Uchambuzi wa Kitabu cha How To Live On 24 Hours A Day: Jinsi ya kuishi masaa 24 katika siku.

Habari rafiki yangu mpendwa ambaye umeendelea kujifunza kupitia Makala za uchambuzi wa vitabu ambazo nimekuwa nashirikisha jamii kupitia mtandao wa FIKRA ZA KITAJIRI. Karibu katika uchambuzi wa kitabu cha leo ambacho ni cha 7 kati ya vitabu 30 ambavyo nimejiwekea lengo kuvisoma katika kipindi cha mwaka huu 2020.

Kama bado hujajiunga na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI kwa ajili ya kupata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, tafadhali JIUNGE SASA.

Kitabu ninachokushirikisha kupitia makala hii ni How To Live on 24 Hours A Day” kutoka kwa mwandishi Arnold Bennett. Mwandishi anatumia kitabu hiki kutushirikisha namna ambavyo kila mmoja anaweza kutekeleza majukumu yake ya siku kwa furaha na ufanisi. Mara nyingi katika jamii watu wengi huwa wanafanya kazi kwa nguvu na kwa bidii ya kiwango cha juu katika masaa mawili ya mwanzo kazini. Mfano, kama ni wafanyakazi masaa ambayo yanatumika ipasavyo kwa ajili ya uzalishaji ni masaa mawili ya awali na masaa sita yalibakiwa kwenye muda wa kazi yanatumiwa kwa kiwango cha kawaida cha utendaji kazi.

Hata hivyo, tunatakiwa kutambua kuwa siku ina masaa 24, hivyo baada ya kumaliza majukumu ya mwajiri wako au majukumu ya biashara zako kwa muda wa kawaida wa kazi unatakiwa kujiuliza masaa yanayobakiwa yanatumiwa vipi kwa ajili ya kuzalisha mafanikio zaidi kwenye kila sekta ya Maisha yako. Je unatumia muda mwingi kuangalia TV na kusinzia muda mrefu? Kuna mambo mengi ambayo unapuuzia kufanya katika muda wako wa ziada lakini kama yangefanyika yana nafasi ya kubadilisha Maisha yako. Je kila siku asubuhi unashindwa kuamka asubuhi na mapema kabla ya watu wengine hawajaamka ili upangilie majukumu yako ya siku? Anza kuamka mapema lisaa au masaa mawili kabla ya wengine na utaona utofauti katika Maisha yako.

Karibu ushirikiane nami kujifunza machache kati ya mengi ambayo tunashirikishwa katika kitabu hiki:

1. Muda ni zawadi ambayo watu wote wamepewa kwa usawa. Katika siku watu wote tumepewa masaa 24 ambayo kila mmoja ana ratiba yake. Mengi yameandikwa kuhusu jinsi gani watu wanatakiwa kuishi kwa bajeti ya pesa lakini ni machache yameandikwa kuhusu kuishi kwa bajeti ya muda. Wengi tumezoea kusikia kauli kama vile “muda ni fedha”. Ni sahihi kuwa muda ni pesa lakini kauli hii haijitoshelezi kwa kuzingatia kuwa thamani ya muda zaidi ya pesa endapo umetumiwa vyema.

2. Wanasayansi wamefanya kila aina ya chunguzi kuhusiana na ulimwengu na sayari nyinginezo lakini wameshindwa namna ya kupunguza au kuongeza muda. Muda ni rasilimali kwa ajili ya kufanikisha chochote; kupitia muda kila kitu kinaweza kufanyika na pasipo muda hakuna linaloweza kufanyika. Hivyo, muda ni bidhaa ya kipekee ambayo kila mtu anayeishi ana uhakika wa kuimiliki tena bila hofu wala wasiwasi kuwa inawezakuibiwa kama ilivyo kwa bidhaa nyinginezo. Bidhaa hii binadamu wote kila siku tunapewa kiwango sawa kwa maana hakuna anayepata zaidi au pungufu ikilinganishwa na mwenzake.

3. Watu wengi wanaishi katika muda iliopita au muda ujao. Pamoja na kwamba hakuna mwenye uhakika na muda wa baadae lakini bado watu wanashindwa kuishi katika muda uliopo mbele yao. Mfano, ni mara nyingi tunasikia kauli kama vile: “nikipata muda nitatekeleza hilo”, “nikiwa na muda zaidi nitakamilisha….” na kauli nyingine nyingi ambazo zinaonesha kana kwamba watu wana uhakika wa kupata wa ziada nje ya yale masaa 24 kwa siku. Somo kubwa ni kwamba kila saa katika siku tunatakiwa kuishi kwa ukamilisho wa majukumu yenye tija katika Maisha yetu.

4. Tunaishi katika ulimwengu ambao kila mara tunakuwa na matamanio ya kufanikisha baadhi ya vitu kwenye Maisha yetu. Ni kawaida mwanadamu yeyote kutamani katika Maisha kwa kuwa matamanio hayo ndiyo yanafanya Maisha yawe na thamani. Hali hii ya kutamani zaidi katika Maisha inatokana na ukweli kwamba kila siku tunawajibika kisheria kuhakikisha tunajilinda wenyewe pamoja na familia zetu katika hali ya afya bora na salama, kukidhi mahitaji yote ya kifedha, kulipa madeni tuliyonayo, kuwekeza na kuhakikisha kila mara tunaongeza thamani ya rasilimali tunazomiliki. Hili ni jukumu kubwa ambalo ni wachache wanaofanikiwa katika kipindi cha Maisha yao. Wachache hao ni wale ambao wanatambua umuhimu wa kuishi kulingana na muda walionao wa masaa 24 katika kila siku ya Maisha yao. Hata hivyo, ni lazima tukubaliane kuwa hata hao wachache waliofanikiwa kimaisha, Maisha yao kila siku wanakabiliwa na shauku ya kuongezeka zaidi. Hivyo, wote kwa ujumla masaa 24 katika siku yanakabiliwa na hitaji la kutimiza majukumu yetu kwa ajili ya kupata ridhiki zaidi ya Maisha.

5. Siri muhimu ya kufurahia maisha ni kuwa na mpangilio wa majukumu kulingna na muda wa masaa 24 katika siku. Ndani ya masaa hayo 24 unatakiwa kuridhika na yale yanayotekelezeka kwa kutumia uwezo wako wa juu na kuacha yale ambayo yapo nje ya uwezo wako kulingana na nyakati husika. Tumeona kuwa kila siku tunaishi kwa ajili ya kutimiza shauku ya nafsi ya kutaka kuongezeka zaidi katika Maisha, hata hivyo, ni lazima tufahamu kuwa wanaoridhisha nafsi zao ni wale ambao kila mara wapo tayari kuchukua hatua za kuboresha Maisha yao kwenye muda wao wa kila siku. Kama hauchukui hatua zinazolenga kutimiza shauku ya nafsi yako mar azote utajikuta unaishi Maisha yenye msongo wa mawazo na hisia ovu.

6. Uzuri uliopo katika rasilimali ya muda ni kwamba hauwezi kuadhibiwa kwa kunyanganywa au kupunguziwa rasilimali hiyo kutokana na matendo yaliyopelekea upoteze muda katika historia ya Maisha yako. Rasilimali hii inakusubiria katika utimilifu wake kwa siku zote za baadae katika Maisha yako. Mwaka kesho, mwezi ujao, wiki ijayo, kesho na lisaa lijalo vyote vipo katika ukamilifu wake kwa ajili yako kana kwamba haujawahi kupoteza muda. Tafsiri yake ni kwamba kama huko nyuma uliwahi kufanya makosa ambayo yamepelekea kujutia muda uliopotea sasa una nafasi ya dhahabu ya kujifunza kutokana na makosa hayo.

7. Tumeona kuwa nafsi imeumbwa katika hali ya kutoridhika kamwe, hali ya kuhitaji kuongezeka zaidi na hali ya kutaka kujimilikisha kila linalowezekana katika ulimwengu huu. Hivyo ndivyo kwa asili Maisha yetu yalivyo. Hata hivyo, mwandishi anatushirikisha kuwa kuna umuhimu wa kuwa na vipaumbele katika Maisha. Wapo watu wengi ambao wameharibu Maisha yao kutokana na tabia ya kujaribu kila kitu badala ya kukamilisha jambo moja kwa wakati. Hivyo, katika kuhakikisha tunaishi katika ukomo wa muda wa masaa 24 katika siku hatuna budi kukwepa visababishi au viashiria vya kutokufanikiwa kwenye jambo lolote ambalo tumeamua kufanya.

8. Watu wengi wanashindwa kufanikiwa kimaisha kwa kuwa wanaishi katika yaliyopita. Kundi la kwanza linahusisha wale wanaoishi kwa kujivunia mafanikio yaliyopita bila kutambua kuwa hayo yamebaki kuwa historia. Mfano, katika jamii kuna watu wengi ambao wanajivunia mafanikio yao ya darasani enzi za uanafunzi wao. Pia, wapo ambao wanajivunia mafanikio ya kifedha au kikazi waliyowahi kupata katika kipindi cha Maisha yao. Kundi la pili linahusisha wale ambao wanaishi katika huzuni kubwa kutokana na matendo waliyofanya katika Maisha yao au kutokana na familia au malezi waliyopewa enzi za ukuaji wao. Hapa ndipo kuna idadi ya watu wengi ambao wanaishia kusema nilichezea ujana wangu kwa kuwa hakuna la maana nililofanya pasipo kuchukua hatua zinazolenga kurekebisha makosa hayo katika Maisha ya sasa.  Ili ufanikiwe kuishi kwa muda wa masaa 24 katika siku, Mwandishi anatushirikisha kuwa hauna budi kuishi kulingana na wakati uliopo kwa kutekeleza majukumu ya kila siku pasipo kudharau ukubwa au udogo wa kazi.

