Sehemu ya Kwanza: Uchambuzi wa Kitabu cha Raising Great Kids: Namna ya Kumlea Mtoto Vyema.


Habari ya leo rafiki na msomaji wa mtandao wa Fikra za Kitajiri. Naamini unaendelea vyema kiafya, kiroho na kiakili kwa ajili ya kuboresha Dunia hii kuwa mahala pazuri pa kuishi. Kumbuka kuwa lengo la Dunia kuwa mahala pazuri pa kuishi ni lazima lianzie katika maisha yako. Ukiwa na maisha mazuri Dunia hii utaiona sehemu salama pa kuishi na ndivyo ilivyo kwa jamii unayoigusa. Karibu tena katika makala ya uchambuzi wa kitabu cha wiki hii.

Kama bado hujajiunga na mfumo wetu wa kupokea makala za uchambuzi wa vitabu, tafadhali fanya hivyo KWA KUBONYEZA HAPA na kujaza fomu kisha bofya “jiunge/subscribe”. Ni fursa ambayo itakuwezesha kupata uchambuzi wa vitabu kwa lugha rahisi kupitia barua pepe yako.

Kitabu cha wiki hii ni Raising Great Kids” ambacho kimeandikwa na waandishi Dr. Henry Cloud na Dr. John Townsend. Wawili hawa wanatumia kitabu hiki kwa ajili ya kutushirikisha mbinu mbalimbali za malezi wa watoto.

Waandishi hawa wanatushirikisha kuwa linapotajwa suala zima la malezi ya watoto kwa ujumla mambo manne yanaguswa ambayo ni;
a)   Ustawi wa Watoto – Kila mzazi anatamani kuona mtoto wake anakuwa vyema huku akiepuka makucha ya Dunia na kuwa na maadili mema katika maisha yake yote.
b)   Jamii inayomzunguka mtoto – Makuzi ya mtoto ni matokeo ya jamii inayomzunguka kuanzia mazingira ya nyumbani, shuleni, majirani, kanisani/msikitini na hata marafiki zake.
c)   Ustawi wa wazazi – Mafanikio ya mtoto katika kuwa na malezi bora ni jawabu la mafanikio ya mzazi hasa kwenye suala zima la kuwa na ndoa bora. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mzazi anaathirika kwa upande chanya au hasi kutokana na maendeleo ya mtoto wake. Akiwa na maadili mema ni furaha kwa wazazi na kinyume chake ni sahihi.
d)   Kuhusu uimara au mafanikio ya dini – Mafanikio katika kuishi misingi ya dini ni jawabu kuwa watoto wanaishi misingi bora. Hii ni kutokana na ukweli kwamba maadili ya mtoto yanadhihirisha namna anavyozingatia misingi mikuu ya dini yake. 

Hivyo, kufikia malezi bora waandishi hawa wanatushirikisha kuwa ni lazima misingi mikuu ya malezi ifuatayo izingatiwe na kila mzazi:-
a)   Thamani ya Upendo – Upendo ni msingi mkuu wa mahusiano. Hakuna namna ambayo mzazi utafakiwa kumlea mwanao kama hauna upendo wa dhati naye. Kadri watoto wanavyokua wanahitaji kuhisi na kuona kuwa wanapendwa na wazazi wao. Kumbuka kuwa upendo ndio sheria kuu ya Mungu ambayo inatutaka kupendana sisi kwa sisi, hivyo, mtoto naye anahitaji hilo lakini pia anatakiwa kufundishwa umuhimu wa kuwa na upendo.
b)   Thamani ya Ukweli – Upendo pekee hautoshelezi kwani maisha ndani ya familia ili yawe yenye mafanikio ni lazima pasiwepo uongo ndani ya wanafamilia. Watoto wanahitaji kujua umuhimu wa kuwa wakweli na kuambiwa ukweli katika kipindi cha ukuaji wao.
c)   Nafasi ya Tabia – Kazi ya malezi ya mzazi kwa mtoto ni jukumu la muda tu kwani kuna umri ambao mtoto ataanza maisha ya kujitegemea. Katika kipindi hicho cha kujitegemea ataongozwa na maadili ambayo msingi wake ni malezi aliyopata kutoka kwa wazazi. Maadili hayo ndizo tabia atakazokuwa nazo katika kila sekta ya maisha yake.
d)   Uelewa kuhusu dhambi, matendo ya kitoto na kumjua Mungu. Duni imejaa uovu wa kila aina na uovu huo unawasubiri watoto wa jinsia zote kudumbukia katika dhambi hizo. Mzazi ndo wa kumkinga mtoto dhidhi ya makucha mabaya ya dunia katika kipindi chote cha ukuaji wake. Vivyo hivyo, Dunia imejaa mema ambayo Mungu anakusudia kila kiumbe kilichoumbwa kipate kuyafurahia. Mzazi wajibu wako ni kumuandaa mtoto wako aangukie kwenye mema ya Dunia katika kipindi cha maisha yake. Tunaamini kuwa kila mtoto ameumbwa kwa sura ya Mwenyezi Mungu, hivyo mzazi una wajibu wa kuhakikisha sura hiyo haipotei katika maisha ya mwanao katika kipindi cha ukuaji wake.
e)   Thamani ya Uhuru – Wapo wazazi wanaoamini katika kuwadhibiti watoto kwa kufungia ndani na wapo ambao wanaamini katika kuwapa uhuru watoto wao. Jambo la muhimu ni kutambua kuwa kama mzazi unatakiwa kuwapa misingi wanao ambayo itawawezesha kujidhibiti wenyewe na maisha yao kwa ujumla.
f)    Umuhimu wa uwepo wa Mwenyezi Mungu katika maisha yao – Mtoto anapaswa kumjua Mungu, kumuheshimu, kumpenda, kuogopa kwenda kinyume na matakwa yake na hata kuishi amri zake katika maisha yake ya kila siku. Mzazi huo ni wajibu wako wa kuhakikisha mtoto anakua kiroho kadri anavyokua kimwili.
g)    Malezi ni Mchakato – Mchakato wa malezi unaanzia tangu pale mimba inapotungwa na kuendelea katika kipindi cha miaka kadhaa katika ukuaji wa mtoto. Pia, mzazi unatakiwa kutambua kuwa malezi yanabadilika mara kwa mara kulingana na ukuaji wa mtoto.

