NENO LA SIKU_JANUARI 30/2022: Je! Wajua Fumbo Kuu la Maisha Yako Hapa Duniani?
📝Ni siku nyingine ambapo tumefanikiwa kupata kibali cha kuwa hai. Hongera kwa kufanikiwa kupata kibali hiki ambacho ni tiketi ya kuendelea kuboresha maisha yako.
Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA
📝Karibu tena katika makala ya siku ya leo ambapo nitaangazia kuhusu maisha ya mwanadamu dhidi ya mafumbo yanayomkabili katika kipindi chote cha uhai wake. Ni dhahiri kuwa maisha ya mwanadamu yanaanzia kwenye utungisho wa mimba pale manii ya kiume inapokutana na yai la kike hadi ukomo wa maisha hayo, kwa maana, kifo.
📝Kipindi chote cha uhai wa mwanadamu utawaliwa na mafumbo ambayo humfanya mwanadamu kutokuwa na majibu ya moja kwa moja. Kiumbe mwanadamu akiwa bado tumboni mwa mama yake hukabiliwa na fumbo la giza linalomzunguka.
📝Pamoja na giza hilo angalau maisha kwa kiumbe huyu yanakuwa siyo ya wasiwasi ikilinganishwa na maisha baada ya kuzaliwa. Baada ya kuzaliwa mtoto, siku yake ya kwanza anakabiliwa na hofu kutokana na mabadiliko ya ghafla kutoka gizani hadi kwenye nuru.
📝Kipindi chote cha utoto, mwanadamu anakuwa huru kiasi katika kufikiria mafumbo yaliyopo mbele yake kutokana na akili yake kutojisumbua kuwaza kuhusu maisha ya baadae. Hitaji lake kubwa katika kipindi hiki ni kuona anatimiziwa mahitaji muhimu kama vile usalama, chakula au mavazi. Zaidi ya hayo anataka apate muda wa kutosha kwa ajili ya kucheza na watoto wa rika lake.
📝Kipindi cha utoto, hufuatiwa na kipindi cha ujana hadi uzee ambapo mwanadamu mwenye akili timamu hutawaliwa na fumbo kuu la maisha ya baadae. Ni kipindi cha kujiuliza maswali yasiyo na majibu ya uhakika kuhusu kesho itakuwaje kiafya, kiuchumi, kiusalama, kikazi, kibiashara, kimahusiano au kiroho.
📝Kipindi hiki hutawaliwa na maswali mengi kuhusu asili ya mwanadamu (kwa maana yeye ni nani na chanzo cha uhai wake ni kipi); ulimwengu unaomzunguka (kwa maana jamii na mazigira), jinsi ya kuishi kwa fadia (yeye na wanaomzunguka) na hatima ya mwisho wa maisha yake.
📝Kuhusu hatima ya mwisho wa maisha, mwanadamu anajiuliza maswali mengi yanayohusiana na mwisho wa maisha yake na kwa nini bado anaishi ikilinganishwa na wale ambao wametangulia mbele za haki. Kubwa zaidi katika hatua hii ni fumbo la lini na jinsi gani safari yake itahitimishwa kwenye uso wa dunia hii.
📝Kutokana na mafumbo hayo, mwanadamu anajikuta kwenye kutafuta mbinu mbalimbali za kuishi kwa kupunguza uoga wa maisha ya baadae yasiyotabirika (reducing the fear of uncertainty in future life). Hapa ndipo mwanadamu anajaribisha kanuni, mifumo na miongozo mbalimbali ya maisha.
📝Katika majaribio hayo, wapo ambao wanapotea njia na wapo wanaofanikiwa kuishi misingi bora inayopunguza maswali kwenye maisha ya baadae. Wale wanaopotea siyo kwamba wanapotea kwa kupenda, wengi wao wanakosa au huchelewa kupata miongozo sahihi.
📝Kusudi kuu kwangu mimi na wewe ni kuhakikisha tunakuwa miongoni mwa wanadamu wanaofanikiwa kupata majibu ya mafumbo ya maisha ili kufanikiwa kuishi maisha yasiyo na hofu juu ya maisha ya baadae.
📝Tunatakiwa kuishi kwa kupunguza hofu kuhusu mstakabali wa maisha yetu kiafya, kiusalama, kiuchumi, kimahusiano, kikazi, kiroho na utayari wa kukabiliana na kifo katika maisha ya kila siku.
📝Nihitimishe kwa kusema kuwa, katika kuhakikisha napunguza idadi ya watu ambao wanapotea njia kutokana na kukosa au kuchelewa kupata miongozo sahihi ya kuishi maisha yasiyo na hofu kuhusu kesho, nimekuandalia kitabu bora cha MAISHA YENYE THAMANI.
📝Hiki ni kitabu ambacho kitakuwezesha kuishi maisha ambayo yanajikita kwenye misingi ya asili ya kuumbwa kwako ili kupunguza uoga wa maisha yajayo. Ni kitabu ambacho natamani kisomwe na watu wengi ili kupunguza mateso ambayo mwanadamu wa sasa anapitia katika maisha ya kila siku.
📌Karibu ujipatie nakala yako!
Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.
Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.
onclick='window.open(