NENO LA LEO (NOVEMBA 12, 2020): JINSI MFUMO WA SASA WA ELIMU UNAVYOTUJAZA HOFU KULIKO MAFANIKIO
๐๐พHabari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine ambayo naamini tumeamka salama na zaidi ya yote tukiwa na hamasa ya kutosha kwa ajili ya kuendelea pale tulipoishia jana. Kutokana na hali kama hiyo hatuna budi kila mmoja kwa nafasi yake kusema kusema "hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana ninawajibika kumshukuru na kuitumia vyema siku hii ili nipate kuliishi kusudi kubwa la maisha yangu".
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍๐พ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutaona jinsi mfumo wa uliopo umekuwa chanzo cha kutujaza hofu ikilinganishwa na mafanikio tarajiwa. Wote tunakubaliana kuwa tumelelewa katika jamii ambayo inaamini wale wanaoganya vyema darasani ndiyo watafanikiwa kimaisha. Hali imetufanya katika ukuaji wetu kuamini kuwa wale wanaofanya vibaya darasani hawawezi kufanikisha maisha! Mbaya zaidi ni pale ambao wale wanaofanya vibaya wanapachikwa majina ya kila aina ambayo yanafifisha uwezo wa kufanikiwa kimaisha.
✍๐พ Je kufeli mitihani ni uthibitisho tosha kuwa mhusika atafeli maisha?. Siyo kweli kwamba ukifeli mitihani umefeli maisha. Mifano ipo mingi kwa watu ambao shuleni walionekana hawajui lolote lakini katika maisha ni mifano bora ya kuigwa. Mfano Bill Gates aliacha chuo na kujitosa kwenye sekta ya ujasiliamali. Pia, katika jamii tunayoishi wapo watu wengi ambao walishindwa kumudu maisha ya shule lakini kwa sasa wafanyabiashara wakubwa. Pia, wapo wanamochezo wengi ambao darasani hawakufanya vyema lakini kwa sasa wanaishi kupitia vipaji vyao.
✍๐พ Hali hii inatoa picha kuwa mfumo wa elimu wa sasa unaandaa wanafunzi kuwa waajiriwa badala ya kuandaliwa kwenye pande zote za ajira na ujasiliamali. Tafsiri yake ni kwamba unapofeli shule siyo kwamba umefeli maisha bali shule inakuwa imeshindwa kutambua kipaji chako. Baada ya kufeli mitihani unatakiwa kujiamini kuwa upande siyo sehemu yako na badala yake kuna upande ambao unakusubiria.
✍๐พ Asilimia kubwa ya watu ambao wamefanikiwa kufaulu mitihani na kuingia kwenye mfumo rasmi wa ajira wengi wao wanaishi kwa msongo wa mawazo. Hali hii inatokana na ukweli kwamba kiwango cha mshahara wanacholipwa pengine hakiendani na kiwango cha elimu waliyonayo au mshahara hautoshelezi mahitaji yao ya msingi. Mara nyingi katika kusoma wengi wanakuwa na mategemeo makubwa ya kufanikiwa kupitia elimu ikilinganishwa na uhalisia wa maisha. Na hapa ndipo hofu ya maisha inakoanzia.
✍๐พMwisho, neno la tafakari ya leo limetufunulia jinsi ambayo mfumo wa elimu ulivyotuja hofu ikilinganishwa mafanikio tarajiwa. Kama mzazi una nafasi ya kutambua vipaji vya watoto wako zaidi ya kile wanachoonyesha darasani. Kauli hii ya mwanangu nenda shule ukasome kwa bidii ili uwe daktari bingwa imepitwa na wakati. Mpe mwanao kauli ambazo zitamfanya kuwa mdadisi na mtumiaji wa kalama alizojaliwa katika maisha ya kila siku.
๐๐พNakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
๐ฃ๐ฃ Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com