👉🏾Habari ya asubuhi hii rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi nyingine ambayo inatupatia nafasi ya kuanza mwezi wa pili katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2020. Hamasa na nguvu za kutosha ndiyo silaha kubwa ambayo itatuwezesha kuitumia siku hii ya kipekee ambayo ameifanya Bwana. Tuitumie siku hii kwa kuwa na furaha ya nafsi na roho, tumshukuru na kuendelea kusimamia kanuni muhimu za maisha yetu ambazo tunaziishi kwa ajili ya kufikia kusudi la maisha yetu.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo kipekee nawapongeza wafanyakazi wote wa sekta za ajira zilizo rasmi pindi wanaposherekea Siku ya Wafanyakazi wote Duniani. Siku hii ni maalumu kwa ajili ya wafanyakazi kupaza sauti zao kwa waajiriwa wa setka zote ili wasikie kilio, ushauri na mapendekezo wa waajiriwa wao. Ni siku ambayo vyama mbalimbali vya wafanyakazi vinapaaza sauti kwa niaba ya wanachama wao. Hakika ni siku muhimu ambayo waajiri wanapata kufunuliwa hali kuhusu mtazamo wa waajiriwa wao kuhusu kazi wanazifanya kila siku kwenye majukumu yao ya kazi.
✍🏾Baada ya kusema hayo ewe mfanyakazi naomba utafakari haya: Mosi, Je unaipenda kazi unayofanya? Ukweli ni kwamba uzoefu katika jamii tunayoishi wafanyakazi wengi hawapendi kazi walizoajiriwa nazo. Kundi la kwanza linahusisha wafanyakazi wanaopata mshahara mzuri pamoja na malupulupu lakini hawana Uhuru katika maisha yao. Mfano, wafanyakazi wengi kwenye sekta ya Afya na mashirika yasiyo ya Serikali (NGOs) ukiwahoji kuhusu kuipenda kazi yao, asilimia kubwa watakuambia kuwa kazi hiyo inawafanya muda mwingi wasiwe uhuru kutimiza majukumu muhimu kwenye sekta nyingine za maisha.
✍🏾Kundi la pili linahusisha wafanyakazi ambao hawaridhiki na kiasi wanacholipwa lakina hawana namna ya kufanya hivyo kila mara wanaenda kwenye vituo vya kazi wakiwa wananungunika na msongo wa mawazo. Kwa ujumla katika makundi yote mawili tunajifunza kuwa watu wengi hawafanyi kazi za majukumu yao ya kila siku kutokana na msukumo/dhamira kutoka ndani na badala yake wanafanya kazi kwa ajili ya pesa. Kwa maneno mengine watu wanauza uhuru wao kwa ajili ya pesa.
✍🏾 USHAURI, kuanzia sasa tafakari juu ya mapenzi uliyonayo kwenye kazi unayofanya. Kama haupendi kazi unayofanya ni vigumu kazi kukupatia mafanikio unayotamani katika maisha yako. Kumbuka kazi ni kipimo cha mafanikio. Robin Sharma katika kitabu chake cha The Greatness Guide aliandika "kuwa kama unahitaji kufanikisha chochote katika maisha yako ni lazima uanze kuipenda kazi yako. Kama wewe ni mfagiaji wa mtaa tekeleza majukumu yako kama mfagiaji bora aliyewahi kutokea Dunia nzima". Unapoipenda kazi yako inakisaidia kutimiza majukumu yako kiasi ambacho mafanikio katika kutekeleza majukumu hayo yataongea juu yako katika jamii unayoishi. Kwa kufanya hivyo utanyanyuliwa ngazi za juu na nguvu za asili bila ya wewe kutumia nguvu kubwa. Kumbe katika kila unachofanya kwenye majukumu yako ya siku hakikisha unaweka thamani kwanza badala ya kufanya kazi ili mradi tu siku ziende haraka kuelekea mwisho wa mwezi.
