NENO LEO (JANUARI 31, 2020): JANUARI 2020 NENDA KWA AMANI LAKINI UMENIACHAJE?

๐Ÿ‘‰๐ŸพHongera rafiki kwa kufikia siku hii ya mwisho katika mwezi Januari 2020.

๐Ÿ‘‰๐ŸฟHakika siku zinaenda kasi maana ni juzi tulisherekea mwaka mpya 2020 lakini leo hii ni mwaka huo huo ambao umebakiza miezi 11.

๐Ÿ‘‰๐ŸฟMategemeo yangu ni kwamba umeamka salama na upo tayari kuendeleza bidii za kuhakikisha siku zilizobaki katika mwaka huu zinakuwa zenye faida katika kuboresha maisha yako.

✍๐ŸพKaribu katika neno la tafakari ya leo ambalo linalenga kutumbusha malengo ambayo tumejiwekea katika mwaka huu.

✍๐ŸพKatika jamii tunayoishi kila inapofika mwaka mpya utasikia maneno mengi kama vile "mwaka mpya na mambo mapya". Kauli hizi zinaonesha kuwa watu wengi wanahitaji mabadiliko kila wanapoingia mwaka mpya.

✍๐Ÿพ Wengi wanaweka malengo lukuki yanayolenga kubadilisha mazoea na tabia katika kipindi cha mwaka unaoisha ili mwaka unaofuatia uwe wa tofauti katika maisha yao.

✍๐ŸพTafsiri yake ni kwamba kila mtu anahitaji maisha bora. Maisha yenye mafanikio kwenye kila sekta na ndio maana kila mwaka watu wanalenga wabadilike kutoka kwenye maisha ya zamani na kuingia kwenye maisha mapya.

✍๐ŸพHata hivyo ukweli ni kwamba wengi wanahitaji mabadiliko lakini ambao wapo tayari kubadilika ni wachache.

✍๐ŸพWengi wanaweka malengo kila mwaka lakini kadri siku zinavyosegea wanajikuta wamerudi kwenye maisha yale yale waliyozoea. Kumbuka kuwa kama unahitaji mabadiliko ni lazima yaanzie ndani mwako.

✍๐ŸพTafakari jinsi ambavyo mwaka huu umejiwekea malengo na fanya tathimini inayolenga kupima mwenendo wako kuelekea kwenye ufanisi wa malengo hayo. Jiulize maswali yafuatayo:
๐Ÿ‘‰๐ŸฟJanuari umeondoka lakini umeniacha je?.
๐Ÿ‘‰๐ŸฟJe umechukua hatua yoyote inayolenga kufikia malengo uliyojiwekea?
๐Ÿ‘‰๐ŸฟJiulize je kuna mabadiliko yoyote ya kitabia na mazoea ikilinganishwa na mwaka jana?.
๐Ÿ‘‰๐ŸฟJiulize je umeweka jitihada zozote zinazolenga kubadilisha maisha yako?

✍๐ŸพMwisho kama bado upo kama ulivyokuwa mwaka jana, hakika bado hujachelewa. Chukua hatua sasa maana Dunia inasubiri kuandika mema yako ambayo uliyafanya katika kipindi cha uhai wako.

๐Ÿ‘๐ŸพNakutakia kila la kheri katika siku hii leo.

Sehemu ya Kwanza: Uchambuzi wa Kitabu cha Sale Like Crazy; How to Get as Many Clients, Customers and Sales as You Can Possibly Handle: Uza kama kichaa; Jinsi ya kupata wateja na kuongeza mauzo.

Habari ya leo rafiki na msomaji wa mtandao wa Fikra za Kitajiri. Karibu tena katika kitabu chetu cha pili katika kipindi cha mwaka 2020 kati ya vitabu 30 ambavyo nimepanda kuvisoma na kukushirikisha uchambuzi wake.

Pia katika kipindi hiki, mtandao wa Fikra za Kitajiri umedhamiria kuunganisha wafamilia wake kwa kuanzisha kundi la WhatsApp ambalo litatumika kama darasa la kujifunza maarifa mbalimbali yanayolenga kuboresha maisha yetu. Kupata fursa hii ya kuwa sehemu ya kundi hili nitumie ujumbe kupitia barua pepe fikrazakitajiri@gmail.com na utaunganishwa na kundi hili ndani ya muda wa kipindi cha wiki mbili kuanzia sasa.