9. Binadamu wa kawaida ambaye anahitaji kuishi maisha kwa ukamilifu anatakiwa ndani ya fikra zake awe na mpangilio wa kila siku ambayo amebahatika kuishi. Katika majukumu ya kawaida anatakiwa aianze siku kuanzia saa 12 kamili asubuhi na kumaliza siku yake saa 4 usiku. Katika siku anakuwa na jumla ya masaa 16 yaliyokamilika ukiondoa lisaa limoja kwa ajili ya maandalizi baada ya kuamka. Katika masaa hayo anatakiwa kutekeleza majukumu ambayo yanamwezesha kujiendeleza kiroho, kimwili, kiakili na kusaidia jamii inayomzunguka. Muda huo wa masaa 16 siyo kwa ajili ya kukimbizana na presha za Maisha bali ni kufanya kile ambacho roho yako inapenda na inajivunia kujihusisha nacho. Hautakiwi kuwa mtumwa wa pesa bali kupitia upendo kwenye majukumu yako ndipo utalipwa kulingana na thamani unayoitoa kwa wengine.

10. Watu wengi wanapoteza muda mwingi kufuatilia taarifa zisizo na tija katika Maisha yao. Tunaishi katika ulimwengu uliojaa taarifa za uongo au zinazoandikwa kwa makusudi maalumu na taarifa hizi zinadumu kwa muda mfupi sana. Mfano, taarifa nyingi ambazo tunafuatilia kwenye magazeti au vyombo vingine vya habari muda wa uhalisia wa taarifa hizo ni mdogo mno na nyingi zinatolewa kwa lengo la kukuza mauzo au kuongeza idadi ya wafuatiliaji wa chombo husika cha habari. Mwandishi anatushirikisha kuwa baada ya kufahamu ukweli huu kuhusu taarifa zinazoandikwa kila siku hakuna haja ya kuendelea kupoteza muda kwa kusoma magazeti au kuangalia TV.

11. Jenga mazingira yatakayopelekea uwe na majukumu ya thamani baada ya masaa ya kawaida ya mwajiri wako au biashara zako. Mwandishi anatushirikisha kuwa watu wengi katika jamii wameifundisha akili kuhisi uchovu kila baada ya kumaliza masaa ya kazi katika ratiba iliyozoeleka. Mfano, katika masaa 16 ambayo tumeona kuwa mtu wa kawaida anatakiwa awe nayo katika kila siku; asilimia kubwa ya watu huwa wanahesabu masaa yenye tija ni yale ambayo wanatakiwa kwa lazima kuwepo kwenye sehemu zao za kazi. Matokeo yake ni kwamba, baada ya kutoka kazini mtu anazunguka tu mtaani au anakuwepo nyumbani bila kujishughulisha na kazi yoyote yenye tija katika Maisha yake. Ili upate tofauti katika Maisha ni lazima uwe tayari kufanya kazi za ziada baada ya muda wako wa kazi za lazima.

12. Tenga siku moja katika juma kwa ajili ya kuhuisha/kupumzisha mwili. Mwandishi anatushirikisha kuwa unaweza kufanya kazi kwa muda wa siku zote saba katika juma hila kwa asili mwili wa binadamu unahitaji kupata mapumziko. Watu wengi ambao hawana utaratibu wa kupumzika siku moja katika juma mara nyingi huwa wanakabiliwa na kushuka kwa morali ya kazi hali inayosababishwa na mwili kukosa muda wa kupumzika au kubadilisha mazingira. Hali hii huwa inashusha ufanisi wa utendaji wa kazi bila ya ufahamu wa mhusika. Kumbe, unatakiwa kuandaa programu ya kazi kwa muda wa siku sita na kuiacha siku moja bila majukumu yoyote. Siku hii ni kwa ajili ya kuurejesha mwili katika morali ya kazi kwa juma linalofuata.

13. Katika jamii tunazoishi mara nyingi Ofisi nyingi za Serikali zinafunguliwa saa 1:30 asubuhi na kufungwa saa 9:30 alasiri. Hapa kama wewe ni mfanyakazi wa Serikali kati ya masaa 16 ambayo tumeona hapo juu, ukitoa muda wa kuwa kazini (masaa 8) unakuwa umebakiwa na muda wa masaa 8 mengine ambapo kati ya hayo ukitoa muda wa kwenda na kutoka kazi angalau una uhakika wa masaa yasiyopungua 5 kila siku. Ndani ya juma moja (siku 6) utakuwa na masaa yasiyopungua 30 ambayo hakika ukiyatumia vyema utapata mabadiliko makubwa katika Maisha uliyozoa. Vivyo hivyo, kwa upande wa mfanyabiashara, unatakiwa kujifanyia tathimini inayolenga kujua muda unaopoteza nje ya muda wako wa lazima katika biashara yako.

14. Kuishi kwa masaa 24 katika siku ni lazima mhusika awe tayari kubadilisha tabia zilizoeleka katika mfumo wake wa Maisha. Mwandishi anatushirikisha kuwa utakuwa unajidanganya endapo utasema nitaanza kutumia muda wangu vizuri kila siku pasipo kubadirisha tabia. Zipo tabia ambazo kwa sasa zinapelekea upoteze muda na hatua ya kwanza katika kuishi kulingana na masaa 24 katika siku ni kurekebisha tabia ulizozoea katika mfumo wako wa Maisha. Hapa ndipo kuna changamoto maana siyo kazi mtu kusema sitaki kupoteza muda bali kazi kubwa ni kubadilisha tabia. Hali hii inatokana na ukweli kwamba, mabadiliko yoyote ya tabia ni lazima yaambatane na vikwazo pamoja na maumivu kwa mhusika. Mabadiliko hayo yanaambatana na mabadiliko ya mfumo mzima wa Maisha. Hapa ni lazima uwe tayari kutoa sadaka zinazoambatana na kupoteza marafiki au kushindwa kufuatilia vipindi ambavyo awali ilikuwa kila muda wa jioni upo tayari kwenye TV yako.

15. Yote yanawezekana pale tu mhusika akifanikiwa kudhibiti fikra zake. Hakuna mtu anaweza kudhibiti fikra za mwenzake bali ni mhusika pekee ndo mwenye mamlaka ya kudhibiti mfumo wake wa fikra (kiwanda cha kuzalisha na kuchakata mawazo). Hakuna jambo jema au baya linalotokea katika Maisha ya mhusika pasipo kupitia kwenye mfumo wa ubongo ambako ndiko fikra zinatengenezwa na kufanyiwa kazi. Hivyo, kama unahitaji kuwa mtawala mkuu wa Maisha yako ni lazima udhibiti yanayoingia katika mfumo wako wa fikra. Uwezo huu wa kudhibiti fikra ndiyo utakuwezesha kuwa na utulivu kwenye yale unayofanya kulingana na programu ya siku husika. Hivyo, kama unahitaji kuishi Maisha yenye thamani ni lazima uwe mtawala wa fikra zako. Ni lazima uwezo wa kutuliza akili kwenye jambo moja baada ya jingine kwenye ratiba yako ya siku. Kupitia udhibiti wa fikra utaweza kuepuka maovu mengi ya dunia kwa kuwa chanzo cha maovu hayo pamoja na hisia mbaya kama vile hofu, huzuni na chuki ni kupitia mfumo wa fikra.

16. Furaha katika Maisha inaanzia kwa mhusika kujitambua yeye mwenyewe pamoja na uhusiano wake na mazingira yanayomzunguka. Ili mhusika ajitambue mwenyewe ni lazima awe na muda wa kufikiri. Unatakiwa kufikiria kuhusu kila sekta ya Maisha yako kwa kuwa kupitia zoezi hilo utapata kujitambua wewe ni nani na upo duniani humu kwa ajili ya kufanikisha nini. Unapojitambua kuwa wewe ni nani na umeumbwa kwa ajili ya kufanikisha nini moja kwa moja unakuwa umevunja mtego wa mazoea ya watu kuwa furaha inapatikana kutokana na umiliki wa vitu vya Duniani humu. Kumbe, furaha ya kweli chimbuko lake halisi ni kuishi kwa ajili ya ukamilisho wa kusudi maalumu na kuhakikisha Maisha yako yanaendeshwa na kanuni ambazo zinakusogea kwenye kulifikia kusudi hilo. Hivyo, kwa ujumla tunatakiwa kufahamu kuwa furaha ya kweli haipatikani nje ya majukumu yetu ya kila siku bali kadri tunavyotekeleza majukumu hayo ndivyo tunapata furaha katika Maisha. Kwa maneno rahisi ni kwamba furaha ya kweli inapatikana kutokana na ushindi mdogo mdogo wa kila siku kwenye malengo tuliyojiwekea katika kila sekta ya Maisha yetu.

17. Tenga muda wa kusoma kitabu au kusikiliza au kujihusisha na mchezo unaoupenda. Lengo la kuishi saa 24 katika siku ni kuepusha masaa yasiyo na kazi kwa kuwa tufahamu kuwa kukaa bila kazi ni dhambi. Yapo maarifa mengi ambayo unatakiwa kujifunza ili kupitia maarifa hayo upate kufahamu mbinu muhimu za kuendelea kuwa wa thamani katika uhai wako. Pia, unaweza kupata furaha kwa kusikiliza nyimbo au mafundisho mbalimbali sawa na ilivyo kujihusisha kwenye sanaa yoyote unayoipenda kutoka rohoni. Kubwa ni kwamba, chochote unachofanya katika muda husika unatakiwa kuwa na furaha nacho kutoka ndani ya roho yako.

18. Kuishi kwa masaa 24 katika siku ni lazima utambue kuwa tunaishi katika ulimwengu wa kisababishi (cause) na athari (effect). Hivyo, chochote ambacho unahitaji kitokee katika Maisha yako huna budi kutenga muda maalumu kwa ya kujiendeleza kila siku kuelekea kwenye ukamilisho wa hitaji hilo. Lengo la kujiendeleza kila siku ni kwa ajili ya kujiendeleza kimwili, kiakili na kiroho kama sehemu ya utayari kuelekea kwenye hitaji lako.

19. Soma kitabu au Makala ambayo inakufanya utumie akili kujifunza kitu kuhusu Maisha yako. Mwandishi anatushauri kuwa katika kazi za uandishi ambazo zina mafundisho mengi ni kazi za mashairi. Mashairi yana kila aina mafundisho ambayo yatamwezesha mtu yeyote kuwa na hekima na busara kama kipindi cha Maisha yake. Kumbuka katika usomaji wako wa vitabu unatakiwa kuchagua sekta moja ambayo unahitaji kuongeza uelewa wako na kila mara tafuta maarifa yanayolenga kukufanya uwe bora zaidi katika sekta hiyo.

