Mambo Niliyojifunza Kwenye Kitabu cha How To Write a Marketing Plan: Jinsi ya Kuandika Mpango wa Masoko

Habari ya leo rafiki na msomaji wa mtandao wa fikra za kitajiri.

Ni matumaini yangu kuwa unaendelea kupambana kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Karibu tena katika mtandao wa FIKRA ZA KITAJIRI kwa ajili ya uchambuzi wa kitabu cha wiki hii. Leo hii ikiwa ni wiki ya 4 katika kipindi cha mwaka 2018 naendelea kukushirikisha uchambuzi wa vitabu mbalimbali vyenye mafundisho tofauti katika kila sekta ya maisha yako.

Makala hizi za uchambuzi wa vitabu zimekuwa zikikufikia kila wiki kwa kadri ambavyo napata muda wa kukushirikisha kile ninachojifunza kutoka kwenye vitabu hivi. Ni matarajio yangu kuwa muda ninaotumia kukushirikisha uchambuzi wa vitabu umekuwa wa msaada mkubwa kwako katika kubadilisha maisha yako.

Hata hivyo, mtandao huu unahitaji maoni/ushauri au shuhuda kwa namna ambavyo umekuwa wa msaada kwako (tuma maoni/ushauri/ushuhuda wako kupitia barua pepe fikrazakitajiri@gmail.com).

Unaweza kujiunga na mtandao huu, KWA KUBONYEZA BONYEZA HAPA na kujaza fomu kisha bofya “jiunge/subscribe” utakuwa umejiunga na mtandao huu. Kwa kujiunga na mtandao huu utapata makala zinazochapishwa humu moja kwa moja kwenye barua pepe yako bila malipo yoyote.

Kijitabu cha wiki hii ni “How To Write a Marketing Plam” kutoka kwa mwandishi John Westwood. Katika kitabu hiki tunashirikishwa namna ya bora ya kuongeza mauzo ya biashara kupitia kwenye mpango wa masoko.

Karibu tujifunze machache kati ya mengi ambayo mwandishi Robert Kiyosaki anatushirikisha katika kitabu hiki:

1. Biashara ili iwe ya mafanikio ni lazima iwe na mpango. Mpango huu katika sehemu zake ni lazima uwe na mpango wa masoko. Mpango wa masoko unaelezea juu ya namna ambavyo kampuni itapenya kwenye soko kwa kuonesha mbinu zitakazotumika pamoja na kiwango kinachokusudiwa kuingizwa kwenye soko na asilimia soko inayolengwa. Mpango huu ni nyenzo ya mawasiliano ndani ya kampuni kwani unaelezea mpango wa kampuni katika kuingia kwenye soko pamoja na namna kuendelea kulinda soko husika.

2. Katika kuandaa mpango wa masoko ni lazima kwanza utambue kuwa ili kampuni iweze kuzalisha faida ni lazima ifanikishe mauzo ya bidhaa au huduma zake kwenye soko. Hivyo, ili kampuni ifanikishe mauzo ni lazima iangalie uwezo ilionao katika kuzalisha biadhaa au kutoa huduma. Hapa ndipo mpango wa mauzo unahitaji kuzingatia mahitaji ya wateja kwani bila kuzingatia hilo kampuni haitaweza kuongeza mauzo yake. Kutokana na hilo, mpango wa mauzo ni lazima uzingatie sehemu tatu ambazo ni (a) uwezo wa kampuni kwenye kuzalisha bidhaa au kutoa huduma (b) mahitaji ya wateja kwenye soko husika na (c) mazingira ya soko husika.

3. Mpango wa mauzo katika kufikia mahitaji ya soko ni lazima ujikite kwenye sehemu kuu nne juu ya bidhaa/huduma zake. Sehemu hizi ni (a) aina ya bidhaa/huduma inayouzwa (b) sera ya mauzo kwa maana ya bei (c) namna ya kutangaza bidhaa/huduma zake na (d) njia za kusambaza bidhaa/huduma husika.

4. Usambazaji na utangazaji wa bidhaa/huduma vinahitajika hasa pale unapoingia kwenye soko jipya wakati bidhaa/huduma pamoja na bei vinalenga kwenye namna ya kuendelea kumridhisha mteja.

5. Mpango wa masoko unaandaliwa kwa kutumia taarifa za soko ambalo kampuni inalenga kuuza bidhaa/huduma zake. Hii ni maana kwamba kabla ya kuandaa mpango wa mauzo ni lazima ufanye ukaguzi wa soko husika kwa ajili ya kutafiti taarifa muhimu za soko na uzalishaji wa bidhaa za kampuni. Na mara nyingi inahusisha utafiti juu ya bidhaa, bei yake, njia sahihi za kutangaza bidhaa na njia sahihi ya kusambaza bidhaa husika.

