Habari ya leo rafiki na msomaji wa
mtandao wa Fikra za Kitajiri.
Naamini Mungu ni mwema na anaendelea kukuwezesha kupata pumzi kiasi ambacho unaweza kusoma makala hii. Wote kwa pamoja tuseme ASANTHE MUNGU KWA UPENDELEO WAKO.
Kama nilivyokuahidi kukushirikisha funguo 365 za hekima kutoka kwa
Mwandishi Mike Murdock, leo hii utafaidika na funguo za mwezi Aprili hadi Juni. Nimebakiza funguo za nusu ya pili ya mwaka katika siku 365. Tuombeane ili funguo zote nipate kukushirikisha.
Kama bado hujajiunga kwenye mfumo wetu wa
kupokea makala za uchambuzi wa vitabu, tafadhali fanya hivyo KWA KUBONYEZA BONYEZA HAPA na
kujaza fomu kisha bofya “jiunge/subscribe”. Kwa kujiunga na mtandao huu utaendelea kupata uchambuzi wa vitabu kwa lugha rahisi
kupitia barua pepe yako.
Karibu
ushirikiane nami kujifunza machache kati ya mengi ambayo mwandishi
anatushirikisha katika katika sehemu hii ya tatu ya mwendelezo wa kitabu hiki:
Aprili 1 (91): Kutoa
ni uthibitisho wa kuishinda tamaa. Katika maisha tunatakiwa kutambua kuwa pamoja
na kukabiliana na changamoto ya kutimiza malengo tuliyonayo bado tuna wajibu wa
kutimiza kwa kutoa msaada kwa jamii inayotuzunguka. Kumbuka kadri tunavyotoa
ndivyo tunabarikiwa zaidi.
Aprili 2 (92): Ikiwa
muda unaponya, Mungu si wa muhimu. Pamoja na umuhimu wa kutumia vyema muda wetu
bado tuna wajibu wa kuhakikisha Mungu anapewa nafasi yake katika majukumu yetu
ya kila siku.
Aprili 3 (93): Upweke
si matokeo ya kukosekana kwa upendo bali kukosekana kwa miongozo sahihi.
Tunahitaji kuwa na miongozo sahihi kuhusiana na mahusiano yetu na jamii
inayotuzunguka ili kuepuka upweke katika maisha yetu ya kila siku.
Aprili 4 (94): Pesa
ni tuzo ya kutatua matatizo ya jamii. Kumbe katika maisha tunahitaji kuwa na
lengo kuu la kutatua matatizo ya jamii tunayoishi. Katika kufanya hivyo
tunazawadiwa pesa kulingana na jitihada au ubunifu tunaouweka katika kutatua
matatizo hayo.
Aprili 5 (95): Utayari
wa kufikiwa ni changamoto ya kudumu katika maisha. Tunahitaji kujiuliza ni mara
ngapi tumekuwa tayari kufikiwa na jamii yenye mahitaji ya msaada wa aina yoyote
ile ambao upo chini ya uwezo wetu.
Aprili 6 (96): Uchovu
unapoingia na Imani nayo inaanza kupotea. Mara zote unapojihisi kuchoka huwa na
morali ya kuendelea kukamilisha kile unachofanya huwa inaisha. Hata hivyo,
uchovu ni hisia za mwili hivyo kuna wakati ambao hatuna budi wa kujilazimisha
kwenda hatua za ziada kwa ajili ya kupata matokeo ya ziada.
Aprili 7 (97): Uvumilivu
ni silaha inayopelekea uongo kufunuliwa. Kumbe kadri tunavyovumilia ndivyo
tunapata nafasi ya kujifunza zaidi uongo uliopo kwenye kile tunachovumilia.
Aprili 8 (98): Hatua
yoyote kuelekea kwenye utoshelevu wa nafsi ni hatua inayokuweka mbali na Mungu.
Kubwa ni kutambua kuwa katika kila tunalofanya tunakiwa kufanya kwa ajili ya
kuboresha/kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii yetu. Kwa kutatua changamoto
hizo na sisi tunapata riziki yetu kulingana na jitihada tunayoiweka kwenye
kazi.
Aprili 9 (99): Ujinga
ni silaha pekee ambayo shetani anaweza kutumia kuangamizi nafsi yako. Kumbe,
tunahitaji kupata maarifa sahihi katika kila sekta ya maisha yetu kwa ajili ya
kukwepa kuangamizwa na muovu.