20. Pamoja na kuwa na programu ya siku nzima, mwandishi anatushauri kuwa hatupaswi kuwa watumwa wa programu hiyo. Kama ambavyo tumeona kuwa unatakiwa kufurahia majukumu uliyonayo pia, unatakiwa uwe tayari kuruhusu mabadiliko ya lazima yanayotokea nje ya uwezo wako. Zaidi ya yote ili utimize majukumu yako kulingana na programu ya siku ni lazima husiruhusu mtu achezee ratiba yako. Pia, unatakiwa kuhakikisha unaepuka kushiriki semina au mkutano ambao una maudhui ambayo ni kinyume kanuni unazoziishi.   

Kupitia kitabu hiki mwandishi ameweza kutushirikisha namna ya kuishi kulingana na masaa 24 katika siku. Maisha yanakuwa na thamani pale ambapo kila siku unaitumia kwa faida. Jiunge na mtandao wa Fikra za Kitajiri kwa  KUBONYEZA HAPA.


Karibuni kwenye fikra za kitajiri ili upate elimu isiyokuwa na mwisho.


Born to Win ~ Dream Big 


Mwalimu Augustine Mathias

Namba ya Simu:      +255 786 881 155
Mwanzilishi wa Mtandao wa 
fikrazakitajiri.blogspot.com

Barua pepe:  fikrazatajiri@gmail.com


NENO LA LEO (MEI 12, 2020): AMINI KATIKA WAZO LAKO MPAKA PALE LITAKAPOKAMILISHWA KATIKA UHALISIA WAKE

๐Ÿ‘‰๐ŸพHabari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni kwa mara nyingine tumepewa kibali cha kuendeleza bidii zinazolenga kuyafanya maisha yetu yawe na thamani hapa Duniani. Ni katika asubuhi hii ninakusisitizia umuhimu wa kuwa na hamasa binafsi ili husikatishwe tamaaa na mtu yeyote. Basi kila mmoja aianze siku kwa kusema hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍๐ŸพKaribu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha umuhimu wa kujiamini hasa katika wazo ulilonalo kichwani. Kabla ya kukushirikisha neno la tafakari ya leo hebu kwa pamoja tuangalie mfano mmoja kutoka kwenye kitabu cha Think and Grow Rich cha Napoleon Hill. Wengi wetu tutakuwa tunafahamu magari aina ya V8, magari haya yanatengenezwa na kampuni ya Ford iliyoko Marekani. Henry Ford ambaye ndiye aligundua magari haya baada ya kupata wazo la kutengeneza injini yenye silinda nane, Wataalamu (Waandisi) wake walimkataliwa kuwa haiwezekani silinda zote hizo kukaa katika injini moja.

✍๐ŸพBaada ya Waandisi kumpa hilo la kuwa HAIWEZEKANI, Henry Ford alichowajibu ni kwamba yeye anaamini inawezekana na kila mmoja katika kitengo hicho ana wajibu wa kuhakikisha hilo gari la aina hiyo linatengenezwa. Moja kwa moja wataalamu wakaanza kulifanyia kazi. Baada ya miezi 6 wakampa jibu kuwa IMESHINDIKANA, Henry Ford akawajibu hataki kusikia jibu kama hilo bali anachohitaji ni kusikia wamefanikisha plani aliyowapa. Hawakuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kubuni namna yakufanikisha kutengeneza injini yenye silinda 8. Baada ya miezi kadhaa wakafanikiwa kwa mara ya kwanza kutengeneza injini yenye silinda 8 na ikawa mwanzo wa kuingiza sokoni magari aina ya V8.

TUNAJIFUNZA NINI KATIKA MFANO HUU

✍๐Ÿพ Moja, ukiwa na wazo jipya kuwa tayari kupingwa. Tunaishi katika Ulimwengu wenye watu ambao hawataki kusumbua vichwa hivyo kila lililojipya kwao wanaona HALIWEZEKANI. Hapa ndipo unatakiwa kujiamini katika wazo lako kuwa ni wazo hai ambalo litafanikiwa.

✍๐Ÿพ Mbili, umuhimu wa msimamo husiyoyumbishwa. Mara nyingi kwa kutokuwa na msimamo tumejikuta tumepoteza mawazo ambayo yangebadilisha maisha yetu kwa ujumla. Tumekubali kuwasikiliza walimwengu ambao wametuaminisha kuwa tunachowaza ni ndoto za mchana. Henry Ford hakuwa tayari kuyumbishwa na Wataalamu wake bali msimamo wake uliendelea kuwa hai mpaka wazo lake likajidhihirisha katika uhalisia wake.

✍๐ŸพMwisho, neno la tafakari ya leo limetukumbusha umuhimu wa kuishi katika wazo ulilonalo hadi pale ambapo litafanikiwa. Hata hivyo, ili ufanikishe wazo lako hauna budi kukataa vishawishi vyote ambavyo vinalengo la kukutoa kwenye mstari. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

๐Ÿ‘€ Kwa nini mpaka sasa haujajipatia nakala ya uchambuzi wa kitabu cha ‘Kanuni za Pesa”?. Nakala ya uchambuzi wa kitabu hiki bado inapatikana kwa bei ya Ofa ya Tshs. 5,000/= na ndani ya nakala hiyo utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa namna ya kutengeneza, kuwekeza na kutumia pesa.
 
๐Ÿ‘๐ŸพNakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias 
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

NENO LA LEO (MEI 11, 2020): JIFUNZE KUISHI KWA UKAMILIFU NDANI YA MASAA 24 KILA SIKU

๐Ÿ‘‰๐ŸพHabari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi nyingine katika wiki nyingine ambayo tunazawadiwa katika Maisha yetu kwa ajili ya kuendeleza bidii inayolenga kuyaboresha maisha yetu. Ni asubuhi hii naendelea kukusitiza uendelee kuthamini umuhimu wa ushindi mdogo mdogo ambao unatengenezwa kila siku. Basi kila mmoja aianze siku kwa kusema hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuliishi kuongeza thamani ya maisha yangu.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍๐ŸพKaribu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha umuhimu wa kuishi maisha ya ukamilifu kwenye masaa 24 kila siku ambayo unazawadiwa uhai katika maisha yako. Muda ni rasilimali pekee ambayo binadamu wote tumepewa kipimo kimoja. Ndani ya siku wote tuna masaa 24 na katika lisaa wote tuna dakika 60. Hakuna mtu ambaye amenyimwa au anapunguziwa baadhi ya dakika kama hadhabu kutokana na tabia ya kupoteza muda.

✍๐ŸพHata hivyo, pamoja na kupewa kipimo sawa wote tunafahamu kuwa yale ambayo binadamu wanafanya kwenye ratiba yao ndiyo yatofautisha viwango vyao vya mafanikio. Tumezoea kusikia kauli kama vile: "muda ni pesa" au "muda ni mali". Kauli zot hizi zinauhalisia katika maisha yetu kutokana na ukweli kwamba hakuna kinachoweza kufanyika bila ya uwepo wa muda.

✍๐ŸพPia tunafahamu kuwa katika jamii wapo watu ambao kila kukicha ndani ya kila  SAA katika ratiba yao wapo bize lakini bado wanaangaika kimafanikio. Hiki ni kiashiria kuwa kwetu kuwa siyo tu suala la kuwa bize kwenye kila dakika ndani ya masaa 24 bali ni suala la kujiuliza upo bize kwa kufanya nini. Kumbe, katika maisha tunatakiwa kufahamu kuwa tunafanikiwa kutumia rasilimali muda pale tu tunapotekeleza majukumu yenye tija maisha yetu.

✍๐ŸพPia tunafahamu kuwa lipo kundi kubwa la watu ambalo kila mara linajutia makosa ya awali ambayo yalipelekea kupoteza muda mwingi katika historia ya maisha yao. Mbaya zaidi wengi katika kundi hili ni wale ambao wanateswa na historia yao lakini hawapo tayari kubadilika. Wanaendelea kujiadhibu kiasi ambacho matukio waliyofanya huku nyuma yanakuwa mzigo wa kuendeleza kuharibu muda uliobakia katika kipindi cha uhai wao hapa Duniani. Hili ni tatizo kwa kuwa maisha hayana thamani kama tunaishi kwa kuumizwa na historia.

✍๐ŸพMwisho, neno la tafakari ya leo limetukumbusha umuhimu wa kuishi kulingana na muda tulionao. Tusiishi kulingana na matukio ya yaliyopita kwa kuwa hatuna mamlaka tena ya kubadilisha muda uliopita hila mamlaka tulionao ni kupangilia vyema muda tulionao sasa. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

๐Ÿ‘€ Kwa nini mpaka sasa haujajipatia nakala ya uchambuzi wa kitabu cha ‘Kanuni za Pesa”?. Nakala ya uchambuzi wa kitabu hiki bado inapatikana kwa bei ya Ofa ya Tshs. 5,000/= na ndani ya nakala hiyo utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa namna ya kutengeneza, kuwekeza na kutumia pesa.

๐Ÿ‘๐ŸพNakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

NENO LA LEO (MEI 10, 2020): FAHAMU KWA NINI HAUKUZALIWA KUWA MTU WA WASTANI WALA MASIKINI

๐Ÿ‘‰๐ŸพHabari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya katika Maisha yetu ambayo tumepewa kibali kwa ajili ya kuendeleza pale tulipoishia jana. Ni zawadi ya kipekee katika Maisha yetu hasa tunapoendelea tunapotambua kuwa ukamilisho wa Maisha yetu ni pale tunapojitoe kuishi Maisha ya thamani kwa viumbe vinavyotuzunguka. Basi kwa pamoja tuianze siku kwa kusema hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana, tufurahi, tumshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuliishi kusudi la maisha yetu.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍๐ŸพKaribu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha jinsi ambayo umekuwa ukiishii Maisha ya wastani au kimasikini wakati hayo siyo Maisha uliyoumbiwa. Uliumbwa na kupewa mamlaka ya kutawala viumbe vyote vya angani, baharini na nchi kavu. Zaidi ya mamlaka yako yanakuwezesha kutumia kila kilichoumbwa kwa ajili ya kukuwezesha kuishi Maisha yenye furaha na amani. Hata hivyo kutokana na njia ambayo kila mtu ameifuata amejikuta akipoteza mamlaka hayo ambayo ni kurithishwa vizazi na vizazi. Pamoja na kupoteza mamlaka hayo, mhusika anapojitambua kuwa yeye ni nani na ameumbwa kwa ajili ya kufanya nini hapa Duniani anapata nafasi mpya ya kurejesha mamlaka aliyopoteza.

