Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MUDA. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MUDA. Onyesha machapisho yote

FUNGUO 5 ZA KUTHIBITISHSA KUWA UTAJIRI NI HAKI YAKO YA KUZALIWA.

       NENO LA LEO (APRILI 18, 2021): FUNGUO 5 ZA KUTHIBITISHSA KUWA UTAJIRI NI HAKI YAKO YA KUZALIWA.

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine tunapewa kibali cha uhai. Ni siku ambayo tunaalikwa kuendelea kuwa bora katika maisha yetu. Je! ubora wa maisha yetu unapatikana wapi? Hili ni swali ambalo kila siku asubuhi tunatakiwa kujiuliza kabla ya kuzama katika majukumu ya siku husika. Kwa maana tunakuwa bora kupitia yale tunayofanya katika maisha yetu ya kila siku. Una nafasi ya kuyaboresha au kuyaharibu maisha yako kupitia matendo ya kila siku.

Je unahitaji kupata mafundisho ya aina hii kila siku? Jiunge kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, tafadhali BOFYA HAPA KUJIUNGA.

Karibu katina neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza funguo tano tofauti za kuthibitisha kuwa utajiri ni haki yako ya kuzaliwa kupitia maandiko matakatifu. Kwanza tunatakiwa kutambua kuwa Mungu ameumba mfumo wa kuzalisha utajilisha kwa kila mwanadamu ambao hauwezi kushindwa kutimiza hitaji hilo. Pesa inajibu kila hitaji la mwanadamu kwa ajili ya ukamilisho wa maisha ya utakaso wake.

Tunaweza kusema kuwa pesa ni halamu katika mtazamo hasi wa mafundisho ya dini lakini tukitafakari kwa msaada wa roho mtakatifu tunagundua kuwa Mungu anataka tuishi maisha ya kujitosheleza, naam maisha ya utajiri (soma Mhubiri 10:19). Mungu anataka uwe na pesa za kutosha kwa sababu tatu kuu: Moja, upate kufadhili kazi za kitume – enendeni Ulimwenguni kote na kuhibiri injiri. Mbili, kuhistili vyema familia yako – familia yako inatakiwa kuwa sehemu ya furaha na siyo sehemu ya manunguniko yanayotokana na kupungukiwa kifedha. Tatu, kuitawala dunia – tumepewa mamlaka ya kuitawala dunia kwa faida ya maisha yetu.

Soma: MAISHA YA UTAJIRI AU UMASIKINI: JE NI IPI HAKI YAKO YA KUZALIWA?

Ufunguo #1: Mungu ndiye chanzo halisi cha utajiri (Wafilipi 4:19). Hivyo, tuna kila sababu ya kutambua kuwa utajiri halali unatoka kwa Mungu ikiwa tunafanya kazi za kiroho ambazo zinamruhusu Mungu kuwa chanzo chako cha pekee cha utajiri. Pia maandiko matakatifu yanasema, "Hasiyefanya kazi, hapaswi kula" (2 Wathesalonike 3:10), na Mungu ndiye Muumba wa kazi. Hivyo, kwa Mungu tunapata nguvu za kuzalisha mali, tunapata kila rasilimali kwa ajili ya kukua kipesa, tunapata uwezo wa kiakili kutumia rasilimali zinazotuzunguka, na tunapata baraka ya kuzalisha mali zaidi (Kumbukumbu la Torati 8:18). Tafsiri yake ni kwamba, Daima Mungu atakupa kitu cha kuweka mikono kwenye yako, atakupaka mafuta uwezo wako, na atakupa baraka za kufanikiwa zaidi ikiwa unatii amri zake.

Ufunguo #2: Biashara ni Mfumo wa kukuwezesha kutengeneza utajiri (Luka 19:13). Hakuna utajiri ambao unapatikana bila mfumo maalumu wa uzalishaji mali. Hiyo haimaanishi kwamba kila mtu ameitwa kumiliki biashara-lakini kila mmoja wetu atajihusisha na biashara kwa namna moja au nyingine, iwe ni kwenye kazi, katika ununuzi au uwekezaji. Biashara ni kubadilishana bidhaa au huduma kwa faida au faida ya kiuchumi. Unapoajiriwa, unauza huduma zako. Hiyo inakufanya uwe sehemu ya mfumo. Japo pamoja na kuajiriwa bado una nafasi ya kujifunza zaidi kuhusu mfumo husika ili siku moja na wewe umiliki biashara yako. Hivyo, wote tumeitwa kumiliki na kutawala vitu vyote ili Ulimwengu huu uwe mahala pazuri pa kuishi.

Ufunguo #3: Kila aina ya biashara inakutaka ufanye kazi. Na kila kazi inayofanywa kwa bidii na maarifa inamzawadia mhusika faida na kutegemea faida bila kufanya kazi ni kujitafutia umasikini (Mithali 14:23). Kumbe, biashara ni kazi ni kazi ni biashara. Pia, tunatakiwa kutambua kuwa kazi siyo laana, na sio taabu. Hivyo, ikiwa unahitaji utajiri halali ambao tumeona kuwa ni haki yako ya kuzaliwa ni lazima uepuke malalamiko au manung’uniko kuhusu kazi. Kwa tafsiri hiyo, kazi unayoifanya unatakiwa kuitazama katika jicho la zaidi ya malipo, kwa maana chimbuko la kufanya kazi ni kutoka kwa Mungu ambaye anasema atabariki kazi ya mikono yako na kukuwezesha kuwa tajiri.

Ufunguo #4: Umiliki wa ardhi siyo wa hiari. Amri ya kwanza kabisa ambayo mwanadamu baada ya kuumbwa alipewa kulingana na maandiko matakatifu ni kuzaa na kuitawala dunia (Mwanzo 1:28). Hivyo, tumeumbwa kuwa watawala na katika msingi huo kumiliki ardhi siyo ubinafsi, siyo anasa bali ni kuitikia amri hiyo. Hatupaswi kuwa chini ya udhibiti wa Ulimwengu bali tunatakiwa kutumia kila kilichopo ndani yake kwa ajili ya kufikia ukuu katika kila sekta ya maisha yetu. Unapofanikiwa kutambua msingi wa amri hii katika kuvuta kila hitaji la maisha yako, utaingia katika viwango vya ustawi ambao haujawahi kuota katika kipindi cha maisha yako. Ni wakati wako kumiliki ardhi ambayo ni msingi wa biashara nyingi (Walawi 25: 23 – 28).

Ufunguo #5: Tumeumbwa katika sura na mfano wake. Tunasoma katika sura ya mwanzo ya Mwanzo kuwa Mungu alituumba kwa mfano wake, kulingana na sura yake (Mwanzo 1:26 – 28) na kumpa binadamu jukumu la uumbaji mdogo kwa kumuelekeza kuijaza na kuitawala dunia. Kupita amri sura na mfano wake tunatakiwa kuumba (ubunifu) vitu mbalimbali ambavyo vitaifanya ukuu wa Mungu uonekane katika uso wa Dunia. Kwa sura na mfano wake tumepewa uwezo wa kutengeneza vitu kupitia malighafi ambazo Mungu ametupa kwa wingi. Hivyo, sisi ni mawakili wa Mungu katika kutumia, kumiliki na kuumba (Zaburi 50: 10 – 12). Somo la kujifunza hapa ni kwamba mali tunazomiliki na tunazokusudia kumiliki tunapata kupitia uwezo ambao Mungu ametupatia. Utajiri tulionao ni wake na lazima utumike kulingana na matakwa yake. Tutafute na kuomba Mungu atupatie utajiri unabariki familia, jamii, na nchi. Baraka hiyo ni pamoja na kushiriki katika imani na upendo, kufanya kazi ambazo zina maana na zinaonyesha ubunifu wa Mungu ndani mwetu.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI

Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo nimekushirikisha funguo tano ambazo zinaonesha kuwa utajiri ni haki yako ya kuzaliwa. Mungu hapendi tuwe masikini na tunaposhindwa kuidai haki yetu ya kuzaliwa (haki ya kuwa tajiri) tunakuwa tunatenda dhambi. Mungu ametupatia kila kitu kwa ajili ya kutumia vitu hivyo kumiliki utajiri tunaotamani. Kumbuka, mbegu ikidondoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganishi hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema OFA hii.

๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

MAFANIKIO NI WATU, FAHAMU MBINU AMBAZO UNAWEZA KUZITUMIA KUVUTA WATU CHANYA KWAKO.

NENO LA LEO (APRILI 14, 2021): MAFANIKIO NI WATU, FAHAMU MBINU AMBAZO UNAWEZA KUZITUMIA KUVUTA WATU CHANYA KWAKO.

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni wakati mwingine tumepata bahati ya kuwa hai huku tukiwa na deni la kuishi kulingana na ndoto kuu ya maisha yetu. Je umeshaitambua ndoto hiyo na tayari umeanza kuiishi katika maisha yako ya kila siku? Maisha yenye thamani yanakutaka uwe na ndoto ambayo kila siku kuna jambo unalifanya kupitia majukumu yako ya kila siku. Matendo yako katika kila siku ambayo umebahatika kuwa hai yanatakiwa kuwa sawa na uwekezaji unachangia ukamilisho wa ndoto kuu ya maisha yako.

 Je unahitaji kupata mafundisho ya aina hii kila siku? Jiunge kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, tafadhali BOFYA HAPA KUJIUNGA.

Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza jinsi ambavyo tunaweza kuvuta watu chanya katika maisha yetu. Ndoto yoyote ambayo umeichagua kuyatoa maisha yako kwa ajili ya ukamilisho wake inahitaji watu tena watu wenye mtazamo chanya. Hivyo, katika kila aina ya mafanikio unayoyataka kama matokeo ya ukamilisho wa ndoto ya maisha yako ni lazima utambue aina ya watu ambao wanatakiwa kukuzunguka sambamba na wale ambao unatakiwa kujitenga nao.

Soma: TABIA 10 AMBAZO ZITAONESHA KUWA UNAKIMBIZANA NA HELA MAISHA YAKO YOTE. 

Ikiwa unahitaji kuwa na mtazamo chanya ni lazima uzungukwe na watu wenye mtazamo chanya. Hata hivyo, kuzungukwa na watu wenye mtazamo chanya ni lazima ujue mbinu za kuwavuta watu aina hiyo. Kuvutia watu chanya kwako ni kunaanzia kwenye mtazamo wako. Kupitia mtazamo kuna vitu ambavyo utatakiwa kuvifanya kila mara na hatimaye vitu hivyo vitakuwa sehemu ya tabia zako. Karibu tujifunze mbinu ambazo unaweza kuzitumia kuwavuta watu chanya:-

Mbinu #1: Jisemee kauli chanya kabla ya kwenda kwenye matukio ya kijamii.

Mara zote sisi ni zao la kauli na imani tunazoamini dhidi ya nafsi zetu. Ili kuvuta watu chanya katika maisha yako ni lazima kwanza uwe na imani chanya juu ya nafsi yako. Kabla ya kukutana na makundi ya watu ni lazima uwe kauli zinazoifanya nafsi yako iaminiwe na watu. Pia, unatakiwa kuwa na kauli chanya kuhusu watu unaonenda kukutana nao. Kwa kufanya hivyo, utajisikia mwenye furaha na msisimko kukutana watu wengine kwa kuwa unajiamini kila katika kila hali. Hii itafungua akili yako na kukusaidia kuwa chanya na hatimaye kuvutia watu chanya kwa kuwa watu wanapenda watu wanajiamini na wacheshi.

Mbinu #2: Jitenge na watu wenye mtazamo hasi. Ikiwa umezungukwa na watu hasi katika maisha yako ni vigumu sana kwako kuwa na mtazamo chanya. Watu hasi mara zote watakufanya ujisikie uzembe wa kufanya kazi, mara zote utakuwa haujiamini katika maongezi yako au kila unalofanya, na utakuwa mtu wa kulalamika. Kuvuta watu chanya, ni lazima kwanza upunguze mawasiliano na ukaribu na watu wenye mtazamo hasi. Kwa kukimbia watu wa aina hii utaanza kushangaa uwezo wako kwa maana utaweza kufanya vitu ambavyo awali ulidhani haviwezekani.

Mbinu #3: Kuwa mtu Shukrani. Kwanza unatakiwa kwanza ujikubali na kushukuru jinsi ulivyo na kila ulichonacho. Kitendo cha kujikubali na kushukuru kwa kadri unavyotendewa, kitawafanya watu wavutiwe kuwa karibu nawe. Pia, mtu wa shukrani inajumuisha kuwa tayari kupokea mazingira mapya pamoja na watu wapya katika maisha yako.

Mbinu #4: Nenda kwenye matukio yaliyopo nje ya ukanda wako wa faraja. Kukutana na kuvutia watu wenye mtazamo chanya, ni lazima uondoke kwenye mazingira uliyozoe. Ni lazima ushiriki matukio ambayo haujazoe kushiriki. Ni lazima uwe tayari kushiriki mikusanyiko ambayo itakuongezea changamoto mpya za maisha. Ni lazima uwe tayari kushiriki matukio ambayo yanaongeza hali na msisimko wako dhidi ya watu na mazingira kwa ujumla. Hii haimaanishi kuwa kila mara unapaswa kwenda nje na kushiriki kila aina ya sherehe, badala yake inakukumbusha umuhimu wa kwenda kwenye hafla za kijamii ambazo ni mpya kwako na zinakukutanisha na watu wapya. Mfano, unaweza kushiriki semina mbalimbali, kujiunga na makundi mapya ya watu, kutoka nje kwa ajili ya chaku au kinywaji kwenye sehemu ya hadhi, au kwenda kwenye karamu ya chakula cha jioni na watu maalum.

Mbinu #5: Kuwa mnyumbulifu. Ili kuvuta watu chanya ni lazima uwe tayari kupokea mawazo na imani mpya zenye kukinzana na mawazo na imani ulizonazo. Ikiwa utafanikiwa kupokea mawazo na imani mpya bila bila kukasirika au mabishano yasiyo na tija, utavutia zaidi watu watu wenye mtazamo chanya upande wako.  Maisha yamejaa matukio yasiyotarajiwa, hivyo, watu wanapenda watu ambao wapo tayari kuendana na mabadiliko kwa urahisi. Ikiwa unaweza kuzoea hali yoyote kwa urahisi, itakuwa rahisi kuvutia watu chanya upande wako.

Mbinu #6: Kuwa mtu wa upendo na wasaidie wengine. Kusaidia wengine na kutoa upendo kwa wengine bila kutegemea mrejesho ni chambo cha kuvuta watu chanya bila kutarajia. Ishara za upendo na matendo ya kusaidia wengine wala siyo lazima zihusishe vitu vya gharama, vitu vya kawaida iwapo vimefanywa kwa upendo vinapelekea watu wakuamini na kukupenda. Kumbuka, toa kwa njia ya upendo wala sio kwa njia ambayo itakufaidisha kwa baadae. Haupaswi kutarajia malipo yoyote katika matendo ya upendo au msaada unaotoa kwa wengine.

Mbinu #7: Tumia mbinu za utulivu wa akili. Moja ya mbinu za kutuliza akili ni kupitia tajuhudi (meditation) ambayo inahusisha utulivu wa akili kwenye kufikiria juu mazingira na watu wanaokuzunguka. Utulivu wa fikra kwenye maisha yako kwa kuzingatia mawazo yako kwa wakati uliopo tu na jinsi unavyohisi wakati huo huo. Kupitia tajuhudi utakutana na mioyo ya watu wengine wenye mtazamo wako. Unaweza kufanya tajuhudi kwa kuifanya akili yako ijikite kuzingatia ulimwengu unaokuzunguka. Angalia vitu unavyogusa, unasikia nini, unaona nini au unanusa nini (tumia milango yako ya fahamu kuituliza akili yako). Mfano, ikiwa unakula, zingatia ladha na jinsi unavyohisi juu hiyo ladha. Zingatia kutuliza akili yako kwenye jambo unalojihusisha nalo kwa wakati husika.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI

Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza mbinu ambazo tunaweza kutumia kuvuta watu chanya katika maisha yetu ya kila siku. Mafanikio ni watu, hivyo tuna kila sababu ya kujifunza kuvuta watu sahihi katika maisha yetu ya kila siku. Kumbuka, mbegu ikidondoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganishi hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema OFA hii.

๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Uchambuzi wa Kitabu cha The One Thing: Mwongozo wa kufanikiwa kimaisha kwa kujikita kwenye jambo moja baada ya jingine.

Habari rafiki yangu mpendwa, hongera kwa kuendelea kujifunza kupitia Makala za uchambuzi wa vitabu ambazo nimekuwa nashirikisha jamii kupitia mtandao wa FIKRA ZA KITAJIRI. Karibu katika uchambuzi wa kitabu cha leo ambacho ni cha 8 kati ya vitabu 30 ambavyo nimejiwekea lengo kuvisoma katika kipindi cha mwaka huu 2020.

Kama bado hujajiunga na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI kwa ajili ya kupata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, tafadhali JIUNGE SASA.

Kitabu ninachokushirikisha kupitia makala hii ni The One Thing” kutoka kwa mwandishi Garry Keller. Kupitia kitabu hiki mwandishi anatushirikisha mbinu mbalimbali kwa ajili ya kuepuka kugusa gusa mambo mengi katika Maisha ili kuhakikisha kila mara tunafanikisha jambo mojo baada ya jingine. Kuna msemo wa Warusi kuwa “ukifukuza sungura wawili kwa wakati mmoja utajikuta umeshindwa kumkamata hata mmoja wao”. Tafsiri yake ni kwamba, tunafanikiwa kimaisha pale tunapokuwa na utaratibu wa kufanikisha jambo moja baada ya jingine.

Tunafanikiwa kwa kuchagua kitu kimoja na kuhakikisha tunaweka jitihada kubwa za kuhakikisha kitu hiko kinafanikishwa katika nyakati husika. Hivyo, mafanikio makubwa yanapatikana kwa kuweka nguvu ya pamoja kwenye jambo moja kwa wakati husika. Unapofanya mambo mengi kwa wakati mmoja unatawanya nguvu na rasilimali ambazo zingetumika kufanikisha jambo moja kwa muda mfupi. Kutokana na mtawanyiko huo wa nguvu na rasilimali, mara nyingi huwa ni mwanzo wa kukata tamaa kwa kuwa hakuna tija kwenye yale unayofanya.

Watu wote tuna muda sawa lakini tunatofautiana kimaendeleo, wapo wanaofanya kazi nyingi kwa ufanisi, wapo wanaopata zaidi, wapo wanaingiza pesa nyingi na wapo wanaoangaika kimaisha. Kama kipimo cha muda ni sawa kwa wote kwa nini pawepo tofauti hizo? Mwandishi anatushirikisha kuwa wale wenye mafanikio katika Maisha wamejifunza mbinu ya kufanya jambo moja baada ya jingine kwa wakati husika. Ni kupitia siri hii, watu wenye mafanikio wanatekeleza majukumu yao kulingana na orodha ya vipaumbele. Ni kupitia siri hii, watu wenye mafanikio wanatambua kuwa mafanikio makubwa katika Maisha yanapatikana kwa kufanya vitu vichache kwa ufanisi mkubwa. Kumbe, mafanikio yanapatikana kwa kufanya vitu vichache vyenye athari chanya badala ya kufanya vitu vingi vyenye athari hasi.

Karibu ushirikiane nami kujifunza machache kati ya mengi ambayo tunashirikishwa katika kitabu hiki:

UTANGULIZI

1. Kulingana na gunduzi za kisayansi, kitu kidogo katika mpangilio wa vitu vyenye mfanano wa mapana hila urefu tofauti kina uwezo wa kusababisha mwendo ambao utaharibu utulivu wa vitu vyote kwa mfuatano hadi kufikia kiwango cha mshindo mkubwa. Kwa maneno rahisi ni kwamba, jambo dogo ambalo limetekelezwa kwa ufanisi lina uwezo wa kusababisha matokeo makubwa katika Maisha. Ili ufanikishe matamanio au ndoto ulizonazo ni lazima utambue ni ‘vitu vipi vidogo ambavyo utajitoa kuvifanyia kazi kila siku kwa ajili ya ufanisi mkubwa katika kipindi cha muda maalumu’. Mafanikio kwenye jambo dogo yanazaa mafanikio zaidi na kadri unavyoendelea kufanikiwa ndivyo mafanikio yanaongezeka zaidi na zaidi.

2. Makampuni na biashara nyingi zinatambua umuhimu wa kujikita kwenye jambo moja, ndiyo maana tunashuhudia kampuni zinazofahamika kwa kuzalisha aina moja ya bidhaa au kutoa huduma moja kwa wateja. Kadri unavyojikita kwenye jambo moja ndivyo unajitangaza kupitia jambo hilo na hatimaye kila mmoja atakufahamu, na hivyo ndivyo mafanikio yanavyopatikana. Hivyo, ili ufanikiwe hauna budi kuchagua bidhaa au huduma moja na kuhakikisha kila siku unatekeleza majukumu yanayolenga kuiboresha bidhaa/huduma hiyo.

3. Ili ufanikiwe unatakiwa kutambua MTU MMOJA ambaye ndiye anashikiria mafanikio yako. Katika historia ya Maisha yako fikiria mafanikio ambayo umewahi kupata kwa asilimia kubwa yalichangiwa na nani? Jiulize ndoto/matamanio ya mafanikio katika Maisha uliyonayo kwa sasa unahitakiji kupata mtu wa aina gani kwa ajili ya kufikia matamanio/ndoto hazo. Hakuna mtu mwenye mafanikio ambaye amefikia mafanikio hayo pasipo kushikwa mkono na watu wengine kwa namna moja au nyingine. Mtu huyo mmoja anaweza kuwa mzazi, mwenza wako, rafiki, bosi, ndugu au mtu awaye yeyote katika jamii kwa kuwa ulimwengu wa sasa umeunganishwa kuwa kitu kimoja. Hivyo, tambua kuwa hakuna anayefanikiwa peke yake.

4. Ili ufanikiwe unatakiwa kutambua na kuendeleza KIPAJI au UJUZI maalum. Mwandishi anatushirikisha kuwa mafanikio yanahusisha kutumia vipaji tulivyozaliwa navyo au ujuzi ambao tunao kwa ajili ya kuzalisha bidhaa au kutoa huduma kwa jamii. Watu wengi wanashindwa kufanikiwa kimaisha kwa kuwa wameshindwa kutambua ubora wao upo wapi. Mafanikio yanakutaka ujitambue mwenyewe kwanza ikiwa ni pamoja na kufahamu Maisha yako ni kwa ajili ya kufanikisha nini Duniani hapa.

SEHEMU YA KWANZA: AINA ZA UONGO 6 AMBAO TUMEAMINISHWA KUWA KWELI

5. Uongo #1: Kila kitu kina umuhimu sawa (everything matters equally). Usawa ni uongo ambao dunia imeubadilisha uonekane kuwa ukweli. Katika hali yoyote chini ya maamuzi ya mwanadamu Duniani hakuna usawa. Tulipokuwa Watoto tulijukuta katika hali ya utegemezi kwenye kila tulichohitaji kufanya katika Maisha yetu. Kipaumbele namba moja katika umri huo ilikuwa ni kucheza michezo ya kila aina na yeyote ambaye alikusudia kututoa kwenye kipaumbele hicho kwetu alionekana mtu mbaya. Kadri miaka ilivyopita ndivyo tulijikuta tunabadilika kutoka kwenye hali ya utegemezi na kuanza kutakiwa kujitegemea wenyewe na pengine kuanza kutegemewa. Katika kipindi hiki cha Maisha ya kujitegemea na kutegemewa ni lazima uwe tayari kufanya maamuzi sahihi. Maisha yetu ni matokeo ya maamuzi tunayofanya kila siku kwenye kila sekta. Katika kufanya maamuzi haya ndipo tunatakiwa kutambua kuwa hakuna usawa Duniani, hivyo, chochote unachofanya hakikisha umeongozwa na mfumo wako wa maamuzi.