Karibu ushirikiane nami kujifunza machache kati ya mengi ambayo tunashirikishwa katika kitabu hiki:
SEHEMU YA KWANZA: KUMKUZA MTOTO MWENYE MAADILI
1. Kila mzazi anataka kuwa na mtoto mwenye maadili mema hata hivyo ni wazazi wachache ambao wanasaidia watoto kupata maadili hayo. Waandishi wanatushirikisha kuwa wajibu mkubwa wa kuitwa mzazi ni kuhakikisha unawasaidia watoto wako wawe na maadili mema, tabia njema au wawe watoto wema kwa ujumla wake. Wajibu unaambatana na majukumu ambayo wewe mzazi unatakiwa kuyatimiza katika kila muda unaokuwa na watoto wako. Majukumu ya kuwa mlezi ni pamoja na kuhakikisha mtoto anafundishwa misingi ya kiroho, tamaduni, upendo kwa jamii inayomzunguka na viumbe vinavyomzunguka, umuhimu wa kufanya kazi sambamba na kufahamu wajibu wake kama mtoto.

2. Kila mzazi anatamani kumuona mtoto wake akikua kutoka hatua moja hadi nyingine katika kila sekta ya maisha yake. Shuleni anatamani kuona mtoto anatoka hatua moja hadi nyingine kimasomo. Kazini anatamani kuona mtoto wake anatoka nafasi moja hadi nyingine. Vivyo hivyo, katika mahusiano kila mzazi anatamani kuona mtoto wake akiwa na mahusiano yanaozalisha ndoa bora. Ndivyo ilivyo kwenye sekta ya kiroho, kiuchumi, kitabia na kwenye urafiki na wenzake. Kwa bahati mbaya sio watoto wote wanakua kulingana na mategemeo ya wazazi. Hapa ndipo kila mzazi anaona kuwa alitimiza wajibu wake na mengine yaliyobakia ilikuwa nafasi ya mtoto mwenyewe. Hata hivyo, mzazi analaumiwa na jamii kuwa hakutimiza wajibu wake. Waandishi wanatushirikisha kuwa wajibu ni kwa wote kwa maana mzazi na mtoto lakini mzazi ndo anatangulia kwanza na baadae mtoto anafuata.

3. Lengo kubwa la mzazi katika malezi kwa watoto ni kuwa na watoto wenye maadili au tabia njema. Tabia njema zinaambatana na uhuru wa mtoto katika yale anayofanya, uwezo wa kujiamini, uwezo wa kutatua changamoto zinazomkabili, uwezo wa kujitegemea kwa kutimiza wajibu wake katika kazi, uadilifu, maadili mema na kuishi misingi ya kiroho. Kwa ujumla tabia ni ule uwezo wa namna ya kutumia vipaji vyetu kulingana na matakwa ya Muumba wetu. Na ni katika kipindi cha utoto ndipo mzazi unatakiwa kujenga misingi ya tabia njema kwa mtoto wako. Hapa ndipo jukumu kubwa la mzazi lilipo, kuhakikisha anamjengea misingi bora mtoto wake ili misingi hiyo izae tabia tabia njema katika maisha yake ya baadae.

4. Katika hatua za malezi ya mtoto, mzazi anatakiwa kuhusisha mbinu mbili za za kulea ambazo ni (a) kunfundisha ujuzi na maarifa muhimu kwa mtoto na (b) kutumia uzoefu wa vitendo. Mwandishi anatushirikisha kuwa ili mtoto awe na misingi bora ya tabia njema ni lazima ashirikishwe kwenye majukumu mbalimbali ambayo yanamjenga kujifunza kwa vitendo. Ukweli ni kwamba ni rahisi kujifunza kwa vitendo kuliko kutumia nadharia. Mfano, hauwezi kuendesha baiskeli kwa kutegemea kusoma mbinu za kuendesha baiskeli kwenye kitabu badala yake ni lazima ujifunze kwa vitendo ambavyo vitahusisha kuanguka hadi pale ambapo utaweza kuendesha kwa ufasaha. Vivyo hivyo, tabia njema katika mtoto kwenye kila sekta ya maisha yake zinajengwa kwa kumhusisha mtoto kupitia vitendo katika maisha ya kila siku ndani ya familia. Mfano, kwa kutaja tu baadhi mtoto anatakiwa kushiriki kwa vitendo katika kufanya kazi za nyumbani, kazi za kujenga uchumi, matendo ya huruma na matendo ya kiroho.

5. Kadri mtoto anavyokua ni lazima ufundishwe kuwa na NEEMA ndani mwake. Waandishi wanatushirikisha kuwa neno neema linatafsiriwa “kuwa tayari kwa wengine”. Neno hili linajumuisha matendo kama vile: Upole, huruma, msamaha, fadhira, shukrani, uelewa, utoaji, upendo na msahada. Haya yote ni lazima mtoto afundishwe katika kila hatua za ukuaji wake. Mzazi hapa lengo lako ni kutaka mwanao atambue kuwa maisha yake si kwa ajili yake tu bali ni kwa ajili ya jamii inayomzunguka. Tafsri pana ni kwamba mtoto anatakiwa kufahamu kuwa maisha yanategemeana.