Tumia mbinu hizi nne kurejesha mamlaka ya kiutawala ambayo umepewa toka enzi za kuumbwa kwako:-

✍๐Ÿพ Mbinu #1: Acha kabisa tabia ya kuridhika na hali uliyonayo. Kila mara unakiwa uwe na kiu ya kuwa bora zaidi. Maisha yanakuwa na thamani pale ambapo kila siku unatamani kuongezeka zaidi ya ulivyokuwa jana (Life is worthy if we seek the expression of increasing more). Haijalishi kwa sasa unateseka kiasi gani kutokana na changamoto za Maisha, muhimu ni kuendelea kuwa na tumaini kuwa changamoto hizo ni za muda na kesho iliyo bora ipo inakusubiria. Hapa ndipo unatakiwa kuachana na tabia ya kulinganisha mafanikio yako na watu wengine na badala yake hakikisha unajiwekea viwango binafsi ambavyo vinakusukuma kuendeleza ubora katika kile unachofanya.

✍๐Ÿพ Mbinu #2: Hakikisha unakuwa mlevi wa mambo yanayofanywa na waliofanikiwa. Mafanikio ya maisha yako ya baadae ni matokeo ya tabia na maamuzi yako ya sasa. Ulevi wa tabia mabaya ni adui namba moja kwa watu wanaotaka kufikia mafanikio makubwa sana katika maisha yao. Kwa ufupi ulevi huu ni kati ya visababishi ambavyo vimekufanya upoteze mamlaka yako ya kiutawala. Hata hivyo, ulevi wa aina hiyo unaweza kuubadilisha na kuwa na ulevi wa kuishi tabia za watu wenye mafanikio. Kila mara Maisha yako yanatakiwa kutawaliwa na kiu ya matamanio ya mafanikio makubwa katika Maisha (Be obsessed with the desire for success).

✍๐Ÿพ Mbinu #3: Ruhusu macho yako ya ndani kuona fursa zinazokusubiria. Kadri mtu anavyobadilisha maisha ya ulevi wa mambo mabaya na kuelekea kwenye ulevi wa mafanikio ndivyo macho yake ya ndani yanavyoanza kuona fursa nyingi ambazo awali hakuwahi kuziona au kuhisi kama zinawezekana. Ipo hazina kubwa ndani mwako ambayo haijatumiwa kuwa bado haujajisumbua kuitumia hazina hiyo. Siku unapoanza kuishi misingi ya mafanikio ndipo utashangaa kuona jinsi fursa nyingi zitakavyoanza kumiminika zaidi na zaidi. Na kadri utakavyokuwa mlevi wa tabia/misingi ya mafanikio ndivyo utashangaa unaanza kupendwa na watu wengi ikilinganishwa ule ulevi wa tabia mbaya.

✍๐Ÿพ Mbinu #3: Kila siku toa thamani kubwa kupitia kazi yako kuliko malipo unayopokea. Hauwezi kufanikiwa kama haujibidishi na kazi na siyo kazi bora kazi tu bali kazi inayokuwezesha kufanikiwa ni ile ambayo ina thamani kubwa kwa walengwa/watendewa. Kumbe, mafanikio yanapatikana kutokana na yale tunayoyafanya kila siku. Na hayo tunayoyafanya kwa njia moja au nyingine ni lazima yaguse Maisha ya watu wengine. Na kadri unavyogusa Maisha ya watu wengi zaidi ndivyo na huduma zako zinavyopendwa zaidi. Hivyo, tunaweza kutumia thamani tunayoitoa kupitia kazi zetu kama sumaku ya kuvuta watu wengi kwa kadri iwezekanavyo katika huduma zetu.

✍๐Ÿพ Mbinu #4: Tambua kuwa matamanio ya mafanikio kimaisha ni zawadi ambayo kila mmoja amerithishwa. Ili zawadi iwe na tija ni lazima itumiwe na mhusika. Unaanza kutumia zawadi hii kwa kufanya maamuzi ya kuondokana na maisha ya kuwa mtu wa kawaida/masikini. Hapa unatakiwa kuamua kuwa gharama zozote ni lazima urejeshe mamlaka uliyopoteza ili uishi maisha ya stahili yako kwani hayo ndiyo Maisha ambayo Muumba alikusudia kwako. Na kadri utakavyoishi maisha haya ndivyo utajitenga na wale ambao wanaishi maisha ya ulevi wa mambo mabaya na kujikuta katika ulimwengu wa watu wenye ulevi wa matamanio ya maisha ya mafanikio tu.

✍๐ŸพMwisho, neno la tafakari ya leo limetufunulia mbinu mbalimbali ambazo kila mtu anaweza kuzitumia kwa ajili ya kufikia matamanio ya mafanikio katika maisha yake. Maamuzi yapo mikononi mwako kuamua kuishi Maisha ya kawaida/umasikini au kurejesha urithi wa mamlaka ya kutawala ambao ulipewa toka enzi za kuumbwa kwako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

๐Ÿ‘€ Kwa nini mpaka sasa haujajipatia nakala ya uchambuzi wa kitabu cha ‘Kanuni za Pesa”?. Nakala ya uchambuzi wa kitabu hiki bado inapatikana kwa bei ya Ofa ya Tshs. 5,000/= na ndani ya nakala hiyo utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa namna ya kutengeneza, kuwekeza na kutumia pesa.

๐Ÿ‘๐ŸพNakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias 
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

NENO LA LEO (MEI 09, 2020): FANYA MAMBO HAYA HAKIKA MAFANIKIO YATAKUKIMBILIA KWA KASI

๐Ÿ‘‰๐ŸพHabari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi ya siku ya jumamosi ambapo naamka nikiwa na furaha, amani, hamasa na nguvu ya kipekee kwa ajili ya kuendeleza pale nilipoishia jana. Sina shaka na siku hii kwa kuwa naamini hii ndiyo aliyoifanya Bwana, wajibu wangu ni kufurahi, kumshukuru na kuitumia vyema kwa ajili ya kupata kila lililo bora katika maisha yangu.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍๐ŸพKaribu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha jinsi unaweza kufanikiwa kwenye kila sekta ya maisha yako kwa kutekeleza vitu ambavyo hinaonekana vidogo hila thamani yake katika maisha ni kubwa. Katika maisha watu wengi huwa wanathamini vitu vikubwa ambavyo mara nyingi vipo nje ya uwezo wao na kudharau vitu ambavyo vinaonekana vidogo.

Kwa pamoja karibu tupitie mbinu hizi ambazo ni za kawaida hila zinaweza kubadilisha maisha yako kwa ujumla kama utaziishi kila siku.

✍๐Ÿพ Mbinu #1: Anza kutekeleza chochote unachowaza wakati wengi wanahairisha au wanajipanga kuwa sawa. Ugonjwa wa kuhairisha au kusogeza mbele (procrastination disease) ni adui namba moja wa kufifisha au kuua ndoto za watu. Dalili za ugonjwa huu ni kila mhusika kujiona hajawa tayari kutekeleza wazo alilonalo kichwani. Matokeo yake siku zinasogea na utayari hauonekani. Hivyo, kama unahitaji kufanikisha wazo lolote tumia kauli mbiu ya kuwa "hakuna wakati ulio bora zaidi ya sasa". Bila kujali utaanza kwa hatua fupi sana muhimu ni kuanza huku ukiwa na picha kubwa kule unakotaka kufika.

✍๐Ÿพ Mbinu #2: Jifunze wakati wengine wamelala au wamefunikwa na maisha ya mazoea. Ili tuendelee kuishi kwa thamani ni lazima tuishi kwa ajili ya kujiendeleza kimwili, kiroho na kiakili. Mara nyingi watu wanaweka mikakati ya kujiendeleza kimwili na kiroho na kusahau kuendeleza upande wa kiakili ambao ndiyo msingi wa maendeleo ya sekta hizo nyingine. Kubwa ni kwamba watu waliofanikiwa kila siku ni dirisha jipya kwa ajili ya nuru ya kujifunza maarifa muhimu ya kujiendeleza kwenye kila sekta ya maisha yao. Hivyo, kama kweli unahitaji kuondokana na maisha ya kawaida na kufikia mafanikio makubwa ni lazima utenge muda wa kujifunza.

✍๐Ÿพ Mbinu #3: Fanya kazi nyakati ambazo wengine wanaishia kutamani kile unachofanya. Ni mara nyingi nimekuwa nikisisitiza kuwa kazi ni kipimo cha utu au kazi ni kipimo cha mafanikio au kazi ni kipimo cha thamani ya maisha yako. Kupitia kazi tunatafsiri mawazo tulinayo kwa vitendo kufanikisha kutoa thamani kwa wengine. Na kupitia thamani hiyo tunayoitoa kwa wengine ndivyo tunapata kulipwa kulingana na jitihada na ubunifu wetu katika kazi. Hivyo, kama unahitaji kufanikiwa kuwa tayari kutoa thamani kwa wengine kupitia kazi yako.

✍๐Ÿพ Mbinu #4: Wekeza wakati wengine wakitumia kila kitu. Kama unatumia kila shilingi inayoingia mikononi mwako bila kuwekeza chochote itakuwa vigumu sana kwako kufanikiwa. Kumbuka kuwa ili uwe kundi la waliofanikiwa ni lazima ufanye vitu vya tofauti. Tafsiri yake ni kwamba ili ufanikiwe ni lazima uepuke tabia ambazo zinafanywa na kila mtu na kuishi tabia ambazo zinafuatwa na watu wachache. Tabia mojawapo ambayo watu wenye mafanikio wanaiishi ni kuwekeza kwenye kila shilingi inayoingia mikononi mwao. Wekeza kwenye ardhi, majumba, biashara mbalimbali, hisa, hatifungani za serikali au kwenye mifuko ya uwekezaji wa pamoja.