Aprili 10 (100): Ni
nadra akili iliyochoka kufanya maamuzi sahihi. Kuwa makini na maamuzi ambayo
unafanya wakati ambao tayari akili imechoka. Pia, mara zote akili yako
inatakiwa kulishwa na maarifa sahihi kwa ajili kufanya maamuzi sahihi katika
maisha yako ya kila siku.
Aprili 11 (101): Ndoto
isiyo ya kawaida inahitaji uvumilivu usiyo wa kawaida. Tujiulize ni mara ngapi
tumepoteza ndoto au kuchangia kupoteza ndoto za wengine kutokana na kukosa
uvumilivu ili ndoto hizo zifunuliwe kwenye uhalisia wake.
Aprili 12 (102): Chochote
ambacho hauna kimehifadhiwa kwa jirani yako na upendo ndo ramani kuu ya
kunufaika na hazina hiyo. Tunakumbushwa kuwa katika maisha hatujitoshelezi, ni
kupitia upendo wa sisi kwa sisi unaofanikisha kutumia talanta/kalama ambazo
kila mmoja wetu amepewa.
Aprili 13 (103): Uthibitisho
wa ujinga ni kujutia ubora. Mara nyingi tumezoea kuwa majuto huwa ni mjukuu.
Fundisho ni kwamba kile unachojutia hauna nafasi ya kukirekebisha japo una
nafasi ya kuhakikisha haurudii tena kosa la namna hiyo.
Aprili 14 (104): Tabia
iliyoruhusiwa ni tabia iliyofundishwa. Hivyo, kuna tabia ambayo huipendi katika
maisha yako huna budi ya kuacha mazingira ambayo yanapelekea tabia husika
iendelee kujengeka katika akili yako.
Aprili 15 (105): Mbegu
isiyo na faida mara zote uzalisha mazao yasiyo na faida. Tunafahamu juu ya
msemo wa “utavuna ulichopanda” – hivyo, mara zote kama unahitaji mavuno bora
huna budi ya kuhakikisha unapanda mbegu bora. Vivyo hivyo, kama unahitaji
mafanikio katika maisha ni lazima uhakikisha unafanya yale yatakayopelekea
ufanisi mafanikio ya ndoto zako.
Aprili 16 (106): Ushauri
ni hekima isiyo na gharama. Jiulize mara ngapi umekuwa tayari kupokea ushauri
kutoka kwa watu wa karibu yako. Lakini pia katika kila sekta ya maisha
unahitaji kuchagua washauri ambao unaamini wamefanikiwa katika sekta hizo.
Aprili 17 (107):
Udhaifu husipodhibitiwa mara zote huzalisha anguko la maisha. Kama binadamu
mara nyingi tunakuwa hatujakamilika katika sekta zote za maisha yetu. Hata
hivyo, madhaifu mengi tuliyonayo tunayazalisha wenyewe. Kumbe, tunahitaji
kupambana na madhaifu yetu kwa ajili ya kuepuka anguko la maisha.
Aprili 18 (108): Hasira
kwa kifupi ni shauku yenye kuhitaji tafakari ya kipekee. Ni mara nyingi katika
maisha tunakasilishwa na matukio ambayo yanaenda kinyume na mahitaji yetu.
Katika hali kama hiyo tunatakiwa kutafakari matukio husika kwa kina ili kupuka
kufanya maamuzi yenye athari hasi kwa maisha yetu.
Aprili 19 (109): Ni
heri usaliti kuliko uchungu. Ni heri kusalitiwa kuliko kuendelea kuteseka kwa
maumivu ya muda mrefu. Katika maisha, mahusiano ya namna yoyote ile ni heri
kukubali yavunjwe kwa ajili ya kuishi maisha yenye furaha kuliko kuendelea
kuishi maisha ya huzuni.
Aprili 20 (110): Jukumu
lisilo la kawaida mara zote huvutia maadui wasiyo wa kawaida. Tambua kuwa
katika maisha kama unafanya kazi kwa weledi na ubunifu kuliko mazoea ya jamii
inayokuzunguka utapata maadui wengi wenye lengo la kukukwamisha.
Aprili 21 (111): Zawadi
mara zote huwa zinadhihirisha tabia za wale wanaozipokea. Kuwa na kanuni
binafsi zinazoongoza maisha yako ili kuepuka kuendeshwa na kila aina ya tukio
katika maisha ya kila siku.