6. Watu wenye mafanikio wana utaratibu wa kutekeleza majukumu yao kulingana na umuhimu na vipaumbele vya majukumu husika. Hapa ndipo dhana ya kuwa “hakuna usawa Duniani” unapotakiwa kuitumia katika majukumu yako kwa kuwa hata majukumu yetu ya kila siku yana umuhimu na vipaumbele tofauti. Hata hivyo, ili ufanikiwe unatakiwa kuwa na vipaumbele vyenye mwendelezo katika kila siku ya Maisha yako. Badala ya kuandaa orodha ya majukumu ya siku unatakiwa kuondaa orodha ya vitu unavyohitaji kufanikisha katika Maisha yako na kila siku kuhakikisha unapiga hatua kuelekea kwenye ukamilisho wa orodha hiyo.

7. Andaa vipaumbele vya kutekeleza katika siku husika kulingana na tija yake katika kukamilisha orodha ya vitu unavyohitaji kufanikisha. Kumbuka Duniani hakuna usawa, vivyo hivyo, majukumu yako katika siku yana tija tofauti kwenye uzalishaji wa matokeo. Hapa ndipo unatakiwa kuifahamu na kuitumia kanuni ya Vilfredo Pareto mwanauchumi muitaliano ambaye katika karne ya 19 aligundua kuwa “takribani asilimia 80 ya ardhi yote (au uchumi) ilikuwa mikononi mwa asilimia 20 pekee ya idadi ya watu”. Baadaye kanuni iligundulika kuwa inafanya kazi katika sehemu nyingi za Maisha. Mfano, asilimia ya 20 ya pembejeo inazalisha 80% ya mazao; 20% pekee ya wafanyakazi wanazalisha 80% ya matokeo; 20% ya wateja wanaleta 80% ya mapato na zaidi na zaidi. Kwa ujumla unatakiwa kupanga vipaumbele vyako kulingana na tija ya uzalishaji wa matokeo kwenye orodha ya vipaumbele vya mafanikio yako. Kumbe, ufanikiwe unatakiwa kujikita kwenye 20% ya kazi ambazo zinaingiza pato la 80% ya matokeo yote. Asilimia 80 ya kazi zinazobakia inabidi utafute watu wa kuifanya kwa ajili yako. Matokeo makubwa (80) unayohitaji yanatokana na vitu vidogo (20) unavyovifanya kwenye majukumu yako ya kila siku. Na pengine husiishie kwenye asilimilia 20 unaweza kutumia kanuni hii kwa kupunguza vipaumbele kutoka asilimia 100 kuja 20 na kutoka asilimia 20 kuja mpaka asilimia 1.

8. Uongo #2: Kufanya kazi zaidi ya moja kwa wakati mmoja (Multitasking). Kufanya majukumu mawili kwa wakati mmoja ni uongo kwa kuwa kati ya majukumu yote hakuna ambalo litafanyika kwa viwango vinavyotakiwa. Maamuzi ya busara ni kukamilisha kazi moja baada ya nyingine. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, ubongo wa mwanadamu umeumbwa katika mfumo ambao unawezesha kufanya kazi moja kwa ufasaha na siyo kufanya kazi zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Unaweza kuongea na kutembea au kunywa na kuandika lakini kutambua kuwa matokeo yanayopatikana yanakuwa hayana au ubora ule ule ikilinganishwa kama ungefanya kazi moja baada ya nyingine. Dunia ya sasa imejaa visumbufu (distractions) vya kila aina ambavyo vinapoteza utulivu wa akili kwenye kazi iliyopo mezani. Kuna usumbufu unaotokana na watu wa karibu yako (Ofisini au nyumbani), milio ya simu kutoka kwenye simu janja, mitandao ya kijamii, barua pepe na kila aina ya visumbufu ambavyo vinazuia ufanisi wa majukumu ya siku husika. Ufanisi katika unapatikana kwa kutuliza akili kwenye jukumu moja baada ya jingine.

9. Ubongo wa mwanadamu umesukwa katika hali ambayo inawezesha kufanya kazi zaidi ya moja japo katika kazi hizo mhusika hawezi kutuliza akili kwenye kazi zote hizo. Unaweza kusikiliza mziki huku unasoma au unaweza kutembea ukiwa unaongea lakini kati ya vyote hivyo ni lazima ukubali moja lipate kipaumbele mbele ya jingine. Unaweza kuweka utulivu wa akili kwenye matukio zaidi ya moja lakini tafsiri yake ni kwamba akili umeigawa (divided mind) kushughulikia tukio zaidi ya moja na matokeo yake ni ufanisi mdogo katika unayofanya. Kumbe pale tunapofanya jambo zaidi ya moja ni lazima tuwe tayari kulipa gharama kwenye ufanisi/ubora wa matokeo pamoja na muda au athari zinazoweza kujitokeza kama vile ajali. Kazi ambayo ingefanyika kwa muda mfupi itatakiwa kufanyika kwa muda mrefu ili kupata ubora unaohitajika. Watafiti wameonesha kuwa, takribani asilimia 28 ya muda wa kazi katika siku unapotea kutokana na kukosa utulivu kwenye kazi moja. Tafiti zinaonesha pia kuwa zaidi ya asilimia 16 ya ajali za barabarani zinatokana na madereva au watumiaji wa barabara kushindwa kutuliza akili kwenye jambo moja.

10. Uongo #3: Maisha yenye nidhamu. Kuna uongo uliogeuzwa kuwa ukweli kwamba mtu mwenye mafanikio ni lazima awe na nidhamu. Huu ni uongo mwingine ambao tumeaminishwa. Ukweli ni kwamba hatuhitaji nidhamu zaidi ya hii tuliyonayo ili kufikia mafanikio tunayotamani bali tunatakiwa kuwa na mwongozo na usimamizi wa nidhamu tuliyonayo ili kufikia mafanikio tunayotaka. Mafanikio siyo sawa na mbio za marathoni ambazo ukipoteza nidhamu kidogo unaondolewa kwenye mbio na washindani wenzako. Mafanikio yanahusisha utekelezaji wa yale ambayo huyatekelezi wakati unafahamu yana mchango chanya katika kufikia matamanio yako. Hivyo, kwa lugha rahisi tunaweza kusema kuwa mafanikio yanahusisha kujifunza tabia mpya na tabia hizo zikishakuwa sehemu ya Maisha yako (daily routine) huna haja ya kuwa mtumwa kupitia uongo wa nidhamu. Pointi muhimu ambayo mwandishi anatushirikisha ni kwamba, “mafanikio yanapatikana kwa kufanya vitu vilivyo sahihi na siyo kufanya kila kitu kwa usahihi (success is about doing the right thing and not about doing everything right)”

11. Tabia na nidhamu ni ambayo watu wengi hawataki kuyasikia kutokana na ukweli kwamba yanaminya uhuru katika Maisha. Maneno haya yanategemeana na pengine yametumika kumaanisha maana moja. Ukweli ni kwamba katika Maisha unahitaji kuwa na nidhamu kwa ajili ya kujenga tabia mpya. Hivyo, tabia zikishakuwa sehemu ya Maisha hazihitaji nguvu za ziada kuendelea kuziishi. Baada ya kuwa na mkusanyiko wa tabia mpya ndipo mhusika anaonekana kuwa mtu mwenye nidhamu (disciplined person). Kwa tafsiri hii, hautaji kuwa na nidhamu ya kuishi vitendo vya kukuwezesha kufanikiwa bali unatakiwa uwe na nidhamu ya kujifunza tabia mpya ambazo zinawezesha vitendo hivyo kuwa sehemu ya Maisha. Tafiti zinaonesha kuwa inachukua angalau siku 66 mhusika kujenga tabia mpya. Na mhusika hawezi kujenga tabia mpya zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Na kadri mhusika anavyojenga tabia nyingi zenye kumwezesha kufanya vitu nje ya mazoea yake ndivyo anaonekana mwenye mafanikio na nidhamu.