Bado naendelea kukumbusha kuwa, Lengo letu kubwa mwaka 2020 ni kuendelea kuweka bidii kwa kadri ya uwezo wetu kwa ajili ya kuifanya Dunia kuwa mahala pazuri pa kuishi. Kumbuka ili Dunia iwe mahala pazuri pa kuishi ni lazima lianzie katika maisha yako. Ukiwa na maisha mazuri Dunia hii utaiona sehemu salama pa kuishi na ndivyo ilivyo kwa jamii unayoigusa. Karibu tena katika makala ya uchambuzi wa kitabu cha wiki hii.

Kama bado hujajiunga na mfumo wetu wa kupokea makala za uchambuzi wa vitabu, tafadhali fanya hivyo KWA KUBONYEZA HAPA na kujaza fomu kisha bofya “jiunge/subscribe”. Ni fursa ambayo itakuwezesha kupata uchambuzi wa vitabu kwa lugha rahisi kupitia barua pepe yako.

Kitabu cha pili katika mwaka huu ni Sale Like Crazy” ambacho kimeandikwa na mwandishi Sabri Suby. Sabri Suby ni mwanzilishi na mmiliki wa kampuni ya King Kong nchini Australia. King Kong ni Wakala wa Masoko ya Mtandao (Digital Marketing Agency) ambayo katika kipindi cha miaka minne iliweza kutengeneza dolla za kimarekani (USD) milioni 4 (zaidi ya bilioni nane).

UTANGULIZI: KWA NINI MAARIFA YALIYOMO NDANI YA KITABU HIKI NI MUHIMU KATIKA NYAKATI ZA SASA

Mwandishi anatushirikisha kuwa tafiti zinaonesha kuwa asilimia 96 ya biashara zote huwa zinakufa kabla ya kutimiza miaka kumi toka kuanzishwa kwake. Kati ya hizo, takribani asilimia 80 huwa zinakufa ndani ya miaka miwili toka kuanzishwa kwake. Hata hivyo, asilimia 4 ya biashara ambazo zinaweza kumudu kuendelea baada ya miaka 10 haimaanisha kuwa zinafanya vizuri katika kutengeneza faida kwa wamiliki.

Mwandishi anatushirikisha kuwa biashara nyingi zinashindwa kukua zaidi ya miaka kumi kutokana na wamilikiwa kushindwa kutumia mbinu sahihi za kuiendeleza biashara husika. Mbinu namba moja ni kuhakikisha biashara inajiendesha kwa faida kwa maana uwezo wa wa biashara kuendelea kuzalisha mapato. Kwa maneno rahisi, biashara iwe na uwezo wa kuzalisha fedha za kutosha katika hali ambayo itawezesha uendelevu na ukuaji wa biashara. Hii ni kutokana na ukweli kwamba fedha zinazozalishwa na biashara ndo uhai, hewa au chakula cha biashara husika kuendelea kukua zaidi.

Biashara nyingi zinakufa katika kipindi cha awali toka kuanzishwa kwake kwa kuwa waanzilishi wengi wa biashara wanakuwa hawana elimu ya misingi ya bisashara. Mfano, biashara nyingi zinaanzishwa kutokana ujuzi wa mwanzilishi wa biashara katika biashara anayoanzisha. Kwa maana, Mpishi anaamua kuanzisha mgahawa, Mwanasheria anaanzisha Kampuni ya huduma za kisheria au daktari anaanzisha biashara ya huduma za afya. Kubwa, ni kwamba waanzilishi wote hao hawana misingi ya kuendesha biashara husika na matokeo yake ni kwamba biashara zinakufa au zinadumaa.

Kutokana na waanzilishi wengi kushindwa kuwa na misingi sahihi ya biashara wanajikuta biashara zinakuwa ni kazi ya mmiliki (job) badala ya kuwa sehemu ya kuzalisha fedha kwa mmiliki wakati huo huo ikimpunguzia muda wa kufanya kazi. Mfano, biashara nyingi katika jamii ni zile ambazo mmiliki hawezi kutoka kwenye biashara kila siku na hivyo kufanya hivyo anakuwa ni mtumwa wa biashara husika.

