Ujumbe wa Jonathan Lucas KWIYEGA Kuhusu Maudhui ya Kitabu Cha MAISHA YENYE THAMANI

📝Namshukuru sana rafiki yangu Augustine Mathias Mugenyi  kwa kunipa heshima ya kuwa mtu wa kwanza kusoma kitabu cha MAISHA YENYE THAMANI.

📝Kwa heshima hiyo, nimefanikiwa kusoma na kufuatilia kwa karibu sana maudhui ya kitabu hiki kuanzia ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho.

📝Hakika ni kitabu muhimu sana kwa mwanadamu wa karne hii ya 21 kwa kuzingatia kuwa idadi ya watu inaongezeka na kusababisha kasi ya ongezeko la changamoto za maisha katika kila kona ya dunia.

📝Hii ni karne ambayo kuna kila sababu ya mwanadamu aliye hai kimwili na kiroho kufahamu kwa nini anaishi na wajibu wake ni upi kwake yeye mwenyewe, watu wengine, mazingira na kubwa zaidi kwa Muumba wake.

📝Kutambua wajibu huo ni muhimili na msingi muhimu wa kumfanya mwanadamu wa sasa aweze kuishi maisha kamili, tosherevu na yenye furaha. 


📝MAISHA YENYE THAMANI ni kitabu kinachotoa ufafanuzi wa kina kuhusu nyakati za maisha, mahitaji na hatua za ukuaji wa mwanadamu tangu kuzaliwa hadi kufa.

📝Katika kitabu hiki mwandishi ameelezea namna mwanadamu anavyoweza kujitambua na kuishi maisha yenye manufaa, furaha na amani. Ameelezea kwa kina namna ambavyo nadharia mbalimbali za maendeleo na ukuaji wa mwanadamu zinavyoathiri utu wa mwanadamu ambao ni msingi mkuu wa maadili katika jamii.

📝Pia, mwandishi ameainisha misingi ya imani na mapokeo ya dini mbalimbali jinsi inavyojibu swali kuu la msingi wa kitabu hiki, yaani majibu kuhusu “chanzo na maana ya maisha hapa duniani.”

📝Mwanadishi amefafanua falsafa mbalimbali za maisha na jinsi zinavyoeleza mahitaji na mchango wa nafsi ya mwanadamu anayeweza kujitambua na kutoa mchango wake katika jamii.

📝Aidha, Mwandishi ameleezea kwa kina namna sahihi ambayo kila mwanadamu anavyoweza kutumia falsafa hizo kufanyika mtu wa thamani hasa kuwa mtu mwenye maono, mwenye kuwekeza katika maeneo ya uwezo binafsi na kuzalisha huduma na bidhaa zinazobadili au kuleta mabadiliko chanya katika mazingira yake.

📝Vile vile, Mwandishi amefafanua umuhimu wa  busara na hekima ya uongozi katika kuongoza wengine ili kuleta mabadiliko chanya wakati mwanadamu anapoishi ndoto yake ama kutekeleza maono yake kwa furaha.

📝Mwandishi pia amegusia mambo yanayomfanya mwanadamu kupoteza thamani ya maisha, ambayo kwa sehemu kubwa yanatokea ndani ya nafsi ya mwanadamu na mazingira yake ya karibu.

📝Pia, katika kuhakikisha unapata mwongozo wote wa maisha yenye kuacha alama, Mwandishi amechambua changamoto zinazokabili dunia ya sasa na kuonyesha jinsi gani kila mmoja wetu anaweza kushiriki katika utatuzi wa changamoto hizo.

📝Kama hiyo haitoshi, Mwandishi ameelezea baadhi ya Sheria za Asili (Universal Laws) ambazo ni msingi wa ufanisi katika maisha.

📝Hakika haya ni mambo ambayo mtu akifanikiwa kuyafahamu na kujua namna ya kuyaishi, inamuiya rahisi kuishi maisha yenye thamani kubwa sana kwa kizazi chake na kuacha alama kwa vizazi vijavyo.


📝Kitabu hiki ni muhimu sana kusomwa na kila mtu hasa vijana na watu wazima. Ni kitabu muhimu sana kwa wazazi na walezi wa familia, viongozi wa taasisi na ngazi zote ili kujiongezea uwezo na ufahamu wa maisha.

📝Nimalizie kwa kusema kuwa, kitabu cha MAISHA YENYE THAMANI ni msaada wa kumfanya kila mtu apate kuishi maisha yenye mchango chanya katika jamii.

📝Ni maono yangu kuwa katika jamii iliyoshiba maudhui ya kitabu hiki kutakuwa na amani, furaha, uadilifu, utosherevu na maendeleo endelevu.

📝Mtu akisoma kitabu hiki kwa makini anapata shauku  na hamasa kubwa ya kuacha alama, kuhudumia jamii  na taifa lake kwa uadilifu akijua kwamba amepewa kuishi mara moja na kwamba kila siku ni muhimu kwake kukua, kuchanua  na kuonesha tunu iliyopo ndani mwake.

Jonathan Lucas Kwiyega

🖊️Mkurugenzi wa Shirika la Wanasihi wa Uhifadhi na Mandhari ya Nchi (LCMO); 

🖊️Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Chemichemi za Urejesho (SRM); na 

🖊️Mwandishi wa Vitabu zaidi ya Nane (8) vya Maarifa mbalimbali.


Kitabu hiki kwa sasa kinapatikana kwa mfumo wa Nakala tete (soft copy) kwa bei ya zawadi ya Tshs. 10,000/= badala ya Tshs. 20,000/=



Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.

onclick='window.open(