6. Pia mtoto ni lazima afundishwe kuwa tabia njema zinahusisha kuwa mkweli katika maisha yake. Waandishi wanatushirikisha kuwa neno ukweli linatafsiriwa kama kuwa mwaminifu dhidi ya nafsi yako na mwenye kuaminiwa na jamii inayokuzunguka. Kwa tafsiri pana ni kwamba mtoto anatakiwa kufahamu mipaka yake katika kile anachofanya au matamanio yake. Kutokana na tafsiri hiyo, ukweli katika maisha unajumuhisha: maadili mema, matarajio, maamuzi, hukumu dhidi ya wengine, tabia, nidhamu, uadilifu na uaminifu. Mtoto anatakiwa kutambua umuhimu tabia zote hizo katika maisha yake akiwa mtoto na hata katika kipindi cha utu uzima.

7. Changamoto kubwa kwa mzazi ni namna gania atawezesha kumpa mtoto matendo ya neema na ukweli kwa wakati mmoja. Matendo haya ni muhimu kwa kuwa kila linapotajwa neno malezi ni lazima lihusishwe na upendo kwa watoto (matendo ya faraja/neema) sambamba na mipaka kwa watoto (ukweli). Mfano, ni kawaida mtoto mara zote anathamini kucheza kuliko kitu chochote katika maisha yake. Kama mzazi haupaswi kumkatisha tamaa mwanao kwenye michezo anayopendelea zaidi lakini pia haupaswi kusahau kuwa mtoto anatakiwa kutimiza majukumu yake mengine ya kila siku. Hivyo, huna budi kutumia sentensi ambazo zinamtia moyo na kumhamasisha kwanza kutimiza jukumu husika kabla ya kwenda kucheza. Mfano, tumia sentensi kama “natambua kuwa unahitaji kwenda kucheza na ni vigumu kusubiria lakini nahitaji kwanza ukamilishe “home work” uliyopewa shuleni au ukamilishe kwanza kazi hii….”.

8. Tabia au matendo yoyote ambayo unataka mwanao awe nayo ni lazima utumie muda mwingi kumfundisha, kumsahihisha, kumhamasisha, kumpa changamoto na hata kumkanya. Kama mzazi/mlezi huna budi kutenga muda kila siku kwa ajili ya kuhakikisha mwanao anafundishwa kile ambacho unatamani awe nacho katika maisha yake ya baadae. Pia, unatakiwa kutafuta watu maalum wa kumfundisha mwanao ujuzi/maarifa ambayo yapo nje ya uwezo wako. Mfano, kama ana kipaji cha kuimba tafuta watu ambao watamsaidia kukuza kipaji hicho kadri anavyokua kiumri. Vivyo hivyo, kama ni mpenzi wa michezo, hakikisha anapata mwongozo sahihi wa kukuza kipaji chake katika mchezo husika.

9. Ukuaji wa mtoto ni sawa na mti. Mti baada ya kupandwa ni lazima umwagiliwe au kupaliliwa pamoja na kuhakikisha matawi yasiyofaa yanaondolewa ili kubaki matawi bora. Hata hivyo, unaweza kupanda mti na husifanye chochote na mti huo utaendelea kukua tu na mwisho wake hautapata kile ulichotamani. Ndivyo ilivyo kwa mtoto, ukuaji ni lazima uendelee bila kuzingatia kuwa anajengewa tabia zipi. Waandishi wa kitabu wanashauri kuwa mzazi/mlezi una wajibu wa kuhakikisha una muda wa kutosha kwa ajili ya kuwa karibu na watoto na hata pale ambapo haupo ni lazima ufuatilie tabia zao. Lengo ni kuhakikisha kuwa tabia mbaya zinadhibitiwa katika kipindi cha ukuaji wa mtoto. Hii ni kutokana na ukweli kwamba katika hatua za ukuaji watoto wanajifunza mengi kutoka kwenye Dunia inayowazunguka. Kumbuka kuwa Dunia hiyo ndo imejaa mabaya na mazuri.

10. Katika hatua za ukuaji hakikisha mtoto anajenga uwezo katika: namna kukamilisha au kueleza mahitaji; kukabiliana na madhaifu yake; kukabiliana na hatari za maisha; kudhibiti maumivu ya kimaisha; kukabiliana na huzuni katika maisha; kudhibiti hasira; uwezo wa kutoa maoni au kujieleza; kukuza kipaji chake; kujiamini na uwezo wa mahusiano kijinsia. Ukiangalia vipengele vyote hivyo vinalenga kumjenga mtoto katika kukuza uwezo wake kwenye mahusiano na jamii ya watu wanaomzunguka. Kwa kifupi mzazi una nafasi kubwa ya kumjenga mtoto ili katika maisha yake ya baadae awe mtu wa kujiamini na kujitegemea. Na hauwezi kufanikisha lengo hilo kama hauna muda wa kutosha wa kuwa karibu na mtoto wako.

