Habari ya leo rafiki yangu na msomaji wa
mtandao wa Fikra za Kitajiri.
Nianze kwa kukuomba radhi
kuwa wiki hii kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu, sitaweza
kukuletea makala ya uchambuzi wa kitabu. Hii ni kutokana na siku za wikiendi
nipo safarini hivyo sijapata muda wa kutulia kukuchambulia kitabu kama ambavyo
nimekuwa nafanya.
Kwa muda huu mdogo
nilioupata nimeona ni vyema niongee na rika la waajiriwa ambao kila mwisho wa
mwezi wana uhakika wa kupata mshahara kama ujira wa kazi zao. Kubwa ni kwamba waajiriwa
wote wana sifa moja ya kuwa na uhakika wa kupata mshahara kila mwisho wa mwezi
bila kujali mshahara ni mdogo au mkubwa kiasi gani.
Sifa ya pili ambayo
inafanana kwa kundi hili ni kwamba asilimia kubwa ya waliopo katika kundi hili mishahara
yao haiungi na hivyo wengi wanateseka kwa kusubiria kwa hamu mwisho wa mwezi
ufike. Ukitaka kugundua ukweli wa hili tembelea taasisi za benki kwenye tarehe
ambazo mishahara inalipwa.
Sifa ya tatu ambayo inafanana na sifa ya pili
ni kwamba asilimia kubwa ya kundi hili wanaishi kwa mikopo iwe kwenye taasisi
za kifedha au mikopo ya wajasiliamali wadogo katika maeneo wanakoishi. Na asilimia
kubwa kati ya wenye mikopo wamekopa kwa hasara na mikopo hiyo inaendelea
kutafuna maisha yao kutokana na ufinyu wa mshahara baada ya kuondoa makato ya
mikopo.
Sifa ya nne kwa kundi hili ni kwamba asilimia
kubwa kila mara wanaona mishahara yao haitoshi hivyo wanalalamikia
kupandishwa vyeo sambamba na nyongeza ya mshahara ya kila mwaka.
Sifa ya tano ya kundi hili ni kwamba wengi ni
watumiaji wa kubwa (spenders) kwa maana matumizi yao ni makubwa kuliko kipato
walichonacho. Na hii inasababishwa na tabia ya wengi wao kuishi maisha ya
kuigiza katika jamii zinazowazunguka.
Sifa ya sita ni kwamba wengi walio katika
kundi hili hawana muda wa kujifunza maarifa mapya kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi,
kiroho au kijamii. Sifa hii inatokana na ukweli kwamba walio wengi katika kundi
hili wanajiona kukamilika katika kila sekta hivyo hakuna haja ya kujifunza
zaidi nje ya fani walizosoma darasani au wanazofanyia kazi.
Sifa ya saba ni kwamba kundi hili wengi wao
wanatumia kila wanachopata bila kutenga kiasi chochote kwa ajili ya dharura au
uwekezaji wa maisha yao ya baadae. Ni wachache sana katika kundi hili ambao
ukitaka wakupatie angalau milioni moja wanaweza kufanya hivyo bila kuathiri
maisha yao. Hii ni kutokana na kushindwa kutambua kuwa maisha ya kesho
yanaandaliwa leo.
Sifa hizi zinatoa
picha kuwa waajiriwa wengi wanakumbwa na changamoto nyingi ambazo msingi wake
ni kukosa maarifa sahihi katika sekta muhimu. Sekta ya fedha. Nasema sekta ya fedha kwa kuwa bila fedha hakuna
kinachofanyika katika maisha yetu ya kila siku. Wapo wachache ambao watasema
fedha sio muhimu lakini ukweli katika nyoyo zao wanatambua msongo wa mawazo
walionao kutokana na mahitaji makubwa ya kifedha katika maisha yao ya kila
siku.
Kumbe makala hii inakulenga wewe ambaye ni mwajiriwa
au una ndoto za kuajiriwa. Lengo kubwa la makala hii ni kuona kuanzia leo
unafanya maamuzi ya kukuza pato lako ili kupunguza utegemezi wa mshahara mwezi
kwa mwezi au siku nenda rudi. Makala hii inalenga kuanzia sasa nione unaanzisha
utaratibu mpya wa kutenga kiasi cha pesa kutoka kwenye mshahara wako kwa ajili
ya KUJILIPA KWANZA.
Wachina wana msemo ambao unatafsiliwa kwa Kiswahili
kama “Muda
mzuri wa kupanda mti ilikuwa jana lakini muda mzuri zaidi wa kupanda mti ni leo (The best time to plant a tree was
yesterday but the second best time is to day)”. Hivyo,
kutokana na msemo huu wa Wachina ni wazi kuwa wakati sahihi wa KUJILIPA KWANZA NI SASA. Weka malengo
ya kuwa mwezi huu katika mshahara wako ni lazima utenge asilimia yake kwa ajili
malengo ya kesho.