12. Uongo #4: Nguvu ya utashi mara zote ni nguvu ya wito. Mwandishi anatushirikisha kuwa msemo wa “kwenye utashi/nia mara zote kuna njia” umewapotosha watu wengi ikilinganishwa na jinsi ulivyowasaidia. Msemo huu ukitafsiriwa katika upande mmoja unatoa nafasi kwa mhusika kuwa na hamasa ya kufanikisha hitaji lake. Hata hivyo, msemo huu unaacha kigezo cha umuhimu wa muda katika kufikia hitaji lako. Ukweli ni kwamba ni vigumu kwa binadamu wa kawaida kuwa na nia/utashi wa kufanikisha hitaji lake kila siku. Kuna siku ambazo anakuwa kwenye viwango vya juu vya utashi wa kutekeleza kwa vitendo hitaji lake na zipo nyakati ambazo hajisikii kabisa kujihusisha na lolote. Nguvu ya utashi kwa binadamu pamoja na kwamba inaweza kuhuishwa (renewable) inapatikana kwa uchache (scarcity supply) kila siku. Kutokana na ukweli huu, kama unahitaji kuwa na ufanisi mzuri huna budi kuhakikisha nguvu hiyo inatumiwa kutekeleza vitu vya muhimu katika vipaumbele vya siku husika.

13. Tumeona kuwa nguvu ya utashi inapatikana kwa uchache (limited supply). Mfano, unapoamka asubuhi unakuwa na kiwango cha juu cha utashi wa kufanya kazi na kadri muda unavyoenda ndivyo molali ya kazi inapungua. Kumbe, kama nguvu ya utashi inapatikana kwa uchache (scarcity) kuna kila sababu ya kuhakikisha nguvu hiyo inatumika ipasavyo. Kumbuka, tunapozungumzia nguvu ya utashi moja kwa moja tunazungumzia uwezo wa akili au ubongo kustahimili kazi iliyopo mbele ya mhusika. Ubongo wa mwanadamu ni takribani 1/50 ya uzito wa mwili wa mwanadamu japo kiungo hiki kinatumia takribani 1/5 ya nishati yote mwilini. Na sehemu ya ubongo yenye matumizi makubwa ya nishati ni ubongo wa mbele (prefrontal cortex) ambayo inahusika na utulivu (focus), kutunza kumbukumbu za muda mfupi, kutatua changamoto na kuhusika na uratibu wa vichocheo ambavyo mwili unatakiwa kuitikia. Kumbe, ili sehemu hii ya ubongo iendelee kufanya kazi ni lazima iwe na nishati ya kutosha kumwezesha mhusika kuwa katika kiwango cha juu cha utashi wa kazi. Hivyo, ili sehemu hii ya ubongo iendelee kufanya kazi kwa ufasaha ni lazima mhusika ajaze tenki lake la nishati kwa kutumia vyakula au vinjwaji ambavyo vinahamsa kiwango cha sukari katika mzunguko wa damu.

14. Kila siku pasipo uelewa wetu tunajikuta kwenye kiwango cha chini cha utashi wa kazi pasipo kujua kuwa sisi wenyewe ndo tumesababisha hali hiyo. Katika nyakati ambazo utashi wa kufanya kazi upo kwenye kiwango cha juu tunatakiwa kutekeleza majukumu ya vipaumbele vya muhimu ili kuepuka kupoteza nguvu ambayo ikipotea hairudi tena. Kumbe, katika majukumu yetu ya kila siku tunapoteza nguvu ya utashi wa kufanya kazi kutokana na sababu zifuatazo:-

รผ  Kujaribu kuishi tabia mpya katika majukumu yetu ya kila siku;

รผ  Kuchuja usumbufu unaojitokeza mara kwa mara;

รผ  Kupambana na vishawishi vinavyolenga kutuondoa kwenye vipaumbele;

รผ  Kupambana na hisia mbaya;

รผ  Kujaribu kuwaridhisha wengine;

รผ  Kutatua changamoto za mara kwa mara;

รผ  Kupambana na hofu;

รผ  Aina ya vyakula au vinywaji tunavyokula; au

รผ  Kujihusisha na kazi ambayo hauipendi kutoka rohoni.

15. Uongo #6: Maisha ya mlinganyo (A balanced life). Hakuna mlinganyo katika Maisha japo ni uongo ambao umeendelea kukubaliwa na wengi kuwa ili ufanikiwe ni lazima uwe na mlinganyo katika Maisha. Maisha yanaundwa na nguzo tatu ambazo ni: Kusudi, Maana na Faida. Ni lazima Maisha yawe na Kusudi maalum, Maisha ni lazima yawe na Maana na Maisha ni lazima yawe na Faida kwa mhusika pamoja na jamii inayomzunguka. Utatu huu hauwezi kuupata kwa kuishi Maisha yenye mlinganyo kama ambavyo inaelezwa na watu wengi. Badala ya kupambana kuishi Maisha ya mlinganyo unatakiwa kuishi Maisha yanayozingatia kutekeleza vitu vya kipaumbele muhimu na si vinginevyo. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kadri unavyotumia muda mwingi kwenye majukumu ya kipaumbele ndivyo inakuwa vigumu kuishi Maisha yenye mlinganyo kwa kuwa mambo yasiyo na kipaumbele yananyimwa nafasi.

16. Kuishi Maisha mlinganyo maana yake ni kwamba uwe na uwezo wa kuwa katikatika ya Kazi (majukumu) na Maisha ya kila siku. Maana yake ni kwamba hautakiwi kujikita kwenye kazi zaidi na kusahau Maisha mengine nje ya kazi na kinyume chake ni sahihi. Kama mlinganyo huu ungekuwa unawezekana ingekuwa ni jambo lenye heri lakini ukweli kwamba Maisha ya kila siku yanatulazimisha kutoa nafasi kwa baadhi ya vipaumbele na kuachana na mambo mengine kutokana na uchache wa muda na rasilimali. Matokeo makubwa yanayoonekana kuwa muujiza yanapatikana kwa kutekeleza majukumu ya kipaumbele na kuhakikisha kila mara nguvu kubwa imewekwa kwenye maeneo hayo. Hata hivyo, mwandishi anatushirikisha kuwa pamoja na kufanya kazi kwa kutekeleza majukumu ya kipaumbele tunatakiwa kukumbuka umuhimu wa Maisha nje ya kazi.

17. Muda haumsubirii mtu yeyote. Dunia imejaa watu wengi ambao wanahairisha mambo kwa matarajio kuwa ipo siku watakuwa na muda wa kuyarudia. Mfano, unaweza kupata muda wa kutekeleza majukumu yako ya kila siku na kujikuta unakosa muda wa kukamilisha mahitaji muhimu katika Maisha binafsi. Wafanyakazi au wafanyabiashara wengi wanakosa muda wa kuwa karibu na familia zao kutokana na kubanwa na majukumu yao ya kazi. Mwandishi anatushirikisha kuwa, muda haurudi nyuma wala haumsubiri mtu hivyo kadri unavyopata muda hakikisha unatekeleza mahitaji yako muhimu katika Maisha. Tenga muda kwa ajili ya kukamilisha vipaumbele vyako vya kazi, familia, masuala ya kijamii na

18. Uongo #6: Kubwa ni baya (Big is bad). Huu ni uongo mwingine ambao umezoeleka katika jamii. Ukweli ni kwamba “kikubwa kinaweza kuwa kibaya na kibaya kinaweza kuwa kikubwa bila kusahau kuwa kidogo pua kinaweza kuwa kibaya na kinyume chake ni sahihi”. Kutokana na uongo huo tumeaminishwa kujikita kwenye hatua fupi fupi kwa kuogopa kuwa tukianza na hatua ndefu tutaanguka. Fursa kubwa ni bora kuliko changamoto ndogo na changamoto kubwa ni mbaya kuliko fursa ndogo. Hivyo, ukubwa hauna uhusiano wowote na ubaya maana uzuri au ubaya unategemeana na hali ya tukio husika. Huu ni moja ya uongo kandamizi kwa kuwa kama unaogopa mafanikio makubwa kwa kigezo kuwa mafanikio makubwa ni dhambi (ubaya) kamwe hauwezi kupata mafanikio hayo.

