Mwendelezo wa Uchambuzi wa Kitabu cha 365 Wisdom Keys of Mike Murdock: Funguo za Hekima 365 za Mike Murdock


Habari ya leo msomaji wa mtandao wa Fikra za Kitajiri.


Naamini unaendelea vizuri na mapambano yanaendelea kwa ajili ya kuhakikisha kesho inakuwa bora zaidi.

Leo hii naendelea kukushirikisha funguo 365 za hekima kutoka kwenye kitabu cha Mike Murdock. Katika Makala hii nakushirikisha funguo za mwezi Julai na lengo langu ni kumaliza funguo zilizobakia kabla ya mwezi Januari 2020.

Karibu tujifunze wote funguo za hekima ambazo mwandishi anatushirikisha katika sehemu hii:


Julai 1 (182): Mbegu yako itadhihirisha tabia ya udongo. Kumbuka tunafahamu kuwa katika hali ya kawaida, udongo wenye rutuba unatoa mbegu zenye ubora wa hali ya juu. Vivyo hivyo katika maisha ya kawaida matunda yako katika jamii yatadhihirisha tabia zako.

Julai 2 (183): Zawadi tatu za Mwenyezi Mungu ni Kusamehe, Urafiki na Matumaini katika maisha ya baadae. Hakikisha zawadi hizo zinakuwa sehemu ya maisha yako ya kila siku. Jifunze kusamehe, hakikisha unakuwa rafiki mwema na hakikisha unakuwa na tumaini bora katika maisha yajayo.

Julai 3 (184): Uadilifu hauwezi kuthibitishwa bali kinachofanyika ni kuutambua tu. Hivyo katika jamii unahitaji kuwa na vipimo vyako kuhusu uadilifu katika maisha yako ya kila siku.

Julai 4 (185): Tatizo unalotatua linadhihirisha zawadi ambazo utapokea katika maisha yako. Kumbuka kuwa tunapata tuzo kwa kutatua changamoto zilizopo katika jamii tunamo ishi. Ukitatua tatizo dogo utapokea zawadi zinazoendana na udogo wa tatizo hilo na kinyume chake ni sahihi.

Julai 5 (186): Watu hawakumbuki unachosema bali wanakumbuka hisia walizopata kulingana na maneno yako. Kabla ya kutamka neno lolote jiulize litapokelewa vipi na jamii unayoilenga. Ni bora kunyamaza kuliko kutamka neno lenye hisia hasi kwa wengine.

Julai 6 (187): Lengo la adui ni kubadilisha haiba au mwonekano wako katika jamii inayokuzunguka. Hakikisha haumpi nafasi adui kujua undani wako kwani kufanya hivyo unamwongezea nafasi ya kufahamu mapungufu yako.

Julai 7 (188): Wakati utafunua yale ambayo hawezi kufunuliwa katika mahojiano. Kupitia mahojiano unaweza kuongea lolote kuhusu maisha yako lakini ni muda pekee amabo unaweza kudhihirisha ukweli wa kile ulichosema.

Julai 8 (189): Ubora wa udongo unaamua ubora wa mbegu. Ukiwa na udongo bora utapata mbegu bora na kinyume chake ni sahihi. Vivyo hivyo, mafanikio katika maisha yanategemea na matendo yako.

Julai 9 (190): Mapenzi ya Mungu ni tabia sio mahali. Chochote ambacho kinakamilisha tabia njema katika jamii kinadhihirisha uwepo wa Mungu. Hivyo, tenda mema kwa kadri uwezavyo kwani kufanya hivyo unatumia hazina/kalama ambayo umepewa na Mungu.

Julai 10 (191): Ufanye wakati ujao uwe mkubwa sana kwani jana imeshapotea. Ishi leo kwa ajili ya kesho kwani ya jana hayana nafasi tena. Muhimu ni kuhakikisha unatumia ya jana kuepuka makosa katika matendo ya leo na hatimaye kuboresha maisha yajayo.

Julai 11 (192): Ubora wa maswali yako hudhihirisha ubora wa uvumbuzi wako. Husikubali kuridhika na hali inayokuzunguka badala yake katika kila hali jiulize ni kipi unachoweza kufanya ili kuboresha hali husika.

Julai 12 (193): Umaarufu ni pale unapopendwa na watu lakini furaha ni pale unapojipenda mwenyewe. Jiulize je yale unayofanya yanamchango chanya katika kukamilisha furaha yako au yanalenga kutafuta umaarufu tu.

Julai 13 (194): Marafiki wa kweli wana maadui wanaofanana. Kumbuka msemo kuwa ndege wanaofanana huruka pamoja. Kama ni urafiki wa kweli ni lazima muwe mnashirikiana na kutatua changamoto zinazowakabili na kufanya hivyo mnatengeneza maadui. Kumbuka wapo ambao hawapendi urafiki au mahusiano yenu.

Julai 14 (195): Pale unapopenda kitu ndani yake kuna matamanio japo pale unapoheshimu kitu ndani yake kuna uthamani. Hivyo, tofauti katika ya kupenda na kuheshimu ni matamani na thamani. Tanguliza thamani katika kile unachopenda ili kudumisha upendo huo.