11. Chochote unachomfundisha mtoto wako unatakiwa kutambua kuwa inachukua muda hadi mtoto aelewe na kuweka yale anayofundishwa kwenye mfumo wa kumbukumbu zake. Husitegemee kuwa kile unachomfundisha mtoto atakielewa hapo hapo na kuanza kukitekeleza katika maisha yake. Hapa ndipo wazazi/walezi wengi wanapokosea na matokeo yake wanatumia adhabu za mara kwa mara kwa watoto. Hali hii inapelekea watoto wanakuwa na uoga au wasiwasi wakati wa kujifunza. Kumbe, mzazi/mlezi unatakiwa kutambua kuwa mtoto kujifunza ni mchakato ambao unahusisha hatua 5 ambazo ni:
รผ  Mfundishe mtoto kuhusu ukweli au kile ambacho unataka awe nacho – watoto hawaelewi chochote hivyo wanatakiwa kufundishwa kuhusu kanuni, mila, wazo au tabia;
รผ  Wape muda wa kuvuka mipaka au ukomo wa uwezo wao kuhusu tabia husika – Mtoto anapofundishwa kitu kipya katika maisha yake hawezi kukitekeleza kwa ufasaha hivyo ni lazima apewe muda wa kujifunza kutokana na makosa;
รผ  Msaidie mtoto kubadilisha makosa yake ili yaendane na kile alichofundishwa – mtoto anapokosea kutimiza alichofundishwa kuna hisia zinajengeka katika akili yake. Mzazi wajibu wako ni kutumia sentensi zenye upendo ndani yake ili aondokane na hisia hizo na hatimaye hamasa ya kujifunza iendelee;
รผ  Msaidie mtoto kutambua ukweli katika kile anachojifunza – baada ya mtoto kuhamasishwa sasa mzazi/mlezi unatakiwa kumsaidia katika hatua za kujifunza maarifa mapya au tabia kwa kuwa karibu nae ili utambue sehemu anazokwama na mwisho umrekebishe; na
รผ  Mhamasishe mtoto kurudia tena vitendo vinavyoendana na kile alicofundishwa – mtoto anavyorudia mara kwa mara inamsaidia tabia husika kuwa sehemu ya maisha yake.  

Haya ni machache niliyojifunza kutoka katika sehemu ya kwanza ya kitabu hiki. Kupata nakala ya uchambuzi wa kitabu hiki lipia Tshs. 10,000 na utatumiwa nakala tete kwa njia ya barua pepe. Kama bado haujajiunga na Mtandao wa huu, jiunge kwa  KUBONYEZA HAPA.

Tuma pesa yako kwa njia ya M-pesa au Airtel Money kupitia namba zifuatazo:-


M – Pesa tumia namba: 0763 745 451 (Augustine Mathias Mugenyi)
Airtel Money tumia namba: 0786 881 155 (Augustine Mathias Mugenyi)

Karibuni kwenye fikra za kitajiri ili upate elimu isiyokuwa na mwisho.


Born to Win ~ Dream Big 

Augustine Mathias Bilondwa

Namba ya Simu:      +255 786 881 155
Mwanzilishi wa Mtandao wa 
fikrazakitajiri.blogspot.com
Barua pepe:  fikrazatajiri@gmail.com

PATA UCHAMBUZI WA VITABU vifuatavyo kwa kulipia Tshs. 5000.00 kila kitabu (Ukinunua vitabu vyote vitatu utapata kwa ofa ya Tshs 10,000.00).

1.    Kitabu cha Kwanza ni “THE RULES OF MONEY (KANUNI ZA PESA)” kutoka kwa Mwandishi Richard Templar
Katika kitabu hiki utafahamu kanuni 107 za pesa. Ndani ya kanuni hizo utagundua kuwa utajiri ni haki ya kila mtu hivyo ni wajibu wako kuwa tajiri. Kanuni zote (107) zimechambuliwa kwa kina na kuandaliwa kwa lugha Kiswahili. Uchambuzi huu unapatikana kwa kijitabu kidogo chenye kurasa 39 ambazo unaweza kusoma kwenye simu yako ya mkononi (simu janja – smart phone) au kwenye kompyuta mpakato (pc).

2.    Kitabu cha pili “THE RULES OF LIFE (KANUNI ZA MAISHA)” kutoka kwa mwandishi Richard Templar
Mwandishi kupitia kitabu hiki anatushirikisha kanuni 106 za maisha. Kanuni hizi zimechambuliwa kwa kina kwa lugha ya Kiswahili na unaweza kukisoma kupitia simu janja au kompyuta mpakato. Kanuni zote zinagusa kila sekta ya maisha yako hivyo ni kitabu ambacho hautojutia pesa unayoitoa kwani utajifunza maarifa mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maisha yako.

3.       Kitabu cha tatu ni “I CAN I MUST I WILL (NAWEZA, NALAZIMIKA, NITAFANYA)” kutoka Mwanamafanikio na Mtanzania Mwenzetu Marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi
Kwa ujumla kupitia kitabu hiki Dr. Mengi anatushirikisha maisha yake kuanzia akiwa mtoto, akiwa mwanafunzi, wakati anaanzisha biashara yake ya kwanza, namna alivyopanua biashara zake, wajibu aliokuwa nao kwa jamii, misimamo yake kwenye mfumo wa Serikali kwa awamu zote tano, wajibu wake kwenye uhifadhi wa mazingira na matarajio yake kwenye kukuza biashara kwa siku za baadae.

Kupata uchambuzi wa vitabu hivi tuma pesa yako kwa njia ya M-pesa au Airtel Money kupitia namba zifuatazo:-
M – Pesa tumia namba: 0763 745 451 (Majina ni Augustine Mathias)
Airtel Money tumia namba: 0786 881 155 (Majina ni Augustine Mathias)

Baada kutuma pesa hiyo nitumie ujumbe kwenye namba ya airtel (0786 881 151 451) ukiwa na barua pepe yako ili nikutumie uchambuzi wa kitabu husika.

UTAJIRI NI HAKI YAKO YA KUZALIWA "BEING RICH IS YOUR BIRTH RIGHT"


Mambo Niliyojifunza kwenye kitabu cha How To Get Rich: Jinsi ya kuwa Tajiri.


