👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi ya siku ya jumamosi ambapo naamka nikiwa na furaha, amani, hamasa na nguvu ya kipekee kwa ajili ya kuendeleza pale nilipoishia jana. Sina shaka na siku hii kwa kuwa naamini hii ndiyo aliyoifanya Bwana, wajibu wangu ni kufurahi, kumshukuru na kuitumia vyema kwa ajili ya kupata kila lililo bora katika maisha yangu.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha jinsi unaweza kufanikiwa kwenye kila sekta ya maisha yako kwa kutekeleza vitu ambavyo hinaonekana vidogo hila thamani yake katika maisha ni kubwa. Katika maisha watu wengi huwa wanathamini vitu vikubwa ambavyo mara nyingi vipo nje ya uwezo wao na kudharau vitu ambavyo vinaonekana vidogo.
Kwa pamoja karibu tupitie mbinu hizi ambazo ni za kawaida hila zinaweza kubadilisha maisha yako kwa ujumla kama utaziishi kila siku.
✍🏾 Mbinu #1: Anza kutekeleza chochote unachowaza wakati wengi wanahairisha au wanajipanga kuwa sawa. Ugonjwa wa kuhairisha au kusogeza mbele (procrastination disease) ni adui namba moja wa kufifisha au kuua ndoto za watu. Dalili za ugonjwa huu ni kila mhusika kujiona hajawa tayari kutekeleza wazo alilonalo kichwani. Matokeo yake siku zinasogea na utayari hauonekani. Hivyo, kama unahitaji kufanikisha wazo lolote tumia kauli mbiu ya kuwa "hakuna wakati ulio bora zaidi ya sasa". Bila kujali utaanza kwa hatua fupi sana muhimu ni kuanza huku ukiwa na picha kubwa kule unakotaka kufika.
✍🏾 Mbinu #2: Jifunze wakati wengine wamelala au wamefunikwa na maisha ya mazoea. Ili tuendelee kuishi kwa thamani ni lazima tuishi kwa ajili ya kujiendeleza kimwili, kiroho na kiakili. Mara nyingi watu wanaweka mikakati ya kujiendeleza kimwili na kiroho na kusahau kuendeleza upande wa kiakili ambao ndiyo msingi wa maendeleo ya sekta hizo nyingine. Kubwa ni kwamba watu waliofanikiwa kila siku ni dirisha jipya kwa ajili ya nuru ya kujifunza maarifa muhimu ya kujiendeleza kwenye kila sekta ya maisha yao. Hivyo, kama kweli unahitaji kuondokana na maisha ya kawaida na kufikia mafanikio makubwa ni lazima utenge muda wa kujifunza.
✍🏾 Mbinu #3: Fanya kazi nyakati ambazo wengine wanaishia kutamani kile unachofanya. Ni mara nyingi nimekuwa nikisisitiza kuwa kazi ni kipimo cha utu au kazi ni kipimo cha mafanikio au kazi ni kipimo cha thamani ya maisha yako. Kupitia kazi tunatafsiri mawazo tulinayo kwa vitendo kufanikisha kutoa thamani kwa wengine. Na kupitia thamani hiyo tunayoitoa kwa wengine ndivyo tunapata kulipwa kulingana na jitihada na ubunifu wetu katika kazi. Hivyo, kama unahitaji kufanikiwa kuwa tayari kutoa thamani kwa wengine kupitia kazi yako.
✍🏾 Mbinu #4: Wekeza wakati wengine wakitumia kila kitu. Kama unatumia kila shilingi inayoingia mikononi mwako bila kuwekeza chochote itakuwa vigumu sana kwako kufanikiwa. Kumbuka kuwa ili uwe kundi la waliofanikiwa ni lazima ufanye vitu vya tofauti. Tafsiri yake ni kwamba ili ufanikiwe ni lazima uepuke tabia ambazo zinafanywa na kila mtu na kuishi tabia ambazo zinafuatwa na watu wachache. Tabia mojawapo ambayo watu wenye mafanikio wanaiishi ni kuwekeza kwenye kila shilingi inayoingia mikononi mwao. Wekeza kwenye ardhi, majumba, biashara mbalimbali, hisa, hatifungani za serikali au kwenye mifuko ya uwekezaji wa pamoja.
✍🏾 Mbinu #5: Sikiliza wakati ambao kila mtu anaoongea. Nimewahi kuandika kuwa katika maisha tunatakiwa kusikiliza mara zaidi ya tunavyoongea. Ndiyo maana tuna masikio mawili ikilingnishwa na mdomo mmoja. Busara hii nilijufunza kutoka kwa Robin Sharma kupitia kitabu chake cha The Greatness Guide. Hivyo, kuanzia sasa jifunze kusikiliza zaidi kuliko unavyoongea. Kupitia tabia hii utajifunza na kujiepusha na mengi kutoka kwa jamii inayokuzunguka.
✍🏾 Mbinu #6: Vumilia wakati wengine wanapokata tamaa. Katika maisha kuna nyakati ambazo utajaribiwa kwenye kile unachofanya. Zipo nyakati ambazo utajikuta badala ya kupata faida kama ulivyokusudia unaishia kupata hasara na madeni juu. Nyakati za changamoto ndizo nyakati sahihi ya kujifunza na kuimarika zaidi. Hivyo, hakikisha unakuwa mvumilivu katika yale unayofanya kuliko watu wengine waliopo kwenye fani au biashara hiyo.
✍🏾 Mbinu #7: Fanya maamuzi nyakati ambazo wengine wanajishauri. Watu waliofanikiwa huwa wana tabia ya kwenda hatua moja mbele zaidi ya wengine. Wakati ambao kila mtu anatafakari kama achukue maamuzi wenye mafanikio wanakuwa tayari wameshatangulia kimaamuzi. Matokeo yake ni kwamba wakati ambao kila mtu anachukua maamuzi wao wanakuwa walishaonja mazuri na mabaya yaliyopo kwenye fursa husika.
✍🏾 Mbinu #8: Kuwa na furaha nyakati ambazo wengine wanahuzunika. Furaha ya nafsi na roho ni silaha pekee ambayo itakuwezesha kuimarika kiafya. Ukiwa na afya bora utafanikiwa kutimiza majukumu yako ya kila siku na hivyo kuendelea kufanikiwa zaidi.
✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limetuanishia baadhi ya vitu ambavyo vinaonekana kuwa vya kawaida sana hila thamani yake ni kubwa katika maisha. Mafanikio yaananzia kwenye kuchukua maamuzi sahihi, wakati sahihi na sehemu sahihi. Na wakati sahihi, sehemu sahihi na maamuzi sahihi ni sasa. Kumbuka, mbegu ikidondoka ardhini itaota na kuzaa matunda, nami naiombe mbegu hii niliyoidondosha leo ipate kuzaa matunda katika maisha yako. Kwa ni mpaka sasa haujajipatia nakala ya uchambuzi wa kitabu cha ‘Kanuni za Pesa”?. Nakala ya uchambuzi wa kitabu hiki bado inapatikana kwa bei ya Ofa ya Tshs. 5,000/= na ndani ya nakala hiyo utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa namna ya kutengeneza, kuwekeza na kutumia pesa.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(