Aprili 22 (112): Kutoa
kunapunguza kapu lako kwa sasa kwa ajili ya kufanikisha kujaza kapu hilo kwa
siku zijazo. Katika kila hali tunatakiwa kukumbuka kuwa tunawajibika kurudisha
fadhira kwa jamii inayotuzunguka.
Aprili 23 (113): Utii/unyenyekevu
ni kitu pekee Mwenyezi Mungu anahitaji kutoka kwa Mwanadamu. Tunapaswa kuwa
wanyenyekevu kwa jamii inayotuzunguka bila kujali hatua tunazopiga katika
maisha yetu ya kila siku.
Aprili 24 (114): Biashara
mara zote ni kutatua changamoto za jamii kwa ajili ya thawabu iliyokubaliwa.
Kumbe, kila changamoto katika jamii inayokuzunguka ni fursa ambayo inakusubiri
uitatue ili hatimaye upate thawabu kulingana na ukubwa wa tatizo pamoja na
jitihada utakazoweka.
Aprili 25 (115):
Mikondo ya upendeleo uongezeka zaidi kadri unavyotatua shida za watu. Kumbe,
utapata zawadi zaidi na zaidi kwa kutatua shida za jamii. Kumbuka unavyomsaidia
mtu mmoja kwa viwango vinavyotakiwa ndivyo sifa zako zitaenea zaidi.
Aprili 26 (116):
Waliofanikiwa wapo tayari kupoteza upande mmoja kwa ajili ya kulinda upande
wenye maslahi zaidi. Husinganganie jambo ambalo unaona linakuumiza zaidi. Kuwa
tayari kusema sasa basi kwa ajili ya kulinda maslahi mapana ya malengo binafsi
katika maisha ya baadae.
Aprili 27 (117): Adui
ambaye hajazidhibitiwa mara zote upanuka/kukua zaidi. Fanya tathimini ya maadui
katika kila sekta ya maisha yako na anza kukabiliana nao mara moja. Kumbuka
adui wengine unaweza kuwa unawatengeneza mwenyewe bila kujua. Mfano, maadui wa
afya yako wanaweza kuwa wanatengenezwa kupitia mlo, vinjwaji na ratiba yako ya
siku.
Aprili 28 (118): Mungu
ameumba majira na kupitia ugunduzi mbalimbali mwanadamu amepanga namna ya
kuishi kwa ufanisi kulingana na msimu husika. Je katika kila msimu maisha yako
yamepangiliwa vipi kwa ajili ya kupata ufanisi unaohitaji kwenye maisha yako.
Aprili 29 (119): Mwenyezi
Mungu alikuwa na mtoto wa kiume japo alihitaji familia zaidi hivyo alimtoa
mwanae kwa ajili ya kupanua familia yake. Kumbe katika maisha ni lazima uwe
tayari kutoa sadaka kwa ajili ya kupata kile unachohitaji. Muhimu hakikisha
sadaka yako ni halali kwa Mungu na jamii inayokuzunguka.
Aprili 30 (120): Mwenyezi
Mungu alimtoa mwanae japo alibakiza kitabu chake. Kuwa tayari kutoa sadaka vitu
muhimu katika maisha yako kwa ajili ya kuokoa maisha ya wengine. Hata hivyo,
kila unapotoa hakikisha unatoa kwa maslahi mapana ya misingi ya kiroho
inayokuongoza kulingana na Imani yako.
Mei 1 (121): Kama
haupo tayari kutoa sadaka ndivyo pia nafasi yaw ewe kupata zaidi ni finyu. Kumbuka
katika maandiko tunaambiwa kuwa tunawajibika kutoa asilimia kumi ya pato letu
kama sadaka. Kadri unavyotoa ndivyo Baraka zaidi zinafunguka kwa ajili ya
mafanikio zaidi.
Mei 2 (122): Wabobevu
wa mafanikio wapo tayari kufanya chochote ambacho hawapendi kwa ajili ya
kuanzisha au kupata kile wanachopenda. Tunahitaji kutambua kuwa ili ufanikiwe
ni lazima upitie kwenye hatua na misukosuko ambayo hauipendi. Kumbuka kuwa hata
dhahabu ili iwe dhahabu ni lazima kwanza ichomwe.