Katika kitabu hiki mwandishi anashirikisha mfumo halisi wa mauzo ambao yeye binafsi ameutumia kukuza biashara nyingi kutoka kwenye biashara za kawaida hadi kwenye za mabilioni. Mbinu hizi amezitumia kusaidia wafanyabiashara wengi kuepukana na karaha ya kufanya kazi zaidi masaa 80 kwa wiki hadi 32 huku wakiwa hawana msongo wa mawazo wa kupata wateja wapya. Hali hii imewawezesha wamiliki wa biashara hizo kuwa na biashara ambazo wanaweza kutengeneza zaidi ya asilimia 700% ikilinganishwa na kiasi cha fedha walichokuwa wanatengeneza awali katika biashara husika.

Karibu ushirikiane nami kujifunza machache kati ya mengi ambayo tunashirikishwa katika kitabu hiki:

1. Kama unahitaji kuwa bilionea huna budi kuhakikisha unakuwa na fikra/mawazo za kibilionea. Tena unatakiwa na fikra za bilionea ambaye unatafuta utajiri mwenyewe na si kutegemea hela za kurithi au bahati na sibu. Unahitaji kufahamu namna ambavyo mabilionea namna ambavyo wanafanya maamuzi yao kuhusiana na maisha ya kawaida pamoja na maamuzi ya kibiashara. Kwa kifupi, unatakiwa kufahamu sehemu ambazo mabilionea wanawekeza muda na rasilimali zao.

Mwandishi anatushirikisha kuwa baada kufanya tafiti kwa muda mrefu kuhusiana na maisha ya watu wenye mafanikio ya kifedha amegundua kuwa, watu hawa wanawekeza sana kwenye vitu ambavyo vina mrejesho chanya (positive return). Watu hawa wanajali sana rasilimali ambazo hazirejereshwi (non-renewable resource) kuliko kitu chochote. Kwa kifupi, wanajali sana muda wao na wanautumia kwenye kazi ambazo zinazalisha kipato zaidi. Moja, ya sababu ambazo zinapoteza muda ni kukua kwa teknolojia ya habari ambayo inawafanya watu kila baada ya dakika kadhaa watamani kufungua simu au kompyuta zao kujua kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii au kwenye barua pepe. Matajiri wengi hawatumi mitandao kijamii au barua pepe kwa hasara badala yake wanaitumia kwa ajili ya kutengeneza pesa zaidi.

2. Maisha yetu yamejaa usumbufu wa kila aina na ni usumbufu huo ambao unawafanya watu wengi kuwa bize muda wote. Kumbe, ili kuwa bilionea unahitaji kujiepusha kazi ambazo zinakupotezea mtiririko wa fikra na kujikita kwenye kazi muhimu pekee. Pia, biashara ili ikue zaidi unatakiwa uwe na timu kubwa kwa maana ya kupanua wigo wa biashara kutoka kwenye kufanywa na mtu mmoja (mmiliki) kwa kufungua matawi zaidi. Uwezo wa kuuza bidhaa/huduma yako ndio unaamua ukuaji wa bidhaa/huduma husika. Hivyo, ukuaji wa biashara yako utategemea na uwezo wako wa kutafuta masoko kwa ajili ya wateja wapya. Kubwa kuliko, biashara yako inatakiwa kuwa na mfumo ambao utawezesha biashara kukua kwa haraka katika kipindi cha muda mfupi. Kwa kutaja tu baadhi sifa za mfumo huo ni kama:
รผ  Wateja wanapaswa kukimbilia bidhaa/huduma zako na sio wewe kuwakimbilia;
รผ  Uwe na utabiri na uthabiti ambao unatoa fursa mpya, wateja wapya na mapato zaidi;
รผ  Unaongea na wateja watarajiwa wengi zaidi kuliko wezo wako wa kuwahudumia. Maana yake ni kwamba mahitaji ya bidhaa/huduma zako ni wa kiwango cha juu;
รผ  Uwepo wa mfumo wa moja kwa moja ambao unawezesha upatikanaji wa wateja wapya kwa kutumia nguvu kidogo zaidi; na
รผ Una una muda wa kutosha kwa ajili ya kufanya kazi muhimu pekee ambazo zinakuwezesha kutengeneza kipato zaidi.

