Mambo Niliyojifunza Kwenye Kitabu cha A Gift To My Children: Zawadi kwa Wanangu (Mwongozo wa maisha na uwekezaji).

Habari ya leo rafiki na msomaji wa mtandao wa Fikra za Kitajiri.

Naamini kuwa rafiki yangu unaendelea vizuri na mapambano ya kila siku kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Kama kawaida yangu, leo katika uchambuzi wa vitabu kupitia mtandao wa Fikra za Kitajiri nakushirikisha uchambuzi wa kitabu cha wiki hii.

Kama bado hujajiunga kwenye mfumo wetu wa kupokea makala za uchambuzi wa vitabu, tafadhali fanya hivyo KWA KUBONYEZA BONYEZA HAPA na kujaza fomu kisha bofya “jiunge/subscribe” utakuwa umejiunga na mtandao huu. Ni fursa ya bure ambayo utaendelea kupata uchambuzi wa vitabu kwa lugha rahisi kupitia barua pepe yako.

Kitabu cha wiki hii ni A Gift To My Childrenambacho kimeandikwa na mwandishi Jim Gogers. Mwandishi ametumia kitabu hiki kutushirikisha uzoefu wake wa maisha pamoja na uwekezaji. Uzoefu anaotushirikisha umetokana na maisha aliyoishi kama baba wa familia lakini pia kama mwekezaji kwenye upande wa fedha. Ikumbukwe pia kuwa Rogers ni mtu wa kwanza kuweka rekodi za dunia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuzunguka mabara sita (Dunia) kwa kutumia pikipiki.

Karibu ushirikiane nami kujifunza machache kati ya mengi ambayo mwandishi anatushirikisha katika kitabu hiki:

1. Maisha unayoishi ni yako mwenyewe hivyo kumbuka kutegemea sana akili yako pindi unapofanya maamuzi muhimu katika maisha yako. Mwandishi anatushirikisha kuwa katika maisha kuna watu wanatuzunguka ambao wapo tayari kutoa ushauri hata kama hawajaombwa kufanya hivyo. Mara nyingi washauri hawa wengi wao huwa wanashauri hata kwenye masuala ambayo hawana uelewa mpana. Jifunze kwa mapana juu ya changamoto inayokukabili ili kuwa na uelewa wa kutosha kuliko washauri wanaokuzunguka. Kumbuka wewe ndo wa kuchagua namna unavyotaka maisha yako yawe kabla ya kutegemea wengine wakusaidie kufanya hivyo.

2. Mtu akidharau wazo lako au mipango yako ya mafanikio itazame hali hiyo kama deni lako la kufanikiwa zaidi. Mwandishi anatushirikisha kuwa ni wewe pekee mwenye uhakika na wazo au mipango yako ya mafanikio na kutambua hivyo husijali pale ambapo mtu au kundi la watu wanashindwa kukuelewa. Husikabali kutoka kwenye mstari wako wa mafanikio kutokana na maneno ya watu. Muhimu ni kuhakikisha una uelewa wa kutosha kwenye kile ambacho umekusudia kutekeleza katika safari ya maisha yako.

3. Husifanye manunuzi ya vitu au starehe za hanasa kwa sababu ya kwamba una uwezo badala yake hakikisha kila unachoamua kinafanyika kwa kuongozwa na fikra za ndani mwako. Hapa mwandishi anatushirikisha kuwa tusipende kuishi maisha ya kuigiza bali kila tunachofanya kiongozwe na macho ya ndani mwetu. Kumbuka kuwa badala ya kuwekeza katika kununua vitu vya gharama na hanasa ili kutafuta umaarufu wa nje tuwekeze tulichonacho kwa ajili ya kuwa na maisha ya baadae kuliko tuliyonayo sasa.

4. Husikubali umri wako uwe kizuizi cha kutimiza ndoto yako. Mwandishi anatushirikisha kuwa pale unapochagua nini unataka kutimiza katika maisha yako moja kwa moja unatakiwa kuanza kufanyia kazi machaguo yako pasipo kutazama umri wako au nafasi uliyonayo kwa wakati husika. Muhimu katika kila hatua ni kufanya kufanya kufanya kufanya...... bila kikomo kuliko kuendelea na maneno yasiyokuwa na utekelezaji.

5. Njia rahisi ya kufanikiwa ni kufanya kazi ya tamanio la roho yako na kuhakikisha unawekeza jitihada/bidii ya kutosha kwa ajili kazi hiyo kuwa bora kila siku. Mwandishi anatushirikisha kuwa katika maisha hasa katika ukuaji utafanya kazi nyingi lakini katika zote chagua kazi ambayo ni tamanio la moyo wako na kuhakikisha unaweka bidii ya kutosha. Hata hivyo, unatakiwa kulenga kuikuza kazi hiyo kutoka kwenye hali yake ya sasa ili kila siku iwe bora. Kumbuka kuwa hata husipofanikiwa kuwa tajiri kupitia kazi hiyo utakuwa na furaha katika maisha yako ya kila siku na utafanikiwa kukamilisha kazi iliyokuleta duniani humu.