Mei 3 (123): Kila
kitu kilichoumbwa ni Mwenyezi Mungu ni suluhisho kwa ajili ya kutatua tatizo.
Hii inamaanisha kuwa chochote kinachotuzunguka kwenye mazingira yetu ni kwa
ajili ya kutatua matatizo katika jamii. Tumia vitu hivyo kwa ajili ya kuboresha
maisha ya jamii inayokuzunguka na kufanya hivyo utafikia ndoto za maisha yako.
Mei 4 (124): Kila
urafiki/mahusiano kuna mazuri au madhahifu utajidhihirisha ndani yake. Pima
mahusiano yako na jamii inayokuzunguka au watu wako wa karibu kwa ajili ya
kugundua mema au madhahifu yaliyopo katika mahusiano husika. Yaendeleze mema na
kufanyia kazi madhaifu yaliyopo ili kuboresha zaidi.
Mei 5 (125): Nyakati
mbaya katika maisha huwa zinawakutanisha watu wema kwa pamoja. Katika kila
nyakati ngumu unazopitia hakikisha unakutana na watu wema kwa ajili ya kuboresha
maisha yako.
Mei 6 (126): Siku
moja yenye mashaka uzalisha siku 365 za maumivu. Maumivu tunayokutana nayo
katika maisha yanazalishwa na matendo yetu katika maisha ya kila siku.
Mei 7 (127): Mara
zote Mungu huwa haombi kitu ambacho hauna bali anaomba kitu ambacho unahitaji
kukaa nacho. Jiulize na mara ngapi umegoma kutoa kile ulichonacho kwa
kusingizia kuwa hauna. Tunahitaji kulenga kutoa zaidi ili kwa kufanya hivyo
tufanikiwe kujaza ghara letu.
Mei 8 (128): Mungu
anataka tutimize sheria zake. Sheria tunazopewa na Mwenyezi ni kwa ajili ya
kuishi maisha bora katika jamii inayotuzunguka. Hivyo, tukitimiza sheria hizo
ni wazi kuwa maisha yetu pia yatakuwa bora zaidi.
Mei 9 (129): Ubunifu
ni kwa ajili ya kuongeza vipaumbele na kufanya mambo yale yale ni njia ya
kupunguza vipaumbe hivyo. Katika kila unachofanya unahitaji kwenda hatua ya
ziada nje ya mazoea ya majii.
Mei 10 (130): Kama
haujui wapi unaelekea mara zote utaridhika na hali ulinayo. Katika kila sekta
ya maisha yako huna budi ya kuhakikisha unachora msitari au ramani ya
kukuonesha ni nini hasa unataka kukamilisha katika maisha ya baadae.
Mei 11 (131): Toa
huduma kwa wengine kiasi ambacho huduma hiyo hawawezi kuipata kwingineko sawa
na viwango vyako na watendelea kuhitaji huduma hiyo. Jamii inayokuzunguka
inahitaji huduma bora hivyo chochote unachofanya kitekeleze kwa viwango vya
hali ya juu na jamii itaendelea kuja kwako.
Mei 12 (132):
Uvumilivu unapunguza maadui zako. Kumbuka kuwa kadri unavyovumilia ndivyo
unajifunza zaidi na hivyo kuongeza nafasi ya kufanikisha kile uchofanya. Pia,
kwa kadri unavyofanikiwa ndivyo unapunguza maadui kandamizi ambao wamekuwa
wakikuzuia kusonga mbele.
Mei 13 (133): Miujiza
haiendi sehemu inakotakiwa bali inaelekea sehemu ambapo inatarajiwa. Kubwa hapa
ni kutambua kuwa unapotarajia muujiza flani katika maisha ni lazima kuweka
mikakati ya kuufanya muujiza huo ujitokeze katika maisha yako.
Mei 14 (134): Kile
ulichonacho katika mikono yako hakitoshelezi kuwa mavuno basi kinatakiwa kuwa
mbegu kwa ajili ya mavuno unayoyataka. Tambua kuwa chochote unachomiliki kwa
sasa pasipo kujali udogo/ukubwa wake kina thamani kubwa ya kukupatia mafanikio
zaidi kulingana na ndoto ulizonazo.
