DONDOO 10 KUHUSU MAFANIKIO KUTOKA KWA ALEX FERGUSON

 

NENO LA LEO (MACHI 09, 2021): DONDOO 10 KUHUSU MAFANIKIO KUTOKA KWA ALEX FERGUSON

Habari ya leo rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine ambayo ni matarajio yangu kuwa umeianza kwa kutekeleza yale ambayo yanakupa muunganiko wa matokeo kila siku. Ikiwa kila siku unafanikiwa kuunganisha jitihada zako hakika husikate tamaa kwa kuwa moja jumlisha moja haijawahi kuwa moja.

Kama bado hujajiunga na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI kwa ajili ya kupata neno la tafakari kila siku, tafadhali JIUNGE SASA.

Katika tafakari ya leo nitakushirikisha dondoo kumi za mafanikio kutoka kwa aliyewahi kuwa Kocha wa Timu ya Manchester United. Kocha huyu mwenye mafanikio makubwa kupitia Kitabu cha “Alex Ferguson My Autobiography” ameshirikisha hisitoria ya maisha yake. Itakumbukwa kuwa Sir Alex Ferguson ni kati ya makocha ambao hauwezi kutaja mafanikio ya klabu ya Manchester United pasipo kutaja jina lake kutokana na heshima ya mafanikio aliyojijengea kwa kipindi chote cha miaka 27 (1986/17 – 2012/13) akiwa timu hii. Karibu ujifunze dondoo kumi kati ya mengi anayotushirikisha katika kitabu hicho:-

Moja, Ili kupata mafanikio ya muda mrefu ni lazima uwe na uvumilivu. Maisha ya mafanikio yanaanzia kwenye kilima ambacho mwanzo wa safari utaona kama vile ni ndoto kufanikiwa kupanda kilima hicho. Hii ni kutokana na hali ambayo yeye mwenyewe alikumbana nayo kipindi anakabidhiwa timu mwaka 1986.

Mbili, Ili ufanikiwe ni lazima uwe na watu wanaokusapoti kwanza kabisa ukianzia na familia yako. Mara nyingi tumekuwa tukisikia msemo wa “kila kwenye mafanikio ya mwanamme fahamu kuwa kuna mwanamke nyuma yake”. Kocha Sir Alex Ferguson amedhihirisha msemo huu kwa kutuambia kuwa mafanikio yake kwa ujumla yalichangiwa na sapoti ya mwenza wake na watoto wake kwa ujumla.

Tatu, Mafanikio ya kesho yanajengwa na msingi imara wa leo. Sir Alex Ferguson anatushirikisha kuwa katika maisha yake kuna kipindi alifikiria kuwa angefukuzwa kutokana na imani yake ya kujenga timu ya vijana jambo ambalo lilipelekea timu kuyumba katika michezo ya ligu kuu. Lakini kwa vile alikuwa na nia thabiti kwenye kazi yake alifanikiwa kuwashawishi viongozi wake na hatimaye akajenga timu imara ambayo ilishinda mataji mengi.

Nne, Ili upate mafanikio ni lazima utafute changamoto mpya kwa kuhama mazingira uliyokulia na kutafuta sehemu mpya. Sir Alex Ferguson alianzia kazi yake nchini mwake (Scotland) lakini baada ya kuhamia Uingereza alifanikiwa kupata changamoto nyingi ambazo zilimjenga katika kazi na hatimaye kufanikiwa kustaafu akiwa kocha mwenye mafanikio zaidi.

Tano, Ili ufanikiwe ni lazima dhamira yako yote iwekwe kwenye kazi husika unayofanya. Sir Alex Ferguson anatushirikisha kuwa kuna kipindi aliwahi kuhojiwa kuwa kwa nini timu yake ikiwa uwanjani hajawahi onekana akiwa na tabasamu na yeye alijibu kuwa timu yake ikiwa inacheza sio sehemu ya kutabasamu bali ni sehemu ya kutafuta ushindi basi. Muhimu hapa tunafundishwa kuthamini kazi zetu kwa kutuliza akili zetu (mind concentration) pindi tunapowajibika.

Sita, Mafanikio ya aina yoyote ile yanajengwa kwenye msukumo wa dhati wa kuhitaji mafanikio kwa kila hali. Sir Alex Ferguson anatushirikisha kuwa yeye binafsi baada kuondoka Scotland na kuhamia Uingereza alienda akiwa na nia moja nayo si nyingine bali ni kufanikiwa katika kazi yake mpya.

Saba, Jamii inayokuzunguka inatazama mabaya yako na kusahau mema uliyotenda. Hii ni sawa na msemo uliyotumiwa na Bwana Yesu kuwa “watu wanataka mikate” kwa maana ya kwamba watu wapo kwa ajili ya mazuri unayofanya na hasa kwa faida yao na pale unapoteleza kidogo hakuna hata mmoja atakumbuka wema wako wa jana. Sir Alex Ferguson anatushirikisha kuwa katika kipindi chake chote ilikuwa ni kawaida mashabiki kumtukaba kutokana na timu kupoteza mchezo mmoja tu huku wakisahau makombe yote waliyowahi kushinda akiwa kocha wa timu.

Nane, Muda wote kuwa tayari kwa changamoto na fursa mpya pasipo kujali umri wako ili kuepuka kukaa bila kazi. Sir Alex Ferguson anatushirikisha kuwa yeye binafsi baada kustaafu akiwa na umri wa zaidi ya miaka sabini aliamua kutafuta fursa mpya ili apate changamoto na uzoefu mpya na hatimaye kuepuka kukaa bila kazi.

Tisa, Kubali kuteseka kwa ajili ya mafanikio ya baadae. Mwandishi anatushirikisha kuwa katika miaka 39 aliyofanya kazi ya ukocha mara nyingi alipata hamasa ya kusonga mbele pasipo kujali ugumu wa matokeo kwani aliamini katika msemo wa mazuri yanakuja kutokana na mateso ya sasa. Kwa maana nyingine mafanikio yako ya kesho yanaandaliwa na bidii na jitihada zako za sasa.

Kumi, Chimbuko/asili yako haina nafasi ya kuamua hatma ya mafanikio yako. Sir Alex Ferguson anatushirikisha kuwa wapo wengi ambao walimbeza kutokana na chimbuko lake hasa ikizingatiwa kuwa alizaliwa katika wilaya ambayo shughuli kubwa ya kiuchumi ilikuwa kutengeneza meli. Wengi walidhani kuwa hakuwa na lolote katika tasnia ya mpira ingawa kadri muda ulivyosogea walinyamazishwa na mafanikio yake. Na hapa mwandishi anatushirikisha kuwa ukifuatilia maisha ya watu wengi wenye mafanikio utagundua kuwa wengi wao wamekulia katika mazingira magumu kuanzia kwenye familia hadi jamii zilizowazunguka.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI 

Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza dondoo kumi kuhusu mafanikio kutoka kwa Sir Alex Ferguson. Ni dondoo rahisi ambazo tunaweza kuzitumia katika maisha ya kila siku na hatimaye kufanikiwa kupiga hatua katika yale tunayofanya. Kumbuka, mbegu ikidondoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(