yake ni kujihusisha na kila linalokuja mbele yao. Katika hali kama hiyo wanajikuta wameshindwa kufanikiwa katika mambo mengi na mwisho wake ni kukata tamaa. Anza kwa kujiuliza nahitaji nini katika kipindi hiki cha mwaka 2021.

Ushauri #2: Je tayari una bajeti yam waka 2021? Bajeti ni dira ya kukuongoza kwenye vipaumbele vyako. Bajeti ni mwongozo unaokuwezesha vipaumbele vyako viendane na mapato yako. Zaidi ya yote kupitia bajeti unajipima na kugundua sehemu zipi unatakiwa kupambana ili kuongeza kipato zaidi kwa ajili ya kutosheleza mahitaji yako. Vile vile, kupitia bajeti utaweza kudhibiti matumizi ya pesa zako. Hapa ndipo wengi wanaanguka mapema, kwa kutokuwa na bajeti kila pesa wanayopata inaelekezwa katika matumizi ambayo hayakuwa sehemu ya malengo na mwisho wake ni kutofanikisha yale waliyokusudia.

Ushauri #3: Badili mtazamo wako. Maisha ni sasa kwa ajili ya maisha ya kesho. Ikiwa miaka iliyopita umekuwa mtu wa kutofanikiwa kuanzia sasa jisemee kuwa huu ni mwaka wa tofauti na kipekee kwangu kuvunja minyororo ya kutokufanikiwa. Jione ukiwa mtu mpya katika mwaka mpya, historia mpya na uwezo mpya. Unahitaji kuwa mtu wa mtazamo chanya katika kila hali iliyopo mbele yako. Jione wewe ni mtu wa kufanikiwa, jione wewe ni mtu wa kupendwa zaidi, jione wewe ni mtu wa kutoa upendo kwa wengi na zaidi ya yote jione ukikamilisha malengo yote ambayo umejiwekea.

Ushauri #4: Kubali kuanza upya kama kila ulichonacho kipo kinyume na malengo yako. Ili ufanikiwe zipo sehemu ambazo unalazimika kujikana kwa ajili ya kupata hitaji la msingi. Kuna mazingira unapaswa ya kuyakimbia kwa ajili ya kupata changamoto mpya. Kuna kundi la marafiki au ndugu unatakiwa kujiweka mbali nao ili kupata nafasi ya kutafakari upya. Kuna tabia ambazo zinaenda kinyume na mahitaji yako hauna budi kuzitupilia mbali. Na mengine mengi ambayo hayana tija katika mwelekeo mpya wa mwaka huu.

Ushauri #5: Kuwa mtu wa vitendo. Vitendo bila kujali ukubwa (intensinty) wa vitendo hivyo ni njia pekee ambayo itaufanya mwaka huu uwe wa tofauti. Mwanzoni mwa mwaka unakuwa mtu wa matamanio (wishes) na njia pekee ya kubadilisha matamanio hayo ni vitendo. Katika kila lengo ambalo umejiwekea kutokana na matamanio yako una wajibika kuweka mikakati au shughuli ya kutekeleza lengo husika. Hapa ndipo unatakiwa kujikana! hapa ndipo unatakiwa kujiumiza! hapa ndipo unatakiwa kujinyima! hapa ndipo unatakiwa kujitoa sadaka! Hapa ndipo unatakiwa kuongeza maarifa mapya! Hapa ndipo unatakiwa kupunguza masaa ya kuwa kwenye kitanda chako!

Ushauri #6: Kuwa tayari kujiamini na kuamini njia unazotumia. Kelele zitakuwa nyingi katika kipindi hiki ambacho unatamani kuona mwaka 2021 unakuwa wenye mafanikio. Kelele hizo zitatoka kwa watu wako wa karibu ambao wengi wamezoea kukuona katika maisha ya zamani na sasa wanatamani maisha hayo yaendelee. Ni lazima ufahamu mapema kuwa siyo wote wataelewa dhamira yako. Upinzani wa mtazamo wako mpya unaweza kuanzia ndani ya familia yako, marafiki au ndugu kutokana na ukweli kwamba katika maisha mapya kuna mambo mengi waliyozoea awali na sasa hawatayapata tena. Simama imara songa mbele, husikubali kuchanganywa na miruzi mingi njiani.