Habari ya leo rafiki na msomaji wa mtandao wa Fikra za Kitajiri. Naamini unaendelea vyema kiafya, kiroho na kiakili kwa ajili ya kuboresha Dunia hii kuwa mahala pazuri pa kuishi. Kumbuka kuwa lengo la Dunia kuwa mahala pazuri pa kuishi ni lazima lianzie katika maisha yako. Ukiwa na maisha mazuri Dunia hii utaiona sehemu salama pa kuishi na ndivyo ilivyo kwa jamii unayoigusa. Karibu tena katika makala ya uchambuzi wa kitabu cha wiki hii.

Kama bado hujajiunga na mfumo wetu wa kupokea makala za uchambuzi wa vitabu, tafadhali fanya hivyo KWA KUBONYEZA HAPA na kujaza fomu kisha bofya “jiunge/subscribe”. Ni fursa ambayo itakuwezesha kupata uchambuzi wa vitabu kwa lugha rahisi kupitia barua pepe yako.

Kitabu cha wiki hii ni How to Get Rich -  Jinsi ya kuwa Tajiri” ambacho kimeandikwa na tajiri nguri na mwanasiasa Donald J. Trump. Linapotajwa jina la Trump naamini hakuna haja ya kumuelezea ni nani kutokana na mafanikio ambayo amepata katika ulimwengu wa utajiri sambamba na mafanikio ya kisiasa. Kwa yule ambaye hamjui basi naomba atambue kuwa kitabu cha leo kiliandikwa na Rais wa Marekani ambaye hadi sasa yupo madarakani. Pia, naomba atambue kuwa kitabu hiki kimeandikwa na tajiri mkubwa katika ardhi ya Marekani na Dunia nzima kwa ujumla.

Mwandishi anatushirikisha kuwa aliamua kitabu hiki kukipa jina hilo kwa kuwa hilo ndilo swali ambalo amekuwa akiulizwa mara nyingi. Kuwa anaulizwa swali hilo mara kwa mara kwa kuwa yeye ni bilionea. Kwa maana, mtengeneza mikate ataulizwa namna ya kutengeneza mkate na tajiri anaulizwa namna ya kutengeneza pesa hadi kufikia utajiri.

Karibu ushirikiane nami kujifunza machache kati ya mengi ambayo tunashirikishwa katika kitabu hiki:

1. Kufanikiwa kibiashara ni lazima ufahamu mambo mengi. Mwandishi anatushirikisha kuwa mafanikio ya kibiashara ni lazima ufanye kazi na watu wa kila aina, taaluma/uzoefu tofauti au umri tofauti. Ili ufanikiwe kupata kile unachohitaji kutoka kwao huku ukitimiza matakwa yao ni lazima uwe na uelewa wa mambo mengi. Ukiwa mtendaji mkuu unatakiwa katika kila kitengo cha biashara ufahamu vitu muhimu ambavyo vinatekelezwa na kitengo husika. Ili ufanikishe adhima hiyo ni lazima ufanye kazi kama Jenelali wa Jeshi, kwa maana kila maamuzi unayofanya yana umuhimu kwako na watu unaofanya nao kazi.

2. Kadri unavyokua kibiashara hakikisha unajenga timu ya ushindi kuputia watua unaowaajiri. Mwandishi anatushirikisha kuwa unapokuwa tajiri unakuwa na miradi mikubwa ambayo ili iendeshwe kwa faida ni lazima uwe na wafanyakazi bora kitaaluma na kiutendaji. Wanyakazi hawa ni lazima wakurahisishie usimamizi wa miradi kwa kuwa hauwezi kusimamia kila mradi kutokana na wingi wa miradi uliyonayo. Ukiwa na wafanyakazi bora utakuwa na usimamizi au uendeshaji mzuri na vivyo hivyo ukiwa na usimamizi mzuri utakuwa na wafanyakazi bora. Kanuni ya kujifunza hapa ni kwamba “fanya kazi na mwajiriwa ambaye anatambua wajibu wake na hakikisha unamtimizia matakwa yake”.

3. Hakikisha husibweteke kutokana na mafanikio unayopata kiasi cha kupoteza dira ya picha kubwa ya mafanikio. Mwandishi anatushirikisha namna ambavyo alipoteza dira baada ya kufanikiwa kiuwekezaji. Matumizi katika vitu vidogo vidogo au starehe za hapa na pale ni chanzo kikubwa kwa watu kupoteza dira ya mafanikio. Hivyo, kadri unavyokuwa kibiashara unatakiwa kuendelea kuishi misingi ya maisha ambayo ulijiwekea awali. Kwa maana nyingine unatakiwa kabla ya kuwa tajiri uwe na mpango wa namna utakavyokuza utajiri wako na kuainisha utajiri huo utautumia kufanikisha au kutekeleza yapi katika maisha yako.

4. Hakikisha haupotezi kasi kadri unavyofanikiwa kibiashara. Mwandishi anatushirikisha kuwa watu wengi wanashindwa kufikia kwenye kilele cha mafanikio kwa kuwa wanapoteza kasi njiani. Na wengi wanapoteza kasi kwa kuwa wanaridhika na mafanikio wanayopata na hivyo wanapunguza kuwekeza nguvu katika ubunifu wa kufanya kazi zaidi au kuboresha yale waliyofanikisha. Ushauri ni kwamba katika kila hatua jifanyie tathimini ili kutambua sehemu za kuboresha na kuendelea kukua zaidi kibiashara.

5. Kuwa na msaidizi bora. Mwandishi anatushirikisha kuwa timu ya ushindi katika mchezo wa utajiri inaanzia nyumbani kwako. Hivyo, omba Mungu akupatio Mke au Mme bora ambae mtakaa meza moja na kujadiliana mipango ya maendeleo. Pia, pale mnapobahatika kuwa na watoto hakikisha mnawalea katika misingi ambayo itawezesha wawe na uelewa mpana wa kusimamia miradi yenu. Kwa kifupi ni kwamba kila mmoja ndani ya familia anatakiwa ashiriki katika kuhakikisha gurudumu la mafanikio linasonga mbele.