Julai 15 (196): Ubora wa mbegu yako unaamua ubora wa mavuno. Mara zote katika maisha fikiria zaidi kuboresha mbegu ambazo ni sawa na msingi wa nyumba ili kuwa na mavuno bora au nyumba imara. Tatizo ni kwamba asilimia kubwa katika jamii inahitaji mavuno bora bila kuwekeza kwenye kuboresha ubora wa mbegu ambazo katika maisha tunaweza kusema ni matendo au tabia yako.

Julai 16 (197): Kazi za Mwenyezi Mungu haziendani na hitaji lako bali maarifa uliyonayo kuhusu yeye. Jiulize je umewekeza kiasi gani katika maarifa yanayolenga kufunua makuu ya Mwenyezi Mungu katika maisha yako.

Julai 17 (198): Ni heri kutokuwa na kitu chochote ambacho Mwenyezi Mungu hajataka uwe na nacho. Yawezekana umeomba sana bila majibu na pengine umekata tamaa, kumbe unahitaji kutambua kuwa Mungu ana makusudi ya kutokupa kile unachoomba.

Julai 18 (199): Msimu wa tafiti sio msimu wa kutangaza bidhaa. Kumbuka kila msimu una matukio yake hivyo unahitaji kuhakikisha yale unayofanya yanaendana na msimu husika. Kuna wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna hivyo husilazimishe kuvuna wakati wa kupanda.

Julai 19 (200): Awaye yoyote katika shida ni mlango wako wa kutokana na shida. Shida zako zinamalizwa kwa kutatua shida zinazowakabili wengine katika jamii au mazingira yanayokuzunguka.

Julai 20 (201): Vita ni ushuhuda kuwa adui yako amefahamu kesho yako. Hakikisha unaifanya mipango yako kuwa siri ili kuepuka mapambano na adui wasiopenda upige hatua katika maisha yako ya baadae.

Julai 21 (202): Yale unayosikia hudhihirisha yale ambayo upo tayari kubadilisha katika jamii yako. Chochote ambacho umedhamiria kufanya katika maisha yako ni lazima utumie muda mwingi kupata taarifa zake. Unatahiji kuwa na taarifa za kutosha kuhusu changamoto ambazo unakusudia kutatua.

Julai 22 (203): Mbegu inayoondoka mikononi mwake kamwe haiondoki katika maisha yako badala yake inaingia katika maisha yako ya baadae ambapo huwa inaongezeka zaidi au inazaa matunda. Kumbe unapoendelea kuishikilia mbegu uliyonayo itaendelea kudumaa jinsi ilivyo na hakuna siku itazaa matunda.

Julai 23 (204): Kuna njia mbili za kuongeza hekima nazo ni: kupitia makosa au kupitia kwa walimu/washauri. Jifunze kutokana na makosa au jifunze kutoka kwa wengine ambao unaweza kuwa kujifunza kwa kusoma maarifa mbalimbali au watu ambao unatamani kuwa kama wao (role models). Mfano, ningekuwa mchezaji wa mpira ningetamani mara zote nifanye vitu anavyofanya Ronaldo au Messi hivyo ningetumia muda mwingi kujifunza kuhusu uwezo wao.

Julai 24 (205): Macho yaliyochoka ni nadra kuona yajayo. Na kama macho yako hayawezi kuona yajayo hauna tumaini la baadae katika maisha. Na kama hauna tumaini katika maisha ya baadae ni vigumu sana kupata mafanikio katika kila sekta ya maisha yako.

Julai 25 (206): Wanaoridhika na madhaifu yako wanaweza kuwa maadui katika kufikia malengo yako. Kumbe unatakiwa kujiuliza kama wanaokusifia wanafanya hivyo kwa kumaanisha au wanafanya kwa lengo la kukudumaza husipige hatua zaidi. Husiridhike na hatua ulizofikia bali endelea kuboresha zaidi kwa kupunguza madhaifu yaliyopo.

Julai 26 (207): Yupo mtu ambaye mara zote anakuangalia na yupo tayari kubariki kazi ya mikono yako. Kumbe katika kila tendo unalofanya katika maisha yako unapaswa kukumbuka kuwa ipo nafsi inakuangalia na unaweza kubarikiwa au kulaaniwa kupitia tendo hilo.

Julai 27 (208): Hauwezi kushinda kile ambacho haupo tayari kukichukia. Hivyo, kama kuna tabia au matendo ambayo huyapendi katika maisha yako, hatua ya kwanza ya kubadilisha tabia au matendo hayo ni kuyachukia.

Julai 28 (209): Chochote unachojaribu kuishi bila mafanikio ni kwa sababu haujakipa thamani inatakiwa. Kumbe ili ufanikishe chochote katika maisha ni lazima kwanza ukithamini. Kwa maana hiyo tunafakiwa kupata vitu ambavyo vimepewa thamani katika maisha yetu.

Julai 29 (210): Kutoa zaka sio malipo ya deni bali ni kukubali kuwa ni sehemu ya majukumu yako. Hakikisha unalipia zaka kulingana na taratibu za Imani yako.

