Ardhi Ni Mali: Fahamu Kwa Nini Unapaswa Kuwekeza Kwenye Ardhi - Sehemu ya Pili

Habari ya leo rafiki na msomaji wa fikra za kitajiri. Nimatumaini yangu kuwa upo vizuri na unaendelea kupambana kwa ajili ya kuyaboresha maisha yako. Ni jambo la heri kuona kijana kama wewe umefanya uamzi wa hatma ya maisha yako. Kama ambavyo nimeendelea kukusihi kupitia mtandano huu kuwa suala la mafanikio ya maisha yako lipo mikononi mwako na hivyo wewe ndo mwenye wajibu wa kuhakikisha kila iitwapo leo unapambana kuhakikisha unatimiza ndoto za maisha yako.

Katika makala yangu ya wiki iliyopita kuhusu uwekezaji kwenye ardhi nilikushirikisha sababu muhimu ambazo zinaifanya rasilimali ardhi iendelee kuwa kati ya vitega uchumi ambavyo ni msingi wa shughuli nyingi za kukuza utajiri kwa wale ambao wametambua umuhimu wa rasilimali hii. Kwa ufupi tuliona namna ambavyo ongezeko la watu linavyozidi kuongezeka siku hadi siku na hivyo kuongeza kasi ya mahitaji ya ardhi kwa ajili ya shughuli za uzalishaji, makazi na biashara.


Katika makala ya leo nitakushirikisha kwenye aina ya maeneo ambayo unapaswa kuyapa kipaumbele pale unapotaka kuwekeza kwenye ardhi. Karibu ujifunze kitu kwa ajili ya kuyaboresha maisha yako:-

1. Maeneo ya Ardhi ya Bondeni. Ardhi ya bondeni ni kati ya maeneo ambayo yanatafutwa kwa kasi kutokana na mahitaji yake makubwa kwenye shughuli za kilimo. Hii ni kutokana na maeneo haya kuwa na faida kubwa ikilinganishwa na maeneo mengine. Baadhi ya faida ya ardhi ya bondeni ni uwepo wa rutuba nyingi na ukaribu wa vyanzo vya maji (chanzo kinaweza kuwa mto au kuchimba kisima). 

Somo kubwa ambalo nalenga ulipate hapa ni kuhakikisha unamilikia ardhi ambayo utaitumia kwa uzalishaji wa shughuli za kilimo/ufugaji kwa kipindi chote cha mwaka mzima. Unaweza kuwekeza kwenye kilimo cha mbogamboga, ndizi, mahindi ya kiangazi, miwa pamoja na ufugaji wa kuku, nguruwe au mbuzi kutokanana na uhakikika wa maji katika maeneo haya.

2. Maeneo ya Senta/Mitaa ya Pembezoni mwa Miji. Kama nilivyokushirikisha katika makala yangu ya kwanza kuwa mojawapo ya sababu muhimu ya kuwekeza kwenye ardhi kuwa ni kukua kwa miji/majiji. Leo hii nataka nikufahamishe kuwa kama kwa sasa hauna mtaji wa kutosha wa kununua ardhi katikati ya mji unachotakiwa kufanya ni kwenda kwenye senta/mitaa ambazo zinachipukia kimaendeleo kuzunguka mji/jiji. 

Katika maeneo kama haya ni rahisi kupata ardhi ya kutosha kwa bei nafuu na hatimaye eneo hilo kuongezeka thamani kutokana na kukua kwa kasi miji. Kwa baadae unaweza kuomba kibali kwa ajili ya kupima eneo lako na kulirasimisha kwenye mpango wa ardhi wa mji/manispaa/jiji.

3. Maeneo yanayofaa kwa ajili ya Kilimo cha Miti. Katika sehemu ya kwanza ya mwendelezo wa makala za umuhimu wa uwekezaji kwenye ardhi nilikushirikisha kuwa unaweza ukapanda miti kwenye eneo lako kama sehemu ya kulinda ardhi yako hisivamiwe na watu. Leo naomba ufikirie upandaji miti kwa mtazamo wa uwekezaji wa kilimo biashara cha miti. Unaweza kuwekeza kwenye kilimo cha miti ya mbao au matunda na hivyo kimsingi unatakiwa kuangalia maeneo yanayofaa kwa ajili ya ustawi wa miti. Mfano, katika nchi ya Tanzania mikoa ya Iringa, Njombe, Morogoro, Kagera, Mbeya, Moshi na Arusha ni mikoa inayoongoza kwa kuwa na ardhi inayofaa kwa kilimo cha Miti ya Mbao na Matunda. 

Haya ndiyo machache niliyokushirikisha katika sehemu ya pili ya makala hii ambazo kwa pamoja zimekupa mwanga wa kwanini unapaswa kumiliki ardhi. Naamini ukitumia elimu hii itakusaidia kufikia ndoto za maisha yako. Nakutakia mapambano mema.

Ili kupata makala za namna hii moja kwa moja kwenye barua pepe BONYEZA HAPA. 

Karibuni kwenye fikra za kitajiri ili upate elimu hisiyokuwa na mwisho.

Born to Win~Dream Big
Augustine Mathias Bilondwa
0786881155
fikrazatajiri@gmail.com



Jiunge na Mtandao wa Fikra za Kitajiri kwa Kujazo Fomu Hii

*Lazima ijazwe

onclick='window.open(