NENO LA LEO (MEI 02, 2020): [HUSISHANGAE] NDIVYO WATU WALIVYO

👉🏾Habari ya asubuhi hii rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi ya kipekee ambayo tumezawadi tena kwa ajili ya kuendeleza bidii zinazolenga kutufikisha kwenye mafanikio ya lengo kuu la maisha yetu. Muhimu in kwamba hatupaswi kupoteza hamasa katika siku hii aliyoifanya Bwana bali tufurahi, tumshukuru na kuitumia vyema katika kufikia kusudi kuu la maisha yetu.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha jinsi wanadamu walivyo. Unapoamua kuishi maisha yanayofuata kanuni za mafanikio hakuna nyingine zaidi ya kuelewa kwa undani tabia na saikolojia ya watu wanaokuzunguka katika jamii unayoishi. Kupitia makala hii hebu jaribu kutafakari ukweli wa tabia za wanadamu jinsi walivyo:-

✍🏾 Ukweli Na. 1: Fanya mema 100 lakini jambo 1 baya litafuta mema yako yote. Kwa ujumla watu wanahitaji uwatendee mema pekee na katika kutenda mema hayo husitegemee kupokea mema kutoka kwa unaowatendea.

✍🏾 USHAURI, husipambane kuwaridhisha watu badala yake pambana kutimiza malengo uliyojiwekea kwenye kila sekta ya maisha yako.

✍🏾 Ukweli Na. 2: Kumbuka watu watajiuliza mara mbili kuhusu uhalali wa mafanikio yako lakini cha ajabu wataamini mara moja bila kujiuliza zaidi pale wanaposikia kuwa umetenda kosa. Huyo ndiyo mwanadamu mara zote anaishi kwa wivu dhidi ya watu wanaomzunguka. Mwanadamu hataki kuona anazidiwa na mwenzake kimafanikio bila kujali utofauti wa mbinu na jitihada wanazoweka kwenye kazi.

✍🏾 USHAURI, husiumizwe na maneno ya uongo yanayoenezwa dhidi yako kwa ajili ya kuchafua jina lako. Ziba masikio na endelea kupiga kazi ili mafanikio yako yaendelee kuwaziba midomo.

✍🏾 Ukweli Na. 3: hakuna anayeuliza mbinu ulizotumia kufikia ngazi za mafanikio uliyonayo zaidi wanachojadili ni matokeo uliyonayo kwa sasa. Kwa kuwa hakuna anayehitaji kujua mbinu ulizotumia kuwa tayari kusikia kila aina uongo unaopakaziwa kwa ajili ya kuharamisha mafanikio yako.

✍🏾 USHAURI, endelea kuwa msiri kwenye mbinu unazotumia kufikia mafanikio makubwa katika maisha. Toa siri hizo kwa baadhi ya watu ambao hakika unaona kuwa wanahitaji kufikia pale ulipofikia. Badala ya kuwapa samaki watu wa hiyo wafundishe namna ya kuvua samaki.

✍🏾 Ukweli Na. 4: kuwa tayari kukataliwa na kupingwa kuhusu imani na kanuni ambazo umejiwekea kuhusu maisha. Hakuna anayejisumbua kutafuta imani na kanuni mpya kuhusu maisha yenye mafanikio. Wengi wanaendelea kuishi katika imani na mbinu za maisha ambazo zimekuwepo toka enzi za mababu zao na mbinu hizo hazikuleta tija katika kipindi cha uhai wao. Kwa wengi hawajusumbui kuumiza kichwa na wanahitaji maisha laini au mafanikio ya haraka wanaendelea kujifunga ndani ya imani na mbinu hizo bila kufahamu kuwa Dunia inakimbia kwa kasi   na kupelekea mambo mengi kupitwa na wakati.

✍🏾 USHAURI, endelea kujielimisha kila mara ili upate maarifa, imani na kanuni mpya kuhusu namna ya kufikia mafanikio unayotamani.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limetukumbusha baadhi ya kweli ambazo tunatakiwa kuzijua kuhusu wanadamu wenzetu tunaoishi nao. Husishangae matendo hayo ya wanadamu bali endelea kujielimisha zaidi kuhusu tabia na saikolojia za mwanadamu. Kumbuka, mbegu ikidondoka ardhini ni lazima iote na kukua zaidi nami naiombea mbegu niliyoidondosha siku ya leo ipate kuota na kubadilisha maisha ya watu wengi katika jamii. Kwa nini mpaka sasa haujajipatia nakala ya uchambuzi wa kitabu cha ‘Kanuni za Pesa”?. Nakala ya uchambuzi wa kitabu hiki bado inapatikana kwa bei ya Ofa ya Tshs. 5,000/= na ndani ya nakala hiyo utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa namna ya kutengeneza, kuwekeza na kutumia pesa.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(