3. Sifa kubwa ambayo mfanyabiashara yeyote anatakiwa kuwa nayo ni kutambua kuwa bidhaa/huduma yake ni kwa ajili ya kutatua matatizo ya wateja. Tafsiri yake ni kwamba fedha zinatengenezwa kwa kuwa na uwezo wa kumshawishi mteja atambue thamani ya bidhaa/huduma zako katika kutatua changamoto zake. Kumbe, ili kutengeneza pesa zaidi unatakiwa kutambua maumivu, hamu, hofu, tumaini na hitaji la mteja wako katika kutumia bidhaa/huduma zako. Pale unapokidhi hitaji la mteja moja kwa moja bei ya bidhaa zako inakuwa sio changamoto tena kwa kuwa wateja wapo tayari kulipia gharama yoyote endapo wana uhakika wa kupata kile wanachotaka.


4. Hakikisha unafahamu kanuni ya Vilfredo Pareto ya 80/20% na namna ya kuitumia katika biashara yako. Pareto aligundua kuwa 80% ya uchumi wa nchi upo mikononi mwa 20% ya idadi ya watu. Pareto aligundua pia kuwa kanuni hii inafanya kazi katika sehemu nyingi za maisha ya mwanadamu. Mfano, asilimia ya 20 ya pembejeo inazalisha 80% ya mazao; 20% pekee ya wafanyakazi wanazalisha 80% ya matokeo; 20% ya wateja wanaleta 80% ya mapato na zaidi na zaidi. Kwa ujumla unatakiwa kufahamu kuwa katika biashara 20% ya kazi zinazohusiana na biashara inazalisha 80% ya matokeo yote. Kumbe, mmiliki makini wa biashara unatakiwa kujikita kwenye 20% ya kazi ambazo zinaingiza pato la 80% ya biashara yote. Asilimia 80 ya kazi zinazobakia inabidi uamue kutafuta watu wa kuifanya kwa ajili yako. Unachotakiwa kufanya kama mmiliki wa biashara ni kuanisha kazi ambazo zinaingiza pato kubwa kwenye biashara na kujikita kwenye usimamizi wa kazi hizo kwa ufasaha.

5. Thamani ya muda wako inapatikana kwa kugawanya kiwango unacholipya dhidi ya idadi ya masaa unayofanya kazi. Mfano, kama kwa wiki unafanya kazi masaa 40 na unaingiza 1,000,000.00; thamani ya muda wako kwa saa ni 25,000.00. Hivyo, ili kuongeza thamani ya muda wako unatakiwa kuangalia ni kazi zipi ambazo unaweza kuzipunguza ili zifanywe na wasaidizi wako. Kwa kufanya hivyo utakuwa umepunguza masaa ya kazi na kuongeza pato lako kwa wiki.

6. Mmiliki wa biashara jukumu lako namba moja ni kuhakikisha unakuza mauzo ya bidhaa/huduma. Hivyo, muda, nguvu na umakini wako unatakiwa kuuwekeza sana kwenye usimamizi wa mauzo kuliko kitu chochote kile. Unatakiwa kuwa mbobevu wa mauzo ya bidhaa yako kuliko mtu yoyote yule ambaye unafanya nae kazi. Hakikisha unawekeza muda wako kwenye shughuli ambazo zinahusiana na mauzo ya bidhaa/huduma. Hata hivyo, hii hainamanishi kuwa kazi zote zinazohusiana na mauzo ufanye mwenyewe bali lengo ni kukupa angalizo la kuhakikisha chochote kinachofanyika kuhusiana na mauzo unakuwa na uelewa wa kutosha.