6. Kuwa makini katika kila taarifa unayopata. Mwandishi anatushikisha kuwa siri kubwa inayotofautisha waliofanikisha maisha na watu wengine ni kuchukulia kila taarifa kwa umakini wake. Hii ni muhimu kutokana na ukweli kwamba kuwa taarifa ndizo zinachambuliwa kwa ajili ya kufanyiwa kazi iwe kwenye uwekezaji au mahusiano na watu wanaokuzunguka. Hivyo, ni muhimu kujenga utamaduni wa kufanya tafiti za kina juu ya taarifa zinazokufikia kabla ya kuzifanyia maamuzi. Tafiti hizi zinatakiwa kuongozwa na bidii ya kutaka kujua zaidi hasa juu ya kile ambacho umeamua kufanyia kazi katika maisha yako.


7. Hakikisha unaishi maisha yenye ndoto tena ndoto kubwa ambayo inakuogopesha. Mwandishi anatushirikisha kuwa katika kufanya kazi ya matanio ya moyo wako ni lazima uwe na ndoto ambayo ni chachu kwako kuendeleza kufanya makubwa katika maisha. Kadri unavyoendelea kuifanyia kazi ndoto yako utagundua kuwa kukamilika kwa ndoto hiyo ni mwanzo wa ndoto nyingine tena kubwa ambazo hukuwahi kuzitarajia katika maisha yako.

8. Kumbuka sio kweli kuwa kila jibu unaloambiwa ni HAPANA kweli ni hapana na kila unachoambiwa NDIYO kweli ni ndiyo. Mwandishi anatushirikisha katika safari ndefu ya maisha hatutakiwi kukubaliana na mitazamo ya watu moja kwa moja na badala yake ni lazima tuwe na kanuni zinazotuongoza ambazo hata hivyo sio lazima zikubaliwe na watu wanaotuzunguka.

9. Tembea na kuona mapana ya dunia na kujifunza mengi kwenye kila nchi unayotembelea. Mwandishi anatushirikisha kuwa ili kufanikiwa kimaisha unahitaji kujifunza tamaduni mbalimbali zaidi ya eneo ambalo umekulia. Hata hivyo, unatakiwa kutumia tamaduni hizo katika kufanikisha safari yako ya uwekezaji au mafanikio ya maisha kwa ujumla. Ni kupitia kutembea utaweza kujijua vyema na pia kuweza kuifahamu vyema nchi yako kwa kulinganisha na mazingira ya nchi nyingine. Ni katika kutembea pia utajifunza kuwa watu wote ni sawa na hivyo unaweza kuishi mahali popote na kutengeneza maisha unayotaka.

10. Kuwa muwazi kwa watu wote bila kujali tamaduni, asili au rangi zao. Mwandishi anatushirikisha kuwa siri ya kufanikiwa kimaisha ni kuhakikisha watu watu wote unawapa uzito sawa. Siri hii itakufanya uishi na watu wa aina mbalimbali hata kama upo kwenye mazingira ya ugenini.
                                               
11. Wekeza kwenye nchi au maeneo ambayo hayana ubaguzi wa rangi. Mwandishi anatushirikisha kuwa uwepo wa ubaguzi wa rangi hasa kwenye baadhi ya nchi zilizoendelea imesababisha uwepo wa machafuko mengi katika maeneo hayo. Hii ni pamoja na kuendelea kukua kwa matukio ya ugaidi ambayo chanzo chake kikubwa ni mwendelezo wa chuki baina ya watu wa asili au imani tofauti.

12. Katika hatua zote za ukuaji kuwa na fikra uhuru na jitahidi kuwa raia wa mataifa au dunia kwa ujumla wake. Mwandishi anatushirikisha kuwa kizazi cha sasa kipo kwenye zama za fikra huru na chenye nafasi kubwa ya kuishi kidunia zaidi kuliko vizazi vilivyotangulia. Hii ni kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano ambayo imerahisisha upatikanaji wa taarifa kutoka pande zote za dunia. Ukiwa na fikra uhuru za namna hii utaishi maisha yenye furaha hasa kwenye kile ambacho umeamua kufanya katika maisha yako na hii ndio itakufanya uwe uhuru kuishi na watu wa asili tofauti. Kumbuka kuwa kama kila mtu angeishi kama raia wa dunia, dunia hii ingekuwa ni mahali pazuri na salama kwa kila kiumbe kuishi.

