[UFUNUO] FAHAMU KUWA PESA HAINA THAMANI

NENO LA LEO (NOVEMBA 11, 2020): [UFUNUO] FAHAMU KUWA PESA HAINA THAMANI

πŸ‘‰πŸΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Hongera kwa siku nyingine mpya katika uhai wetu hapa Duniani. Ni siku ambayo tuna wajibu wa kuendelea kuwa bora ili maisha yetu yawe ya thamani kwa manufaa ya nafsi zetu na jamii inayotuzunguka. Basi kila mmoja wetu aseme "hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii ili nipate yaliyo bora katika maisha."

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.   

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza ni kwa namna gani pesa haina thamani. Katika makundi ya kijamii kwa sasa ni vigumu kueleweka pale unaposema pesa haina thamani. Hali hii inatokana na ukweli kwamba toka pesa ilipogunduliwa imeendelea kutumika kama nyenzo ya kubadilishana kati ya huduma/bidhaa na kipimo cha pesa. Pesa imekuwa msingi wa watu katika jamii kufanikisha mahitaji yao.

✍🏾 Hata hivyo, ukweli unabakia kuwa "thamani ya pesa ni pale inapotumika kufanikisha upatikanaji wa vitu vyenye thamani". Vile vile, tunaweza kusema kwamba uthamani wa pesa ni pale pesa husika inapokuwa kwenye mzunguko. Tafsiri yake ni kwamba ikiwa pesa haitumiki kupata vitu vya thamani pesa hiyo haina thamani. Mfano, unaweza kupata milioni leo hii na katika hali ya kawaida ukaiona ni pesa nyingi, cha kushangaza milioni hiyo ukiiweka kwenye matumizi ghafla utajikuta inaisha ndani ya dakika chache tu.  

✍🏾 Ikiwa pesa haitumiki kununua vitu vyenye thamani au kuwekezwa sehemu ambapo thamani yake inaongezeka moja kwa moja pesa hiyo inayeyuka kana kwamba haikuwahi kuwepo mikononi mwako. Jiulize kiwango cha juu cha pesa ambacho umewahi kupata na jinsi ulivyotumia pesa hiyo. Ikiwa hauwezi kuiona pesa hiyo katika wakati wa sasa moja kwa moja ni dhahiri kuwa pesa hiyo uliitumia kwenye vitu ambavyo havina thamani.

✍🏾 Hapa ndipo wanafanya makosa kwa kuweka mipango ya kiwango cha pesa ambacho wanahitaji kupata badala ya kuweka mipango ya vitu vya thamani ambavyo wanahitaji kumiliki maishani mwao. Unatakiwa kuainisha mahitaji yako ya msingi katika maisha na kupitia mahitaji hayo ndipo unapata kiwango cha pesa ambacho unahitaji. 

✍🏾 Mwisho, neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa pesa haina thamani na badala yake thamani ya pesa ipo kwenye vitu unavyonunua kupitia pesa husika. Pia tumeona kuwa lengo kubwa katika safari ya pesa linatakiwa liwe kwenye mahitaji ya msingi ambayo unatamani kumiliki kama vile ardhi, viwanda, nyumba, biashara, umiliki hisa au uwekezaji kwenye mifuko ya uwekezaji wa pamoja na uwekezaji kwenye hati fungani za Serikali. Kumbuka, mbegu ikidondoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(