Nini
maana ya JILIPE KWANZA? Kujilipa kwanza ni kuhakikisha unatenga
asilimia flani ya kila shilingi inayoingia mkononi mwako kwa ajili ya
kufanikisha mipango yako ya kifedha kwa siku za baadae.
Ili uwe na mafanikio ya kifedha (uhuru wa
kifedha) ni lazima katika kila shilingi inayoingia mikononi mwako uhakikishe kabla
ya kupanga matumizi ya fedha hizo unatenga asilimia yake kwa ajili ya kufanikisha
ndoto ulizonazo katika sekta ya fedha kwa siku zijazo.
Siri hii ndio inaendelea kutofautisha
waliofanikiwa na wale ambao ni masikini au wenye pato la kati katika jamii
inayotuzunguka. Matajiri wanatumia siri hii kuendelea kuwa matajiri zaidi
wakati masikini pamoja na kwamba wanaifahamu siri hii kwa kutoitumia
wanaendelea kuwa masikini.
Kwa kuwa ninakupenda, nakuthamini na ninatamani uwe kati ya matajiri wa kesho, natumia makala hii kukushirikisha siri ya JILIPE
KWANZA ili uweze kuungana nami katika safari ya kuutafuta utajiri. Toka
nilipoifahamu siri hii kupitia kitabu cha Robert Kiyosaki cha “Rich Dad Poor
Dad” hakika nilisema lazima nibadilishe maisha yangu kwa kutumia siri hii
ambayo matajiri wanaitumia kutengeneza utajiri wao.
Hakika hadi sasa siri hii imetenda muujiza
mkuu katika maisha yangu na nitaendelea kuitumia kufikia mafanikio makubwa sana
ya kifedha katika maisha yangu yajayo. Namuomba Mwenyezi Mungu anipe maisha
marefu ili nifike pale ninapokusudia kufika katika ulimwengu wa fedha.
Hata hivyo, siri ya utajiri unaotafutwa
kupitia siri hii si utajiri wa kulala masikini na kuamka tajiri bali ni utajiri
ambao unahitaji mipango maalumu ya kuufikia utajiri huo. Hapa ni lazima uwe na
mipango ya muda mfupi, wa kati na muda mrefu.
Kwa nini nakutaka uanze KUJILIPA KWANZA?
Nakuhamasisha ujilipe kwanza kwa kuwa:-
a) Mfumo
wa ukokotoaji wa mishahara haujawahi kukidhi mahitaji ya waajiriwa. Hata kama
utalipwa fedha nyingi kiasi gani hakuna siku utaridhika na kiwango unacholipwa.
Hivyo, ni muhimu uanze kuzalisha pato lako nje ya mshahara;
b) Unapojenga
utamaduni wa kujilipa kwanza unajiweka kwenye mazingira salama ya kuwa na akiba
kwa ajili ya kufanikisha maendeleo katika siku zako za baadae. Maana halisi ya ukuaji
wa mwanadamu ni kukua kiuchumi, kiakili, kiroho, kijamii na kiumri. Husikubali kuendelea
kukua kiumri na kuacha sehemu nyingine zimedumaa;
c) Maono
yangu ni kuona unafanikiwa kuwa na uhuru wa kifedha kwa kutenga fedha kidogo
kutoka kwenye mshahara wako. Kumbuka hesabu hii rahisi: 1+0=1 lakini 1+1=2. Hii
ni hesabu rahisi lakini katika ulimwengu wa kifedha ina maana kubwa sana. Kila unapojilipa
unaongeza thamani ya fedha ulizonazo kwa ajili ya uwekezaji; na
d) Nataka
UJILIPE KWANZA ili kuongeza idadi ya Vijana ambao wapo tayari kuibadilisha Duni
hii kuwa mahala pazuri pa kuishi kwa viumbe vyote.
Hivyo nikiwa Mwalimu
na Mhamasishaji natambua kuwa hauwezi kuelewa maana halisi ya kujilipa kwanza
kupitia makala hii. Ili twende pamoja nimedhamiria kushirikisha Siri hii ya
KUJILIPA KWANZA kupitia kundi la WhatsApp la “JILIPE KWANZA” nikiwa na lengo kuu la kuwajumuisha vijana wa rika
tofauti na wenye maono ya kuwa na uhuru wa kifedha katika maisha yao ya baadae.
Kundi hili limepewa
jina la JILIPE KWANZA kwa kuwa
linalenga kuzalisha Mamilionea wa kesho kupitia elimu na miongozo watakayopata.
Kwa ujumla vijana hawa watafundishwa namna ya kujilipa kwanza kwa kutenga
asilimia flani ya sehemu ya pato lao na kuiwekeza sehemu salama kwa ajili ya
kufanikisha maisha yenye uhuru wa kifedha katika maisha yao ya baadae.