6. Endelea kufanya kazi kwa bidii kuliko yeyote katika biashara yako. Mwandishi anatushirikisha kuwa ni vigumu wafanyakazi wako kufanya kazi kwa bidii kama wewe mwenyewe haujishughulishi ipasavyo. Ili kufikia malengo ni lazima ujibidishe kwa kadri uwezavyo kuliko mtu yeyote kwenye kampuni ili uwe mfano kwa kila mmoja ndani ya timu yako. Lengo la kufanya kazi kwa bidii ni kuona kampuni zako zinakua siku hadi siku. Hapa ndipo unatakiwa kuitazama biashara sawa na kiumbe hai, kuwa ni lazima ilishwe na lazima iendelee kupumua na ni lazima ikue zaidi ili izalishe faida unayotaka. Hivyo, hakikisha unatafisri namba zinazoingia na kutoka katika biashara yako.

7. Kila mwajiriwa mpya ni sawa na kucheza kamali kuna kupata na kukosa. Mwandishi anatushirikisha kuwa mchakato wa kutafuta mwajiriwa mpya unaanzia kwa kupokea wasifu (CV) za wanaoomba kazi, baada ya hapo ni kufanya mahojiano na mwisho ni kumpa ajira yule ambaye amekuwa bora katika vigezo vya kampuni. Hata hivyo, ukweli ni kwamba sio kile kinachoonekana kwenye michakato yote hiyo ndo kitapima ubora wa mfanyakazi husika. Kwa uzoofu wapo wafanyakazi ambao uonekana wa hovyo kwenye mchakato wa kuomba kazi lakini baadae kiutendeji wanakuwa bora zaidi na kinyume chake ni sahihi. Fundisho, ni lazima uhakikishe unalinda wafanyakazi wako ambao wako bora ili kuepukana na kukimbiwa na wafanyakazi kila mara.


8. Kuwa na fikra pana na endelea kuishi kama mfalme. Mwandishi anatushirikisha kuwa ni kupitia fikra vitu vinaumbika. Vitu vinavyoumbwa vinaweza kuwa kwenye upande chanya au upande hasi. Katika safari ya utajiri ni lazima fikra zako zilenge kutengeneza utajiri zaidi. Hata hivyo, kadri unavyotengeneza utajiri zaidi ni lazima maisha yako yaendane na utajiri ulionao, unatakiwa kuishi maisha ya kitajiri lakini mara zote katika maisha hayo hakikisha milango ipo wazi kwa kila mwenye uhitaji wa kukufikia kwa ajili ya msaada au mawazo,

9. Tengeneza pesa kupitia mchezo unaopenda zaidi katika maisha ya kila siku. Mwandishi anatushirikisha kuwa kila mtu ni mpenzi wa mchezo flani. Ni kutokana na mapenzi hayo watu wengi wanapoteza fedha na muda kwa ajili ya kufuatilia mchezo wanaoupenda. Katika safari ya utajiri ni sahihi kuendelea kuwa mpenzi michezo lakini fikiria zaidi ni kwa jinsi gani unaweza kutengeneza pesa kutokana uhusika wako kwenye mchezo husika. Hata kama hautatengeneza faida kubwa lakini utaendelea kuburudika/kufurahia kupitia michezo husika. Na hilo ndilo kusudi la maisha – kuwa na furaha maishani. Mfano, Trump mwenyewe kutokana na kupenda mchezo wa Golf aliamua kuanzisha klabu za michezo hiyo ambazo pia zinamwingizia kipato.

10. Tengeneza brendi ya jina lako kadri unavyofanikiwa kibiashara. Mwandishi anatushirikisha kuwa jina lako ni kitu muhimu kama utaliendeeleza katika kila unachofanya. Kwa kuzingatia hilo majengo yake yote au uwekezaji kwenye sekta mbalimbali amekuwa akitumia jina lake. Faida kubwa ya kutumia jina lako ni kujitangaza na kukuza jina hilo katika jamii inayokuzunguka. Unavyokuza thamani ya jina lako kuna malipo ndani yake ambayo yanaambatana na kila mtu ambaye atahitaji kutumia jina hilo katika biashara zake. Hata hivyo, ili kulinda ubora au thamani ya jina lako ni lazima uhakikishe unatoa huduma au kila unachofanya unakitekeleza kwa viwango na ubora wa hali ya juu.

11. Kufanikiwa kibiashara ni matokeo ya kujiamini. Mwandishi anatushirikisha kuwa sifa kubwa ya mjasiliamali ni kujiamini kuwa unaweza kufanikisha chochote kile ambacho umedhamiria kufanya. Kujiamini huko kunatokana na msukumo wa ndani ambao upo imara katika kila changamoto ambazo utakumbana nazo katika safari ya mafanikio. Msukumo huu ndo utakuunganisha na dili za kibiashara au kuvuta muhimu katika maisha yako. Kumbuka kuwa binadamu wa kawaida anatumia asilimia 5 tu ya sehemu ya ubongo katika maisha yake ya kila siku. Kupitia matumizi sahihi ya msukumo wa ndani tunaweza kutumia sehemu ya asilimia 95 na kupata matokeo makubwa sana.

12. Mara zote kuwa na mtazamo chanya sambamba na kutegemea kupata kilicho bora lakini tayari kupokea matokeo ya aina zote. Mwandishi anatushirikisha kuwa kutegemea kilicho bora kwenye kila unalofanya ni hatua ya awali ya kufanikiwa. Hata hivyo, mara nyingi katika uhalisia kuna kupanda na kushuka – ni lazima unapotazamia juu ya nyakati bora ufikirie pia namna ya kupambana na nyakati ngumu kwenye kila unachofanya. Kwa kutazamia nyakati ngumu katika mipango yako kunapunguza maumivu au kuepuka kujutia mara baada ya nyakati hizo kutokea.