6. Katika utafiti wa soko ni muhimu kuzingatia taarifa muhimu kama vile namna ambavyo soko linabadirika mara kwa mara, ukubwa wa soko, mchanganuo wa wapinzani wako wa karibu, hali ya soko, bidhaa zipi zinapendwa sana sokoni hasa zile ambazo zinaendana na bidhaa zako, taarifa muhimu za Serikali, kisiasa na kijamii. 

7. Mpango wa masoko ni lazima uweze kutofautisha mahitaji tofauti ya wateja katika soko husika. Mwandishi anatushirikisha kuwa sio wateja wote katika soko watahitaji aina moja au radha moja ya bidhaa zako. Ndio maana katika soko la vinjwaji mfano, kampuni ya Pepsi au Cocacola utakutana na radha zote. Hii ni pamoja na kuzingatia vifungashio vyenye ujazo tofauti kwa ajili ya kutofautisha bei ya bidhaa husika. Hali hii inamfanya mteja apate machaguo anayohitaji.

8. Unapoandaa mpango wa masoko ni lazima ufanye tathimini ya uwezo wako (strength), madhaifu ya kampuni yako (weakness), fursa zilizopo (opportunity) na hali hatarishi zilizopo (threat). Tathmini hii itakuwezesha kufahamu sehemu muhimu za kuboresha, kuchangamkia au hatua za kuchukua dhidi ya changamoto.

9. Mpango wa masoko ni lazima uwe na malengo ya mauzo na malengo haya ni lazima yawe na mikakati/njia zitakazotumika kutimiza malengo. Malengo haya ni lazima yajikite kwenye bidhaa/huduma inayotolewa kwenye soko husika wakati mikakati/njia inapaswa kujikita kwenye bei ya bidhaa/huduma, njia za usambazaji pamoja na mbinu za kujitangaza. Mikakati ya kufikia malengo ni lazima itengenezewe malengo pamoja na mikakati ya kufikia kusudio lengwa.

10. Malengo ya mauzo ni lazima yawe yanajieleza, yanapimika na yanatekelezeka. Malengo haya yanaweza kutengenezwa kwa asilimia au namba ili iwe rahisi kufanya tathimini ya utekelezaji wake. Hii itasaidia kutoa mwelekeo wa kampuni kwenye soko husika. 

11. Katika mpango wako wa mauzo ni lazima utambue kuwa bidhaa/huduma yako kwenye soko itapitia hatua kuu sita za mauzo. Hatua hizi ni; (i) kutambulika sokoni (ii) ukuaji wa mauzo ya awali (iii) ukuaji wa mauzo wa haraka/ghafla (iv) hatua ya ukomavu – mauzo ya bidhaa/huduma yamefikia hatua ya juu (v) hatua ya uwepo wa bidhaa/huduma kwa kiwango kikubwa na (vi) hatua ya kushuka kwa mauzo.

12. Katika kila hatua kampuni inabidi iwe na mbinu za kuendelea kuongeza mauzo ili iendelee kuteka soko. Mfano, katika hatua ya sita kampuni inaweza kubadilisha vifungashio au kuongeza ujazo kwa ajili ya kuendelea kuridhisha wateja.

13. Kadiri unavyoteka soko ndivyo unakuwa na nguvu kuuza bidhaa/huduma kwa bei unayopenda. Katika kuandaa mpango wa masoko ni lazima ujikite kwenye kuteka soko kutokana na bidhaa/huduma zako. Hii ni lazima ianzie kwenye ubora wa bidhaa/huduma unazotoa pamoja na uwezo wako wa kuzalisha/kutoa huduma husika. Pia, inabidi kukumbuka kuwa ili uteke soko husika ni lazima mzunguko wa fedha inayoingia kutokana na mauzo uwe juu.

14. Sera ya bei ya kampuni katika kuingia kwenye soko jipya inaweza kuwa (a) kuuza bidhaa kwa bei ya juu – kadri unavyouza kwa bei ya juu ndivyo faida inakuwa kubwa lakini idadi ya wateja inakuwa ndogo au (b) kuuza kwa bei ya chini – kadri unavyoingia kwenye soko jipya kwa bei chini ndivyo mauzo ya bidhaa/huduma yanavyoongezeka na ndivyo unavyoongeza uhitaji wa bidhaa/huduma husika kwenye soko.

15. Usambazaji wa bidhaa/huduma kama sehemu ya mpango wa soko ni lazima ieleze mtawanyiko wa masoko, njia za kusafirisha na huduma kwa wateja. Muunganiko wa vitu hivi ndivyo unakamilisha mpango wa usambazi kama sehemu ya mpango wa masoko.