✍๐Ÿพ Mbinu #5: Sikiliza wakati ambao kila mtu anaoongea. Nimewahi kuandika kuwa katika maisha tunatakiwa kusikiliza mara zaidi ya tunavyoongea. Ndiyo maana tuna masikio mawili ikilingnishwa na mdomo mmoja. Busara hii nilijufunza kutoka kwa Robin Sharma kupitia kitabu chake cha The Greatness Guide. Hivyo, kuanzia sasa jifunze kusikiliza zaidi kuliko unavyoongea. Kupitia tabia hii utajifunza na kujiepusha na mengi kutoka kwa jamii inayokuzunguka.

✍๐Ÿพ Mbinu #6: Vumilia wakati wengine wanapokata tamaa. Katika maisha kuna nyakati ambazo utajaribiwa kwenye kile unachofanya. Zipo nyakati ambazo utajikuta badala ya kupata faida kama ulivyokusudia unaishia kupata hasara na madeni juu. Nyakati za changamoto ndizo nyakati sahihi ya kujifunza na kuimarika zaidi. Hivyo, hakikisha unakuwa mvumilivu katika yale unayofanya kuliko watu wengine waliopo kwenye fani au biashara hiyo.

✍๐Ÿพ Mbinu #7: Fanya maamuzi nyakati ambazo wengine wanajishauri. Watu waliofanikiwa huwa wana tabia ya kwenda hatua moja mbele zaidi ya wengine. Wakati ambao kila mtu anatafakari kama achukue maamuzi wenye  mafanikio wanakuwa tayari wameshatangulia kimaamuzi. Matokeo yake ni kwamba wakati ambao kila mtu anachukua maamuzi wao wanakuwa walishaonja mazuri na mabaya yaliyopo kwenye fursa husika.

✍๐Ÿพ Mbinu #8: Kuwa na furaha nyakati ambazo wengine wanahuzunika. Furaha ya nafsi na roho ni silaha pekee ambayo itakuwezesha kuimarika kiafya. Ukiwa na afya bora utafanikiwa kutimiza majukumu yako ya kila siku na hivyo kuendelea kufanikiwa zaidi.

✍๐ŸพMwisho, neno la tafakari ya leo limetuanishia baadhi ya vitu ambavyo vinaonekana kuwa vya kawaida sana hila thamani yake ni kubwa katika maisha. Mafanikio yaananzia kwenye kuchukua maamuzi sahihi, wakati sahihi na sehemu sahihi. Na wakati sahihi, sehemu sahihi na maamuzi sahihi ni sasa. Kumbuka, mbegu ikidondoka ardhini itaota na kuzaa matunda, nami naiombe mbegu hii niliyoidondosha leo ipate kuzaa matunda katika maisha yako. Kwa ni mpaka sasa haujajipatia nakala ya uchambuzi wa kitabu cha ‘Kanuni za Pesa”?. Nakala ya uchambuzi wa kitabu hiki bado inapatikana kwa bei ya Ofa ya Tshs. 5,000/= na ndani ya nakala hiyo utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa namna ya kutengeneza, kuwekeza na kutumia pesa.

๐Ÿ‘๐ŸพNakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

NENO LA LEO (MEI 08, 2020): ULIZALIWA TAJIRI HILA IMANI HIZI KUHUSU PESA ZIMEPOTEZA UTAJIRI WAKO

๐Ÿ‘‰๐ŸพHabari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi ya kipekee ambayo tumezawadiwa kwa mara nyingine tena ili kuendeleza pale tulipoishia jana. Ni wakati kama huu nasema asanthe kwa Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuamka salama ili niendelee kutengeneza ushindi mdogo mdogo katika kila sekta ya maisha yangu. Sina maneno mengine kwa Muumba zaidi ya kusema hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana, sina budi kufurahi, kumshukuru na kuitumia vyema kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍๐ŸพKaribu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha jinsi kauli ulizofundishwa kutoka kwa ulimwengu zimekufanya upoteze utajiri uliorithishwa toka enzi ulipozaliwa. Katika neno la tafakari ya jana tuliona jinsi ambavyo kila mtoto anazaliwa akiwa na uwezo wa hali ya juu kwenye kila sekta ya maisha yake. Hata hivyo, tuliona kadri mtoto anavyokua ndivyo uwezo wake unazidi kuathiriwa na ulimwengu kutokana na aina ya malezi, mazingira anayokulia na mafundisho anayopata kutoka kwa watu wote wanaomzunguka. Katika neno la tafakari ya leo hebu kwa pamoja tujifunze jinsi kauli hizi kuhusu pesa zilivyopoteza utajiri wako:-

✍๐Ÿพ Kauli #1: Ili utengeneze pesa unatakiwa kuwa na pesa. Kauli hii imepoteza uwezo wa watu wengi katika kuthubutu kuanzisha mipango ya kifedha kwa kuwa kila mara wanajiona hawana pesa za kutosha kwa ajili ya kuanzisha mradi wanaoufikiria. Hivyo, kauli hii inakandamiza uwezo wa kubuni na kuanzisha vitu vipya kutoka kwenye vitu vinavyotuzunguka (asili).

✍๐Ÿพ Kauli #2: Kupenda sana pesa ni uovu. Kauli hii imekandamiza uwezo wa watu wengi kwa kuwa wanaepuka kuonekana warafi, wachoyo na wenye tamaa ya kupindukia katika jamii inayowazunguka. Chanzo kikuu cha kauli hii ni kutoka kwa wazazi au walezi kutokana na imani waliuonayo kuhusu pesa. Kama mzazi/ mlezi ni masikini matokea yake na ni kumjaza mtoto wake kila aina ya hofu alizonazo kuhusu pesa.

✍๐Ÿพ Kauli #3: Pesa ni kwa ajili ya watu wachache waliobarikiwa kuwa nazo. Kauli hii imetufanya tuamini kuwa kuna watu wachache walioumbwa kwa ajili ya kumiliki pesa nyingi kwa kadri wapendavyo na kundi kubwa la watu limeumbiwa umasikini. Hii ni kauli kandamizi ambayo kila inakufanya uone uchache (scarcity) wa pesa hivyo kujiona kuwa hauwezi kupata pesa za kutosha. Matokeo yake ni kuanzia kuridhika na uchache wa pesa unazopata na kujifariji kuwa siyo lazima wote tuwe matajri. Kuanzia sasa kataa kauli hiyo kwa kuwa tumeumbwa kuishi maisha ya utajiri.

✍๐Ÿพ Kauli #4: Ili uwe tajiri ni lazima ujitoe nafsi au uwe mchawi. Kauli hii inatifanya tuwaone Matajiri kuwa ni watu wabaya kwa kuwa wameuza nafsi zao kwa majini au msema uliozoeleka katika jamii yetu ya sasa ni FREE MASONRY. Ukweli ni kwamba unaweza kuwa tajiri bila kuuza nafsi yako.

✍๐ŸพMwisho, neno la tafakari ya leo limetukumbusha kuwa wote tulizaliwa tukiwa tajiri hila imani tulizopata zimetufanya kupoteza utajiri wetu. Ni muda muhafaka wa kutafakari kuhusu imani na mtazamo wetu kuhusu pesa. Kumbuka, mbegu ikidondoka ardhini itaota na kuzaa matunda, nami naiombe mbegu hii niliyoidondosha leo ipate kuzaa matunda katika maisha yako. Kwa ni mpaka sasa haujajipatia nakala ya uchambuzi wa kitabu cha ‘Kanuni za Pesa”?. Nakala ya uchambuzi wa kitabu hiki bado inapatikana kwa bei ya Ofa ya Tshs. 5,000/= na ndani ya nakala hiyo utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa namna ya kutengeneza, kuwekeza na kutumia pesa.

๐Ÿ‘๐ŸพNakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

Uchambuzi wa Kitabu cha The Science of Getting Rich: Sayansi ya Kuwa Tajiri.


Habari rafiki yangu mpendwa ambaye umeendelea kujifunza kupitia Makala za uchambuzi wa vitabu ambazo nimekuwa nashirikisha jamii kupitia mtandao wa FIKRA ZA KITAJIRI. Karibu katika uchambuzi wa kitabu cha leo ambacho ni cha 5 kati ya vitabu 30 ambavyo nimejiwekea lengo kuvisoma katika kipindi cha mwaka huu 2020.

Kama bado hujajiunga na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI kwa ajili ya kupata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, tafadhali JIUNGE SASA nafasi ni chache.

Kitabu ninachokushirikisha kupitia makala hii ni The Sience of Getting Rich” kutoka kwa mwandishi Wallace D. Wattles. Kupitia kitabu mwandishi anatushirikisha mbinu na kanuni ambazo zinaweza kutumiwa na mtu yeyote kwa ajili ya kutengeneza utajiri anaotamani. Mwandishi anatushirikisha kuwa kwa kutumia mbinu zilizopo katika kitabu hiki milango ya kipato chako itafunguka na pato lako litaanza kuongezeka mara mbili, mara tatu na zaidi na zaidi. Pia, kwa kutumia kanuni hizi utashangaa unaanza kupata marafiki wapya ambao watawezesha kupata taarifa na fursa ambazo zitafanikisha ukuaji wa biashara zako.

Msingi wa kanuni zinazoshirikishwa kitabu hiki ni Imani. Kanuni unazoshirikishwa katika kitabu hiki badala ya kuhoji uhalisia wake unatakiwa kutanguliza Imani kuwa sayansi ya kanuni hizi imefikiwa baada ya kutumiwa na watu wengi kufanisha utajiri. Hivyo, unachotakiwa kufanya ni kutumia sayansi hii katika Maisha yako bila kuhofu wala kuhairisha.

