Habari ya leo rafiki na msomaji wa mtandao wa Fikra za Kitajiri.
Naamini unaendelea vizuri na mapambano ya kila siku kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Kama kawaida yangu, leo katika uchambuzi wa vitabu kupitia mtandao wa Fikra za Kitajiri nakushirikisha uchambuzi wa kitabu cha wiki hii.
Naamini unaendelea vizuri na mapambano ya kila siku kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Kama kawaida yangu, leo katika uchambuzi wa vitabu kupitia mtandao wa Fikra za Kitajiri nakushirikisha uchambuzi wa kitabu cha wiki hii.
Kama bado hujajiunga kwenye mfumo wetu wa
kupokea makala za uchambuzi wa vitabu, tafadhali fanya hivyo KWA KUBONYEZA BONYEZA HAPA na kujaza
fomu kisha bofya “jiunge/subscribe” utakuwa umejiunga na mtandao huu. Ni fursa
ya bure ambayo utaendelea kupata uchambuzi wa vitabu kwa lugha rahisi kupitia
barua pepe yako.
Leo
hii nakushirikisha funguo 31 za hekima sawa na siku za mwezi Januari katika
mwaka (siku 365) ambazo mwandishi anatushirikisha funguo 365 za hekima. Kila wiki
nitakuwa nakushirikisha funguo za hekima kutoka katika kitabu hiki hadi pale
ambapo tutamaliza funguo zote 365.
Karibu
ushirikiane nami kujifunza machache kati ya mengi ambayo mwandishi
anatushirikisha katika kitabu hiki:
Januari 1: Kila
tatizo ni tatizo la kibusara/hekima. Wajibu wako ni kutafuta fundisho lililopo
ndani ya kila tatizo unalokumbana nalo.
Januari 2: Pale
Moyo wako unapochagua kituo cha mwisho katika maisha yako ya kila siku fikra
zako zitatengeneza ramani ambayo itakuwezesha kuufikia mwhisho huo. Hakikisha
moyo wako unachagua mwisho ulio bora ili
Januari 3: Kile
ambacho unaheshimu ndicho unaweza kukivuta katika maisha yako. Jiulize ni yapi
ambayo umekuwa unayaheshimu kiasi ambacho yamepelekea uwe jinsi ulivyo katika
maisha yako ya sasa.
Januari: Siri
ya Maisha yako ya baadae imejificha katika yale unayofanya kila siku. Jiulize
kama yale unayofanya kwa wakati huu yana athari chanya au hasi kwenye maisha
yako ya baadae.
Januari 5:
Baraka unazoweza kupata katika maisha zinatokana na namna ambavyo unawasaidia
wanakuzunguka kutatua matatizo yanayowakabiri. Je umekuwa mtu wa msaada kwa
jamii inayokuzunguka? Kumbuka msaada sio lazima uwe katika mfumo wa pesa.
Januari 6: Yale
unayoyafanikisha yatokee katika maisha ya wengine, Mwenyezi Mungu atawezesha
yatokee katika maisha yako pia. Jiulize kama umekuwa mtu wa kuwezesha mema au
mabaya katika maisha ya jamii inayokuzunguka. Endapo unawezesha mema kwa
wengine tegemea kupata mema katika maisha yako na kinyume chake ni sahihi.
Januari 7: Mbegu
isiyo ya kawaida mar azote inazalisha mavuno yasiyo ya kawaida. Jiulize ni
mbegu ipi unapanda katika maisha yako ya kila siku kama inao uwezo wa
kukuzalishia mavuno unayokusudia.
Januari 8: Neno
la Mungu ni Hekima ya Mwenyezi Mungu. Jiulize hekima hiyo umeitumia vipi katika
maisha yako ya kila siku.
Januari 9: Usahihi
wa malengo yako ni kipimo cha Imani uliyonayo. Jiulize una malengo yapi kwa
ajili ya kila sekta ya maisha yako.
