NENO LA SIKU_JANUARI 27/2022: Kwa Asili Tumeumbwa Kuwa Watafutaji! Kwa Nini Tumepoteza Wajibu Huo?
📝Habari ya rafiki yangu na mfuatiliaji wa masomo ya mtandao wa Fikra za Kitajiri. Ni wakati mwingine napata nafasi ya kukushirikisha machache kwa ajili ya ukombozi wa maisha yetu.
📝Lengo la masomo haya ni kugusa maisha ya wengi ili jamii ipate kutambua kuwa ulimwengu unatudai vitu vya ziada kupitia maisha haya mafupi. Ikiwa wote tutambua Ulimwengu unataka nini kutoka kwetu, maisha kwa viumbe wote yatakuwa endelevu na kwa kufanya hivyo tutapunguza mateso ya kila aina katika maisha yetu.
📝Toka siku ambayo kila mmoja wetu aliumbwa, Ulimwengu ulianza kudai kitu cha ziada kutoka kwenye maisha yake na kitu hiko hauwezi kukilipa ikiwa hautambui thamani ya maisha yako ni ipi! Kumbe, hatua ya kwanza katika kutimiza deni unalodaiwa na Ulimwengu ni kutambua vitu muhimu vinavyoshikilia thamani ya maisha yako.
📝Katika hilo la kudaiwa na Ulimwengu, hatuna budi kutambua kuwa: “Kwa Asili Wote Tumeumbwa Kuwa Watafutaji.” Kwa maana, tumeumbwa kwa ajili ya kuutafuta “ukweli” ambao unahusisha kutafuta majibu ya maswili mengi kama vile: Ni kipi chanzo cha maisha yetu? Kwa nini tunaishi katika ulimwengu huu? Je! Sisi ni nani na maisha yetu ni kwa ajili ya nini? Je! Tunapaswa kufanya nini kwa ajili ya kuishi maisha ambayo yataacha alama vizazi na vizazi?
📝Hata hivyo, pamoja na kwamba kwa asili tumeumbwa kuwa watafutaji, tumepoteza asili kwa kujua au kutokujua. Mwanamahesabu na Mwanafalsafa wa Kifaransa Paschal Braise ndipo aliwaweka watu katika makundi mawili: Watafutaji (Seekers) na Wasio-watafutaji (Non-seekers).
📝Kundi la Watafutaji mara zote wanatamani zaidi kuongeza uzoefu wa maisha na kutumia uzoefu huo kwa faida ya ulimwengu na wao wenyewe. Mara nyingi, Watafutaji hutamani kutazama nyuma kwenye nyakati za maisha yao na kufarijika kutokana na matendo ambayo wameishi huku wakitazamia kuendelea kutoa michango zaidi kwa ulimwengu wa kesho.
📝Kundi la Watafutaji huongozwa na msukumo halisi kutoridhika na kwa kufanya hivyo hujiona wana deni kubwa la kuendelea kutafuta zaidi. Watafutaji ndani mwao huwa wana "hekima angavu" ambayo uwaongoza kuona umuhimu wa kutafuta zaidi kwa faida ya watu wote. Hekima hii angavu mara zote inalia ndani mwao kwa ajili ya kufungua njia mpya za kupunguza mateso kwa wanadamu na viumbe wote.
📝Mfalme Sulemani, mtafutaji na mwandishi wa kitabu cha Mhubiri katika Biblia Takatifu, aliona hekima hii angavu kama zawadi kuu na mzigo mkubwa. Aliiona hekima hii kama hamasa ya kuishi maisha yanayojikita katika kupata wema halisi na yenye thamani ya kweli ambayo inadumu hata baada ya ukomo wa maisha.
📝Kwa kutumia hekima hiyo, Mfalme Sulemani alifanikiwa kuishi maisha yenye kila aina ya mafanikio. Hakuna mtu aliyefanikiwa zaidi katika maisha ya dunia hii kuliko Mfalme Sulemani. Alikuwa tajiri kupita kiasi. Alikuwa mfalme mwenye nguvu zaidi wa siku zake. Alijenga majengo makubwa ya usanifu, alipanda misitu, alilima bustani nzuri, alikuwa na mifugo wengi, dhahabu na kila aina ya utajiri.
📝Mfalme Suleimani, alitumia utajiri wake mwingi kupata na kujionea starehe kuu zinazopatikana katika maisha haya—maisha ya anasa, mamlaka ya kijamii na kisiasa, anasa za kimwili za chakula, vinywaji, na ngono. Hata hivyo alikata kauli kwamba hiyo maisha yalikuwa sawa na “kufukuza upepo” tu ikilinganishwa na ukweli halisi wa kuishi maisha ya thamani aliyoyataka.
📝Hilo ndilo fumbo kuu la maisha, fumbo ambalo watu katika kundi la watafutaji wanatakiwa kuliishi katika maisha yao ya kila siku. Ni kwa bahati mbaya kuwa Ulimwengu tunaoishi una watu wachache sana kwenye kundi la Watafutaji ikilinganishwa na wale ambao hawana la kupoteza yaani wale ambao asubuhi jua lichomoze na jioni jua lizame, kwao kila kitu katika maisha yao ni sawa tu.
📝Hata hivyo, watu wengi wapo kwenye kundi la Wasio-Watafutaji si kwa mapenzi yao bali kwa kuwa hawana msingi sahihi wa kutambua maisha yao si kwa ajili ya kutimiza matakwa yao tu bali faida ya Ulimwengu kwa ujumla.
📝Katika kuhakikisha nakuwa sehemu ya watu ambao wanaishi kwa ajili ya kuacha alama katika Ulimwengu huu, nimetumia kipindi cha maumivu kutokana na ajali niliyopata kuandika kitabu cha MAISHA YENYE THAMANI. Hiki ni kitabu ambacho kinaleta nuru palipo na giza. Hivyo, ni kitabu muhimu kwa ajili ya kupunguza idadi ya watu katika kundi la Wasio-Watafutaji.
📝Ni kitabu ambacho kitakufanya utambue kuwa umepewa kuishi mara moja si kwa faida ya nafsi yako tu au ndugu zako bali faida ya watu wote katika Ulimwengu na viumbe vyote vilivyomo ndani yake.
📝Ni kitabu ambacho kitakufanya kila mara utimize wajibu wako vijana kwa wazee, wazazi, mtumishi wa umma, mfanyabiashara, mkulima au mfugaji, kiongozi wa Serikali, tasisi za dini au taasisi binafsi.
📝Nihitimishe makala hii kwa kusema kuwa: “Hatuwezi kufanikiwa kimaisha ikiwa hatujui misingi halisi ya kuumbwa kwetu sambamba na umuhimu wetu kuendelea kuishi.” Kupitia kitabu cha MAISHA YENYE THAMANI utafanuliwa vya kutosha ili uweze kurudi kwenye misingi ya asili kulingana na makusudi ya kuumbwa kwako.
Kitabu hiki kwa sasa kinapatikana kwa mfumo wa Nakala tete (soft copy) KWA BEI YA ZAWADI ya Tshs. 10,000/= badala ya Tshs. 20,000/=
Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.
Born to Win ~ Dream Big
Mwalimu Augustine Mathias
Namba ya Simu: +255 786 881 155
Mwanzilishi wa Mtandao wa fikrazakitajiri.blogspot.com
Barua pepe: fikrazatajiri@gmail.com