19. Watu wengi ni wahenga (victim) wa kuogopa makubwa kwa kuwa kila panapotajwa matokeo makubwa watu wanayahusisha na ubaya. Mfano, unapotaja neno utajiri kwenye kundi kubwa la watu, watu wengi watakuambia mimi sitaki kuwa tajiri maana utajiri utanifanya nikose muda wa kutosha kupumzika, matajiri ni watu wenye roho mbaya, utajiri utanifanya nikose muda wa kutosha kuwa karibu na familia yangu; na mengine mengine. Unaweza kuona ni jinsi gani uongo huu unaendelea kukandamiza Maisha yetu maana naamini hata wewe mara nyingi umekuwa na hofu kila unafikiria kuanzisha hatua kubwa ambazo zingezaa mafanikio makubwa. Kwa ujumla, kutokana na uongo huu tumekuwa waoga wa matokeo/mafanikio makubwa. Kumbe, badala ya kuwa waoga wa matokeo makubwa kila mara tunatakiwa kufikiria kutatua changamoto kubwa kuhusiana na malengo ya Maisha yetu. Kila mara weka malengo yanayolenga kuongeza mara mbili thamani ya mafanikio yako. Husiridhike na hatua unayofikia maana ili ufikie mafanikio makubwa kila hatua inatakiwa kuwa chanzo cha kufungua hatua kadhaa mbele.

20. Epuka ukanda wako wa mazoea (comfort zone), epuka kufanya vitu kwa mazoea kama ambavyo kila mtu anafanya (acting in a business as usual), fikiria tofauti, kuwa na fikra pana na tekeleza majukumu yako kwa mapana. Hakuna mwenye kujua ukomo (limit) wa uwezo wake katika kufikia mafanikio makubwa hivyo hakuna sababu ya kuwa na fikra finyu ambazo zinaminya uwezo wetu halisi katika kila tunalofanya. Fikra pana ni chachu ya kufikia mafanikio makubwa kutokana na ukweli kwamba mafanikio ni vitendo na vitendo ni zao la fikra. Hivyo, mafanikio makubwa (big success) ni zao la vitendo vya kishindo/tofauti (act big) ambapo ili utende tofauti ni lazima uwe na fikra pana/tofauti (think big). Watu wote tumepewa muda sawa hila kinachotofautisha mafanikio yetu ni yale tunayofanya katika muda huo.

Hii ni sehemu ya kwanza ya uchambuzi wa kitabu hiki. Uchambuzi wa kitabu chote utapatikana kwa gharama ya Tshs. 10,000/=. Jiunge na mtandao wa Fikra za Kitajiri kwa  KUBONYEZA HAPA.

 

Karibuni kwenye fikra za kitajiri ili upate elimu isiyokuwa na mwisho.


Born to Win ~ Dream Big 


Mwalimu Augustine Mathias

Namba ya Simu:      +255 786 881 155
Mwanzilishi wa Mtandao wa 
fikrazakitajiri.blogspot.com

Barua pepe:  fikrazatajiri@gmail.com


Uchambuzi wa Kitabu cha How To Live On 24 Hours A Day: Jinsi ya kuishi masaa 24 katika siku.

Habari rafiki yangu mpendwa ambaye umeendelea kujifunza kupitia Makala za uchambuzi wa vitabu ambazo nimekuwa nashirikisha jamii kupitia mtandao wa FIKRA ZA KITAJIRI. Karibu katika uchambuzi wa kitabu cha leo ambacho ni cha 7 kati ya vitabu 30 ambavyo nimejiwekea lengo kuvisoma katika kipindi cha mwaka huu 2020.

Kama bado hujajiunga na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI kwa ajili ya kupata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, tafadhali JIUNGE SASA.

Kitabu ninachokushirikisha kupitia makala hii ni How To Live on 24 Hours A Day” kutoka kwa mwandishi Arnold Bennett. Mwandishi anatumia kitabu hiki kutushirikisha namna ambavyo kila mmoja anaweza kutekeleza majukumu yake ya siku kwa furaha na ufanisi. Mara nyingi katika jamii watu wengi huwa wanafanya kazi kwa nguvu na kwa bidii ya kiwango cha juu katika masaa mawili ya mwanzo kazini. Mfano, kama ni wafanyakazi masaa ambayo yanatumika ipasavyo kwa ajili ya uzalishaji ni masaa mawili ya awali na masaa sita yalibakiwa kwenye muda wa kazi yanatumiwa kwa kiwango cha kawaida cha utendaji kazi.

Hata hivyo, tunatakiwa kutambua kuwa siku ina masaa 24, hivyo baada ya kumaliza majukumu ya mwajiri wako au majukumu ya biashara zako kwa muda wa kawaida wa kazi unatakiwa kujiuliza masaa yanayobakiwa yanatumiwa vipi kwa ajili ya kuzalisha mafanikio zaidi kwenye kila sekta ya Maisha yako. Je unatumia muda mwingi kuangalia TV na kusinzia muda mrefu? Kuna mambo mengi ambayo unapuuzia kufanya katika muda wako wa ziada lakini kama yangefanyika yana nafasi ya kubadilisha Maisha yako. Je kila siku asubuhi unashindwa kuamka asubuhi na mapema kabla ya watu wengine hawajaamka ili upangilie majukumu yako ya siku? Anza kuamka mapema lisaa au masaa mawili kabla ya wengine na utaona utofauti katika Maisha yako.

Karibu ushirikiane nami kujifunza machache kati ya mengi ambayo tunashirikishwa katika kitabu hiki:

1. Muda ni zawadi ambayo watu wote wamepewa kwa usawa. Katika siku watu wote tumepewa masaa 24 ambayo kila mmoja ana ratiba yake. Mengi yameandikwa kuhusu jinsi gani watu wanatakiwa kuishi kwa bajeti ya pesa lakini ni machache yameandikwa kuhusu kuishi kwa bajeti ya muda. Wengi tumezoea kusikia kauli kama vile “muda ni fedha”. Ni sahihi kuwa muda ni pesa lakini kauli hii haijitoshelezi kwa kuzingatia kuwa thamani ya muda zaidi ya pesa endapo umetumiwa vyema.

2. Wanasayansi wamefanya kila aina ya chunguzi kuhusiana na ulimwengu na sayari nyinginezo lakini wameshindwa namna ya kupunguza au kuongeza muda. Muda ni rasilimali kwa ajili ya kufanikisha chochote; kupitia muda kila kitu kinaweza kufanyika na pasipo muda hakuna linaloweza kufanyika. Hivyo, muda ni bidhaa ya kipekee ambayo kila mtu anayeishi ana uhakika wa kuimiliki tena bila hofu wala wasiwasi kuwa inawezakuibiwa kama ilivyo kwa bidhaa nyinginezo. Bidhaa hii binadamu wote kila siku tunapewa kiwango sawa kwa maana hakuna anayepata zaidi au pungufu ikilinganishwa na mwenzake.

3. Watu wengi wanaishi katika muda iliopita au muda ujao. Pamoja na kwamba hakuna mwenye uhakika na muda wa baadae lakini bado watu wanashindwa kuishi katika muda uliopo mbele yao. Mfano, ni mara nyingi tunasikia kauli kama vile: “nikipata muda nitatekeleza hilo”, “nikiwa na muda zaidi nitakamilisha….” na kauli nyingine nyingi ambazo zinaonesha kana kwamba watu wana uhakika wa kupata wa ziada nje ya yale masaa 24 kwa siku. Somo kubwa ni kwamba kila saa katika siku tunatakiwa kuishi kwa ukamilisho wa majukumu yenye tija katika Maisha yetu.

4. Tunaishi katika ulimwengu ambao kila mara tunakuwa na matamanio ya kufanikisha baadhi ya vitu kwenye Maisha yetu. Ni kawaida mwanadamu yeyote kutamani katika Maisha kwa kuwa matamanio hayo ndiyo yanafanya Maisha yawe na thamani. Hali hii ya kutamani zaidi katika Maisha inatokana na ukweli kwamba kila siku tunawajibika kisheria kuhakikisha tunajilinda wenyewe pamoja na familia zetu katika hali ya afya bora na salama, kukidhi mahitaji yote ya kifedha, kulipa madeni tuliyonayo, kuwekeza na kuhakikisha kila mara tunaongeza thamani ya rasilimali tunazomiliki. Hili ni jukumu kubwa ambalo ni wachache wanaofanikiwa katika kipindi cha Maisha yao. Wachache hao ni wale ambao wanatambua umuhimu wa kuishi kulingana na muda walionao wa masaa 24 katika kila siku ya Maisha yao. Hata hivyo, ni lazima tukubaliane kuwa hata hao wachache waliofanikiwa kimaisha, Maisha yao kila siku wanakabiliwa na shauku ya kuongezeka zaidi. Hivyo, wote kwa ujumla masaa 24 katika siku yanakabiliwa na hitaji la kutimiza majukumu yetu kwa ajili ya kupata ridhiki zaidi ya Maisha.