Mei 15 (135):
Utayari huunda mahitaji, mahitaji huunda matarajio, matarajio huunda usumbufu
na usumbufu husababisha kushindwa au kutofanikiwa. Huu ni mpangilio wa namna
ambavyo wewe mwenyewe unaweza kuwa chanzo cha kutofanikisha malengo yako bila
kugundua kwa vile umekuwa unajihusisha na mpangilio huo kifikra, tabia na
vitendo.
Mei 16 (136): Deni
linapunguza kwenye ghara lako la baadae kwa ajili ya kujalizia mahitaji yako ya
fedha kwa wakati huu. Katika kila deni unaloingia unapaswa kujiuliza litasaidia
vipi kujazilizia mahitaji yako ya pesa katika siku za baadae.
Mei 17 (137): Sehemu
pekee ambapo unatakiwa kujitoa ni pale ambapo jukumu lako kubwa lilipo. Kila
jukumu ulilonalo unapaswa kulitekeleza kwa uwezo wako wote ili kupitia hayo
unayofanya ufanikishe lengo kuu la kuifanya dunia kuwa mahala pazuri pa kuishi
kwa viumbe vyote.
Mei 18 (138):
Mwenyezi Mungu huficha zawadi iliyo na thamani katika vyombo visivyo na thamani
na kwa hiyo ni wachache wenye dhamira na uvumilivu ndio wanaweza kupata zawadi
hiyo. Jiulize ni mara ngapi umepishana na zawadi zilizoelekezwa kwako kwa vile
hukujibidisha kuzipata zawadi hizo.
Mei 19 (139): Walioshindwa
mara nyingi wanajikita kwenye hali wanayopita wakati wenye mafanikio
wanaangalio yanayokuja mbele yao. Kumbe ili ufanikiwe ni lazima kuwaza
kukamilisha malengo ya baadae kwa kuboresha unayofanya kwa sasa.
Mei 20 (140): Ukimya
hauwezi kupotoshwa. Ni vyema kunyamaza kuliko kuongea kitu ambacho hauna
uhakika. Hauwezi kusingiziwa kitu ambacho haukuongea.
Mei 21 (141): Pesa
haikubadilishi bali inakuza zile tabia ambazo tayari unazo. Hivyo ni muhimu
kutambua kuwa pesa haina ubaya wowote bali ubaya au uzuri wa pesa upo ndani
mwako.
Mei 22 (142): Roho
Mtakatifu ni mtu pekee ambaye anaweza kuridhishwa na wewe. Hautakiwi kufanya
kwa ajili ya kuridhisha kila mmoja anayekuzunguka bali tekeleza majukumu yako
kulingana na misingi na kanuni ya maisha yako.
Mei 23 (143):
Kufanya kazi kwa bidii ni sehemu pekee ya kutimiza majukumu yako. Bidii, bidii,
bidii ni njia pekee ya kufikia kwenye kusudio la maisha yako na njia hiyo ni
suluhisho la kufikia kwenye ukamilisho wa maisha yako.
Mei 24 (144): Kukosa
utulivu ni dalili za kuwa maisha yako ya baadae yatakuwa ya kutegemea maagizo
kutoka kwa wengine. Kumbe unahitaji kuwa na utulivu katika yale unayofanya kwa
ajili ya kuboresha maisha yako ya kesho.
Mei 25 (145): Kamwe
Mungu haidhinishi mwanaume kuoa mwanamke ambaye si mnyenyekevu au mwanamke
kuolewa na mwanaume ambaye hawezi kuongoza. Wajibu wa mwanamme ni kuwa kiongozi
wa familia wakati wajibu wa mwanamke ni kuwa mnyenyekevu.
Mei 26 (146): Wanaume
hawafi maji kutokana na kuzama majini bali wanakufa maji kutokana na kuendelea
kukaa katika maji hayo. Kumbe, kinachokumaliza si hiyo hali/tabia
inayokukandamiza bali kinakukwamisha ni wewe kuendelee kubweteka na hali hiyo.
Toka nje ya boksi na fursa nyingi zitafunguka.
Mei 27 (147): Kusudi
la kumbukumbu ni kuruhusu kurudia matukio yaliyo mema katika historia ya maisha
yako. Jiulize yaliyojaza mfumo wako wa kumbukumbu kama ni yale
yanayokufurahisha au kukuhuzunisha katika maisha ya sasa. Achana na kumbukumbu
zenye huzuni katika maisha yako.