✍🏾 Mbili, kazi unayofanya una mpango gani nayo kwa siku za baadaye?. Nimeandika hapo juu kuwa uzoefu unaonesha watu wengi hawaridhiki na kazi zao. Hali inapelelekea kundi kubwa la watu kuendelea kuishi hisia hasi (chuki, hasira, hofu, msongo wa mawazo) katika maisha yao ya kila siku. Matokeo ya hali hii ni kuendelea kuongezeka kwa magonjwa mbalimbali ambayo chanzo chake ni hisia hasi kwa wahusika. Hata hivyo, pamoja na watu kutoridhika na kazi wanazofanya ni wachache sana wanaoamua kubadilisha kazi au kuacha na kujiajiri wenyewe.
✍🏾 USHAURI, Kuwa na mangokazi ambao unautekeleza kila siku kwa ajili ya kuiboresha kazi yako. Timiza majukumu yako kana kwamba haufanyii malipo bali unatimiza matakwa ya msukumo/dhamira yako ya ndani kuhusu kazi husika. Kama unaona kazi yako ya sasa itakuchelewesha kufikia kwenye matamanio ya maisha yako anza sasa kuweka mkakati wa kukuwezesha kuachana na kazi hiyo (exit strategy) ili uweze kuishi maisha yenye Uhuru unaoukosa sasa.
✍🏾 Tatu, nyongeza ya mshahara na kupanda vyeo havijawai kuwa tiba ya matatizo ya kifedha kwa wafanyakazi. Kilio kikubwa cha wafanyakazi wengi siku ya leo ni kutaka waajiri wawaongezee mishahara, malupulupu ya kazi na kupandishwa vyeo. Ukweli ni kwamba vyote hivyo siyo TIBA halisi ya matatizo yako ya kifedha. Hali inatokana na tabia ya wafanyakazi wengi kupandisha gharama za maisha kulingana na ongezeko la mishahara au malupulupu katika sehemu za kazi.
✍🏾 USHAURI, badala ya kusubiria kupandishwa mshahara fikiria uanzishe mradi gani ambao utausimamia kwenye muda wako nje ya masaa ya mwajiri. Unaweza kuanzisha kilimo cha bustani au mazao ya chakula, unaweza kufungua biashara, unaweza kufuga au kuanzisha huduma ya ushauri kulingana na taalamu au uzoefu wako katika kazi.
✍🏾 Nne, ilinde sana pesa yako. Ukweli ni kwamba kazi uliyoajiriwa ni ya muda tu kwa maana kuna kustaafu, kuachishwa kazi au kupata majanga ya kidunia ambayo yatakufanya ushindwe kuendelea na kazi. Hapa ndipo unatakiwa kukumbuka kuwa kazi yako katika familia ni YAKO tu na hakuna anayweza kuirithi hila kile unachopata kama malipo yako endapo kitatumiwa vyema kitarithishwa katika vizazi vyako.
✍🏾 USHAURI, epuka mikopo yenye asilimia kubwa ya riba au kukopa bila mpangilio. Unapohitaji kukopa hakikisha umejiridhisha kuwa mkopo huo utalipwa kwa fedha za wengine kwa maana ya mkopo ulipwe kutokana na faida inayotengenezwa kutoka uwekezaji ambao umeufanya baada ya kuchukua mkopo.
✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo nasaha muhimu si tu kwa wafanyakazi katika sekta rasmi bali kwa wafanya kazi wote. Mbegu ikidondoka ardhini ni lazima iote na kujua zaidi nami naiombea mbegu niliyoidondosha ipate kuota na kubadilisha maisha ya watu wengi katika jamii. Kwa nini mpaka sasa haujajipatia nakala ya uchambuzi wa kitabu cha ‘Kanuni za Pesa”?. Nakala ya uchambuzi wa kitabu hiki bado inapatikana kwa bei ya Ofa ya Tshs. 5,000/= na ndani ya nakala hiyo utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa namna ya kutengeneza, kuwekeza na kutumia pesa.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(