5. Siri muhimu ya kufurahia maisha ni kuwa na mpangilio wa majukumu kulingna na muda wa masaa 24 katika siku. Ndani ya masaa hayo 24 unatakiwa kuridhika na yale yanayotekelezeka kwa kutumia uwezo wako wa juu na kuacha yale ambayo yapo nje ya uwezo wako kulingana na nyakati husika. Tumeona kuwa kila siku tunaishi kwa ajili ya kutimiza shauku ya nafsi ya kutaka kuongezeka zaidi katika Maisha, hata hivyo, ni lazima tufahamu kuwa wanaoridhisha nafsi zao ni wale ambao kila mara wapo tayari kuchukua hatua za kuboresha Maisha yao kwenye muda wao wa kila siku. Kama hauchukui hatua zinazolenga kutimiza shauku ya nafsi yako mar azote utajikuta unaishi Maisha yenye msongo wa mawazo na hisia ovu.

6. Uzuri uliopo katika rasilimali ya muda ni kwamba hauwezi kuadhibiwa kwa kunyanganywa au kupunguziwa rasilimali hiyo kutokana na matendo yaliyopelekea upoteze muda katika historia ya Maisha yako. Rasilimali hii inakusubiria katika utimilifu wake kwa siku zote za baadae katika Maisha yako. Mwaka kesho, mwezi ujao, wiki ijayo, kesho na lisaa lijalo vyote vipo katika ukamilifu wake kwa ajili yako kana kwamba haujawahi kupoteza muda. Tafsiri yake ni kwamba kama huko nyuma uliwahi kufanya makosa ambayo yamepelekea kujutia muda uliopotea sasa una nafasi ya dhahabu ya kujifunza kutokana na makosa hayo.

7. Tumeona kuwa nafsi imeumbwa katika hali ya kutoridhika kamwe, hali ya kuhitaji kuongezeka zaidi na hali ya kutaka kujimilikisha kila linalowezekana katika ulimwengu huu. Hivyo ndivyo kwa asili Maisha yetu yalivyo. Hata hivyo, mwandishi anatushirikisha kuwa kuna umuhimu wa kuwa na vipaumbele katika Maisha. Wapo watu wengi ambao wameharibu Maisha yao kutokana na tabia ya kujaribu kila kitu badala ya kukamilisha jambo moja kwa wakati. Hivyo, katika kuhakikisha tunaishi katika ukomo wa muda wa masaa 24 katika siku hatuna budi kukwepa visababishi au viashiria vya kutokufanikiwa kwenye jambo lolote ambalo tumeamua kufanya.

8. Watu wengi wanashindwa kufanikiwa kimaisha kwa kuwa wanaishi katika yaliyopita. Kundi la kwanza linahusisha wale wanaoishi kwa kujivunia mafanikio yaliyopita bila kutambua kuwa hayo yamebaki kuwa historia. Mfano, katika jamii kuna watu wengi ambao wanajivunia mafanikio yao ya darasani enzi za uanafunzi wao. Pia, wapo ambao wanajivunia mafanikio ya kifedha au kikazi waliyowahi kupata katika kipindi cha Maisha yao. Kundi la pili linahusisha wale ambao wanaishi katika huzuni kubwa kutokana na matendo waliyofanya katika Maisha yao au kutokana na familia au malezi waliyopewa enzi za ukuaji wao. Hapa ndipo kuna idadi ya watu wengi ambao wanaishia kusema nilichezea ujana wangu kwa kuwa hakuna la maana nililofanya pasipo kuchukua hatua zinazolenga kurekebisha makosa hayo katika Maisha ya sasa.  Ili ufanikiwe kuishi kwa muda wa masaa 24 katika siku, Mwandishi anatushirikisha kuwa hauna budi kuishi kulingana na wakati uliopo kwa kutekeleza majukumu ya kila siku pasipo kudharau ukubwa au udogo wa kazi.

9. Binadamu wa kawaida ambaye anahitaji kuishi maisha kwa ukamilifu anatakiwa ndani ya fikra zake awe na mpangilio wa kila siku ambayo amebahatika kuishi. Katika majukumu ya kawaida anatakiwa aianze siku kuanzia saa 12 kamili asubuhi na kumaliza siku yake saa 4 usiku. Katika siku anakuwa na jumla ya masaa 16 yaliyokamilika ukiondoa lisaa limoja kwa ajili ya maandalizi baada ya kuamka. Katika masaa hayo anatakiwa kutekeleza majukumu ambayo yanamwezesha kujiendeleza kiroho, kimwili, kiakili na kusaidia jamii inayomzunguka. Muda huo wa masaa 16 siyo kwa ajili ya kukimbizana na presha za Maisha bali ni kufanya kile ambacho roho yako inapenda na inajivunia kujihusisha nacho. Hautakiwi kuwa mtumwa wa pesa bali kupitia upendo kwenye majukumu yako ndipo utalipwa kulingana na thamani unayoitoa kwa wengine.

10. Watu wengi wanapoteza muda mwingi kufuatilia taarifa zisizo na tija katika Maisha yao. Tunaishi katika ulimwengu uliojaa taarifa za uongo au zinazoandikwa kwa makusudi maalumu na taarifa hizi zinadumu kwa muda mfupi sana. Mfano, taarifa nyingi ambazo tunafuatilia kwenye magazeti au vyombo vingine vya habari muda wa uhalisia wa taarifa hizo ni mdogo mno na nyingi zinatolewa kwa lengo la kukuza mauzo au kuongeza idadi ya wafuatiliaji wa chombo husika cha habari. Mwandishi anatushirikisha kuwa baada ya kufahamu ukweli huu kuhusu taarifa zinazoandikwa kila siku hakuna haja ya kuendelea kupoteza muda kwa kusoma magazeti au kuangalia TV.

11. Jenga mazingira yatakayopelekea uwe na majukumu ya thamani baada ya masaa ya kawaida ya mwajiri wako au biashara zako. Mwandishi anatushirikisha kuwa watu wengi katika jamii wameifundisha akili kuhisi uchovu kila baada ya kumaliza masaa ya kazi katika ratiba iliyozoeleka. Mfano, katika masaa 16 ambayo tumeona kuwa mtu wa kawaida anatakiwa awe nayo katika kila siku; asilimia kubwa ya watu huwa wanahesabu masaa yenye tija ni yale ambayo wanatakiwa kwa lazima kuwepo kwenye sehemu zao za kazi. Matokeo yake ni kwamba, baada ya kutoka kazini mtu anazunguka tu mtaani au anakuwepo nyumbani bila kujishughulisha na kazi yoyote yenye tija katika Maisha yake. Ili upate tofauti katika Maisha ni lazima uwe tayari kufanya kazi za ziada baada ya muda wako wa kazi za lazima.

12. Tenga siku moja katika juma kwa ajili ya kuhuisha/kupumzisha mwili. Mwandishi anatushirikisha kuwa unaweza kufanya kazi kwa muda wa siku zote saba katika juma hila kwa asili mwili wa binadamu unahitaji kupata mapumziko. Watu wengi ambao hawana utaratibu wa kupumzika siku moja katika juma mara nyingi huwa wanakabiliwa na kushuka kwa morali ya kazi hali inayosababishwa na mwili kukosa muda wa kupumzika au kubadilisha mazingira. Hali hii huwa inashusha ufanisi wa utendaji wa kazi bila ya ufahamu wa mhusika. Kumbe, unatakiwa kuandaa programu ya kazi kwa muda wa siku sita na kuiacha siku moja bila majukumu yoyote. Siku hii ni kwa ajili ya kuurejesha mwili katika morali ya kazi kwa juma linalofuata.