Mei 28 (148):
Hakuna kitu kinachotoka mbinguni bila ya kitu kufanyika duniani. Husitegemee
maajabu kama haupo tayari kuishi maajabu hayo. Unatakiwa kuanza kuishi maajabu
hayo hapa duniani ili Baraka kutoka mbinguni zikushukie.
Mei 29 (149): Roho
Mtakatifu ni nafsi pekee unatakiwa kuitii. Kumbuka kuwa hakuna baya au jema
tunalofanya bila ya nguvu ya Roho aliyepo ndani mwetu kutushauri. Kufanikiwa au
kutofanikiwa inategemea ni kwa kiwango gani tunaisikiliza hiyo Roho aliyepo
ndani mwetu.
Mei 30 (150): Kushindwa
sio tukio bali ni vipaumbele tu. Fanya tafakari juu ya vipaumbele vyako katika
kila siku ya maisha yako na kugundua kama vitakufikisha kwenye kusudio la
maisha yako.
Mei 31 (151): Achana
na tabia ya kuangalia sehemu ulizotoka na anza kuangalia sehemu unazotaka
uwepo. Kumbuka kuwa yaliyopita hayana nafasi tena katika kuamua hatima ya
maisha yako endapo upo tayari kuachana na kumbukizi zisizo na faida na kujikita
kwenye yale ambayo ni muhimu kufikia ndoto zako.
Juni 1 (152): Kile
unachosema udhihirisha nini Mungu anataka kukutendea. Unahitaji kuyatafakari
maneno yako kwa kina ili kugundua Mungu ana makusudi gani katika maisha yako.
Kumbuka maneno yanaumba hivyo unahitaji kuhakikisha unanena maneno yaliyo bora.
Juni 2 (153):
Maumivu sio adui yako bali ni ushuhuda wa kuwa umeusika kutengeneza maumivu
hayo. Kumbuka kuwa iwe ni maumivu ya magonjwa, kimahusiano au maumivu ya aina
yoyote ile kwa namna moja au nyingine umehusika kutengeneza maumivu hayo
kupitia matendo yako ya siku zilizopita.
Juni 3 (154): Kujipendekeza
huwa mara nyingi kunapelekea kuzungumza maneno mazuri kwa nia mbaya. Hili liko
wazi katika jamii tunayooishi kuwa ili uonekane mwema zaidi ya wengine ni
lazima uwapakazie uongo wengine. Epuka kufanya kazi kwa kuchafua wengine na
badala yake tenda mema na sifa zako zitasambaa.
Juni 4 (155): Mjinga
ndiye anafanya mashauriano na mtoaji. Pale unapopewa bure kazi yako kubwa ni
kupokea na kushukuru. Kumbe, kwenye kama hiyo hauna nafasi ya kufanya uchaguzi
kulingana na matakwa yako bali unapokea kilichopo.
Juni 5 (156): Mtu
mwenye nguvu ya Mungu anakupa amani na Kanuni za Mungu zinakupa ufanisi katika
yale unayofanya. Hakikisha kila unachofanya kinakuwa katika misingi ambayo
haina madhara kwa jamii inayokuzunguka.
Juni 6 (157): Umaarufu
unaleta harakati, harakati zinaleta mahitaji, mahitaji yanaleta usumbufu na
usumbufu hupelekea kushindwa kufanikiwa. Huu ni mnyororo wa kuelekea kwenye
anguko hivyo kabla ya kutafuta umaarufu jiulize hatima ya umaarufu huo katika
siku sijazo. Badala ya kutafuta sifa za kijinga hakikisha unatekeleza wajibu
wako kwa ubunifu ili hatimaye matendo yako yafahamike kwa walengwa.
Juni 7 (158): Sababu
kubwa ya watu wengi kushindwa kufanikiwa ni kukosa mwelekeo au lengo. Watu wengi
wanaishia kugusa gusa kwenye kila kazi bila kuhakikisha kazi moja inafanywa kwa
viwango vinavyotakiwa mpaka izae matunda. Kuwa na mtazamo katika kazi au mradi
unaofanya mpaka pale utakapoona kuwa kuna matokeo chanya.
Juni 8 (159): Wivu
ni kuamini kuwa mwingine amepata kile ambacho unastahili kupata. Husiwe na wivu
kwa wanaokuzunguka kutokana na ukweli kwamba dunia hii imejaa fursa ambazo
zinakusubiri. Mwenzio kufanikiwa haina maana kuwa amechukua nafasi yako ya
kutimiza malengo.