Julai 30 (211): Utii usio wa kawaida unafungua upendeleo usio wa kawaida. Muhimu ni kujiuliza kuwa utii wako unahusiana na nini. Pia hapa unatakiwa kutofautisha utii na uoga. Watu wengi wanakuwa waoga kwa kudhania kuwa kufanya hivyo wanatii mamlaka iliyopo juu.

Julai 31 (212): Kamwe husilalamike kuhusu hali ya sasa kama haupo tayari kuibadilisha kwa ajili ya mafanikio katika maisha ya baadae. Kumbuka kuwa kesho iliyo bora inatokana na mabadiliko katika mfumo wa maisha leo.

Sehemu hii niliyokushirikisha leo ina funguo za hekima kutoka kwa Mike Murdock ambazo ni katika Julai. Nitaendelea kukushirikisha funguo zilizobakia kwa kadri nitakavyokuwa napata muda. lengo ni kumaliza funguo zote 365 kabla ya mwezi Januari ili funguo hizi uanze kuzitumia katika kipindi cha mwaka 2020. Kupata nakala ya kitabu hiki BONYEZA HAPA na ujiunge na mtandao wa fikra za kitajiri kisha tuma ujumbe wa kuomba kitabu hiki kupitia barua pepe fikrazakitajiri@gmail.com.

Endelea kusambaza makala hizi kwa kadri uwezavyo ili ndugu, jamaa na marafiki wanufaike kwa kujifunza maarifa mbalimbali kutoka kwa waandishi wa vitabu. Kumbuka umepata makala hii bila malipo yoyote hivyo hakikisha na wewe unaisambaza bure. (Unaposambaza makala hizi hakikisha haukopi na kupest badala yake share link). Nakutakia mapambano mema.

Karibuni kwenye fikra za kitajiri ili upate elimu isiyokuwa na mwisho.

Born to Win ~ Dream Big 

Augustine Mathias Bilondwa

Namba ya Simu:      +255 786 881 155
Mwanzilishi wa Mtandao wa 
fikrazakitajiri.blogspot.com
Barua pepe:  fikrazatajiri@gmail.com

PATA UCHAMBUZI WA VITABU vifuatavyo kwa kulipia Tshs. 5000.00 kila kitabu (Ukinunua vitabu vyote vitatu utapata kwa ofa ya Tshs 10,000.00).

1.    Kitabu cha Kwanza ni “THE RULES OF MONEY (KANUNI ZA PESA)” kutoka kwa Mwandishi Richard Templar
Katika kitabu hiki utafahamu kanuni 107 za pesa. Ndani ya kanuni hizo utagundua kuwa utajiri ni haki ya kila mtu hivyo ni wajibu wako kuwa tajiri. Kanuni zote (107) zimechambuliwa kwa kina na kuandaliwa kwa lugha Kiswahili. Uchambuzi huu unapatikana kwa kijitabu kidogo chenye kurasa 39 ambazo unaweza kusoma kwenye simu yako ya mkononi (simu janja – smart phone) au kwenye kompyuta mpakato (pc).

2.    Kitabu cha pili “THE RULES OF LIFE (KANUNI ZA MAISHA)” kutoka kwa mwandishi Richard Templar
Mwandishi kupitia kitabu hiki anatushirikisha kanuni 106 za maisha. Kanuni hizi zimechambuliwa kwa kina kwa lugha ya Kiswahili na unaweza kukisoma kupitia simu janja au kompyuta mpakato. Kanuni zote zinagusa kila sekta ya maisha yako hivyo ni kitabu ambacho hautojutia pesa unayoitoa kwani utajifunza maarifa mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maisha yako.

3.       Kitabu cha tatu ni “I CAN I MUST I WILL (NAWEZA, NALAZIMIKA, NITAFANYA)” kutoka Mwanamafanikio na Mtanzania Mwenzetu Marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi
Kwa ujumla kupitia kitabu hiki Dr. Mengi anatushirikisha maisha yake kuanzia akiwa mtoto, akiwa mwanafunzi, wakati anaanzisha biashara yake ya kwanza, namna alivyopanua biashara zake, wajibu aliokuwa nao kwa jamii, misimamo yake kwenye mfumo wa Serikali kwa awamu zote tano, wajibu wake kwenye uhifadhi wa mazingira na matarajio yake kwenye kukuza biashara kwa siku za baadae.

Kupata uchambuzi wa vitabu hivi tuma pesa yako kwa njia ya M-pesa au Airtel Money kupitia namba zifuatazo:-
M – Pesa tumia namba: 0763 745 451 (Majina ni Augustine Mathias)
Airtel Money tumia namba: 0786 881 155 (Majina ni Augustine Mathias)

Baada kutuma pesa hiyo nitumie ujumbe kwenye namba ya airtel (0786 881 151 451) ukiwa na barua pepe yako ili nikutumie uchambuzi wa kitabu husika.

UTAJIRI NI HAKI YAKO YA KUZALIWA "BEING RICH IS YOUR BIRTH RIGHT"

onclick='window.open(