MAJUTO KWA WANAOKARIBIA KUKATA ROHO – SEHEMU YA TATU.

NENO LA LEO (MACHI 30, 2021): [BURIANI JPM] MAJUTO KWA WANAOKARIBIA KUKATA ROHO – SEHEMU YA TATU.

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku 13 kati ya siku 21 za maombolezo ya kifo cha mpendwa wetu, shujaa wa Afrika, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Naendelea kutumia siku hizi kukuletea tafakari zinazohusiana na kifo kwa maana sisi wote tutapitia njia hiyo. Ikiwa wote tutapitia njia hiyo, hatuna budi ya kuwa na uelewa mpana kuhusiana na kifo. 

SOMA: MAJUTO KWA WANAOKARIBIA KUKATA ROHO – SEHEMU YA PILI.

Katika maisha yetu ya kila siku kifo hakikwepeki, kwa maana, kuna kufiwa na wapendwa wet una siku ikifika kufa wenyewe. Ni kutokana na ukweli huo, kila mmoja wetu anatakiwa kutafuta maarifa ya kutosha kuhusiana na kifo ili kupitia maarifa hayo apate kufanya maamuzi sahihi katika maisha ya kila siku. Karibu tuendelee na mafundisho kuhusu majuto kwa wanaokaribia kukata roho katika sehemu ya tatu.

Kama bado hujajiunga na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI kwa ajili ya kupata neno la tafakari kila siku, tafadhali JIUNGE SASA.

"NINATAMANI NINGEJALI KIDOGO HISIA NA FIKRA ZA WENGINE.” Katika maisha yetu ya kila siku mara nyingi tunapuuza hisia, fikra na mtazamo wa watu wanaotuzunguka. Wapo watu wengi ambao wameishi maisha ya kujikita kwenye mambo wenyewe pasipo kufikiria mahitaji ya jamii inayowazunguka. Wapo watu wanaishi pasipo kujali hata kidogo shida wa watu wanaowazunguka kwa kudhania kuwa haya matatizo hayawahusu. Wapo watu wanaishi ndani ya familia moja lakini hakuna anayejali hisia za mwenza wake. Ishi maisha ambayo unatanguliza hisia zako ili mradi hauvunji sheria lakini toa nafasi ya kuguswa na matatizo au changamoto za watu wanaokuzunguka. Mwanadamu ni kiumbe ambacho kinaishi kwenye makundi ya kijamii, hakikisha unakuwa sehemu ya jamii kihisia, kifikra na kivitendo. Mara zote ishi kwa uhalisia, ishi maisha yasiyo na makuu na maisha yenye furaha huku kuamini na kupenda kile unachofanya na kutambua kuwa mtu pekee wa kukupa raha ya maisha unayoitaka yupo ndani mwako.

"NINATAMANI NISINGEISHI MAISHA YENYE HOFU MUDA WOTE." Katika maisha ya kila siku tunatumia muda mwingi kuwa na wasiwasi. Haijalishi una jukumu gani katika maisha yako, iwe ni kuhusu wewe kama mzazi, mwanafunzi, mtoto, Mkurugenzi, Mfanyabiashara, Mkulima, Mtumishi wa Mungu, au kundi lolote lile, kila siku maisha yanakupa kitu cha kuhangaikia. Lakini, kwa nini unaruhusu wasiwasi huu utawale maisha yako? Kwa nini unaruhusu uzito wa mzigo uliopo kwenye majukumu yako utawale maisha yako? Au, utatoa wasiwasi huu na utambue kuwa ulimwengu huu una wasiwasi sana? Ni lini utapunguza wasiwasi ulionao katika majukumu yako ya kila siku na kutambua kuwa mwanadamu mengi anayohofia si yote yanatokea katika maisha yake? Pamoja na kuendekeza hofu na wasiwasi katika maisha yako ya kila siku tumia muda wako kutafakari kuwa yote unayoangaikia siku ya mwisho wa maisha yako hayatakuwa na maana kwako. Siyo pesa, siyo deni la bili unazodaiwa, siyo matatizo ya wazazi au wanao, siyo majukumu ya kazi yako wala chochote ambacho kitakuwa na umuhimu katika muda kama huo. Kumbe kwa kuwa maisha yetu hapa Duniani ni mafupi mno ni ubatili mtupu kuishi maisha yanayotawaliwa na hofu, huzuni na wasiwasi wa kila aina kutokana na majukumu yetu ya kila siku.

"NINATAMANI NINGELITUNZA/KUJALI AFYA YANGU." Mwili wenye afya bora ndiyo kila kitu kwa mwanadamu. Ikiwa afya yako imeteteleka, huna chochote unachoweza kufanya kwa kufanisi kwa unajikuta katika maisha yasiyo kuwa na tumaini la baadae, hivyo, huna budi kuilinda afya yako. Tumia muda wako kukwepa maradhi au magonjwa ambayo yapo ndani ya uwezo wako wa kuyazuia. Mara zote katika maisha ya kila siku unatakiwa kutambua kuwa una mwili mmoja, akili, na roho moja na hivyo utimamu na ufanisi wake unategemea mwili wenye afya bora.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI 

Mwisho, neno la tafakari ya leo ni mwendelezo wa mafundisho kuhusiana na majuto kutoka watu wanaokaribia kukata roho. Yamkini majuto hayo ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Kumbe, tunaweza kutumia majuto haya kuboresha maisha kila sekta ya maisha yetu. Kumbuka, mbegu ikidondoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Ongeza maarifa yako kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(