NENO LA SIKU_JANUARI 28/2022: Je! Unahitaji Kuishi Maisha Hai? Fahamu Misingi Inayounda Utu Wako!
📝Pole na majukumu ya siku ya leo. Naamini kuwa unaendelea vyema katika majukumu yako ya siku hii ya leo.
📝Karibu kwenye neno la siku ili uendelee kujiongezea maarifa yanayolenga kupanua ufahamu wako kuhusu wewe ni nani katika mazingira yanayokuzunguka.
📝Katika makala hii kwa ufupi nitagusia kwenye ubinadamu wetu katika maisha ya kila siku. Katika ubinadamu huo, kipekee nitaelezea kuhusu utu na misingi inayounda utu wa mwanadamu.
📝Mwanadamu tofauti yake na viumbe wengine ni kupewa zawadi ya Uwezo wa kufikiri (reasoning), Kutatua matatizo yanayomkabili (ability to solve complex problems) na Mfumo wa mawasiliano kupitia lugha (well developed language communication skills).
📝Pamoja na zawadi hiyo, uhusiano wa mwanadamu na watu wengine unakamilishwa na utu wa mhusika ambao ni zao la makuzi, malezi na mazingira ambayo mhusika amekulia.
📝Mwanadamu hasiye na utu dhidi ya jamii inayomzunguka, tabia zake ni sawa na wanyama wengine kama vile Simba, Chui au Mbwa mwitu na wengineo.
📝Hivyo, ndiyo utu unatufanya tuwe mwanadamu na una nafasi kubwa ya kuamua aina ya maisha tunayoishi hapa Duniani.
📝Kumbe, kwa kiumbe mwanadamu ambaye maisha yake hutegemea makundi ya kijamii, utu ni kiungo muhimu kwake katika kudumisha mahusiano. Hata hivyo, utu wetu hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine katika jamii moja.
📝Hapa ndipo tunahitaji kufahamu misingi inayounda utu wetu. Utu wa mtu ni matokeo ya ukuaji au maendeleo ya vitu vitatu ambavyo ni: i) Id ii) EGO na iii) SUPER EGO.
📝Je! Umewahi kujiuliza maneno hayo yanamaanisha nini katika maisha yako?
📝Je! Jinsi ulivyo kwa maana ya mtazamo, tabia na vitendo vyako vya kila siku vina uhusiano gani na maneno hayo?
📝Kwa ufupi sana; Id ni sehemu ya utu inayotokana na hatua ya kwanza ya maendeleo ya ubongo wa mtoto. Mara nyingi huwa ni katika kipindi cha miaka ziro (0) hadi miaka miwili kuelekea mitatu (3) na kuna hatari mtu kuendelea katika hatua hiyo hata katika kipindi cha utu uzima ikiwa hakupata mwongozo sahihi.
📝EGO ni sehemu ya utu katika ubongo ambayo inalenga kupunguza utawala wa Id ili mhusika apate kutambua kuwa kuna wengine zaidi yake. Inahusisha akili ya mwanadamu kuanza kutambua kuwa kuna kanuni ambazo anatakiwa kuzitii. EGO hukua kwa kasi kati ya miaka mitatu (3) hadi mitano (5).
📝SUPER EGO ni sehemu ya tatu inayounda utu katika ubongo wa mwanadamu. Sehemu hii hudhibiti Id kuepuka maamuzi yasiyokubalika katika jamii. Inahusisha mtu kuanza kujua maswala ya kijamii kama vile misingi ya dini kwa ajili ya ukuaji wa kiroho.
📝 Hata hivyo, Id, EGO na SUPER EGO hufanya kazi katika akili zetu kila mara, na mtazamo, tabia na matendo tuliyonayo ni matokeo ya kipi kinatawala dhidi ya wenzake, yaani mshindi kati ya Id, EGO au SUPER EGO.
📝Je! Mitazamo, tabia na vitendo vyako vina uhusiano upi na Id, EGO na SUPER EGO katika hatua ya ukuaji uliopo kwa sasa?
📝Je! Una ufahamu wa kutosha kuhusu Id, EGO na SUPER EGO katika kuboresha mahusiano yako kwenye jamii sambamba na kukuza watoto wako vyema katika misingi ya utu unaofaa?
📝Je! Unahitaji kuboresha ufahamu wako kuhusu utu jinsi unavyoundwa kwa ajili ya kurekebisha mitazamo, tabia na matendo yako au kupata misingi bora ya malezi ya mwanao?
📝Kama ndivyo, husiangaike kwa kuwa kitabu cha MAISHA YENYE THAMANI, kimefafanua kwa mapana jinsi ambavyo tabia zetu zinaundwa kuanzia toka tukiwa watoto hadi kipindi cha uzee.
🖊️Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia kiasi cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.
Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.