Januari, 2017 Umetuachaje?

Habari ya leo rafiki na msomaji wa mtandao wa fikra za kitajiri. Ni matumaini yangu kuwa upo vizuri na unaendeleza mapambano kwa ajili ya kuyaboresha maisha yako. Ni jambo la heri kuona kila siku unapambana kwa ajili ya kesho iliyo bora. Hongera sana rafiki yangu.

Karibu tena katika makala yangu ya leo ambayo inalenga kukumbusha misingi uliyojiwekea mwaka 2017 kwa ajili ya kuyaboresha maisha yako. Imekuwa ni kawaida kwa walio wengi kila tunapoanza mwaka mpya tunajiwekea malengo kemukemu kwa ajili ya kuyatimiza katika kipindi cha mwaka husika.


Pamoja na kujiwekea malengo, kwa walio wengi tumekuwa tunajikuta tunarudia maisha yetu yaleyale na pengine kuyasahau kabisa yale tuliyolenga kutekeleza. Kadri siku zinavyokwenda watu wengi wanasukuma majukumu waliolenga kutekeleza kwenye siku za mbele na hatimaye wanajikuta mwaka unaisha pasipo kutekeleza jambo lolote kati ya yale waliopanga kuyatekeleza kama kawaida wanajisemea haya nitayatekeleza mwaka kesho.

Rafiki yangu leo hii naomba tunapomaliza mwezi wa kwanza katika mwaka 2017 hebu tujiulize mpaka sasa tupo kwenye njia sahihi ya kufikia yale tulopanga hama tunaendelea na mfumo ule ule.

Tunapomaliza mwezi wa kwanza kati ya miezi 12 ya mwaka 2017 karibu tutafakali wote maswali haya:

1# Je mimi ni yuleyule wa mwaka 2016?. Katika swali hili mpendwa rafiki yangu naomba ujiulize maswali ya namna ambavyo umebadilika kifikra, tabia, kimtazamo na vitendo kwa kipindi hiki cha mwezi mmoja ukilinganisha na mwaka 2016. Kama wewe ni yule yule wa mwaka 2016 sahau kabisa mwaka 2017 kupiga hatua kubwa ukilinganisha na mwaka uliopita.


2# Je unakumbuka yale ambayo umelenga kuyakamilisha mwaka huu?. Rafiki wengi tunaishia kusema mwaka mpya na mambo mapya lakini je hayo mapya kweli tunayatambua? Je tumeainisha yale ambayo yanatakiwa kupewa kipaumbele mwaka huu? Je mpaka sasa bado unayakumbuka yale ambayo umejipanga kuyatekeleza. Ushauri kama haukuandika malengo yako kwa mwaka huu bado muda upo nakushauri ufanye hivyo mapema iwezekanavyo na baada kuyaandika yavunjevunje kwa miezi kumi na moja iliyobakia kwa ajili ya kujitathimini kwa muda uliobakia.

3# Je nimeanza kuchukua hatua?. Rafiki malengo pasipo kuweka jitihada za kuyafanikisha ni sawa kutegemea kuendesha gari lisilokuwa na mafuta. Kama kweli unataka mwaka 2017 kuwa wa mafanikio kwako ikilinganishwa na miaka mingine anza mara moja kuchukua hatua pasipo kujali urefu wa hatua zako cha msingi ni wewe kuanza mara moja.


4# Je nimeanza kudhibiti matumizi yangu ya fedha?. Tunafahamu fika kuwa fedha ni muhimili wa kutuwezesha kusonga mbele katika yale tunayofanya. Na bila ya kudhibiti matumizi yetu ya fedha hatuwezi kufanikiwa kusonga mbele hivyo ni vyema kuhakikisha tunapoendelea na mwaka 2017 tujiwekee misingi ambayo itadhibiti matumizi ya fedha tunazopata pasipo kujali kiasi cha fedha hizo.


5# Je nimerejesha uhuru wangu?. Swali hili msingi wake mkuu ni jinsi gani ambavyo tumekuwa watumwa wa simu zetu. Tumeshindwa kudhibiti hisia zetu linapokuja suala la matumizi ya simu kisasa (smart phone) kutokana na ukweli kwamba simu hizi zinatumia muda wetu mwingi hasa kwenye mitandao ya kijamii ambako kila muda kuna meseji za hovyo zinazotumwa. Rafiki kama unataka mwaka 2017 uwe wa mafanikio kwako hakikisha unarejesha uhuru wako kwa kupanga muda unaotakiwa kuingia kwenye simu yako na hata pale unapokuwa kwenye simu yako hakikisha una vipaumbele vya kufanya.

Haya ndiyo maswali ambayo nimekushirikisha tunapomaliza mwezi wa kwanza katika mwaka 2017. Ni matumaini yangu kuwa endapo utayafanyia kazi utabadilisha maisha yako na hivyo kupiga hatua ili  mwaka 2017 uwe wenye mafanikio kwako. Niendelee kukuomba usambaze jumbe hizi kwa kadri uwezavyo ili yale unayojifunza yawafikie wengi na hatimaye tufanikiwe kuibadilisha dunia hii kuwa mahali pazuri pa kuishi. Nakutakia mapambano mema.

Ili kupata makala za namna hii moja kwa moja kwenye barua pepe yako BONYEZA HAPA

Karibuni kwenye fikra tajiri ili upate elimu hisiyokuwa na mwisho.
Born to Win~Dream Big
A.M. Bilondwa
0786881155
fikrazatajiri@gmail.com


Jiunge na Mtandao wa Fikra za Kitajiri

* indicates required

onclick='window.open(