13. Kumbuka kuwa vita haijawahi kuwa na manufaa kwa mtu au hata nchi inayoshinda. Katika hatua za ukuaji na uwekezaji jitahidi kukwepa nchi ambazo zinapigana vita mara kwa mara. Hii ni pamoja na kuwa mmoja kati ya majeshi ya nchi na badala yake jitahidi kufanya kazi ambayo itakuwa ni mapenzi kutoka moyoni mwako lakini pia inakufanya uwe na fikra uhuru na pana katika maisha yako yote kwenye ulimwengu huu.

14. Jifunze falsafa (philosophy) kwani kupitia elimu hiyo utaweza kujitambua na kufikiri kwa kujitegemea. Mwandishi anatushirikisha kuwa njia ya kwanza ya kukamilisha hitaji lolote la maisha yako ni kujitambua kwanza na elimu pekee ambayo inaweza kufanikisha hilo ni kupitia falsafa. Katika elimu hiyo ya falsafa hautaji kuzama sana ili ufanikishe hilo bali unahitaji kujikita kwenye kipengele cha kujitegemea kifikra au fikra huru. Hapa unahitaji kujifunza kufikiri nje boksi kwa maana ya kufikiri nje ya mazoea, kweli, imani au tamaduni zilizojengeka katika jamii unayoishi.

15. Kuna njia mbili za kufikiri na mwisho kufanya maamuzi. Njia ya kwanza ni kufikiri kwa kutegemea uchunguzi au mwonekano/uhalisia wa jambo husika. Njia ya pili ni kufikiri kwa kutegemea nadharia (evidence) za kweli ambazo tayari zimewekwa wazi juu jambo husika (kufikiri kwa mantiki). Mwandishi anatushirikisha kuwa hakuna njia ambayo ni bora kuliko nyingine kati ya hizi njia mbili za kufikiri. Hivyo, unahitaji kujifunza kuzitumia njia zote ili kuwa na mfumo msawazo wa kufikiri (balanced way of thinking).

16. Jifunze historia ya ulimwengu kwa mapana na tumia historia hii kujua mwenendo wa ulimwengu na vilivyomo ndani yake. Katika historia hii unahitaji kupata picha kubwa ya namna ambavyo mabadiliko mbalimbali yametokea katika Dunia hii na hivyo utumie matukio hayo kwa ajili ya kukadiria matukio yanayokuja siku zijazo. Ni kupitia historia hii utajifunza kuwa kilichosahihi leo hii kwenye mitazamo ya watu yawezekana baada ya miaka 10 au 20 hakitakua sahihi tena. Ni kupitia historia ya tamaduni au nchi mbalimbali utafahamu ni sekta ipi unaweza kuwekeza kwa mafanikio.


17. Hakuna jipya chini ya jua. Mwandishi anatushirikisha kuwa matukio yote yanayotokea katika ulimwengu wa sasa yamewahi kuwepo siku za nyuma bali kinachofanyika matukio hayo yanawasilishwa kwa njia zenye ubunifu tofauti lakini asili yake ni ya tokea enzi hizo. Katika safari ya maisha yako unahitaji kuongozwa na kanuni ya kwamba yanayotokea katika ulimwengu wa sasa yamewahi kuwepo na yatatokea katika ulimwengu wa baadae. Hii ndiyo siri kubwa ya kutumia historia kwa ajili ya mafanikio yako hasa katika ulimwengu wa uwekezaji.

18. Jifunze lugha mbalimbali lakini kama utaweza hakikisha unajifunza kichina na kingeleza. Mwandishi anatushirikisha kuwa katika ulimwengu wa uwekezaji mwenyekujua lugha ya sehemu husika ana nafasi kubwa ya kufanikiwa kuliko yule ambaye hajui. Lugha ambazo zinakuwa kwa kasi ni kichina pamoja na kingeleza hivyo katika kujifunza lugha ambazo sio za asili yako hakikisha lugha hizo mbili zinakuwa sehemu ya malengo yako. Kumbuka kuwa ukweli unajionesha wazi kuwa sasa ni karne ya China kuwa taifa kubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii duniani.

19. Jitambue wewe ni nani na muhimu zaidi tambua madhaifu yako ikiwa ni pamoja na namna unavyokabiliana na makosa unayofanya. Mwandishi anatufundisha kuwa njia pekee ya kujifunza kutokana na makosa yetu katika ulimwengu wa uwekezaji au maisha ya kila siku kwanza ni kukubali kuwa tumekosea. Kama haukubali kuwa unakoseaga kamwe hauwezi kujifunza kitu na mara zote utaendelea kufanya makosa yaleyale.