Ushauri #7: Tafuta washauri katika yale unayofanya. Hakuna jipya chini ya jua, lolote unalofanya tayari kuna watangulizi wako ambao wameshawahi kufanya hayo tena kwa mafanikio. Pale ambao unaona mambo yanakuwa magumu na unahitaji kupata mwongozo mpya hakikisha unatafuta washauri wa kukushika mkono. Na pale inanapobidi kuwa tayari kulipia ushauri au mafunzo hayo kwa ajili ya kupata maarifa mapya katika changamoto iliyopo mbele yako.

Ushauri #8: Weka akiba au jilipe kwanza. Njia pekee ya kufanikiwa kifedha ni kuhakikisha unakuwa na akiba kwa ajili ya dharura na maendeleo ya siku zijazo. Kama ulizoea kila shilingi inayoingia mikononi mwako, wakati ni sasa wa kuanza kutenga asilimia flani pato lako kwa ajili ya siku za baadae. Kuna fursa nyingi ambazo zimekuwa zikikupita kutokana na kutokuwa na akiba. Husidharau kiasi kidogo cha pesa unachowekeza ikiwa kiasi hicho kinawekezwa kwa kufuata misingi ambayo umejiwekea. Mfano, fikiria kama siku unaweka Tshs. 1,000 kwa mwaka ni zaidi ya laki tatu na ikiwa kila siku unaweza Tshs. 5,000 kwa mwaka ni zaidi ya milioni moja na nusu. Maamuzi yapo mkononi mwako kulingana na kipato ulichonacho.

Ushauri #9: Jiongezee maarifa. Kila siku hakikisha unakuwa na muda wa kusoma kitu ambacho kitachochea hali au morali ya kusonga mbele. Kumbuka nimetangulia kukuambia kuwa unatakiwa kuwa na mtazamo chanya katika kila hali. Hauwezi kuwa na mtazamo chanya kama hauna utaratibu wa kujisomea maarifa mapya kupitia Makala mbalimbali, vitabu vya mafanikio au kuwa kwenye makundi yenye mafunzo maalum. Katika mipango unayojiwekea hakikisha unaweza na idida ya vitabu ambavyo unatakiwa kusoma mwaka huu pamoja na idadi ya semina ambazo unatakiwa kushiriki.

Ushauri #10: Husipambane peke yako. Binadamu ni viumbe ambao tunaishi katika makundi ya kijamii. Kama una familia hakikisha wanakuwa washirika wako wa karibu katika yale ambayo unafanya. Hata hivyo, unatakiwa kuhakikisha unajenga mtazamo wao ili wote muwe na fikra zinazofanana. Mshirikishe mwenza wako, washirikishe watoto au mshirikishe rafiki wa karibu sana.

Mwisho, katika Makala hii nimekushirikisha mambo 10 ya kuzingatia kwa ajili ya kuwa na mwaka 2021 wenye mafanikio. Lakini katika yote nakukumbusha umuhimu wa kumtanguliza Mungu ili yote unayofanya yawe na kibali mbele ya macho yake. Namalizia kwa kukutakia kila lenye heri katika mwaka mpya 2021. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

 


HAWA NDIYO WEZI 4 KWENYE UZALISHAJI WAKO.

NENO LA LEO (AGOSTI 4, 2020): HAWA NDIYO WEZI 4 KWENYE UZALISHAJI WAKO.

πŸ‘‰πŸΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Hongera kwa asubuhi hii ya leo ambayo ni matumaini yangu kuwa umeamka salama. Ni wakati ambao tuna deni la kusema asante kwa Muumba wetu kutokana na baraka ambazo zimetufikisha siku hii ya leo tukiwa na nguvu na hamasa ya kuendelea kuwa bora zaidi. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza wezi wanne ambao wamekuwa wakikwamisha uzalishaji wetu kwenye sehemu ya kazi au biashara. Tunatambua kuwa mafanikio ni zao la mhusika kuzalisha matokeo yasiyo ya kawaida (extraordinary results) ikilinganishwa na wengine wanaomzunguka. Ili uweze kutoa matokeo yasiyo ya kawaida ni lazima utambue athari ya hawa wezi wanne ambao ninakushirikisha katika makala ya leo:-