Juni 9 (160): Mawimbi
ya Jana yaliyosababishwa na kukosa utiifu yatasababisha madhara katika Kesho
yako. Upo jinsi ulivyo kutokana na yale uliyofanya siku zilizopita. Hivyo,
jinsi utakavyokuwa siku za baadae itategemea na nini unafanya leo hii.
Juni 10 (161): Ubora
wa Taifa lolote unategemea na ubora wa Kiongozi ambaye Mungu amempa mamlaka ya
kutawala Taifa husika. Hivyo, tukiangalia kwenye nafasi yako ubora wa familia unayoiongoza
utategemea na ubora wako. Vivyo hivyo, ubora wa wafuasi wako utategemea na
ubora wako.
Juni 11 (162):
Chochote ulichonacho kitakuwezesha kupata chochote unachohitaji katika maisha
yako ya baadae. Tafakari ni mara ngapi umeshindwa kuchukua hatua kwa kisingizio
cha kutokuwa na hauna nyenzo za kuanzisha hatua ya kwanza.
Juni 12 (163): Uwepo
wa Mungu ni sehemu yoyote katika maisha yako ni njia pekee ya kumaliza madhaifu
yako. Mfanye Mungu atawale maisha yako kwa ajili ya kumaliza madhaifu ambayo
yamekusumbua muda wote. Kumbuka ukitimiza wajibu wako katika kila sekta ndio
kusudio kubwa ambalo Mungu anahitaji kutoka kwako.
Juni 13 (164): Kujikita
kwenye suala moja matokeo yake ni kushindwa kuona masuala mengine
yanayokuzunguka. Muhimu ni kujiuliza kuwa umejikita kwenye masuala yapi katika
maisha yako ya kila siku. Kama muda mwingi unautumia kufanya yasiyo na tija
ndivyo yamekuziba macho husione yale yenye tija.
Juni 14 (165): Maumivu
yako ya zamani yataamua shauku/dhamira yako siku zijazo. Kumbe ni muhimu katika
magumu unayopitia kuhakikisha kuna somo unajifunza ili kuepuka kurudia magumu
hayo katika maisha yako ya baadae.
Juni 15 (166): Mwonekano
wako utabadilika kulingana na namna unavyotaka uwe. Wewe ndo mhusika mkuu wa
maisha yako, kama ni filamu ya maisha basi tunasema wewe ndo stering wa filamu
hiyo. Maamuzi yapo mikononi mwako.
Juni 16 (167): Mara
zote Shetani huwashambulia wale waliopo kwenye mpango wa kuinuliwa. Kadri unavyokaribia
kwenye mafanikio unatakiwa kutambua kuwa vikwazo vitakuwa vingi na vyote
vinalenga ukate tamaa ya kuendelea kusonga mbele.
Juni 17 (168): Tiba
ya haraka ya kutokuwa na shukrani ni kupoteza kile ulichopata na ukashindwa
kushukuru. Jiulize ni mara ngapi umetoa shukrani kwa yale ambayo umebahatika
kupata katika maisha yako.
Juni 18 (169): Upako
unaouheshimu ndio una nafasi ya kuongezeka katika maisha yako. Kumbuka kuwa
chochote kinachopewa nafasi katika maisha yako kina nafasi ya kuongezeka na
kukua zaidi. Kama unatoa nafasi kwa ubaya katika maisha yako utavuna mabaya na
kinyume chake ni sahihi.
Juni 19 (170): Thamani
ambayo Mungu yupo tayari kukulipa inadhihirisha thamani ya mbegu uliyopanda. Hii
ni sheria ya asili kuwa mavuno yako ni lazima yaendane na jitihada unazoweka
kwenye kupanda mbegu, kuimwagilia, kuipalilia na kuongolea matawi.
Juni 20 (171): Tatizo
lililopo karibu yako ni mlango wa kuondokana na shida katika maisha yako. Kumbe
katika kila tatizo ni lazima kutafuta mlango uliopo kwa ajili ya kutatua
matatizo yanayokusumbua.
Juni 21 (172):
Vimelea vya magonjwa hutazama madhaifu kama sehemu ya kuondoka na kinga ya
mwili hutazama madhaifu yako kama sehemu ya kuimalisha ulinzi. Hakikisha unafanya
yale yanayolenga kuimarisha kinga ya mwili kwa ajili kupunguza vimelea vya
magonjwa katika mwili wako.
