NENO LA LEO (MEI 10, 2020): FAHAMU KWA NINI HAUKUZALIWA KUWA MTU WA WASTANI WALA MASIKINI

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya katika Maisha yetu ambayo tumepewa kibali kwa ajili ya kuendeleza pale tulipoishia jana. Ni zawadi ya kipekee katika Maisha yetu hasa tunapoendelea tunapotambua kuwa ukamilisho wa Maisha yetu ni pale tunapojitoe kuishi Maisha ya thamani kwa viumbe vinavyotuzunguka. Basi kwa pamoja tuianze siku kwa kusema hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana, tufurahi, tumshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuliishi kusudi la maisha yetu.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha jinsi ambayo umekuwa ukiishii Maisha ya wastani au kimasikini wakati hayo siyo Maisha uliyoumbiwa. Uliumbwa na kupewa mamlaka ya kutawala viumbe vyote vya angani, baharini na nchi kavu. Zaidi ya mamlaka yako yanakuwezesha kutumia kila kilichoumbwa kwa ajili ya kukuwezesha kuishi Maisha yenye furaha na amani. Hata hivyo kutokana na njia ambayo kila mtu ameifuata amejikuta akipoteza mamlaka hayo ambayo ni kurithishwa vizazi na vizazi. Pamoja na kupoteza mamlaka hayo, mhusika anapojitambua kuwa yeye ni nani na ameumbwa kwa ajili ya kufanya nini hapa Duniani anapata nafasi mpya ya kurejesha mamlaka aliyopoteza.

Tumia mbinu hizi nne kurejesha mamlaka ya kiutawala ambayo umepewa toka enzi za kuumbwa kwako:-

✍🏾 Mbinu #1: Acha kabisa tabia ya kuridhika na hali uliyonayo. Kila mara unakiwa uwe na kiu ya kuwa bora zaidi. Maisha yanakuwa na thamani pale ambapo kila siku unatamani kuongezeka zaidi ya ulivyokuwa jana (Life is worthy if we seek the expression of increasing more). Haijalishi kwa sasa unateseka kiasi gani kutokana na changamoto za Maisha, muhimu ni kuendelea kuwa na tumaini kuwa changamoto hizo ni za muda na kesho iliyo bora ipo inakusubiria. Hapa ndipo unatakiwa kuachana na tabia ya kulinganisha mafanikio yako na watu wengine na badala yake hakikisha unajiwekea viwango binafsi ambavyo vinakusukuma kuendeleza ubora katika kile unachofanya.

✍🏾 Mbinu #2: Hakikisha unakuwa mlevi wa mambo yanayofanywa na waliofanikiwa. Mafanikio ya maisha yako ya baadae ni matokeo ya tabia na maamuzi yako ya sasa. Ulevi wa tabia mabaya ni adui namba moja kwa watu wanaotaka kufikia mafanikio makubwa sana katika maisha yao. Kwa ufupi ulevi huu ni kati ya visababishi ambavyo vimekufanya upoteze mamlaka yako ya kiutawala. Hata hivyo, ulevi wa aina hiyo unaweza kuubadilisha na kuwa na ulevi wa kuishi tabia za watu wenye mafanikio. Kila mara Maisha yako yanatakiwa kutawaliwa na kiu ya matamanio ya mafanikio makubwa katika Maisha (Be obsessed with the desire for success).

✍🏾 Mbinu #3: Ruhusu macho yako ya ndani kuona fursa zinazokusubiria. Kadri mtu anavyobadilisha maisha ya ulevi wa mambo mabaya na kuelekea kwenye ulevi wa mafanikio ndivyo macho yake ya ndani yanavyoanza kuona fursa nyingi ambazo awali hakuwahi kuziona au kuhisi kama zinawezekana. Ipo hazina kubwa ndani mwako ambayo haijatumiwa kuwa bado haujajisumbua kuitumia hazina hiyo. Siku unapoanza kuishi misingi ya mafanikio ndipo utashangaa kuona jinsi fursa nyingi zitakavyoanza kumiminika zaidi na zaidi. Na kadri utakavyokuwa mlevi wa tabia/misingi ya mafanikio ndivyo utashangaa unaanza kupendwa na watu wengi ikilinganishwa ule ulevi wa tabia mbaya.

✍🏾 Mbinu #3: Kila siku toa thamani kubwa kupitia kazi yako kuliko malipo unayopokea. Hauwezi kufanikiwa kama haujibidishi na kazi na siyo kazi bora kazi tu bali kazi inayokuwezesha kufanikiwa ni ile ambayo ina thamani kubwa kwa walengwa/watendewa. Kumbe, mafanikio yanapatikana kutokana na yale tunayoyafanya kila siku. Na hayo tunayoyafanya kwa njia moja au nyingine ni lazima yaguse Maisha ya watu wengine. Na kadri unavyogusa Maisha ya watu wengi zaidi ndivyo na huduma zako zinavyopendwa zaidi. Hivyo, tunaweza kutumia thamani tunayoitoa kupitia kazi zetu kama sumaku ya kuvuta watu wengi kwa kadri iwezekanavyo katika huduma zetu.

✍🏾 Mbinu #4: Tambua kuwa matamanio ya mafanikio kimaisha ni zawadi ambayo kila mmoja amerithishwa. Ili zawadi iwe na tija ni lazima itumiwe na mhusika. Unaanza kutumia zawadi hii kwa kufanya maamuzi ya kuondokana na maisha ya kuwa mtu wa kawaida/masikini. Hapa unatakiwa kuamua kuwa gharama zozote ni lazima urejeshe mamlaka uliyopoteza ili uishi maisha ya stahili yako kwani hayo ndiyo Maisha ambayo Muumba alikusudia kwako. Na kadri utakavyoishi maisha haya ndivyo utajitenga na wale ambao wanaishi maisha ya ulevi wa mambo mabaya na kujikuta katika ulimwengu wa watu wenye ulevi wa matamanio ya maisha ya mafanikio tu.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limetufunulia mbinu mbalimbali ambazo kila mtu anaweza kuzitumia kwa ajili ya kufikia matamanio ya mafanikio katika maisha yake. Maamuzi yapo mikononi mwako kuamua kuishi Maisha ya kawaida/umasikini au kurejesha urithi wa mamlaka ya kutawala ambao ulipewa toka enzi za kuumbwa kwako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

👀 Kwa nini mpaka sasa haujajipatia nakala ya uchambuzi wa kitabu cha ‘Kanuni za Pesa”?. Nakala ya uchambuzi wa kitabu hiki bado inapatikana kwa bei ya Ofa ya Tshs. 5,000/= na ndani ya nakala hiyo utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa namna ya kutengeneza, kuwekeza na kutumia pesa.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias 
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(