20. Jifunze saikolojia. Mwandishi anatushirikisha kuwa pamoja na kujifunza historia, falsafa pamoja na lugha unahitaji zaidi kujifunza saikolojia. Katika ulimwengu wa uwekezaji unahitaji kufahamu zaidi saikolojia ya watu kwa kuwa hii ndio inasababisha mabadiliko ya soko. Ni kutokana na mabadiliko hayo watu wengi wanapaniki kiuwekezaji na hivyo kupelekea kuuza kile walichowekeza kutokana na kuongozwa na hisia. Ni lazima uwe tayari kutumia paniki za watu kwa ajili ya mafanikio yako.

21. Tambua mabadiliko mbalimbali yanayotokea kwenye jamii na yatumie kwa faida yako. Mwandishi anatushirikisha kuwa msingi mkuu wa uchumi unatokana na “kusambaza bidhaa – supply” na “mahitaji ya bidhaa husika – demand”. Mabadiliko yoyote kati ya mahitaji au kusambaza yanaweza kuathiri uchumi wan chi au mtu binafsi endapo hajajua kucheza kulingana na mabadiliko katika soko.

22. Fanya utafiti wa kutosha kwenye sekta ambayo kila mtu anakimbia. Mwandishi anatushirikisha kuwa kutokana na kuongozwa na hisia watu wengi wanakimbia fursa kwa kuongozwa na maneno ya kusikia. Kama unahitaji kuwa mwekezaji makini unahitaji kufanya tafiti zako mwenyewe na wekeza bila kujali kuwa wengi wanakimbia sekta husika. Hii ni pamoja na kuhakikisha kuwa mara zote unahitaji kuwekeza kwenye kitu kipya.

23. Fanyia kazi ndoto yako na kamwe husikubali kukatiza ndoto hiyo kwa vyovyote vile. Mwandishi anatushirikisha kuwa watu wengi wanakatiza ndoto zao kwa vile wanakubali kuyumbishwa na mawimbi wanayokutana nayo njiani. Unahitaji kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kuwa unatimiza ndoto yako.

Haya ni machache ambayo nimeweza kukushirikisha kati ya mengi yaliyo kwenye kitabu hiki. Kupata nakala ya kitabu hiki BONYEZA HAPA na ujiunge na mtandao wa fikra za kitajiri kisha nitumie ujumbe wa kuomba kitabu hiki kupitia barua pepe fikrazakitajiri@gmail.com.

Niendelee kukuomba usambaze jumbe hizi kwa kadri uwezavyo ili yale unayojifunza yawafikie wengi na hatimaye tufanikiwe kuibadilisha dunia hii kuwa mahali pazuri pa kuishi (Unaposambaza makala hizi hakikisha haukopi na kupest badala yake share link). Nakutakia mapambano mema.

Karibuni kwenye fikra za kitajiri ili upate elimu isiyokuwa na mwisho.

Born to Win ~ Dream Big 

Augustine Mathias Bilondwa

Namba ya Simu:      +255 786 881 155
Mwanzilishi wa Mtandao wa 
fikrazakitajiri.blogspot.com
Barua pepe:  fikrazatajiri@gmail.com

PATA UCHAMBUZI WA KITABU CHA THE RULES OF MONEY ( KANUNI ZA PESA)
 
Mwandishi Richard Templar katika kitabu hiki ametushirikisha kanuni 107 ambazo kila mtu anaweza kuzitumia kutengeneza pesa na hatimaye kuwa tajiri. Uchambuzi wa kina wa kanuni zote (107) umeandaliwa kwa mfumo wa pdf na unapatikana kwa gharama ya Tshs. elfu tano tu (5,000/=). Kanuni zote zimechambuliwa na kuandaliwa kijitabu kidogo chenye kurasa 39 ambazo unaweza kusoma kwenye simu ya mkononi (smart phone) au kwenye kompyuta (pc).

Kupata uchambuzi wa kanuni zote tuma pesa yako kwa njia ya M-pesa au Airtel Money kupitia namba zifuatazo:-

M – Pesa tumia namba: 0763 745 451 (Majina ni Augustine Mathias)
Airtel Money tumia namba: 0786 881 155 (Majina ni Augustine Mathias)

Baada kutuma pesa hiyo nitumie ujumbe kwenye namba ya airtel (0786 881 151 451) ukiwa na barua pepe yako ili nikutumie uchambuzi wa kanuni hizi moja kwa moja kwenye mtandao wako.

UTAJIRI NI HAKI YAKO YA KUZALIWA "BEING RICH IS YOUR BIRTH RIGHT"





onclick='window.open(