Januari 10: Yale
unayotumia muda mwingi kuyafikiria ndiyo yanazalisha hisia ulizonazo katika
maisha yako ya kila siku. Unahitaji kutumia muda mwingi kufikiria yale ambayo
unataka yatokee kwenye maisha yako kuliko kufikiria ambayo hayana tija.
Januari 11: Mwonekano
wako unaonesha tabia ulizonazo. Jiulize unaonekana vipi kwa jamii
inayokuzunguka na chukua hatua za kuhakikisha mwonekano wako unaenda sambamba
na matamanio ya maisha yako.
Januari 12: Jinsi
unavyoheshimu muda ni kipimo cha fedha unazoweza kumiliki katika maisha yako
yajayo. Hakikisha unatumia muda wako vizuri kwa kutekeleza yale ambayo
yataboresha kipato chako.
Januari 13: Maamuzi yako ni kipimo cha utajiri wako.
Jiulize maamuzi unayofanya katika matukio ya maisha yako ya kila siku
yanaathari zipi katika safari yako ya kuelekea kwenye utajiri wa ndoto zako.
Januari 14: Maelekezo
unayotekeleza kutoka kwa watu wanaokuzunguka ni kipimo cha maisha yako ya
baadae. Jiulize yale ambayo umekuwa ukitekeleza kama yatakufikisha kwenye
maisha ya matamanio yako.
Januari 15: Maumivu
makubwa kwa Mwenyezi Mungu ni pale unapokuwa na shaka juu yake na furaha yake kubwa
ni pale unapokuwa na Imani thabiti juu yake. Tafakari juu ya Imani uliyonayo
kuhusiana na Muumba wako.
Januari 16: Malengo
yako ndiyo yanachagua aina ya walimu unaotakiwa kuwa nao katika maisha yako.
Fanya tathimi ya kujua kama aina ya walimu ulionao wanaendana na malengo ya
kila sekta ya maisha yako.
Januari 17: Mafanikio
kwenye kila sekta ya maisha yako ni matokeo juu ya yale ambayo unaamua
kutochukulia hatua. Unaweza kuchagua kufanikiwa kwenye kila sekta ya maisha yako
au kuamua kushindwa kulingana na namna gani utatekeleza yale ambayo ni muhimu
lakini umekuwa hauyapi nafasi katika maisha yako ya kila siku.
Januari 18: Hali
ya hewa unayozalisha (mazingira ya maisha yako) ni kipimo cha bidhaa zipi
unaweza kuzalisha katika maisha yako. Jiulize kama mazingira uliyopo
yatakufikisha kwenye mafanikio unayotaka.
Januari 19: Ukubwa
wa adui wako ni kipimo cha mafanikio unayoweza kupata. Jiulize maadui wako ni
wapi katika kufikia mafanikio ya ndoto zako. Weka mikakati inayoendana na
ukubwa wa kila adui kwenye njia ya mafanikio yako na anza kuitekeleza mikakati
hiyo mara moja.
Januari 20: Jukumu
lako kubwa katika maisha ya kila siku ndani yake kuna tatizo ambalo Mwenyezi
Mungu amekusudia ulitatue kwa faida ya jamii inayokuzunguka. Kumbe tunatakiwa kutekeleza
majukumu yetu kwa lengo la kutatua matatizo ya jamii. Kwa kufanya hivyo ndivyo
tunapata mafanikio makubwa.
Januari 21: Yale
ambayo upo tayari kuyakimbia katika maisha yako ya kila siku ni kipimo cha
Baraka ambazo Mungu yupo tayari kukupa. Fanya tathimini juu ya matukio au
wajibu upi umekuwa unakimbia kama ni chanzo cha kupata au kukosa Baraka katika
maisha yako.
Januari 22: Imani
uliyonayo katika kila sekta ya maisha ni kipimo cha maisha yako ya baadae.
Jiulize kama imani ulizonazo ni kandamizi au wezeshi katika kufikia mafanikio
ya maisha yako ya baadae.
Januari 23: Daima
mabadiliko katika maisha yako yanategemea na maarifa uliyonayo. Kumbe
tunatakiwa kuuliza ubongo wetu kila siku kwa ajili ya kuwa na mabadiliko katika
maisha yetu.