Karibu ushirikiane nami kujifunza machache kati ya mengi ambayo tunashirikishwa katika kitabu hiki:

1. Utajiri ni yako ya kuzaliwa. Tunaweza kuongea chochote kuhusiana na Maisha ya umasikini lakini ukweli unabakia kuwa ili mtu aishi Maisha yenye mafanikio ni lazima awe tajiri. Ukweli ni kwamba mtu anaweza kuwa na kipaji lakini ili aweze kuendeleza kipaji hicho ni lazima awe na vitu vya msingi ambavyo vitamwezesha kukuza kipaji chake. Maendeleo ya mtu kiroho, kimwili na kiakili anahitaji amiliki vitu vya msingi ambavyo upatikanaji wake unahitaji mhusika awe na pesa. Kwa tafsiri hiyo uhai wa mtu unahusisha mhusika kupata haki ya kutumia vitu vya msingi ambavyo vitamuwezesha kujiendeleza kimwili, kiroho na kiakili. Kwa maneno mengine ni kila mtu ana haki ya kuwa tajiri.  

2. Kuridhika na hali ya umasikini ni dhambi. Mwandishi anatushirikisha kuwa furaha ya kuishi ni kuendelea kupata zaidi kutoka kwenye mazingira yanayokuzunguka. Na kadri unavyopata zaidi ndivyo unatengeneza utajiri, mamlaka na nguvu ambazo zinakuwesha uishi Maisha ya ukamilifu. Maisha yenye kupata kila hitaji muhimu katika uhai wako. Hakuna maana ya kuridhika na uchache (umasikini) wakati umeumbwa kwa ajili ya kupata zaidi (utajiri). Kwa asili kila mwanadamu anatamani kufikia mafanikio makubwa sana katika Maisha. Dhamira au matamanio hayo amerithishwa toka enzi za kuumbwa kwake. Hata hivyo ili mwanadamu ili afikie mafanikio ya matamanio yake ni lazima atumie vitu vinavyomzunguka na kiwango cha upatikaji wa vitu hivyo kinategemeana na uwezo wa kifedha ambao mhusika anao.

3. Mwanadamu anaishi kwa ajili ya kujiendeleza katika vitu muhimu vitatu ambavyo ni: roho, mwili na akili. Sehemu hizi tatu katika Maisha yeu ni muhimu na hakuna sehemu ambayo ni bora kuliko nyingine hivyo hakuna sehemu ambayo itaishi kwa ukamilifu pale ambapo sehemu nyingine zinaachwa. Siyo sahihi kuendeleza roho na kusahau mwili na akili au kuendeleza akili huku ukisahau mwili na roho. Hapa ndipo tunaona umuhimu wa utajiri kutokana na ukweli kwamba mtu hawezi kujiendeleza kimwili bila mahiaji muhimu ya chakula; mavazi; kinga dhidi ya mvua, jua kali au Wanyama wakali; na vitu muhimu vinavyomuwezesha kufanya kazi. Vivyo hivyo, mtu hawezi kujiendeleza kiakili kama hana uwezo wa kupata vitabu na muda wa kuvisoma; bila kuwa na uwezo wa kutembea nje ya mazingira aliyozoea na kujifunza kwa kuona; au uwezo wa kujifunza kutoka kwa marafiki wenye maarifa mbalimbali. Pia, ili kujiendeleza kiroho mhusika anatakiwa kuishi Maisha ya upendo na ni ukweli mtupu kuwa hakuna upendo katika Maisha ya dhiki kwa kuwa upendo msingi wake mkuu ni Maisha ya kutoa kwa wengine. Kwenye dhiki inayotokana na upungufu wa vitu kila mtu anatanguliza nafsi yake.

4. Kuna sayansi ya kuwa tajiri ambayo inafanya kazi kwa mtu yeyote ambaye anaitumia na kuiheshimu. Umiliki wa pesa na rasilimali za kila aina vyote kwa pamoja vinakuja kutokana na kufanya vitu kwa kufuata misingi na kanuni. Wale wanaofuata misingi na kanuni hizo iwe kwa kufahamu au kwa bahati wanafanikiwa kuwa matajiri wakati wale wasiyofuata misingi na kanuni hizo bila kujali jitihada kiasi gani walizonazo katika kazi wanaendelea kuwa masikini. Hivyo kuwa tajiri siyo swali la mazingira, sura, umri au rangi maana kama ingekuwa hivyo watu wote katika eneo moja au wenye rangi inayofanana wote wangekuwa na utajiri. Ili uwe ajiri ni lazima ufanye kazi njia flani (doing things in a certain way) na ili ufanye vitu katika hali flani ni lazima ufikirie katika njia flani (thinking in a certain way). Hii ni kutokana na ukweli kwamba jinsi tulivyo ni matokeo ya yale tunayoyafikiria kwa muda mrefu.

5. Hakuna mtu ambaye anakosa fursa za kumwezesha kuwa tajiri. Unaweza kushindwa kufanikiwa katika sekta moja lakini kuna sekta kadhaa ambazo zipo wazi kwa ajili yako kufanikiwa kimaisha. Hivyo, hakuna sababu ya kulalamikia hali uliyonayo na badala yake unatakiwa kuanza kufanya vitu kwa kufuata misingi na kanuni za kuwa tajiri. Hakuna mtu ambaye anakuwa masikini kutokana na upungufu wa fursa bali kinachomfanya awe masikini ni kushindwa kuishi misingi na kanuni za kutengeza utajiri. Vitu vinavyoonekana (visible) na visivyooneka (invisible) havijawahi kupungua kwa mtu yeyote anayetaka kufanikiwa kimaisha. Tafsiri yake ni kwama hakuna mtu ambaye ni masikini kwa kuwa asili (nature) imeishiwa vitu muhimu vya kumwezesha kuwa tajiri. Umasikini wa mtu unatokana na jinsi anavyoishi Maisha yake. Asili ina kila kitu muhimu cha kumwezesha mtu yeyote kuwa tajiri.

6. Kanuni ya kwanza ya utajiri: Fikra ni nguvu pekee ambayo inawezesha kuumba vitu vinayoonekana kutoka kwenye visivyoonekana. Kila kitu unachookiona katika ulimwengu kimeanzia kwenye fikra. Kuanzia sekta ya miundombinu, usafirishaji, kilimo, ujenzi na mengine yote yaliyo umbwa kwenye uso wa dunia hii yameanzia kwenye fikra. Hivyo, tunaishi katika ulimwengu wa fikra na kama unahitaji kufanikisha chochote katika Maisha yako ni lazima kitu hicho kianzie kwenye fikra. Hata hivyo, ili kitu hicho kiumbike ni lazima mhusika aendelee kuishi katika fikra hizo kwa kipindi cha muda wote hadi pale ambapo atakuwa amekamilisha uumbaji wa kitu husika. Kutokana na kanuni hii tunatakiwa kutambua kuwa chochote kile ambacho tunahitaji kifanyike katika mikono yetu ni lazima mfumo wa fikra ufanye kazi yake kwanza.

7. Pale mtu anapokuwa na wazo juu ya umbo analotaka kuumba cha kwanza kabisa anatakiwa kufikiria ni malighafi zipi kutoka kwenye asili ambazo atatumi kukamilisha uumbaji wa umbo lake. Hata hivyo tunatakiwa kukumbuka kuwa chanzo cha uumbaji ni Muumba mwenyewe ambaye katika Maandiko Matakatifu anasema “natumfanye mtu kwa mfano wetu, sura yetu..”. Kupitia uumbaji huo mwanadamu alipewa mamlaka ya kuumba vitu vinavyoonekana kutoka katika asili inayomzunguka na anayekamilisha uumbaji huo wa vitu si yeye bali ni nguvu ya Mungu ndani mwake. Hata hivyo, wanadamu hawatumii mamlaka ya uumbaji waliyopewa kwa kuwa ni wachache wenye kuunganisha nguvu ya fikra na inayofanya kazi ndani mwao kwa ajili ya uumbaji wa vitu vipya. Watu wengi wamejikita kwenye kuboresha vitu ambavyo vimeshaumbwa tangu zamani.

8. Kutoka katika kanuni hii tunakumbushwa kuwa:
Moja, kuna nguvu ya fikra yenye uwezo wa hali ya juu na kutoka katika nguvu hiyo inaendelea kuruhusu uumbaji ambao unawezesha kuujaza ulimwengu huu. Nguvu hiyo inawezesha kuumbwa kwa maumbo mbalimbali yenye uhalisia kutoka kwenye picha inayoumbika katika fikra. Hivyo, kila mtu anaweza kuumba vitu kutoka kwenye fikra pale ambapo anaruhusu muunganiko wa kweli wa fikra zake na fikra iliyo kuu ambayo ni Mungu mwenyewe.
Mbili, hatua ya kwanza ya kuwa tajiri ni kuwa na uwezo wa kudhibiti fikra zako, uwezo ambao utakuwezesha kufikiria UKWELI ambao ni upande chanya kwenye kila hali bila kujali hali inayokuzunguka. Mfano, kuhusu umasikini unatakiwa kuifanya akili yako muda wote ione kuwa haiwezekani uwe masikini kwa kuwa asili ina kila kitu cha kukuwezesha uwe tajiri. Mwandishi anatushirikisha kuwa kazi hii ya kudhibiti fikra ni ngumu kuliko kazi yoyote ile hapa Duniani. Mfano, hebu tafakari kufikiria kuwa umeumbwa kwa ajili ya kuwa na afya bora katika kipindi ambacho unazungukwa na magonjwa. Hata hivyo, mtu anayefanikiwa kudhibiti fikra zake anakuwa mtawala wa akili yake na ana nafasi kubwa ya kufanikisha mambo mengi katika Maisha yake.
Tatu, nguvu ya kudhibiti fikra inapatikana kwa kuamini kuwa “kuna nguvu iliyo moja na kipekee ya fikra ambayo ndiyo chanzo cha uumbaji wa kila kitu duniani hapa”. Pale unapoamini katika nguvu hiyo tunapata mamlaka ambayo inatuwezesha kuumba kila kitu ambacho kimejengeka kwenye mfumo wa fikra zetu. Pale tunapogundua ukweli huu tunaondoa shaka na hofu zote kwa maana tunatambua kuwa “tunaweza kuunda kitu chochote kile tunachotaka kuunda, tunaweza kupata kile tunachotaka kuwa nacho, na tunaweza kufikia mafanikio tunayoyataka”.