7. Tambua kuwa mbobevu katika mauzo haina uhusiano na kiwango cha elimu, historia yako au kalama ulizonazo. Kuuza ni sanaa na sayansi ambayo kila mtu anaweza kujifunza na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa. Mwandishi anatushirikisha kuwa ili ufanikiwe kuwa muuzaji bora kwanza unatakiwa kuishinda sauti yako ya ndani ambayo imekuwa ikikuambia kuwa hauwezi. Muhimu, unahitaji kujidhibiti wewe mwenyewe kuliko unavyotakiwa kuwadhibiti wengine. Nidhamu binafsi katika safari ya kuwa muuzaji bora ni nyenzo muhimu ambayo itakutofautisha na washindani wako kwenye soko. Hii ni kutokana na ukweli kwamba nidhamu hiyo ndiyo itakusukuma: kuamka mapema kila siku, kuwa na bidii ya kazi, kuepuka mambo yasiyo ya muhimu katika maisha yako na kuwa na nidhamu kwenye matumizi ya pesa. Mwandishi anatushirikisha kuwa, ili ufanikiwe katika hilo unatakiwa uwe na wigo mkubwa wa sababu zinazokusukuma kufanikiwa kimauzo.

8. Siri kubwa ya kufanikiwa ni kimauzo ni kuhakikisha unatangaza namna ambavyo bidhaa/huduma zako zitamnufaisha mteja tarajiwa. Mwandishi anatushirikisha kuwa watu hawajari ubora wa bidhaa au uimara wa kampuni yako pale ambao unawaelezea juu ya bidhaa/huduma zako kwa mara ya kwanza. Watu wanahitaji kusikia kutoka kwako namna ambavyo bidhaa/huduma zako zitawasaidia kutatua matatizo/changamoto walizonazo. Kumbe, ili ufanikiwe kimauzo haupaswi kutangaza bidhaa bali tangaza namna ambavyo unatatua changamoto za wateja kupitia bidhaa/huduma unazotoa. Pia, badala ya kuuza mlango kwa mlango au mtu kwa mtu ili ufanikiwe kimauzo siri nyingine ni kwamba unatakiwa kuwa na uwezo wa kuandika matangazo ambayo yatavuta wateja wa bidhaa/huduma zako. Uwezo wa kuandaa ujumbe wa bidhaa/huduma zako na jinsi zinavyosaidia wateja kutatua changamoto zao ni sifa ya kipekee katika kufanikisha mauzo. Matangazo/ujumbe wako unatakiwa uwe na sifa za kuvuta wateja wapya sambamba na uwezo kufanikisha mauzo masaa yote katika masaa 24 ya siku katika siku 7 za wiki. Hapa, sasa unakuwa umetengeneza mfumo wa moja kwa moja wa kufanikisha mauzo ya bidhaa/huduma zako.

9. Wekeza kwenye matangazo ya kulipia sawa na ilivyo uwekezaji wa hisa, dhamana au nyumba za biashara. Mwandishi anatushirikisha kuwa kama wewe ni muuzaji na unategemea kuongeza mauzo bila ya kuwekeza kwenye matangazo hakika unajidanganya. Mwandishi anatushirikisha kuwa katika teknolojia ya sasa ili upate jamu (wingi wa watu) wanaofuatilia bidhaa/huduma zako ni lazima uwe tayari kununua jamu hiyo. Wingi wa watu unanunuliwa sawa na ilivyo kwenye manunuzi ya bidhaa nyinginezo unazonunua ‘super market’. Na sehemu ambazo mwandishi anatushirikisha kuwa bidhaa/huduma yako inaweza kufikia wateja tarajiwa zaidi ya mamilioni ndani ya muda mfupi ni kupitia ukurasa wa Kijamii wa Facebook na Mtandao wa Google. Muuzaji makini ni lazima uhakikishe unawekeza fedha nyingi kwenye matangazo ya facebook na Google ili kupata wateja wapya wa bidhaa/huduma zako.

Haya ndio machache ambayo nimekushirikisha katika sehemu ya utangulizi wa kitabu. Husikose nakala yako yenye uchambuzi wa kitabu kizima jumapili ya wiki ijayo. Nakala nzima itapatikana kwa Tshs. 10,000/= tu.

PATA UCHAMBUZI WA VITABU vifuatavyo kwa kulipia Tshs. 5000.00 kila kitabu (Ofa ya mwaka 2020, ukinunua 2 unapewa 3 kwa Tshs 10,000.00).