Juni 22 (173): Mara
nyingi sehemu ya Shetani kuingia katika maisha yako ni kupitia kwa mtu wako wa
karibu. Kuwa makini na watu walio karibu yako.
Juni 23 (174): Wasio
na hofu ya Mungu hutoa zawadi/rushwa kwa ajili ya kushawishi maamuzi wakati wacha
Mungu hutoa zawadi kwa ajili ya kuboresha mahusiano/upendo. Jiulize zawadi
unazotoa zinakusudia nini hasa katika maisha yako ya baadae.
Juni 24 (175): Utoufati
uliopo katika kila msimu ni maagizo. Katika kila Msimu unaagizwa ni ufanye na
kwa wakati upi ili ufanikishe kusudio lako. Ukienda kinyume na maagizo
utaadhibiwa kwa kupata kinyume na makusudio.
Juni 25 (176): Malipo
ya uwepo wa Mungu ni muda. Wote tumepewa muda sawa bila kujali kipato, rangi,
nchi au umri. Unafanya nini katika kila sekunde uliyopewa bure ndicho
kinatutofautisha katika maisha yetu.
Juni 26 (177): Taarifa
zinaongeza uwezo wa kujiamini. Hakikisha una taarifa za kutosha katika yale
unayofanya. Fanya tafiti binafsi katika kila sekta ya maisha yako kwa ajili ya
kujiongezea uwezo wa kujiamini.
Juni 27 (178): Tatizo
ambalo upo tayari kutatua katika jamii linadhihirisha uwezo wako wa kutatua
matatizo zaidi. Kumbuka kuwa kadri unavyotatua tatizo moja ndivyo matatizo
zaidi yanakusubiria kwa ajili ya kutatuliwa. Pia, kumbuka kuwa tunatengeneza
jina na kupata ridhiki yetu kwa kutatua matatizo ya jamii tunakoishi.
Juni 28 (179): Vimelea
vinakutaka ukiwa umepata wakati walinzi wanakutaka ukiwa umejifunza. Katika maisha
kuna watu ambao tabia zao ni sawa na vimelea – ukiwa na mali utapata marafiki
wengi na zikiishi hautojua wamepotelea wapi.
Juni 29 (180): Mapambano/jitihada
ni ushuhuda kuwa bado hazina iliyopo ndani mwako haijatumiwa ipasavyo. Hakikisha
unajibidisha kwa kadri uwezavyo kuhakikisha hazina hiyo inatumiwa ipasavyo na
kufaidisha jamii inayokuzunguka bila kufanya hivyo una deni kwa Muumba wako.
Juni 30 (181): Wasio
na kumbukumbu yako kamwe hawawezi kuhisi maumivu yako. Kadri unavyowagusa wengi
katika jamii ndivyo unatengeneza hisia zaidi kutoka kwa jamii hiyo katika
nyakati zako za maumivu.
Sehemu
hii ya tatu ina funguo za hekima kutoka kwa Mike Murdock ambazo ni katika mwezi
Aprili mosi hadi Juni 30. Nitaendelea na funguo hizi za hekima katika wiki ya pili ya
mwezi Novemba, 2019. Wiki ijayo tukutane kwa ajili ya uchambuzi wa kitabu
kingine kutoka kwa Robert Kiyosaki. Kupata nakala ya kitabu hiki BONYEZA HAPA na
ujiunge na mtandao wa fikra za kitajiri kisha tuma ujumbe wa kuomba kitabu hiki
kupitia barua pepe fikrazakitajiri@gmail.com.
Endelea kusambaza makala hizi
kwa kadri uwezavyo ili ndugu, jamaa na marafiki wanufaike kwa kujifunza maarifa
mbalimbali kutoka kwa waandishi wa vitabu. Kumbuka umepata makala hii bila
malipo yoyote hivyo hakikisha na wewe unaisambaza bure. (Unaposambaza makala
hizi hakikisha haukopi na kupest badala yake share link). Nakutakia
mapambano mema.
Karibuni kwenye fikra za kitajiri ili upate elimu isiyokuwa na
mwisho.
Born to Win ~ Dream Big
Augustine Mathias Bilondwa
Namba ya Simu: +255 786 881 155
Mwanzilishi wa Mtandao wa fikrazakitajiri.blogspot.com
Barua
pepe: fikrazatajiri@gmail.com
|