Habari ya leo rafiki
na msomaji wa mtandao wa Fikra za Kitajiri.
Naamini unaendelea
vizuri na mapambano ya kila siku kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Kwa takribani
kipindi cha miaka 3 sasa nimekuwa nikikushirikisha maarifa mbalimbali kupitia
makala za uchambuzi wa vitabu.
Kupitia makala hizi, kwa
pamoja tumeweza kujifunza maarifa mbalimbali yanayohusu maisha ya mahusiano,
biashara, uwekezaji, uongozi, malezi ya watoto, uhuru wa kifedha na kiroho.
Kutokana na makala
hizi wengi wenu ambao mmekuwa mkinitumia ujumbe wa kushukuru kwa namna makala
zinavyowasaidia kupata maarifa mbalimbali nimekuwa nawasisitiza kuhakikisha
mnafanyia kazi yale mnayojifunza katika kila kitabu ninachowashirikisha.
Katika kipindi hiki
cha miaka 3 nimesoma vitabu zaida 70 vyenye maarifa mbalimbali na bado nitaendelea
kukushirikisha uchambuzi wa vitabu zaidi kwa kadri ya uwezo wangu. Kubwa nilichojifunza
ni kwamba vitabu vyote vya hamasa ya mafanikio ya maisha vinazungumzia maarifa
yale yale japo kwa lugha, muundo na radha tofauti. Hivyo, ni muhimu kuchukua
hatua zinazolenga kutumia maarifa hayo katika maisha yetu ya kila siku.
Kumbe, kinachotakiwa
baada ya kusoma kitabu ni kuhakikisha unapata mbinu za kuboresha au kuanzisha
mikakati mipya ya kufanikisha malengo au ndoto ulizonazo kwenye kila sekta ya
maisha yako. Yapo mengi nimejifunza na yale niliyofanyia kazi hakika
yamebadilisha maisha yangu katika sekta hizo kulingana na ndoto nilizonazo.
Kama Mwalimu wa
kukuhamasisha ambaye nimedhamiria kukushirikisha uchambuzi wa vitabu kwa lugha
rahisi ya Kiswahili, nimeona ni vyema niende hatua moja zaidi ya kuhakikisha
nakusaidia kukupa usimamizi wa karibu ili kwa pamoja tufikie ndoto za maisha
yetu hasa “maisha yenye uhuru wa kifedha”.
Ili kufanikisha
kusudio hilo nimeanzisha kundi la WhatsApp la “JILIPE KWANZA” ambalo linalenga kuwajumuisha vijana wa rika
tofauti wenye maono ya kuwa na uhuru wa kifedha katika maisha yao ya baadae.
Kundi hili limepewa
jina la JILIPE KWANZA kwa kuwa
linalenga kuzalisha Mamilionea wa kesho kupitia elimu na miongozo watakayopata.
Kwa ujumla vijana hawa watafundishwa namna ya kujilipa kwanza kwa kutenga asilimia
ya sehemu ya pato lao na kuiwekeza sehemu salama kwa ajili ya kufanikisha
maisha yenye uhuru wa kifedha katika maisha yao ya baadae.
Kwa kujiunga na kundi
hili wewe kijana ambaye ni tajiri wa kesho utafanikiwa kupata faida zifuatazo:-
ü Kupata elimu ya kina (mentorship) juu ya kujilipa kwanza;
ü Kujiwekea nidhamu ya kutenga asilimia ya sehemu ya pato lako
na kuiwekeza sehemu salama;
ü Kupata elimu juu ya sehemu sahihi ya kuwekeza fedha zako
kwa ufanisi hasa ile fedha unayojilipa;
ü Kuwa sehemu ya vijana wenye maono yanayoendana ambao kwa
pamoja chini ya mwongozo wangu wataweka malengo ya kifedha kila mmoja kwa uwezo
wake;
ü Kuhakikisha kila mwisho wa mwezi wanajumuia waliopo katika
kundi hili wote kwa pamoja wanawajibika kutoa taarifa ya mwenendo wao kwenye sekta
ya fedha; na
ü Kupata nakala za uchambuzi wa vitabu mbalimbali
vinavyohusiana na mafanikio ya uhuru wa kifedha.