✍🏾 Mwizi #1: Kushindwa kusema hapana – Uwezo wa kusema hapana kwenye vitu ambavyo viko nje ya kipaumbele chako ni kipimo cha kuongeza uzalishaji unaotamani. Kila mara utapata vishawishi vinavyokuta uachane na jambo moja ambalo ulikusudia kufanya katika muda maalum ambao umeutenga. Wapo marafiki watahitaji msaada kutoka kwako; wapo watu ambao watahitaji maongezi na wewe; wapo ambao watahitaji ushauri wako; wapo ambao watahitaji mkutane sehemu kwa ajili ya kinjwaji; na wapo ambao watakuhitaji kwa ajili ya mchezo ambao umezoea. Kwa ujumla vishawishi vya kukutoa kwenye kazi ambayo umekusudia kufanya ni vingi kiasi kwamba kama hauwezi kusema HAPANA hautoweza kuendelea na kazi husika. Kadri unavyosema NDIYO kwenye jambo ambalo halikuwa kwenye ratiba yako ni sawa na kusema HAPANA kwenye jambo ambalo ulikusudia kutekeleza katika muda husika. Kumbe, kipaumbele chako kinatakiwa kusema NDIYO kwenye jambo ambalo limeainishwa kutekelezwa katika muda husika na mengine yote husione aibu kusema HAPANA.  Mchekeshaji Bill Cosby aliwahi kunukuliwa kuwa: “sijui ufunguo wa mafanikio ni upi lakini ninachojua ufunguo wa kutokufanikiwa ni kujaribu kumridhisha kila mtu”. 

✍🏾 Mwizi #2: Uoga wa kero – Unapochagua kuishi kwa ajili ya uzalishaji wenye tija yapo mengi ambayo hayatakuwa sehemu ya maisha ya maisha yako. Tafsiri yake ni kwamba yapo ambayo yataonekana kuwa kero kwa vile hujayafanyia kazi. Hali hii inatokana na ukweli kwamba, kadri unavyowekeza muda wako kwa ajili ya uzalisha yapo matukio mengi kwenye jamii ambayo utaona siyo kipaumbele chako. Hali hii itakufanya matukio hayo yaonekane kuwa kero kwako n ahata jamii inayokuzunguka. Hivyo, uoga wa kero ni mwizi mwingine ambaye anaathiri uzalishaji wako. 

✍🏾 Mwizi #3: Tabia mbaya kwa afya yako – Afya bora ina uhusiano mkubwa na uzalishaji wa hali ya juu. Mwili wenye afya njema una uzalishaji mkubwa ikilinganishwa na mwili wenye afya mgogoro. Hivyo tabia ambazo zinadhohofisha afya ni mwizi mkubwa wa uzalishaji katika kutekeleza kusudi la maisha yako. Baadhi ya tabia ambazo zinadhoofisha afya ni pamoja na kukosa muda wa kutosha wa kupumzika; kushindwa kula kwa wakati au kutokula kabisa; kuendekeza vinjwaji vikali; kupenda kula ovyo bila kuzingatia mahitaji ya mwili; uvutaji sigara; pamoja na kutokuwa na muda wa mazoezi. 

✍🏾 Mwizi #4: Mazingira Siyo Mazuri kwa ajili ya malengo yangu kuanza – Mazingira yanajumuisha watu wote unaonana nao pamoja na uzoefu wa majukumu yako kila siku. Hivyo, unapotaja mazingira kuhusiana na malengo yako unamaanisha watu wanaokuzunguka kila siku pamoja na sehemu unazokuwa kwenye mzunguko wa siku nzima. Tafsiri yake ni kwamba ili uongeze uzalishaji ni lazima uhakikishe watu wanaokuzunguka pamoja na vitu au sehemu zinazokamilisha mzunguko wako wa siku ziwe upande wa kufanikisha malengo yako. Hapa ni lazima uhakikishe unazungukwa na watu wenye mtazamo chanya sawa na wako vinginevyo ukiruhusu watu wenye mtazamo hasi ni rahisi na wewe kuiga tabia zao. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mtazamo una athari kwenye tabia na hatimaye afya na matokeo yake ni kwenye uzalishaji wa mhusika. 

Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza sehemu nne ambazo tunaweza kuzitumia kuongeza uzalishaji katika maisha yetu ya kila siku. Kumbuka pale matokeo yanapokuwa kinyume na matarajio yakow ewe ndo mhusika mkuu wa kujilaumu kwa kuwa umejikwamisha mwenyewe. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika maisha yako yatabadilika. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu
πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 


πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com