1. Kitabu cha Kwanza ni “THE RULES OF MONEY (KANUNI ZA PESA)” kutoka kwa Mwandishi Richard Templar
Katika kitabu hiki utafahamu kanuni 107 za pesa. Ndani ya kanuni hizo utagundua kuwa utajiri ni haki ya kila mtu hivyo ni wajibu wako kuwa tajiri. Kanuni zote (107) zimechambuliwa kwa kina na kuandaliwa kwa lugha Kiswahili. Uchambuzi huu unapatikana kwa kijitabu kidogo chenye kurasa 39 ambazo unaweza kusoma kwenye simu yako ya mkononi (simu janja – smart phone) au kwenye kompyuta mpakato (pc).

2.    Kitabu cha pili “THE RULES OF LIFE (KANUNI ZA MAISHA)” kutoka kwa mwandishi Richard Templar
Mwandishi kupitia kitabu hiki anatushirikisha kanuni 106 za maisha. Kanuni hizi zimechambuliwa kwa kina kwa lugha ya Kiswahili na unaweza kukisoma kupitia simu janja au kompyuta mpakato. Kanuni zote zinagusa kila sekta ya maisha yako hivyo ni kitabu ambacho hautojutia pesa unayoitoa kwani utajifunza maarifa mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maisha yako.

3. Kitabu cha tatu ni “I CAN I MUST I WILL (NAWEZA, NALAZIMIKA, NITAFANYA)” kutoka Mwanamafanikio na Mtanzania Mwenzetu Marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi
Kwa ujumla kupitia kitabu hiki Dr. Mengi anatushirikisha maisha yake kuanzia akiwa mtoto, akiwa mwanafunzi, wakati anaanzisha biashara yake ya kwanza, namna alivyopanua biashara zake, wajibu aliokuwa nao kwa jamii, misimamo yake kwenye mfumo wa Serikali kwa awamu zote tano, wajibu wake kwenye uhifadhi wa mazingira na matarajio yake kwenye kukuza biashara kwa siku za baadae.

4.    Kitabu cha nne ni “Raising Great Kids” kutoka kwa Dr. Henry Cloud (Phd) na Dr. John Townsend (Phd)
Katika kitabu hiki utajifunza mbinu muhimu za malezi ya watoto. Pia, wawili hawa wametushirikisha tabia 6 ambazo ni muhimu kila mtoto awe nazo na mbinu za kumfundisha mwanao kuwa na tabia hizo. Kwa pamoja wawili hawa wanatushirikisha kuwa linapotajwa suala zima la malezi ya watoto kwa ujumla mambo manne yanaguswa ambayo ni; Ustawi wa Watoto, Jamii inayomzunguka mtoto, Ustawi wa wazazi na Uimara au mafanikio ya dini.  

5.   Kitabu cha tano ni Hooked: How to Build Habit–Forming Products: Jinsi kutengeneza bidhaa zenye kubadilisha tabia ya mteja. Kitabu kimeandikwa na Nir Eyal
Kwa ufupi katika kitabu hiki mwandishi anatushirikia namna ambavyo mfanyabiashara wa karne ya 21 anavyopaswa kuzalisha au kutoa huduma ambazo zinalenga kuteka akili na hisia za wateja bila ya wao kutambua. Mwandishi anatushirikisha kuwa ili uliteke soko ni katika karne hii ni lazima uwe na bidhaa/huduma ambazo zinaweza kubadilisha mfumo wa akili na hisia za mhusika pasipo yeye kujitambua. Ni lazima bidhaa hiyo imfanye mhusika kutamani kuitumia kila mara. Mwisho, wake ni kwamba mhusika anajikuta amejenga tabia mpya katika maisha yake bila yeye kujigundua kuwa yupo kwenye ulevi/uteja wa bidhaa husika. Hakika wewe mfanyabiashara hakikisha unasoma kitabu hiki kwani kuna mengi ambayo utajifunza kwa ajili ya kuboresha bidhaa/huduma zako.
  
Kupata uchambuzi wa vitabu hivi tuma pesa yako kwa njia ya M-pesa au Airtel Money kupitia namba zifuatazo:-
M – Pesa tumia namba: 0763 745 451 (Majina ni Augustine Mathias)
Airtel Money tumia namba: 0786 881 155 (Majina ni Augustine Mathias)

Baada kutuma pesa hiyo nitumie ujumbe kwenye namba ya airtel (0786 881 151 451) ukiwa na barua pepe yako ili nikutumie uchambuzi wa kitabu husika.