9. Kanuni ya pili: Kila kiumbe kilicho hai ni lazima mara zote kitafute kuongezeka kimaisha kwa kuwa Maisha yenyewe ni kwa ajili ya kuongezeka au kukua zaidi. Mbegu inayodondoshwa ardhini ikiwa hai inaota na kuongezeka na hatimaye inazaa matunda zaidi ambayo yanawezesha upatikanaji wa mbegu zaidi na zaidi. Hali kadhalika binadamu katika kipindi cha Maisha yake anatakiwa ajikite kwenye kuongezeka kithamani. Hii ni kutokana na ukweli kwamba nguvu ya fikra iliyopo ndani mwake inahitaji kuongezeka zaidi. Kila maarifa unayojifunza yanakufanya utamani kujifunza maarifa mapya zaidi, kila kipaji unachoendeleza kinakufanya upanuke zaidi katika sekta nyingine za Maisha. Kwa ujumla tumeumbwa kwa ajili ya kufahamu/kujua zaidi, kufanya zaidi na kuongezeka zaidi. Hilo ndilo hitaji kuu katika Maisha.

10. Kutamani kuwa tajiri ni moja ya hitaji muhimu katika Maisha kwa kuwa tumeona hitaji muhimu katika Maisha ni kutaka kuongezeka zaidi. Hivyo ili tupate zaidi katika Maisha hatuna budi ya kuwa tajiri kwa kuwa huo ndiyo ukamilisho wa Maisha sawa na ilivyo kwa mmea wa aina yoyote ni lazima ujikite kutafuta chakula kwa ajili ya kuongezeka zaidi. Hii ni sheria ya asili ambayo inafaya kazi kwenye kila kiumbe chenye uhai. Dhamira ya Mungu nikuona wewe unakuwa tajiri ili ajidhihirishe kwa wengine kupitia nafasi yako na ataishi ndani mwako kwa kuwa unaendelea kutumia nguvu iliyo kubwa ambayo umepewa toka enzi za kuumbwa kwako. Asili pia inatamani uwe tajiri na ndiyo maana haijawahi kupungukiwa ipo tayari kukuzawadia kila hitaji ulilonalo. Wajibu wako ni kubadilisha fikra na kuona kuwa kila unachohitaji kipo tayari kupatikana kutoka kwenye ulimwengu huu kwa kuwa asili ni rafiki kwa mipango yako.

11. Tengeneza sababu zinazokusukuma kutaka utajiri. Kubwa kabisa unatakiwa kutambua kuwa unahitaji kuwa Tajiri ili upate kula, kunywa huku ukifurahia Maisha wakati wote. Unataka kuwa Tajiri ili uweze kuzungukwa na vitu vizuri, kutembea na kutazama mazuri katika nchi za mbali, kulisha na kukuza akili yako; na ili upende na kufanya mambo mema kwa wengine. Na unahitaji kuwa tajiri ili upate kuwa sehemu ya wanaosaidia walimwengu kuujua ukweli na kuuishi. Katika yote husitafute utajiri kwa ajili ya kuwaumiza au kushindana na wenzako kwa kuwa asili imejaa kila aina kitu kuutosheleza ulimwengu. Husitafute utajiri kwa kuwa kunyang’anya au kudhurumu mali za wengine. Wewe ni Muumbaji kwa nini upoteze muda kwa kuwa na hila au wivu kwenye mali wanazomiliki wenzako? Utajiri ambao unajivunia ni ule ambao unatengenezwa bila kuumiza wala kuangamiza watu wengine. Hivyo, kupitia sheria hii tunakumbushwa kuwa asili inajitosheleza kumpa kila mmoja utajiri anaotaka hivyo hakuna haja ya kushindana.

12. Kanuni ya tatu: Utajiri unakuja kwako kupitia KUTOA thamani kubwa kuliko UNAYOPOKEA. Tafsiri ya kanuni hii ni kwamba kabla ya kulenga kupokea kutoka kwa wengine unatakiwa kulenga kuwa mtu wa thamani. Husimshawishi mtu kumuuzia mtu kitu ambacho unajua hakina thamani yoyote katika Maisha yake. Hivyo, chochote unachouza hakikisha kinaongeza thamani ya matumizi kwenye Maisha ya kila siku ya muhusika. Kwa kufanya hivyo utakuwa umewezesha kurahisisha Maisha kwa wale ambao unafanya nao dili za kibiashara. Kama kuna watu ambao umewaajiri hakikisha unaweka mpango ambao utawezesha kupiga hatua badala ya kuendelea kukutegemea.

13. Tumeona kuwa utajiri unatengezwa kupitia nguvu ya fikra ambayo inawezesha uumbaji wa vitu vipya kutoka kwenye chanzo halisi kisicho na umbo (from a formless substance). Baada ya kujenga picha ya kitu unachohitaji katika akili yako sasa unatakiwa kuwa na imani isiyoyumbishwa juu ya uhakika wa kitu hicho kukamilika katika Maisha yako. Imani hiyo ndiyo itawezesha nguvu iliyo kubwa (supreme power au Mungu) ambayo inafanya kazi kupitia watu wanaokuzunguka kukupatia unachojitaji. Hata hivyo, ili uumbaji ukamilike ni lazima uwe tayari kutafsiri picha ya kitu kilichopo kwenye akili yako kwa vitendo ambapo ni lazima uusishe viungo vya mwili wako kama vile mikono. Hivyo, ndivyo utajiri unavyokuja kwako kupitia nguvu ya fikra ambayo ndiyo chanzo halisi cha uumbaji. Nguvu hiyo ya fikra inafanya kazi kwa watu wote wanaoitumia na wote wanaunganishwa kwa pamoja bila kujali umbali walipo, hivyo pale unapowaza kitu ambacho hauna kuna mwingine mwenye nacho ambaye anahitaji mtu wa kubadilishana nae labda kwa pesa na kitu alichonacho.

14. Hivyo, kwa ujumla tunatakiwa kutambua kuwa: utajiri unakuja kwetu kupitia kujenga picha halisi ya kitu tunachohitaji na kuhakikisha picha hiyo kila mara kwa Imani isiyo na shaka tunaifikisha kwa nguvu kuu ya uumbaji ambayo ni Muumba mwenyewe ambaye tangu enzi za kuumbwa kwa ulimwengu ameendelea kuumba vitu vipya kupitia kwa wanadamu. Mungu hapendi watu wake waishi Maisha ya dhiki kutokana na umasikini bali yupo tayari kuwezesha upatikani wa utajiri kwa kila mmoja ambaye anafanya kazi katika hali ya utofauti (doing things in a certain way). Mungu anafurahi kuona watu wake wakipendeza kupitia mavazi bora, kupata chakula au kinywaji kizuri, wanaishi kwenye nzuri na za kifahari, wanatembelea magari mazuri na mengine mengi ambayo kwa ujumla wake ndiyo hitaji na dhamira ya kila mwanadamu hapa Duniani. Kwa kumiliki na kutumia vitu hivyo Mungu anafurahi na kupata fahari kwa kujivunia uumbaji wake kwa kilichopo Duniani kimetokana na kazi ya mikono yake.

15. Kanuni ya nne: Utajiri unakuja kwa kuwa mtu wa shukrani. Mpaka sasa unaamini kuwa: Moja, kuna nguvu moja iliyo kuu kuliko zote (Muumba) ambayo ndiyo chanzo halisi cha uumbaji wa vitu vyote. Pili, unaamini kuwa nguvu hiyo inao uwezo wa kukupatia kila kitu ambacho unatamani katika Maisha yako. Tatu, kupitia shukrani ya dhati ndipo tunadumu katika muunganiko mkubwa na nguvu iliyo kuu kuliko nguvu zote. Watu wengi wanashindwa kudumu katika muunganiko na nguvu iliyo kuu kwa kuwa baada ya kufanikiwa kupiga hatua moja wanakata mahusiano ya kifikra na nguvu iliyo kuu. Mwandishi anatushirikisha kuwa kama tunahitaji kuwa tajiri ni lazima tukae karibu na chanzo halisi cha utajiri ambacho si kingine bali ni Mungu mwenyewe. Na njia rahisi ya karibu na Mungu wetu ni kuwa na roho ya shukrani. Na kadri unavyoshukuru ndivyo unajiongezea nafasi ya kupewa vingine zaidi ya ulivyonavyo.

16. Roho ya shukrani inakuwezesha kuondokana na Imani kuwa vitu vinapatikana kwa uchache na hivyo kukufungulia milango ya kupata zaidi kutoka kwenye asili ambayo haijawahi kupungukiwa. Ni kutokana na roho ya shukrani unaweza kuendelea kutegemea daima kupata yaliyo bora badala ya kuwaza kuzawadiwa mabaya katika Maisha. Hivyo, kuna kila sababu ya kujenga tabia ya kushukuru kwenye kila jema linalokuja katika Maisha yako. Husitumie muda mwingi kulalamikia mamlaka iliyopo juu yako au kujishusha kutokana na mapungufu uliyonayo na badala yake tumia muda huo kujivunia mazuri uliyonayo kwani kupitia mazuri hayo utaweza kupunguza madhaifu yako.

17. Kanuni ya tano: Utajiri unakuja kwako kwa kutumia uwezo wa kufikiria katika hali flani (thinking in a certain way). Tumeona kuwa kuna nguvu ya fikra iliyo kuu kuliko zote na kupitia nguvu hiyo watu wamendelea kuumba vitu mbalimbali katika uso wa Dunia. Tumeona kuwa ili mhusika aweze kuumba kitu ni lazima kwanza awe na wazo la kitu husika katika akili yake na wazo hilo liambatane na umbo au ramani yenye vipimo kamili. Kwa ujumla ni lazima kitu anachohitaji kiumbike kwanza katika akili yake na picha ya kitu husika iendelee kuwepo akilini mwake muda wote. Hatua inayofuata ni kuwasilisha picha/ramani ya kitu husika kwa nguvu ya fikra iliyo kuu (Muumbaji halisi). Hapa ndipo watu wengi wanashindwa kufanikisha uumbaji wa vitu wanavyotaka katika Maisha yao kwa kuwa wanashindwa kuwa na mpangilio wa umbo au ramani ya vitu hivyo katika akili yao. Ili ufanikiwe kupata unachohitaji ni lazima ufahamu nini hasa unataka na lini unahitaji kitu hicho kiwe kimekamilika. Hatua ya mwisho ni kuhakikisha unakaa katika matamanio yanayokusukuma kuona picha uliyonayo akilini anajidhihirisha katika maumbile yake halisi. Pia, hakikisha picha hiyo inakuwa katika fikra zako kwenye kila unalofanya katika majukumu yako ya kila siku.

