NENO LA LEO (MEI 03, 2020): MBINU HIZI ZITAKUWEZESHA KUFANIKIWA ZAIDI

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi ya siku nyingine tena ambayo tumepewa kwa ajili ya kuendeleza pale tulipoishia jana. Ni zawadi muhimu katika Maisha yetu hasa tunapoendelea kutimiza malengo muhimu katika Maisha yetu. Kwa pamoja tuianze siku kwa kusema hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana, tufurahi, tumshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuliishi kusudi la maisha yetu.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha mbinu mbalimbali ambazo unatakiwa kuzitumia kwa ajili ya kupanua wigo wa mafanikio yako. Kwanza kabisha unatakiwa kufahamu kuwa ili uwe na mafanikio makubwa ni lazima uwe mtu wa tofauti na ufanye vitu kwa njia tofauti ikilinganishwa na watu wanaokuzunguka.

✍🏾Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa ili uwe na mafanikio ni lazima uwe mtu wa hatari katika kila eneo la maisha yako. Inabidi uwe mtu hatari kwa wapinzani wako, mtu hatari kwa wateja wako kwa kuwapatia kile wanachotaka, uwe hatari kwa mwajiri/waajiriwa wako kwa kuhakikisha unatimiza wajibu wako na kuwa mtu hatari kwa watu wako wa karibu ili waendelee kuheshimu muda wako na misingi uliyojiwekea katika maisha yako ya kila siku.

Ili uendelee kuwa mtu hatari unahitaji kufanya yafuatayo;

✍🏾 Moja, Hama kijiji/mji uliokulia na kwenda kuanzisha makazi yako mapya sehemu nyingine kwa ajili ya kupata changamoto na mitazamo mipya. Kuhama kutafanya husiwe kwenye mazingira ya kuridhika ambayo ni hatari kwa wewe kuendelea kutafuta mafanikio zaidi.

✍🏾 Mbili, Muda wote tafuta uhusiano na watu wapya. Hakikisha unatafuta uhusiano wa kikazi na watu wapya hasa waliofanikiwa zaidi yako, wahamasishaji au watu maarufu kwa ajili ya kupata changamoto na elimu mpya.

✍🏾 Tatu, fahamu kuwa mafanikio hayaji kwa kutafuta umaarufu bali endelea kuishi misingi ya maisha yako na kamwe husifanye biashara kwa kutaka uonekane mwema kwa wale unaofanya nao biashara. Kama kuna nafasi ya kuomba punguzo fanya hivyo na muda wote husionekane kuwa muhitaji sana wa bidhaa/huduma husika.

✍🏾 Nne, Kuwa tayari kuwekeza katika mazingira hatarishi (risk), husiogope kuwekeza kwa vile unaogopa risk. Hakikisha kila mara unakokotoa kiwango cha hatari unachohisi katika uwekezaji ambao unahitaji kuingia.

✍🏾 Tano, Jifunze kutumia teknolojia mpya kwa ajili ya kuboresha yale unayoyafanya. Kila mara teknolojia mpya zinagunduliwa kwa ajili ya kurahisisha Maisha ya mwanadamu. Wajibu wako kama mwanamafanikio ni kuhakikisha unatumia teknolojia mpya kuboresha misingi ya utekelezaji wa kazi zako.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limetufunulia mbinu mbalimbali ambazo kila mtu anaweza kuzitumia kwa ajili ya kukuza mafanikio yake. Kila mmoja kwa nafasi yake atafakari namna ambavyo anaweza kuzitumia mbinu hizi katika yale anayofanya kwa sasa. Kwa ni mpaka sasa haujajipatia nakala ya uchambuzi wa kitabu cha ‘Kanuni za Pesa”?. Nakala ya uchambuzi wa kitabu hiki bado inapatikana kwa bei ya Ofa ya Tshs. 5,000/= na ndani ya nakala hiyo utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa namna ya kutengeneza, kuwekeza na kutumia pesa.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(