UTAJIRI NI HAKI YAKO YA KUZALIWA "BEING RICH IS YOUR BIRTH RIGHT"

Orodha ya Vitabu nilivyosoma na namna ya kupata nakala ya uchambuzi wa vitabu hivyo katika mfumo wa Pdf


Habari ya leo rafiki yangu na msomaji wa mtandao wa fikra za kitajiri. Hapa nimeorodhesha vitabu 60 ambavyo nimesoma katika kipindi cha miaka mitatu na namna ya kupata nakala ya uchambuzi wa vitabu hivyo kwa ajili ya rejea yako.

Endapo kuna kitabu umehitaji kupata nakala ya uchambuzi wake nitumie barua pepe kupitia fikrazakitajiri@gmail.com  nami nitakupa maelekezo ya namna ya kulipia.

Karibu uchague madini kwa ajili ya chakula cha ubongo.

SN

JINA LA KITABU

MWANDISHI

NAKALA YA UCHAMBUZI (PDF)

1

Mind Frick

T. Harv Eker

Ipo (Tshs. 4,000.00)

2

The Power of the First Step

Shemeji Melayeki

Ipo (Tshs. 2,000.00)

3

Noble Purpose

William Damon

Ipo (Tshs. 3,000.00)

4

Super coach

Michael Neill

Ipo (Tshs. 4,000.00)

5

Trump University Wealth Building 101

Donald J. Trump (Mhariri)

Ipo (Tshs. 4,000.00)

6

Keys to Leadership

Dr. Myles Munroe

Ipo (Tshs. 3,000.00)

7

Little Red Book of Selling

Jeffrey Gitommer’s

Ipo (Tshs. 3,000.00)

8

A Brief History of Humankind

Yuval Noah Harari

Ipo (Tshs. 5,000.00)

9

I Declare 31 Promises To Speak Over Your Life

Joel Osteen

Ipo (Tshs. 5,000.00)

10

Alex Ferguson Autobiography

Sir Alex Ferguson

Ipo (Tshs. 4,000.00)

11

Brain Rules

John Medina

Ipo (Tshs. 5,000.00)

12

Do More Great Work

Michael Bungay Stanier

Ipo (Tshs. 4,000.00)

13

Healing Your Family History

Rebecca Linder Hintze

Ipo (Tshs. 5,000.00)

14

TED Talks: A guide on Public Speaking

Chris Anderson

Ipo (Tshs. 4,000.00)

15

How Successful People Think: Change Your Thinking, Change Your Life

John C. Maxwell

Ipo (Tshs. 5,000.00)

16

How The Stock Markets Works

Ramon P. DeGennaro

Ipo (Tshs. 5,000.00)

17

How To Negotiate Better Deals

Jeremy G. Thorn

Ipo (Tshs. 5,000.00)

18

Illusions: The Adventures of a Reluctant Messiah

Richard Bach

Ipo (Tshs. 4,000.00)

19

Leading Quietly

Joseph L. Badaracco Jr.

Ipo (Tshs. 5,000.00)

20

Power of Motivation

Michael Bolduc

Ipo (Tshs. 5,000.00)

21

Primary Greatness: The 12 Levers of of Success

Stephen R. Covey

Ipo (Tshs. 5,000.00)

22

Procrastinate on Purpose: 5 Permissions to Multiply Your Time

Rory Vaden

Ipo (Ofa)

23

Screw It, Let’s Do It: Lessons in Life

Richard Branson

Ipo (Tshs. 4,000.00)

24

So Smart But….: How Intelligent People Lose Credibility…

ALLEN N. Weiner

Ipo (Tshs. 4,000.00)

25

Starting Your Business

Shirika la EY

Ipo (Ofa)

26

Strong Mothers, Strong Sons

Meg Meeker, M.D.

Ipo (Tshs. 5,000.00)

27

Strong Fathers, Strong Daughters

Meg Meeker, M.D.