13. Katika jamii tunazoishi mara nyingi Ofisi nyingi za Serikali zinafunguliwa saa 1:30 asubuhi na kufungwa saa 9:30 alasiri. Hapa kama wewe ni mfanyakazi wa Serikali kati ya masaa 16 ambayo tumeona hapo juu, ukitoa muda wa kuwa kazini (masaa 8) unakuwa umebakiwa na muda wa masaa 8 mengine ambapo kati ya hayo ukitoa muda wa kwenda na kutoka kazi angalau una uhakika wa masaa yasiyopungua 5 kila siku. Ndani ya juma moja (siku 6) utakuwa na masaa yasiyopungua 30 ambayo hakika ukiyatumia vyema utapata mabadiliko makubwa katika Maisha uliyozoa. Vivyo hivyo, kwa upande wa mfanyabiashara, unatakiwa kujifanyia tathimini inayolenga kujua muda unaopoteza nje ya muda wako wa lazima katika biashara yako.

14. Kuishi kwa masaa 24 katika siku ni lazima mhusika awe tayari kubadilisha tabia zilizoeleka katika mfumo wake wa Maisha. Mwandishi anatushirikisha kuwa utakuwa unajidanganya endapo utasema nitaanza kutumia muda wangu vizuri kila siku pasipo kubadirisha tabia. Zipo tabia ambazo kwa sasa zinapelekea upoteze muda na hatua ya kwanza katika kuishi kulingana na masaa 24 katika siku ni kurekebisha tabia ulizozoea katika mfumo wako wa Maisha. Hapa ndipo kuna changamoto maana siyo kazi mtu kusema sitaki kupoteza muda bali kazi kubwa ni kubadilisha tabia. Hali hii inatokana na ukweli kwamba, mabadiliko yoyote ya tabia ni lazima yaambatane na vikwazo pamoja na maumivu kwa mhusika. Mabadiliko hayo yanaambatana na mabadiliko ya mfumo mzima wa Maisha. Hapa ni lazima uwe tayari kutoa sadaka zinazoambatana na kupoteza marafiki au kushindwa kufuatilia vipindi ambavyo awali ilikuwa kila muda wa jioni upo tayari kwenye TV yako.

15. Yote yanawezekana pale tu mhusika akifanikiwa kudhibiti fikra zake. Hakuna mtu anaweza kudhibiti fikra za mwenzake bali ni mhusika pekee ndo mwenye mamlaka ya kudhibiti mfumo wake wa fikra (kiwanda cha kuzalisha na kuchakata mawazo). Hakuna jambo jema au baya linalotokea katika Maisha ya mhusika pasipo kupitia kwenye mfumo wa ubongo ambako ndiko fikra zinatengenezwa na kufanyiwa kazi. Hivyo, kama unahitaji kuwa mtawala mkuu wa Maisha yako ni lazima udhibiti yanayoingia katika mfumo wako wa fikra. Uwezo huu wa kudhibiti fikra ndiyo utakuwezesha kuwa na utulivu kwenye yale unayofanya kulingana na programu ya siku husika. Hivyo, kama unahitaji kuishi Maisha yenye thamani ni lazima uwe mtawala wa fikra zako. Ni lazima uwezo wa kutuliza akili kwenye jambo moja baada ya jingine kwenye ratiba yako ya siku. Kupitia udhibiti wa fikra utaweza kuepuka maovu mengi ya dunia kwa kuwa chanzo cha maovu hayo pamoja na hisia mbaya kama vile hofu, huzuni na chuki ni kupitia mfumo wa fikra.

16. Furaha katika Maisha inaanzia kwa mhusika kujitambua yeye mwenyewe pamoja na uhusiano wake na mazingira yanayomzunguka. Ili mhusika ajitambue mwenyewe ni lazima awe na muda wa kufikiri. Unatakiwa kufikiria kuhusu kila sekta ya Maisha yako kwa kuwa kupitia zoezi hilo utapata kujitambua wewe ni nani na upo duniani humu kwa ajili ya kufanikisha nini. Unapojitambua kuwa wewe ni nani na umeumbwa kwa ajili ya kufanikisha nini moja kwa moja unakuwa umevunja mtego wa mazoea ya watu kuwa furaha inapatikana kutokana na umiliki wa vitu vya Duniani humu. Kumbe, furaha ya kweli chimbuko lake halisi ni kuishi kwa ajili ya ukamilisho wa kusudi maalumu na kuhakikisha Maisha yako yanaendeshwa na kanuni ambazo zinakusogea kwenye kulifikia kusudi hilo. Hivyo, kwa ujumla tunatakiwa kufahamu kuwa furaha ya kweli haipatikani nje ya majukumu yetu ya kila siku bali kadri tunavyotekeleza majukumu hayo ndivyo tunapata furaha katika Maisha. Kwa maneno rahisi ni kwamba furaha ya kweli inapatikana kutokana na ushindi mdogo mdogo wa kila siku kwenye malengo tuliyojiwekea katika kila sekta ya Maisha yetu.

17. Tenga muda wa kusoma kitabu au kusikiliza au kujihusisha na mchezo unaoupenda. Lengo la kuishi saa 24 katika siku ni kuepusha masaa yasiyo na kazi kwa kuwa tufahamu kuwa kukaa bila kazi ni dhambi. Yapo maarifa mengi ambayo unatakiwa kujifunza ili kupitia maarifa hayo upate kufahamu mbinu muhimu za kuendelea kuwa wa thamani katika uhai wako. Pia, unaweza kupata furaha kwa kusikiliza nyimbo au mafundisho mbalimbali sawa na ilivyo kujihusisha kwenye sanaa yoyote unayoipenda kutoka rohoni. Kubwa ni kwamba, chochote unachofanya katika muda husika unatakiwa kuwa na furaha nacho kutoka ndani ya roho yako.

18. Kuishi kwa masaa 24 katika siku ni lazima utambue kuwa tunaishi katika ulimwengu wa kisababishi (cause) na athari (effect). Hivyo, chochote ambacho unahitaji kitokee katika Maisha yako huna budi kutenga muda maalumu kwa ya kujiendeleza kila siku kuelekea kwenye ukamilisho wa hitaji hilo. Lengo la kujiendeleza kila siku ni kwa ajili ya kujiendeleza kimwili, kiakili na kiroho kama sehemu ya utayari kuelekea kwenye hitaji lako.

19. Soma kitabu au Makala ambayo inakufanya utumie akili kujifunza kitu kuhusu Maisha yako. Mwandishi anatushauri kuwa katika kazi za uandishi ambazo zina mafundisho mengi ni kazi za mashairi. Mashairi yana kila aina mafundisho ambayo yatamwezesha mtu yeyote kuwa na hekima na busara kama kipindi cha Maisha yake. Kumbuka katika usomaji wako wa vitabu unatakiwa kuchagua sekta moja ambayo unahitaji kuongeza uelewa wako na kila mara tafuta maarifa yanayolenga kukufanya uwe bora zaidi katika sekta hiyo.

20. Pamoja na kuwa na programu ya siku nzima, mwandishi anatushauri kuwa hatupaswi kuwa watumwa wa programu hiyo. Kama ambavyo tumeona kuwa unatakiwa kufurahia majukumu uliyonayo pia, unatakiwa uwe tayari kuruhusu mabadiliko ya lazima yanayotokea nje ya uwezo wako. Zaidi ya yote ili utimize majukumu yako kulingana na programu ya siku ni lazima husiruhusu mtu achezee ratiba yako. Pia, unatakiwa kuhakikisha unaepuka kushiriki semina au mkutano ambao una maudhui ambayo ni kinyume kanuni unazoziishi.   

Kupitia kitabu hiki mwandishi ameweza kutushirikisha namna ya kuishi kulingana na masaa 24 katika siku. Maisha yanakuwa na thamani pale ambapo kila siku unaitumia kwa faida. Jiunge na mtandao wa Fikra za Kitajiri kwa  KUBONYEZA HAPA.


Karibuni kwenye fikra za kitajiri ili upate elimu isiyokuwa na mwisho.


Born to Win ~ Dream Big 


Mwalimu Augustine Mathias

Namba ya Simu:      +255 786 881 155
Mwanzilishi wa Mtandao wa 
fikrazakitajiri.blogspot.com

Barua pepe:  fikrazatajiri@gmail.com