MWENDELEZO WA MASWALI KUHUSU KIFO KULINGANA NA IMANI YA “KARMA”: SEHEMU YA MWISHO.

NENO LA LEO (MACHI 26, 2021): MWENDELEZO WA MASWALI KUHUSU KIFO KULINGANA NA IMANI YA “KARMA”: SEHEMU YA MWISHO.

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni wakati mwingine tena tunapata nafasi ya kutafakari juu ya hatma ya maisha yetu. Leo ni siku ya kipekee ambapo kama taifa tunaenda kumlaza mpendwa wetu, Rais na Jemederi Hayati Dkt. John Joseph Pombe Magufuli katika nyumba yake ya kudumu. Ni ngumu kumeza au kuamini kuwa ndiyo siku ya mwisho ya kuipoteza sura yake lakini hatuna namna zaidi ya kukubaliana na ukweli huo. Neno la tafakari ya leo ni mwendelezo wa kujifunza kuhusu maisha ya mwanadamu na kifo kupitia mafundisho ya “Karma”. Karibu tujifunze kwa pamoja.

Kama bado hujajiunga na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI kwa ajili ya kupata neno la tafakari kila siku, tafadhali JIUNGE SASA. 

Swali #5: Je kuna kuzaliwa upya baada ya kifo. Kulingana na Imani ya Wakristu au Waislamu hakuna kuzaliwa upya kwa mwili baada ya kifo japo Wakristu wanaamini katika ufufuko siku ya mwisho. Hila kulingana na Imani ya Hindu (Hinduism) wanaamini katika kuzaliwa upya kwa mwili na hiyo ni matokeo ya neema ya Mungu ambaye unamwamini. Muhimu ni kushikilia kile ambacho Imani yako inakufundisha japo unaruhusiwa kutumia mafundisho ya dini nyingine kama sehemu ya kukua kiimani. Jambo moja ambalo kila dini inafundisha ni kutenda wema, kuacha dhuruma, kuishi kwa tumaini la maisha ya baadae, na kuishi maisha yanayogusa wengine.

SOMA: MASWALI KUHUSU KIFO KULINGANA NA MAFUNDISHO YA “KARMA”: SEHEMU YA KWANZA

Swali #6: Baada ya kifo roho huwa inaenda wapi? Roho huwa haizaliwi na huwa haifi kwa kuwa ina umilele. Kinachozaliwa na kufa ni mwili. Kulingana na mafundisho ya Imani ya Hindu, baada ya kifo roho huwa inaachana na mwili na wakati huo huo kuingia kwenye tumbo jingine kwa kutafuta yai na manii kwa ajili ya kurutubishwa kwa mwili mpya. Hivyo, kuondoka kwa mwili mmoja ni maandalizi ya mwili mwingine, hivyo hakuna haja ya kuwa na wasiwasi juu ya kile kinachotokea baada ya kufa. Ni kipindi gani roho itaingia kwenye mwili mwingine inategemea na matendo ya mhusika katika kipindi cha uhai wake. Na kulingana na matendo yako inawezapelekea roho ya mhusika kujidhirihisha katika mwili wa Wanyama au kitu kingine kwa kuwa alishindwa kujifunza katika kipindi roho ikiwa kwenye mwili wa kibinadamu.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI 

Mwisho, neno la tafakari ya leo ni mwendelezo wa mafundisho kuhusu kifo hasa kulingana na imani ya dini ya Hindu. Katika kipindi hiki cha msiba wa Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli nimekuwa nikikuletea mafundisho mbalimbali kuhusu kifo na jinsi kukipokea kifo kwa kuwa wote njia yetu ni moja. Hivyo, tutumie mafundisho haya nyakati za huzuni pale tunapoondokewa na wapendwa wetu sambamba na kujiandalia kifo chema. Kumbuka, mbegu ikidondoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Ongeza maarifa yako kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

 👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(