Habari ya leo rafiki yangu na msomaji wa
mtandao wa Fikra za Kitajiri.
Naamini unaendelea
vizuri na mapambano ya kila siku kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Rafiki
yangu leo nakuletea makala maalumu ambayo inalenga kubadilisha mazoea yako kwenye ulimwengu wa fedha.
Makala ya leo inakulenga wewe ambaye ni
mwanafunzi au una ndugu ambaye ni mwanafunzi katika ngazi ya elimu ya juu. Kuwa
Mwanafunzi katika ngazi hiyo ni sifa ya kwanza kwako kufaidika na makala hii.
Sifa ya pili na ya mwisho – makala hii
inamlenga mwanafunzi ambaye ana fikra pana za kutengeneza mafanikio makubwa
katika maisha yake kupitia juhudi binafsi.
Kama wewe una sifa zote hizo karibu sana
nikushirikishe siri moja tu ambayo itakuwezesha kubadilisha maisha yako kwa
ujumla. Siri hii si nyingine bali ni JILIPE
KWANZA.
Nini
maana ya JILIPE KWANZA? Kujilipa kwanza ni kuhakikisha unatenga asilimia
flani ya kila shilingi inayoingia mkononi mwako kwa ajili ya kufanikisha
mipango yako ya kifedha kwa siku za baadae.
Ili uwe na mafanikio ya kifedha (uhuru wa
kifedha) ni lazima katika kila shilingi inayoingia mikononi mwako uhakikishe kabla
ya kupanga matumizi ya fedha hizo utenge asilimia yake kwa ajili ya kufanikisha
ndoto ulizonazo katika sekta ya fedha.
Siri hii ndio inaendelea kutofautisha
waliofanikiwa na wale ambao ni masikini au wenye pato la kati katika jamii
inayotuzunguka. Matajiri wanatumia siri hii kuendelea kuwa matajiri zaidi
wakati masikini pamoja na kwamba wanaifahamu siri hii kwa kutoitumia wanaendelea
kuwa masikini.
Kwa kuwa ninakupenda na ninatamani uwe katika orodha
ya matajiri wa kesho, natumia makala hii kukushirikisha siri ya JILIPE KWANZA
ili uweze kuungana nami katika safari ya kuutafuta utajiri. Toka nilipoifahamu
siri hii kupitia kitabu cha Robert Kiyosaki cha “Rich Dad Poor Dad” hakika
nilisema lazima nibadilishe maisha yangu kwa kutumia siri hii ambayo matajiri
wanaitumia kutengeneza utajiri wao.
Hakika hadi sasa siri hii imetenda muujiza
mkuu katika maisha yangu na nitaendelea kuitumia kufikia mafanikio makubwa sana
ya kifedha katika maisha yangu yajayo. Namuomba Mwenyezi Mungu anipe maisha marefu
ili nifike pale ninapokusudia kufika katika ulimwengu wa fedha.
Hata hivyo, siri ya utajiri unaotafutwa
kupitia siri hii si utajiri wa kulala masikini na kuamka tajiri bali ni utajiri
ambao unahitaji mipango maalumu ya kuufikia utajiri huo. Hapa ni lazima uwe na
mipango ya muda mfupi, wa kati na muda mrefu.
Mimi tayari nimeianza safari hii na nitafurahi
zaidi kama na wewe baada ya kusoma makala hii utafanya maamuzi sahihi ya
kuianza safari hii kwa kujijengea nidhamu ya kujilipa kwanza kutoka kwenye kila
shilingi inayoingia mkononi mwako kwa mfumo wa “Boom” au chanzo chochote kile
cha mapato.
Kwa nini na kuhamasisha uanze KUJILIPA KWANZA?
Nakuhamasisha ujilipe kwanza kwa kuwa:-
a) Mfumo
wa ajira kwa sasa hautabiriki. Wapo wasomi wengi ambao wapo mtaani na kila
kukicha wanatembea na bahasha kwa ajili ya kutafuta ajira bila mafanikio;
b) Ukianza
kujilipa kwanza ukiwa bado chuoni na umri mdogo unatengeneza nafasi nzuri za
kufanikiwa kifedha kwa vile hata baada ya kumaliza masomo yako utakuwa na
uzoefu wa kutosha wa kupangilia vizuri kila shilingi unayoipata;
c) Nataka
uwe tofauti na mazoea ya jamii inayokuzunguka. Badala ya kumaliza Chuo ukimiliki
masanduko ya nguo, simu janja, speaker za mziki au ukiwa umejenga jina mtaani
hasa kwenye sehemu za vileo na starehe – nahitaji umalize elimu yako ukiwa na
pochi nene kwenye akaunti yako ya benki au ukiwa unamiliki rasilimali kama Viwanja,
Mashamba, Mifugo, Nyumba, Biashara n.k; na
d) Nataka
UJILIPE KWANZA ili kuongeza idadi ya Vijana ambao wapo tayari kuibadilisha Duni
hii kuwa mahala pazuri pa kuishi kwa viumbe vyote.
Hivyo nikiwa Mwalimu na
Mhamasishaji ambaye nimedhamiria kushirikisha Siri hii ya KUJILIPA KWANZA, nimeanzisha
kundi la WhatsApp la “JILIPE KWANZA”
nikiwa na lengo kuu la kuwajumuisha vijana wa rika tofauti wenye maono ya kuwa
na uhuru wa kifedha katika maisha yao ya baadae.
Kundi hili limepewa
jina la JILIPE KWANZA kwa kuwa
linalenga kuzalisha Mamilionea wa kesho kupitia elimu na miongozo watakayopata.