13. Jifunze kuongea mbele za watu na mara zote hakikisha unafikisha ujumbe sahihi kwa wanaokusikiliza. Mwandishi anatushirikisha kuwa kadri unavyotengeneza utajiri kuna watu wengi ambao wanahitaji kusikiliza namna ambavyo umefanikiwa kibiashara. Kumbuka kuwa wapo wengi ambao wapo tayari kulipia kwa ajili ya kuingia kwenye semina zako au kununua vitabu kwa ajili kufahamu namna ambavyo unatengeneza pesa kiasi cha kufikia utajiri ulionao. Kumbe, ili ufanikiwe katika upande huo ni lazima ujifunze mbinu za kuongea na hadhira. Mbinu moja wapo ambayo mwandishi ametushirikisha ni kuhakikisha hadhira (watazamaji au wasikilizaji wako) unawapa kipaumbele cha kwanza kwa ajili ya kusikia kutoka kwako na wewe pia kujifunza kutoka kwao.


14. Hakikisha tabia zako zinaendana na matamanio ya mafanikio uliyonayo. Maana nyingine ni kwamba unahitaji kuhakikisha video yako inaendane audio. Ni lazima uwe tayari kubadilika kitabia. Kufanikiwa na kibiashara ni lazima kuanzie na mabadiliko ndani mwako. Kama unahitaji kuwa tajiri lakini haupo tayari kufanya yale ambayo matajiri wanafanya hakika hilo sio hitaji bali ni ndoto ya mchana. Unahitaji kujenga tabia za kuthubutu, kuondoa uoga na kujikita kwenye fikra chanya. Kwa ujumla ni lazima uwe tayari kuachana na tabia zote mbaya ambazo hazichangii chochote kwenye safari ya kufikia utajiri wa hitaji lako.

15. Jifunze kusoma vitabu kwa ajili ya kujifahamu kwa undani wewe ni nani na kuifahamu pia jamii inayokuzunguka. Kwa maana nyingine jifunze saikoloji, falsafa na vitabu vya mafanikio mbalimbali. Epuka kukaa bila kuwa na kazi yoyote unayofanya kwa kufanya hivyo unamkaribisha Shetani maisha mwako. Huo muda ambao hauna cha kufanya utumie kwa ajili ya kujifunza maarifa mapya katika maisha yako. Kumbuka kuwa msitari mmoja unaousoma kwenye makala au kitabu unaweza kubadilisha maisha yako kwa ujumla.

16. Kuwa na muda wa kutafakari angalau masaa matatu kila siku. Mwandishi anatushirikisha kuwa ni katika kipindi cha utulivu mtu anaweza kutafakari mambo ambayo ametekeleza katika siku husika. Pia, katika kipindi hicho ndipo mtu anapima hatua zake kuelekea kwenye picha kubwa aliyonayo katika maisha yake. Ni katika kipindi hiki unatakiwa kusoma na kutafakari kuhusu maisha yako.

17. Kuwa mshauri binafsi wa masuala yako ya kifedha. Mwandishi anatushirikisha kuwa utajiri unatengenezwa kupitia maamuzi sahihi ya masuala ya pesa. Unaweza kutumia washauri wanaojihusisha na huduma za ushauri wa masuala ya pesa. Mwandishi anashauri kuwa ni muhimu kuhakikisha unajitegemea kwa maana ya kujifunza kwa vitendo katika sekta nzima ya fedha zako. Watu wengi wamepoteza mali nyingi na pengine kufisilika kutokana na kusikiliza mawazo mabaya kutoka kwa washauri wa masuala ya kifedha. Kumbe, ni muhimu kujitegemea zaidi katika maamuzi ya kifedha na hata pale ambapo utahitaji ushauri hakikisha umefanya utafiti binafsi kabla ya kutekeleza ushauri husika. Hapa ndipo unatakiwa kusoma makala, majarida na hata magazeti ya biashara kwa ajili ya kujifunza zaidi kuhusiana na pesa na uwekezaji wake.

18. Wekeza kwa kadri uwezavyo lakini hakikisha unawekeza sehemu ambayo unafahamu uendeshaji wake. Kumbuka kuwa tunapozungumza kuhusu kuwekeza tunazungumzia pesa, na pesa ndio pumzi ya kuendeleza biashara zako ili ziendelee kukua zaidi. Pia, unatakiwa kufahamu kuwa hauwezi kuwa tajiri kama hauwekezi pesa unayopata. Kumbuka kuwa pesa inatakiwa izalishe pesa zaidi. Kwa kutambua hilo, unatakiwa utumie akili zaidi katika kila sehemu ambayo umeamua kuwekeza. Husifanye maamuzi ya uwekezaji kwa kurupuka kwani kwa kufanya hivyo unaweza kujiingiza kwenye hasara na kupoteza kile ulichonacho.


19. Kuwa na mkataba wa makubaliano unaolinda mali zako. Mwandishi anatushirikisha kuwa katika maisha ya mahusiano yapo mengi yanaweza kujitokeza mbele ya safari kiasi ambacho unaweza kupoteza uwekezaji wako wote. Ili kuepukana na tatizo hilo ni vyema mali unazomiliki zilindwe na mkataba wa makubaliano maalumu ili kujua nani anamiliki ni nini na kwa utaratibu upi.