Januari 24: Thawabu
ya uchungu itategemea ni kwa kiasi gani upo tayari kubadilika. Utaendelea kuishi
maisha ya uchungu na maumivu kama haupo tayari kujitafakari wapi unakosea
katika maisha. Kumbe ili uishi maisha mapya ni lazima uwe tayari kubadilika.
Januari 25: Chochote
kinachopewa nafasi katika maisha yako ni lazima kiongezeke. Jiulize na yapi
yanapewa nafasi katika maisha yako ili kugundua kama ongezeko lake lina athari
chanya au hasi.
Januari 26: Chochote
kinachotawala akili yako umekuwa mtumwa wake. Jiulize umekuwa mtumwa wa vitu
vipi katika maisha yako. Fanya tathimini ili kugundua kama umekuwa mtumwa wa
vitu vyenye tija katika maisha yako ya kila siku.
Januari 27: Jinsi
maisha yako yalivyo ni matokeo ya yale ambayo umeamua kukumbuka mara kwa mara. Je
ubongo wako umejazwa na kumbukumbu zipi? Kumbe jinsi ulivyo ni matokeo ya kumbukumbu
zilizojaza ubongo wako.
Januari 28: Pale
unapotaka kitu kipya katika maisha ni lazima uwe tayari kufanya jitihada mpya zinazolenga
kupata kitu hicho. Utaendelea kupata matokeo yale yale kama unatumia hatua zile
zile za zamani. Kwa hali kama hiyo husitegemee kupata matokeo mapya.
Januari 29: Yale
unayoyasikia mara kwa mara mwisho wake unayaamini kuwa ni ukweli. Kumbe unahitaji
kujiuliza kama kweli yale unayoamini yana ukweli halisi au yamekuwa kikwazo
kwako kufikia kwenye ukweli wenyewe.
Januari 30: Binadamu
wote huwa wanaanguka hila wenye nguvu zaidi wanaamka na kuendeleza jitihada za
kufikia mafanikio waliyokusudia kabla ya anguko. Tambua kuwa wewe sio wa kwanza
kuanguka kwani wapo walioanguka zaidi yako. Katika anguko hilo walijipima na
kugundua kwa nini wameanguka na hatimaye wakaweka mikakati ya kusimama na
kusonga mbele zaidi.
Januari 31: Hauwezi
rekebisha kosa ambalo haupo tayari kukiri kuwa umekosea. Makosa ni sehemu ya
kujifunza japo ili ujifunze ni lazima kwanza ukiri kosa. Baada ya kukiri kosa
ndipo utajifunza kutokana na kosa husika.
Hizi ni
funguo 31 za hekima kati ya funguo 365 ambazo mwandishi Mike anakusudia
kutushirikisha katika kitabu hiki. Panapo majaliwa tukutane wiki ijayo kwa
ajili ya funguo zinazofuatia katika siku 365 za mwaka kutoka kwa mwandishi wa
kitabu hiki. Kupata nakala ya kitabu hiki BONYEZA HAPA na
ujiunge na mtandao wa fikra za kitajiri kisha tuma ujumbe wa kuomba kitabu hiki
kupitia barua pepe fikrazakitajiri@gmail.com.
Endelea kusambaza makala hizi kwa kadri
uwezavyo ili ndugu, jamaa na marafiki wanufaike kwa kujifunza maarifa
mbalimbali kutoka kwa waandishi wa vitabu. Kumbuka umepata makala hii bila
malipo yoyote hivyo hakikisha na wewe unaisambaza bure. (Unaposambaza makala
hizi hakikisha haukopi na kupest badala yake share link). Nakutakia
mapambano mema.
Karibuni kwenye fikra za kitajiri ili upate elimu isiyokuwa na
mwisho.
Born to Win ~ Dream Big
Augustine Mathias Bilondwa
Namba ya Simu: +255 786 881 155
Mwanzilishi wa Mtandao wa fikrazakitajiri.blogspot.com
Barua
pepe: fikrazatajiri@gmail.com
|