NENO LA LEO (MEI 11, 2020): JIFUNZE KUISHI KWA UKAMILIFU NDANI YA MASAA 24 KILA SIKU

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi nyingine katika wiki nyingine ambayo tunazawadiwa katika Maisha yetu kwa ajili ya kuendeleza bidii inayolenga kuyaboresha maisha yetu. Ni asubuhi hii naendelea kukusitiza uendelee kuthamini umuhimu wa ushindi mdogo mdogo ambao unatengenezwa kila siku. Basi kila mmoja aianze siku kwa kusema hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuliishi kuongeza thamani ya maisha yangu.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha umuhimu wa kuishi maisha ya ukamilifu kwenye masaa 24 kila siku ambayo unazawadiwa uhai katika maisha yako. Muda ni rasilimali pekee ambayo binadamu wote tumepewa kipimo kimoja. Ndani ya siku wote tuna masaa 24 na katika lisaa wote tuna dakika 60. Hakuna mtu ambaye amenyimwa au anapunguziwa baadhi ya dakika kama hadhabu kutokana na tabia ya kupoteza muda.

✍🏾Hata hivyo, pamoja na kupewa kipimo sawa wote tunafahamu kuwa yale ambayo binadamu wanafanya kwenye ratiba yao ndiyo yatofautisha viwango vyao vya mafanikio. Tumezoea kusikia kauli kama vile: "muda ni pesa" au "muda ni mali". Kauli zot hizi zinauhalisia katika maisha yetu kutokana na ukweli kwamba hakuna kinachoweza kufanyika bila ya uwepo wa muda.

✍🏾Pia tunafahamu kuwa katika jamii wapo watu ambao kila kukicha ndani ya kila  SAA katika ratiba yao wapo bize lakini bado wanaangaika kimafanikio. Hiki ni kiashiria kuwa kwetu kuwa siyo tu suala la kuwa bize kwenye kila dakika ndani ya masaa 24 bali ni suala la kujiuliza upo bize kwa kufanya nini. Kumbe, katika maisha tunatakiwa kufahamu kuwa tunafanikiwa kutumia rasilimali muda pale tu tunapotekeleza majukumu yenye tija maisha yetu.

✍🏾Pia tunafahamu kuwa lipo kundi kubwa la watu ambalo kila mara linajutia makosa ya awali ambayo yalipelekea kupoteza muda mwingi katika historia ya maisha yao. Mbaya zaidi wengi katika kundi hili ni wale ambao wanateswa na historia yao lakini hawapo tayari kubadilika. Wanaendelea kujiadhibu kiasi ambacho matukio waliyofanya huku nyuma yanakuwa mzigo wa kuendeleza kuharibu muda uliobakia katika kipindi cha uhai wao hapa Duniani. Hili ni tatizo kwa kuwa maisha hayana thamani kama tunaishi kwa kuumizwa na historia.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limetukumbusha umuhimu wa kuishi kulingana na muda tulionao. Tusiishi kulingana na matukio ya yaliyopita kwa kuwa hatuna mamlaka tena ya kubadilisha muda uliopita hila mamlaka tulionao ni kupangilia vyema muda tulionao sasa. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

👀 Kwa nini mpaka sasa haujajipatia nakala ya uchambuzi wa kitabu cha ‘Kanuni za Pesa”?. Nakala ya uchambuzi wa kitabu hiki bado inapatikana kwa bei ya Ofa ya Tshs. 5,000/= na ndani ya nakala hiyo utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa namna ya kutengeneza, kuwekeza na kutumia pesa.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(