20. Ondoa au epuka madalali katika dili za biashara unazofanya. Mwandishi anatushirikisha kuwa madalali au watu wa kati kwa ujumla wao wanatumia nafasi hiyo kwa ajili ya kujinufaisha. Kundi hili linahusisha wanasheria, washauri wa sekta mbalimbali na madalali kwa ujumla wao. Kama unahitaji kufanikiwa ni lazima uwe tayari kupata taarifa ambazo watu wa kati wanakuwa nazo katika kila dhamira unahitaji kutekeleza. Hii ni kutokana ukweli kwamba kundi la watu hawa lipo tayari kukugeuza kuwa mtaji kwa ajili ya kufanikisha malengo yao.

21. Wafundishe watoto wako thamani ya pesa katika hatua zote za ukuaji wao. Watoto wako ndio warithi wa mali mnazotengeneza hivyo bila kuwashirikisha hakika mali hizo hazitokuwa endelevu. Kumbe, unatakiwa ushirikishe kila hatua kwenye usimamizi wa mali zako ili watambue thamani ya pesa na umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii. Wanatakiwa watambue kuwa pesa haipatikana kirahisi na hivyo haipaswi kutumika ovyo ili mradi tu kwa kuwa ipo mfuko au benki. Wanapotambua thamani ya pesa wanakuwa na nafasi kubwa kumiliki pesa nyingi maishani mwao.

22. Jifunze kufanya makubaliano ya biashara. Mwandishi anatushirikisha kuwa kukua kibiashara kunahusisha kufanya makubaliano na makundi mbalimbali. Mara zote katika makubaliano ya kibiashara lenga sehemu zote kufanikiwa kwa maana husiangalie upande wako tu. Unatakiwa kuangalia utafanikiwa vipi bila kuumiza upande mwingine. Hivyo, unatakiwa kubadilika kulingana na matakwa ya unaofanya nao makubaliano japo bila kuathiri matakwa ya kampuni yako.

Haya ni machache niliyojifunza kutoka katika kitabu hiki, nimeona nikushirikishe kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Jiunge na mtandao wa Fikra za Kitajiri kwa  KUBONYEZA HAPA.

Endelea kusambaza makala hizi kwa kadri uwezavyo ili ndugu, jamaa na marafiki wanufaike kwa kujifunza maarifa mbalimbali kutoka kwa waandishi wa vitabu. Kumbuka umepata makala hii bila malipo yoyote hivyo hakikisha na wewe unaisambaza bure. (Unaposambaza makala hizi hakikisha haukopi na kupest badala yake share link). Nakutakia mapambano mema.

Karibuni kwenye fikra za kitajiri ili upate elimu isiyokuwa na mwisho.

Born to Win ~ Dream Big 

Augustine Mathias Bilondwa

Namba ya Simu:      +255 786 881 155
Mwanzilishi wa Mtandao wa 
fikrazakitajiri.blogspot.com
Barua pepe:  fikrazatajiri@gmail.com

PATA UCHAMBUZI WA VITABU vifuatavyo kwa kulipia Tshs. 5000.00 kila kitabu (Ukinunua vitabu vyote vitatu utapata kwa ofa ya Tshs 10,000.00).

1.    Kitabu cha Kwanza ni “THE RULES OF MONEY (KANUNI ZA PESA)” kutoka kwa Mwandishi Richard Templar
Katika kitabu hiki utafahamu kanuni 107 za pesa. Ndani ya kanuni hizo utagundua kuwa utajiri ni haki ya kila mtu hivyo ni wajibu wako kuwa tajiri. Kanuni zote (107) zimechambuliwa kwa kina na kuandaliwa kwa lugha Kiswahili. Uchambuzi huu unapatikana kwa kijitabu kidogo chenye kurasa 39 ambazo unaweza kusoma kwenye simu yako ya mkononi (simu janja – smart phone) au kwenye kompyuta mpakato (pc).

2.    Kitabu cha pili “THE RULES OF LIFE (KANUNI ZA MAISHA)” kutoka kwa mwandishi Richard Templar
Mwandishi kupitia kitabu hiki anatushirikisha kanuni 106 za maisha. Kanuni hizi zimechambuliwa kwa kina kwa lugha ya Kiswahili na unaweza kukisoma kupitia simu janja au kompyuta mpakato. Kanuni zote zinagusa kila sekta ya maisha yako hivyo ni kitabu ambacho hautojutia pesa unayoitoa kwani utajifunza maarifa mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maisha yako.

3.       Kitabu cha tatu ni “I CAN I MUST I WILL (NAWEZA, NALAZIMIKA, NITAFANYA)” kutoka Mwanamafanikio na Mtanzania Mwenzetu Marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi
Kwa ujumla kupitia kitabu hiki Dr. Mengi anatushirikisha maisha yake kuanzia akiwa mtoto, akiwa mwanafunzi, wakati anaanzisha biashara yake ya kwanza, namna alivyopanua biashara zake, wajibu aliokuwa nao kwa jamii, misimamo yake kwenye mfumo wa Serikali kwa awamu zote tano, wajibu wake kwenye uhifadhi wa mazingira na matarajio yake kwenye kukuza biashara kwa siku za baadae.

Kupata uchambuzi wa vitabu hivi tuma pesa yako kwa njia ya M-pesa au Airtel Money kupitia namba zifuatazo:-
M – Pesa tumia namba: 0763 745 451 (Majina ni Augustine Mathias)
Airtel Money tumia namba: 0786 881 155 (Majina ni Augustine Mathias)

Baada kutuma pesa hiyo nitumie ujumbe kwenye namba ya airtel (0786 881 151 451) ukiwa na barua pepe yako ili nikutumie uchambuzi wa kitabu husika.

UTAJIRI NI HAKI YAKO YA KUZALIWA "BEING RICH IS YOUR BIRTH RIGHT"