Ipo (Ofa)

28

Teach Your Child How To Think

Dr. Edward De Bono

Ipo (Tshs. 6,000.00)

29

The Art of Power

Thich Nhat Hanh

Ipo (Tshs. 5,000.00)

30

The Effective Executive

Peter F. Drucker

Ipo (Ofa)

31

The Right Hook: How To Tell Your Story in Noisy Social World

Gary Vaynerchuk

Ipo (Tshs. 5,000.00)

32

The Seven Principles For Making Marriage Work

John M. Gottman

Ipo (Tshs. 5,000.00)

33

The Warren Buffet Way

Robert G. Hagstrom

Ipo (Tshs. 5,000.00)

34

Raising A Positive Kid in A Negative World

Zig Ziglar

Ipo (Tshs. 5,000.00)

35

ZERO to One

Peter Thiel

Ipo (Tshs. 4,000.00)

36

The Power Of Now: A Guide to Spiritual Enlightenment

Eckhart Tolle

Ipo (Tshs. 5,000.00)

37

Hiring and Keeping the Best People

Harvard University

Ipo (Tshs. 4,000.00)

38

Be Obsessed or Be Average

Grant Cardone

Ipo (Tshs. 5,000.00)

39

The Rules of Money: How to Make It and How to Hold on to It

Richard Templar

Ipo (Tshs. 10,000.00)

40

How to Think like Leonardo da Vinci

Michael J. Gelb

Ipo (Tshs. 5,000.00)

41

A Note From a Friend

Anthony Robins

Ipo (Ofa)

42

Rich Kid Smart Kid

Robert Kiyosaki

Ipo (Tshs. 5,000.00)

43

Ultimate Trading Systems

David Jenyns

Ipo (Tshs. 5,000.00)

44

How To Write a Marketing Plan

John Westwood

Ipo (Tshs. 4,000.00)

45

Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Ipo (Ofa)

46

Powerful People Skills

Heather Hansen

Ipo (Tshs. 3,000.00)

47

The Rules of Life

Richard Templar

Ipo (Tshs. 10,000.00)

48

The Craving Mind

Judson Brewer

Ipo (Tshs. 4,000.00)

49

Winning The Loser’s Game

Charles D. Ellis

Ipo (Tshs. 4,000.00)

50

Se Habla Dinero (Pesa zinaongea)

Lynn Jimenez

Ipo (Tshs. 5,000.00)

51

Everything I Know About Sales Success

Gerhard Gschwandtner

Ipo (Ofa)

52

How to Build a Multi–Billion Dollar Business in Africa

Strive Masiyiwa

Ipo (Tshs. 5,000.00)

53

A Gift To My Children

Jim Rogers

Ipo (Tshs. 5,000.00)

54

Automatic Millionaire: A Powerful One-step Plan to Live and Finish Rich

David Bach

Ipo (Tshs. 5,000.00)

55

I Can I Must I Will

Dr. Reginald Abraham Mengi

Ipo (Tshs. 10,000.00)

56

365 Wisdom Keys of Mike Murdock

Mike Murdock

Bado inafanyiwa kazi

57

Be Rich and Happy

Robert Kiyosaki

Ipo (Tshs. 6,000.00)

58

An Hour to Live an Hour to Love

Richard Carlson na Kristine Carlson

Ipo (Tshs. 5,000.00)

59

How To Get Rich

Donald J. Trump

Ipo (Tshs. 5,000.00)

60

Raising Great Kids

Dr. Henry Cloud na Dr. John Townsend

Ipo (Tshs. 10,000.00)

61

Hooked; How To Build Habit Forming Products

Nir Eyal

Ipo (Tshs. 5,000.00)

62

Sale Like Crazy

Sabri Suby

Ipo (Tshs. 5,000.00)

63

Rules of Life

Richard Templar

Ipo (Tshs. 5,000.00)

64

Principles and Power of Motivation

Dr. Myles Munroe

Ipo (Tshs. 5,000.00)

65

How To Stop Worrying and Start Living

Dale Carnegie

Ipo (Tshs. 5,000.00)

66

The Science of Getting Rich

Wallace D. Wattles

Ipo (Tshs. 5,000.00)

67

How To Live on 24 Hours A Day

Arnold Bennett

Ipo (Tshs. 5,000.00)

68

The One Thing

Garry Keller

Ipo (Tshs. 5,000.00)