18. Hata hivyo, haitoshi kuwa na picha halisi ya kitu ambacho unahitaji katika Maisha yako maana ukiishia hatua hiyo inakuwa ni ndoto. Nyuma ya maono ya fikra zako inatakiwa kuwa IMANI THABITI ambayo inakufanya ujione tayari unamiliki kitu husika katika Maisha yako ya kila siku. Kama ni nyumba jione tayari upo ndani ya nyumba husika kulingana na ramani uliyonayo kichwani. Kama ni gari kwa Imani jione upo ndani ya gari husika ukiendesha na kama ni shamba jione tayari shamba husika lipo ndani ya miliki yako. Maandiko Matakatifu yanasema “chochote ambacho mtaomba kwa Imani na kuamini kuwa mtapata, hakika mtapewa…”. Hivyo, kufanikiwa kupata hitaji lako kutoka kwenye nguvu ya fikra iliyo kuu ni lazima ujifunze kudumu katika sara.

19. Kanuni ya sita: Ili utajiri uje kwako ni lazima uondoe vikwazo vyote vinavyotokana na historia ya Maisha yako. Changamoto za kifedha, historia ya umasikini katika familia uliyokulia au madhahifu yako yote yanatakiwa kuwekwa pembeni. Bila kufanya hivyo utakuwa na picha mbili zinazokinzana (picha ya umasikini na picha vitu unavyotaka) katika mfumo wako wa fikra. Pia, unatakiwa kuweka pembeni Imani zote ambazo zinaenda kinyume na ukamilisho wa picha uliyonayo kichwani. Husisome vitabu au Makala ambazo zinapingana na kanuni hizi za kutengeneza utajiri. Kaa mbali na makundi ya watu ambao wana mtazamo hasi kuhusiana na utajiri. Mara zote jivunie mema ya nchi ambayo yana uwezo wa kukupatia utajiri kuliko kujikita kwenye majanga ya nchi ambayo huwa yanarudisha nyuma jitihada za watu. Akili na mtazamo wako wote uwe kwenye utajiri badala ya umasikini. Kila unapoongea na watu onesha kuwa kila mtu anaweza kuwa tajiri na rasilimali za kuwezesha kila mmoja kufikia utajiri anaotamani zipo za kutosha hivyo hakuna haja ya kushindana.

20. Kanuni ya saba: Utajiri unakuja kwako kwa kufanya vitu katika hali flani (acting in certain way). Kuwa na fikra na pamoja na picha ya vitu unavyotaka katika akili yako hakujitoshelezi bila ya kuchukua hatua za kivitendo. Fikra zinatakiwa kuunganishwa na vitendo katika majukumu yako ya kila siku. Kupitia fikra unaweza kuvuta chochote katika umiliki wako lakini umiliki huo unakamilika kwa kupitia vitendo. Kumbuka unatakiwa kutoa thamani kubwa kwa wengine ili nao wakupatie kile unachohitaji. Husidhurumu au kuiba kwa ajili ya kufanikisha kupata kitu kilichopo katika akili yako na badala yake unatakiwa kutumia mbinu halali za kuvuta vitu kwenye umiliki wako. Kwa ujumla ni lazima utambue kuwa vitu unavyovitaka vipo kwenye mikono ya watu wengine na vinapatikana kwa kubadilishana thamani kwa thamani.

21. Kupitia fikra kitu unachohitaji kinakuja kwako hila unapokea au kumiliki kitu husika kupitia vitendo. Hivyo, tunapokea kupitia vitendo na kama hauweki bidii katika kazi kwa maana una tabia za uvivu unajikwamisha kumiliki vitu unavyotamani kupitia mfuko wako wa fikra. Na unatakiwa kuchukua hatua mara moja bila kuhairisha kwa maana wakati sahihi ni sasa na mazingira sahihi ni hayo uliyonayo. Hauwezi kufanya katika yaliyopita au yajayo lakini unachoweza kufanya ni kuanzia pale ulipo. Kile ulichonacho ni msingi namba moja katika kuelekea kwenye mahitaji yako mapya.   

22. Kanuni ya nane: Utajiri unakuja kwako kwa kutekeleza majukumu yako kwa ufanisi. Ulimwengu unaendelezwa na wale ambao wanatekeleza majukumu yao kwa ufasaha na wale ambao hawatekelezi majukumu yao ipasavyo ni mzigo kwa serikali, ndugu au wazazi. Hivyo, kutokutekeleza majukumu yako kwa ufanisi ni kukwamisha kasi ya maendeleo katika jamii unayoishi. Kila siku ipo kwa ajili yako kufanikiwa au kutofanikiwa na majumuisho ya siku unazofanikiwa ndiyo yanaamua mafanikio yako. Kama kila siku unashindwa kufanikiwa kulingana na mipango ya siku husika kamwe husitegemee kuwa ipo siku utafanikiwa kuwa tajiri. Husidharau kufanya vitu vidogo vidogo kwa kuwa vitu hivyo kwa pamoja vinatengeneza ushindi mkubwa. Kila siku hakikisha unafanya yote ambayo yalitakiwa kufanyika katika siku husika kwa ufanisi mkubwa kwa maana haujui kesho itakuwaje.

23. Kila kitendo unachofanya katika kutekeleza majukumu yako ni lazima kiwe na uhusiano wa moja kwa moja na picha iliyopo katika fikra zako. Hivyo kila hatua unayopiga ni ukamilisho wa vitendo ambavyo kwa pamoja vinapelekea ushindi. Hivyo, muunganiko wa nguvu ya akili (mental power) na nguvu ya mwili (physical power) ni muhimu kwa kuwa vyote vinafanya kazi kwa kutegemeana kwa ajili ya kukamilisha hitajili kuu kwa wakati husika.

24. Kanuni ya tisa: Utajiri unakuja kwako kwa kuchagua sekta au fani sahihi ya kufanyia kazi. Kila mtu amepewa kalama na vipaji ambavyo anatakiwa kuvitumia kwa ajili ya kutengeneza utajiri anaohitaji. Kwa ujumla ili uwe tajiri unatakiwa kuchagua fani ambayo itakufanya utumie ipasavyo kalama na vipaji vyako. Pia, unatakiwa kutambua kuwa vipaji vinaendelezwa hivyo kama kuna sekta ambayo unaona ni muhimu kwako hila hauna uzoefu wa kutosha mamlaka ya kujiendeleza katika sekta hiyo ipo ndani ya uwezo wako. Kwa ujumla katika kuchagua kazi au fani hakikisha unachagua kazi/fani ambayo unaipenda kutoka rohoni. Hii ni kutokana na ukweli kwamba ni rahisi kufanikiwa kikazi kupitia fani unayoipenda kuliko kwenye kazi ambayo umeingia ili mradi tu kwa kuwa umekosa mbadala. Kazi unayoipenda kutoka rohoni inaambatana na msukumo wa matamanio ya kufanya kazi na msukumo huo ndiyo kichocheo cha kujituma katika kazi.

25. Kama upo kwenye kazi au fani ambayo huipendi unaweza kuitumia kazi hiyo kwa ajili ya kujiendeleza kufikia kwenye fani/kazi ya matamanio yako. Husiridhike kuendelea kuishi katika mazingira ya kazi ambayo haikufanyi ufurahie Maisha kutokana na majukumu yako ya kila siku. Pale inapobidi kuwa tayari kubadilisha mazingira ya kazi kwa ajili ya kuiridhisha nafsi yako na kuyafurahia Maisha kwa mapana yake. Pale unapokuwa na shaka katika maamuzi yako hakikisha unaongeza muda kutafakari na kutoa shukrani ili ufunuliwe zaidi kwenye maamuzi ambayo unakusudia kuchukua. Ondoa wasiwasi na hofu kwenye maamuzi unayokusudia kufanya kwa kuwa ipo nguvu kuu ambayo inakuongoza kufanya maamuzi sahihi.

26. Kanuni ya kumi: Utajiri unakuja kwako kwa kama una mtazamo wa kuongezeka au kukua zaidi (the impression of increase) na mtazamo huo unatakiwa kuunesha kwa kila mtu ambaye unabahatika kukutana nae. Kuongezeka au kukua zaidi ni hitaji la kila mtu kwa kuwa ni kupitia kukua/kuongezeka mwanadamu anatumia vipaji vyake vyote kwa faida ya viumbe wote. Hali hii kila mwanadamu amerithi toka enzi za kuumbwa kwake na ni kutokana na hali hiyo kila mtu anahitaji kupata chakula zaidi, kuwa na mavazi bora, kupata nyumba nzuri, kutembelea sehemu zenye mvuto na msisimko au kumiliki kila rasilimali zenye viwango bora. Pale msukumo wa kukua au kuongezeka zaidi unapoisha ni dalili za kuwa mhusika Maisha yake yanahitimishwa. Hivyo, kutoridhika na hali ya uliyonayo siyo dhambi bali ni hatua muhimu katika Maisha kwa ajili ya kuongezeka au kukua zaidi.

Haya ni machache kati ya mengi ambayo mwandishi ametushirikisha katika kitabu hiki. Kuna sayansi ya kuwa tajiri na kupitia kitabu hiki tumeshirikishwa mbinu muhimu za kuvuta utajiri katika Maisha yetu. Sayansi hii inafanya kazi pale ambapo una dhamira ya kweli ya kufanikiwa kimaisha hila kama dhamira yako inayumbayumba utaona kuwa mbinu zilizoshirikishwa katika kitabu hiki ni za uongo. Jiunge na mtandao wa Fikra za Kitajiri kwa  KUBONYEZA HAPA.

Karibuni kwenye fikra za kitajiri ili upate elimu isiyokuwa na mwisho.

Born to Win ~ Dream Big 

Mwalimu Augustine Mathias

Namba ya Simu:      +255 786 881 155
Mwanzilishi wa Mtandao wa 
fikrazakitajiri.blogspot.com
Barua pepe:  fikrazatajiri@gmail.com