Kwa kujiunga na kundi
hili – kijana ambaye ni tajiri wa kesho utafanikiwa kupata faida zifuatazo:-
ü Kupata elimu ya kina (mentorship) juu ya kujilipa kwanza;
ü Kujiwekea nidhamu ya kutenga asilimia ya sehemu ya pato
lako na kuiwekeza sehemu salama;
ü Kupata elimu juu ya sehemu sahihi ya kuwekeza fedha zako
kwa ufanisi hasa ile fedha unayojilipa;
ü Kuwa sehemu ya vijana wenye maono yanayoendana ambao kwa
pamoja chini ya mwongozo wangu wataweka malengo ya kifedha kila mmoja kwa uwezo
wake;
ü Kuhakikisha kila mwisho wa mwezi wanajumuia waliopo katika
kundi hili wote kwa pamoja wanawajibika kutoa taarifa ya mwenendo wao kwenye
sekta ya fedha; na
ü Kupata nakala za uchambuzi wa vitabu mbalimbali
vinavyohusiana na mafanikio ya uhuru wa kifedha.
Ili kuwa sehemu ya kundi hili unatakiwa kulipia ada ya Tshs.
2,000/= kwa mwezi sawa na Tshs. 24,000/= kwa mwaka.
Kama unahitaji kuwa
sehemu ya matajiri wa kesho nitumie ujumbe kupitia barua pepe fikrazakitajiri@gmail.com au kwa kupitia namba yangu ya WhatsApp +255 786 881 155
nitakupa maelekezo ya kulipia ada yako na baada ya kulipia utaunganishwa kwenye
kundi hili.
KARIBU
KATIKA KUNDI LA “JILIPE KWANZA” ILI KWA PAMOJA TUIANZE SAFARI YA UMILIONEA.
Kumbuka kama bado
hujajiunga kwenye mfumo wetu wa kupokea makala za Mtandao wa Fikra za Kitajiri,
tafadhali fanya hivyo KWA KUBONYEZA HAPA na
kujaza fomu kisha bofya “jiunge/subscribe”. Ni fursa ambayo itakuwezesha kupata
makala zenye maarifa mbalimbali kupitia barua pepe yako.
PATA UCHAMBUZI WA VITABU vifuatavyo kwa kulipia Tshs. 5000.00 kila
kitabu (Ukinunua vitabu vyote vitatu utapata kwa ofa ya Tshs 10,000.00).
1. Kitabu cha Kwanza ni “THE RULES
OF MONEY (KANUNI ZA PESA)” kutoka kwa Mwandishi Richard Templar
Katika kitabu hiki utafahamu
kanuni 107 za pesa. Ndani ya kanuni hizo utagundua kuwa utajiri ni haki ya
kila mtu hivyo ni wajibu wako kuwa tajiri. Kanuni zote (107) zimechambuliwa
kwa kina na kuandaliwa kwa lugha Kiswahili. Uchambuzi huu unapatikana kwa
kijitabu kidogo chenye kurasa 39 ambazo unaweza kusoma kwenye simu yako ya
mkononi (simu janja – smart phone) au kwenye kompyuta mpakato (pc).
2. Kitabu cha pili “THE RULES OF
LIFE (KANUNI ZA MAISHA)” kutoka kwa mwandishi Richard Templar
Mwandishi kupitia kitabu hiki anatushirikisha
kanuni 106 za maisha. Kanuni hizi zimechambuliwa kwa kina kwa lugha ya
Kiswahili na unaweza kukisoma kupitia simu janja au kompyuta mpakato. Kanuni
zote zinagusa kila sekta ya maisha yako hivyo ni kitabu ambacho hautojutia
pesa unayoitoa kwani utajifunza maarifa mbalimbali kwa ajili ya kuboresha
maisha yako.
3. Kitabu cha tatu ni “I CAN I
MUST I WILL (NAWEZA, NALAZIMIKA, NITAFANYA)” kutoka Mwanamafanikio na
Mtanzania Mwenzetu Marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi
Kwa ujumla kupitia kitabu hiki Dr.
Mengi anatushirikisha maisha yake kuanzia akiwa mtoto, akiwa mwanafunzi,
wakati anaanzisha biashara yake ya kwanza, namna alivyopanua biashara zake,
wajibu aliokuwa nao kwa jamii, misimamo yake kwenye mfumo wa Serikali kwa
awamu zote tano, wajibu wake kwenye uhifadhi wa mazingira na matarajio yake
kwenye kukuza biashara kwa siku za baadae.
Kupata
uchambuzi wa vitabu hivi tuma pesa yako kwa njia ya M-pesa au Airtel Money
kupitia namba zifuatazo:-
M –
Pesa tumia namba: 0763 745 451 (Majina ni Augustine Mathias)
Airtel Money tumia namba: 0786 881 155 (Majina ni Augustine Mathias)
Baada
kutuma pesa hiyo nitumie ujumbe kwenye namba ya airtel (0786 881 151 451)
ukiwa na barua pepe yako ili nikutumie uchambuzi wa kitabu husika.
UTAJIRI NI HAKI YAKO YA KUZALIWA "BEING RICH IS YOUR BIRTH RIGHT" |