Kwa ujumla vijana hawa watafundishwa namna ya kujilipa kwanza kwa kutenga
asilimia flani ya sehemu ya pato lao na kuiwekeza sehemu salama kwa ajili ya
kufanikisha maisha yenye uhuru wa kifedha katika maisha yao ya baadae.
Kwa kujiunga na kundi
hili – kijana ambaye ni tajiri wa kesho utafanikiwa kupata faida zifuatazo:-
ü Kupata elimu ya kina (mentorship) juu ya kujilipa kwanza;
ü Kujiwekea nidhamu ya kutenga asilimia ya sehemu ya pato
lako na kuiwekeza sehemu salama;
ü Kupata elimu juu ya sehemu sahihi ya kuwekeza fedha zako
kwa ufanisi hasa ile fedha unayojilipa;
ü Kuwa sehemu ya vijana wenye maono yanayoendana ambao kwa
pamoja chini ya mwongozo wangu wataweka malengo ya kifedha kila mmoja kwa uwezo
wake;
ü Kuhakikisha kila mwisho wa mwezi wanajumuia waliopo katika
kundi hili wote kwa pamoja wanawajibika kutoa taarifa ya mwenendo wao kwenye
sekta ya fedha; na
ü Kupata nakala za uchambuzi wa vitabu mbalimbali vinavyohusiana
na mafanikio ya uhuru wa kifedha.
Ili kuwa sehemu ya kundi hili unatakiwa kulipia ada ya Tshs.
2,000/= kwa mwezi sawa na Tshs. 24,000/= kwa mwaka.
Kama unahitaji kuwa
sehemu ya matajiri wa kesho nitumie ujumbe kupitia barua pepe fikrazakitajiri@gmail.com au kwa
kupitia namba yangu ya WhatsApp +255 786 881 155 nitakupa maelekezo ya kulipia
ada yako na baada kulipia utaunganishwa kwenye kundi hili.
KARIBU
KATIKA KUNDI LA “JILIPE KWANZA” ILI KWA PAMOJA TUIANZE SAFARI YA UMILIONEA.
Kumbuka kama bado
hujajiunga kwenye mfumo wetu wa kupokea makala za Mtandao wa Fikra za Kitajiri,
tafadhali fanya hivyo KWA KUBONYEZA HAPA na
kujaza fomu kisha bofya “jiunge/subscribe”. Ni fursa ambayo itakuwezesha kupata
makala zenye maarifa mbalimbali kupitia barua pepe yako.
PATA UCHAMBUZI WA VITABU vifuatavyo kwa kulipia Tshs. 5000.00 kila
kitabu (Ukinunua vitabu vyote vitatu utapata kwa ofa ya Tshs 10,000.00).
1. Kitabu cha Kwanza ni “THE RULES
OF MONEY (KANUNI ZA PESA)” kutoka kwa Mwandishi Richard Templar
Katika kitabu hiki utafahamu
kanuni 107 za pesa. Ndani ya kanuni hizo utagundua kuwa utajiri ni haki ya
kila mtu hivyo ni wajibu wako kuwa tajiri. Kanuni zote (107) zimechambuliwa
kwa kina na kuandaliwa kwa lugha Kiswahili. Uchambuzi huu unapatikana kwa
kijitabu kidogo chenye kurasa 39 ambazo unaweza kusoma kwenye simu yako ya
mkononi (simu janja – smart phone) au kwenye kompyuta mpakato (pc).
2. Kitabu cha pili “THE RULES OF
LIFE (KANUNI ZA MAISHA)” kutoka kwa mwandishi Richard Templar
Mwandishi kupitia kitabu hiki
anatushirikisha kanuni 106 za maisha. Kanuni hizi zimechambuliwa kwa kina kwa
lugha ya Kiswahili na unaweza kukisoma kupitia simu janja au kompyuta
mpakato. Kanuni zote zinagusa kila sekta ya maisha yako hivyo ni kitabu
ambacho hautojutia pesa unayoitoa kwani utajifunza maarifa mbalimbali kwa
ajili ya kuboresha maisha yako.
3. Kitabu cha tatu ni “I CAN I
MUST I WILL (NAWEZA, NALAZIMIKA, NITAFANYA)” kutoka Mwanamafanikio na
Mtanzania Mwenzetu Marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi
Kwa ujumla kupitia kitabu hiki Dr.
Mengi anatushirikisha maisha yake kuanzia akiwa mtoto, akiwa mwanafunzi,
wakati anaanzisha biashara yake ya kwanza, namna alivyopanua biashara zake,
wajibu aliokuwa nao kwa jamii, misimamo yake kwenye mfumo wa Serikali kwa
awamu zote tano, wajibu wake kwenye uhifadhi wa mazingira na matarajio yake
kwenye kukuza biashara kwa siku za baadae.
Kupata
uchambuzi wa vitabu hivi tuma pesa yako kwa njia ya M-pesa au Airtel Money
kupitia namba zifuatazo:-
M –
Pesa tumia namba: 0763 745 451 (Majina ni Augustine Mathias)
Airtel Money tumia namba: 0786 881 155 (Majina ni Augustine Mathias)
Baada
kutuma pesa hiyo nitumie ujumbe kwenye namba ya airtel (0786 881 151 451)
ukiwa na barua pepe yako ili nikutumie uchambuzi wa kitabu husika.
UTAJIRI NI HAKI YAKO YA KUZALIWA "BEING RICH IS YOUR BIRTH RIGHT" |