Ili kuwa sehemu ya kundi hili unatakiwa kutoa ada ya Tshs.
24,000/= kwa mwaka sawa na Tshs. 2,000/= tu kwa mwezi.
KARIBU KATIKA KUNDI LA “JILIPE KWANZA” ILI
KWA PAMOJA TUIANZE SAFARI YA UMILIONEA.
Kama bado hujajiunga
kwenye mfumo wetu wa kupokea makala za uchambuzi wa vitabu, tafadhali fanya
hivyo KWA KUBONYEZA BONYEZA HAPA na
kujaza fomu kisha bofya “jiunge/subscribe” utakuwa umejiunga na mtandao huu. Ni
fursa ya bure ambayo utaendelea kupata uchambuzi wa vitabu kwa lugha rahisi
kupitia barua pepe yako.
PATA UCHAMBUZI WA VITABU vifuatavyo kwa kulipia Tshs. 5000.00 kila
kitabu (Ukinunua vitabu vyote vitatu utapata kwa ofa ya Tshs 10,000.00).
1. Kitabu cha Kwanza ni “THE RULES
OF MONEY (KANUNI ZA PESA)” kutoka kwa Mwandishi Richard Templar
Katika kitabu hiki utafahamu
kanuni 107 za pesa. Ndani ya kanuni hizo utagundua kuwa utajiri ni haki ya
kila mtu hivyo ni wajibu wako kuwa tajiri. Kanuni zote (107) zimechambuliwa
kwa kina na kuandaliwa kwa lugha Kiswahili. Uchambuzi huu unapatikana kwa
kijitabu kidogo chenye kurasa 39 ambazo unaweza kusoma kwenye simu yako ya
mkononi (simu janja – smart phone) au kwenye kompyuta mpakato (pc).
2. Kitabu cha pili “THE RULES OF
LIFE (KANUNI ZA MAISHA)” kutoka kwa mwandishi Richard Templar
Mwandishi kupitia kitabu hiki
anatushirikisha kanuni 106 za maisha. Kanuni hizi zimechambuliwa kwa kina kwa
lugha ya Kiswahili na unaweza kukisoma kupitia simu janja au kompyuta
mpakato. Kanuni zote zinagusa kila sekta ya maisha yako hivyo ni kitabu
ambacho hautojutia pesa unayoitoa kwani utajifunza maarifa mbalimbali kwa
ajili ya kuboresha maisha yako.
3. Kitabu cha tatu ni “I CAN I
MUST I WILL (NAWEZA, NALAZIMIKA, NITAFANYA)” kutoka Mwanamafanikio na
Mtanzania Mwenzetu Marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi
Kwa ujumla kupitia kitabu hiki Dr.
Mengi anatushirikisha maisha yake kuanzia akiwa mtoto, akiwa mwanafunzi,
wakati anaanzisha biashara yake ya kwanza, namna alivyopanua biashara zake,
wajibu aliokuwa nao kwa jamii, misimamo yake kwenye mfumo wa Serikali kwa
awamu zote tano, wajibu wake kwenye uhifadhi wa mazingira na matarajio yake
kwenye kukuza biashara kwa siku za baadae.
Kupata
uchambuzi wa vitabu hivi tuma pesa yako kwa njia ya M-pesa au Airtel Money
kupitia namba zifuatazo:-
M –
Pesa tumia namba: 0763 745 451 (Majina ni Augustine Mathias)
Airtel Money tumia namba: 0786 881 155 (Majina ni Augustine Mathias)
Baada
kutuma pesa hiyo nitumie ujumbe kwenye namba ya airtel (0786 881 151 451)
ukiwa na barua pepe yako ili nikutumie uchambuzi wa kitabu husika.
UTAJIRI NI HAKI YAKO YA KUZALIWA "BEING RICH IS YOUR BIRTH RIGHT" |