NENO LA LEO (MEI 08, 2020): ULIZALIWA TAJIRI HILA IMANI HIZI KUHUSU PESA ZIMEPOTEZA UTAJIRI WAKO

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi ya kipekee ambayo tumezawadiwa kwa mara nyingine tena ili kuendeleza pale tulipoishia jana. Ni wakati kama huu nasema asanthe kwa Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuamka salama ili niendelee kutengeneza ushindi mdogo mdogo katika kila sekta ya maisha yangu. Sina maneno mengine kwa Muumba zaidi ya kusema hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana, sina budi kufurahi, kumshukuru na kuitumia vyema kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha jinsi kauli ulizofundishwa kutoka kwa ulimwengu zimekufanya upoteze utajiri uliorithishwa toka enzi ulipozaliwa. Katika neno la tafakari ya jana tuliona jinsi ambavyo kila mtoto anazaliwa akiwa na uwezo wa hali ya juu kwenye kila sekta ya maisha yake. Hata hivyo, tuliona kadri mtoto anavyokua ndivyo uwezo wake unazidi kuathiriwa na ulimwengu kutokana na aina ya malezi, mazingira anayokulia na mafundisho anayopata kutoka kwa watu wote wanaomzunguka. Katika neno la tafakari ya leo hebu kwa pamoja tujifunze jinsi kauli hizi kuhusu pesa zilivyopoteza utajiri wako:-

✍🏾 Kauli #1: Ili utengeneze pesa unatakiwa kuwa na pesa. Kauli hii imepoteza uwezo wa watu wengi katika kuthubutu kuanzisha mipango ya kifedha kwa kuwa kila mara wanajiona hawana pesa za kutosha kwa ajili ya kuanzisha mradi wanaoufikiria. Hivyo, kauli hii inakandamiza uwezo wa kubuni na kuanzisha vitu vipya kutoka kwenye vitu vinavyotuzunguka (asili).

✍🏾 Kauli #2: Kupenda sana pesa ni uovu. Kauli hii imekandamiza uwezo wa watu wengi kwa kuwa wanaepuka kuonekana warafi, wachoyo na wenye tamaa ya kupindukia katika jamii inayowazunguka. Chanzo kikuu cha kauli hii ni kutoka kwa wazazi au walezi kutokana na imani waliuonayo kuhusu pesa. Kama mzazi/ mlezi ni masikini matokea yake na ni kumjaza mtoto wake kila aina ya hofu alizonazo kuhusu pesa.

✍🏾 Kauli #3: Pesa ni kwa ajili ya watu wachache waliobarikiwa kuwa nazo. Kauli hii imetufanya tuamini kuwa kuna watu wachache walioumbwa kwa ajili ya kumiliki pesa nyingi kwa kadri wapendavyo na kundi kubwa la watu limeumbiwa umasikini. Hii ni kauli kandamizi ambayo kila inakufanya uone uchache (scarcity) wa pesa hivyo kujiona kuwa hauwezi kupata pesa za kutosha. Matokeo yake ni kuanzia kuridhika na uchache wa pesa unazopata na kujifariji kuwa siyo lazima wote tuwe matajri. Kuanzia sasa kataa kauli hiyo kwa kuwa tumeumbwa kuishi maisha ya utajiri.

✍🏾 Kauli #4: Ili uwe tajiri ni lazima ujitoe nafsi au uwe mchawi. Kauli hii inatifanya tuwaone Matajiri kuwa ni watu wabaya kwa kuwa wameuza nafsi zao kwa majini au msema uliozoeleka katika jamii yetu ya sasa ni FREE MASONRY. Ukweli ni kwamba unaweza kuwa tajiri bila kuuza nafsi yako.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limetukumbusha kuwa wote tulizaliwa tukiwa tajiri hila imani tulizopata zimetufanya kupoteza utajiri wetu. Ni muda muhafaka wa kutafakari kuhusu imani na mtazamo wetu kuhusu pesa. Kumbuka, mbegu ikidondoka ardhini itaota na kuzaa matunda, nami naiombe mbegu hii niliyoidondosha leo ipate kuzaa matunda katika maisha yako. Kwa ni mpaka sasa haujajipatia nakala ya uchambuzi wa kitabu cha ‘Kanuni za Pesa”?. Nakala ya uchambuzi wa kitabu hiki bado inapatikana kwa bei ya Ofa ya Tshs. 5,000/= na ndani ya nakala hiyo utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa namna ya kutengeneza, kuwekeza na kutumia pesa.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(