16.Kama kampuni ni lazima kufahamu sehemu masoko yalipo na ili kutambua njia ya kuwafikia wateja ambayo ni bora katika kupunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa/huduma. Hata hivyo, mpango wa usambazaji ni lazima uunganishwe na utoaji huduma kwa wateja kama sehemu ya kujitangaza zaidi.

17. Katika sehemu ya mpango wa usambazaji ni lazima uainishe mfumo wa mauzo ambao utatumika hadi kufikisha bidhaa/huduma kwenye soko. Je utatumia mfumo wa mauzo wa moja kwa moja au utatumia mfumo Wauzaji wa jumla na reja reja. Mfumo wa kampuni kuuza bidhaa/huduma zake moja kwa moja kwenye soko ni mgumu na kiuchumi ni wa gharama kubwa. Hata hivyo kuamua ni mfumo upi utumike itategemea na aina ya bidhaa/huduma inayotolewa na kampuni husika.

18. Utekelezaji wa mpango wa masoko ni lazima ndani yake pawepo mpango wa matangazo. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mauzo ya bidhaa ni matokeo ya uwepo wa taarifa sahihi kwa mteja ambazo zimeambatana na uwepo wa bidhaa/huduma kwa muda sahihi. Kufanikisha zoezi hili ni lazima kampuni ianishe mbinu za matangazo zitakazotumika kwa ajili ya kuwafikia wateja. Je utatumia matangazo ya runinga, redio, magazeti au mitandao.

19. Kwa ajili ya ufanisi wa mpango wa masoko ni lazima bajeti/gharama za usambazaji pamoja na matangazo zianishwe kwenye mpango. Hii itasaidia kwenye utekelezaji wa mpango wa usambazaji na matangazo kama ulivyoainishwa kwenye mpango wa masoko.

20.  Mpango wa masoko ni lazima uhuishwe mara kwa mara kwa ajili ya kuingiza mabadiliko yanayojitokeza. Kutokana na ukweli huu ni lazima mpango husika uwe unafanyiwa tathimini kwa ajili ya kujipima utekelezaji wake katika nyakati tofauti.

Haya ni machache ambayo nimeweza kukushirikisha kati ya mengi yaliyo kwenye kitabu hiki. Kupata nakala ya kitabu hiki BONYEZA HAPA na ujiunge na mtandao wa fikra za kitajiri kisha nitumie ujumbe wa kuomba kitabu hiki kupitia barua pepe fikrazakitajiri@gmail.com.

Niendelee kukuomba usambaze jumbe hizi kwa kadri uwezavyo ili yale unayojifunza yawafikie wengi na hatimaye tufanikiwe kuibadilisha dunia hii kuwa mahali pazuri pa kuishi (Unaposambaza makala hizi hakikisha haukopi na kupest badala yake share link). Nakutakia mapambano mema.

Karibuni kwenye fikra za kitajiri ili upate elimu isiyokuwa na mwisho.

Born to Win ~ Dream Big 

Augustine Mathias Bilondwa

Namba ya Simu:      +255 786 881 155
Mwanzilishi wa Mtandao wa 
fikrazakitajiri.blogspot.com
Barua pepe:  fikrazatajiri@gmail.com

PATA UCHAMBUZI WA KITABU CHA THE RULES OF MONEY ( KANUNI ZA PESA)
 
Mwandishi Richard Templar katika kitabu hiki ametushirikisha kanuni 107 ambazo kila mtu anaweza kuzitumia kutengeneza pesa na hatimaye kuwa tajiri. Uchambuzi wa kina wa kanuni zote (107) umeandaliwa kwa mfumo wa pdf na unapatikana kwa gharama ya Tshs. elfu tano tu (5,000/=). Kanuni zote zimechambuliwa na kuandaliwa kijitabu kidogo chenye kurasa 39 ambazo unaweza kusoma kwenye simu ya mkononi (smart phone) au kwenye kompyuta (pc).

Kupata uchambuzi wa kanuni zote tuma pesa yako kwa njia ya M-pesa au Airtel Money kupitia namba zifuatazo:-

M – Pesa tumia namba: 0763 745 451 (Majina ni Augustine Mathias)
Airtel Money tumia namba: 0786 881 155 (Majina ni Augustine Mathias)

Baada kutuma pesa hiyo nitumie ujumbe kwenye namba ya airtel (0786 881 151 451) ukiwa na barua pepe yako ili nikutumie uchambuzi wa kanuni hizi moja kwa moja kwenye mtandao wako.

UTAJIRI NI HAKI YAKO YA KUZALIWA "BEING RICH IS YOUR BIRTH RIGHT"




onclick='window.open(