👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni kwa mara nyingine tumepewa kibali cha kuendeleza bidii zinazolenga kuyafanya maisha yetu yawe na thamani hapa Duniani. Ni katika asubuhi hii ninakusisitizia umuhimu wa kuwa na hamasa binafsi ili husikatishwe tamaaa na mtu yeyote. Basi kila mmoja aianze siku kwa kusema hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha umuhimu wa kujiamini hasa katika wazo ulilonalo kichwani. Kabla ya kukushirikisha neno la tafakari ya leo hebu kwa pamoja tuangalie mfano mmoja kutoka kwenye kitabu cha Think and Grow Rich cha Napoleon Hill. Wengi wetu tutakuwa tunafahamu magari aina ya V8, magari haya yanatengenezwa na kampuni ya Ford iliyoko Marekani. Henry Ford ambaye ndiye aligundua magari haya baada ya kupata wazo la kutengeneza injini yenye silinda nane, Wataalamu (Waandisi) wake walimkataliwa kuwa haiwezekani silinda zote hizo kukaa katika injini moja.
✍🏾Baada ya Waandisi kumpa hilo la kuwa HAIWEZEKANI, Henry Ford alichowajibu ni kwamba yeye anaamini inawezekana na kila mmoja katika kitengo hicho ana wajibu wa kuhakikisha hilo gari la aina hiyo linatengenezwa. Moja kwa moja wataalamu wakaanza kulifanyia kazi. Baada ya miezi 6 wakampa jibu kuwa IMESHINDIKANA, Henry Ford akawajibu hataki kusikia jibu kama hilo bali anachohitaji ni kusikia wamefanikisha plani aliyowapa. Hawakuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kubuni namna yakufanikisha kutengeneza injini yenye silinda 8. Baada ya miezi kadhaa wakafanikiwa kwa mara ya kwanza kutengeneza injini yenye silinda 8 na ikawa mwanzo wa kuingiza sokoni magari aina ya V8.
TUNAJIFUNZA NINI KATIKA MFANO HUU
✍🏾 Moja, ukiwa na wazo jipya kuwa tayari kupingwa. Tunaishi katika Ulimwengu wenye watu ambao hawataki kusumbua vichwa hivyo kila lililojipya kwao wanaona HALIWEZEKANI. Hapa ndipo unatakiwa kujiamini katika wazo lako kuwa ni wazo hai ambalo litafanikiwa.
✍🏾 Mbili, umuhimu wa msimamo husiyoyumbishwa. Mara nyingi kwa kutokuwa na msimamo tumejikuta tumepoteza mawazo ambayo yangebadilisha maisha yetu kwa ujumla. Tumekubali kuwasikiliza walimwengu ambao wametuaminisha kuwa tunachowaza ni ndoto za mchana. Henry Ford hakuwa tayari kuyumbishwa na Wataalamu wake bali msimamo wake uliendelea kuwa hai mpaka wazo lake likajidhihirisha katika uhalisia wake.
✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limetukumbusha umuhimu wa kuishi katika wazo ulilonalo hadi pale ambapo litafanikiwa. Hata hivyo, ili ufanikishe wazo lako hauna budi kukataa vishawishi vyote ambavyo vinalengo la kukutoa kwenye mstari. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
👀 Kwa nini mpaka sasa haujajipatia nakala ya uchambuzi wa kitabu cha ‘Kanuni za Pesa”?. Nakala ya uchambuzi wa kitabu hiki bado inapatikana kwa bei ya Ofa ya Tshs. 5,000/= na ndani ya nakala hiyo utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa namna ya kutengeneza, kuwekeza na kutumia pesa.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(