Karibu msomaji wa makala zangu ambazo zaidi
zinajikita katika jinsi gani ambavyo waweza amua kuwa tajiri kwa kubadilisha
mtazamo wako. Mpendwa msomaji wangu ni matumaini yangu kuwa uko vizuri na unaendelea
na mapambano ya kubadilisha maisha yako kila iitwapo leo.
Kama ndo hivyo nakupongeza kwa jitihada zako kwani naamini ni kupitia jitihada hizi pamoja tutaibadilisha nchi hii kuwa mahala pazuri pa kuishi badala ya kuishia kulalamikia wanasiasa kuwa wameshindwa kutimiza matarajio yetu.
Kama ndo hivyo nakupongeza kwa jitihada zako kwani naamini ni kupitia jitihada hizi pamoja tutaibadilisha nchi hii kuwa mahala pazuri pa kuishi badala ya kuishia kulalamikia wanasiasa kuwa wameshindwa kutimiza matarajio yetu.
Ni jambo la kushangaza kulalamikia wanasiasa
kuwa wameshindwa kukupa ajira kumbe wewe mwenyewe ni chanzo cha tatizo hilo kwani
kila mmoja wetu Mwenyezi Mungu amemuumba na kumkilimia rehema tele za
kubadilisha mahala alipo kuwa mahala pazuri pakuishi. Hivyo basi badala ya
kulalamikia kukosekana kwa ajira jiulize unafanya nini leo hii ili uweze
kuzalisha ajira kwa kizazi cha sasa au kizazi kijacho? You need to be problem solvers rather than problem creators.
Tuachane na hayo ya siasa na badala yake
ngoja nijikite kwenye mada yangu ya leo ambao itajikita kwenye jinsi gani ambavyo
utapata utajiri kwa kubadilisha fikra zako. Katika makala iliyopita nilielezea
kuwa misingi mikuu ya kuwa tajiri ni kupitia (i) Fikra (ii) Malengo (iii) Elimu
ya fedha na (iv) Kujali muda.
Leo hii naanza kwa kukuchambulia na
kukufunulia siri ambayo huwajahi kuhifikiria kuwa ni muhimili mkuu wa kukufanya
uwe tajiri tena tajiri mkubwa zaidi ya wale unaowaona kwenye vyombo vya habari
na mitandao mbalimbali. Upo tayari kujua ni siri ipi hiyo?? Kama upo tayari
hebu endelea kusoma ili husipitwe na uondo huu ambao utabadilisha maisha yako.
Kila unalofanya linatokana na fikra
zako za kila siku
Kila jambo linalofanyika katika maisha yako
ya kila siku lazima lianzie katika mfumo wako wa mawazo. Mfumo huu wa mawazo
umetengenezwa kiasi kwamba unafanyia kazi fikra zako ambazo unaziwaza mara kwa
mara katika mazingira yako ya kila siku. Kwa maana hiyo kile ambacho unakiwaza sana
ndicho mfumo wako wa ndani wa mawazo (subconscious mind) unakifanyia kazi na
kukuwezesha wewe kukiweka katika hali ya umbile lake. Hebu tuangalie mfumo huu wa
ndani wa mawazo unafanyaje kazi:-
Nguvu ya fikra hasi
Kadri unavyoufanya mfumo wako wa mawazo
utawaliwe na fikra hasi ndivyo mfumo wako wa mawazo wa ndani utakavyo tafsiri
fikra hizo na kukuletea matokeo hasi. Kinyume chake ni kuwa kama mfumo wako wa
mawazo utataliwa na fikra chanya ndivyo mfumo wako wa mawazo wa ndani utakavyo
kuletea matokeo katika umbile chanya. Mfano kama wewe unawaza kuwa hauwezi kuwa
tajiri moja kwa moja tafsiri ya mfumo wako wa mawazo wa ndani utakuletea
matokeo katika maumbile ya kiumaskini. Kumbuka kuwa binadamu tupo jinsi tulivyo
kutokana na mitazamo yetu ya ndani (“The outermost
of human being is the reflection of his/her innermost”). Kama wewe muda
mwingi unawaza kutokukubalika katika jamii vivyo hivyo matokeo yake yatakuwa
kutokukubalika. Kama unawaza kushindwa katika yale unayoyafanya matokeo yake
yatakuwa kutofanikiwa katika yale unayoyafanya. Kama unawaza kutokupendwa
ndivyo hivyo matokeo yake yatakavyokuwa.
Nguvu ya fikra chanya
Kutokana na tulichojifunza hapo juu, yafaa
tujifunze kuwa na mawazo ambayo yataumba mambo na vitu tunavyovihitaji pekee na
si vile vyenye kutuletea maumbile hasi. Jambo jingine la kushika ni kuwa huwezi
kutenda kile usichowaza. Matendo yote ni matokeo ya mawazo. Na kama mtu akisema
hutenda pasipo kuwaza, hiyo siyo kweli. Ubongo wa binadamu unazo sehemu kadha
wa kadha zinazohusika na kumbukumbu na takwimu mbalimbali na kupitia ubongo huu
ndimo kuna mfumo wa mawazo wa ndani wa mtu husika. Kwa mantiki hii kila
tunachoamua ni matokeo ya taarifa fulani ambazo zimeshakuwamo katika mfumo wa
mawazo wa ndani huko nyuma. Yawezekana hata muhusika hasiwe na habari kuwa
taarifa hizo zipo katika mfumo wake wa mawazo wa ndani (subconscious mind),
lakini kutofahamu huku hakuzuii taarifa hizo kuendelea kutumika katika maamuzi
na maumbile mbalimbali.
Wapo watu ambao hujikuta wanafanya uamuzi
wasioupenda ama wanapata matokeo wasiyoyapenda. Tatizo si matokeo, tatizo ni
fikra ambazo zinakuja kwa sababu ya taarifa zinazoujaza ubongo
wako. Nimesema kuwa ili upate matokeo unayoyataka ni lazima akili yako
ijikite katika kutafakari yale tu unayoyataka. Hivyo basi siri kubwa ya kuwa
tajiri ni kuufanya mfumo wako wa mawazo wa ndani utafakali juu ya neema za
utajiri. Kufikilia juu ya maisha yako ya kitajiri unataka yaweje, kwa maana
hiyo ubongo wako unatakiwa uujaze picha ya vitu vya kitajiri ambavyo ni
matarajio yako kuvimiliki.
Hitimisho
Nahitimisha kwa kutoa angalizo kuwa kawaida
asili ya binadamu inaongozwa na woga/mashaka. Tunakuwa na woga/mashaka kwa
vitu vile ambavyo kutokea kwake hatuna nguvu ya kuvizuia ili visitokee. Hivyo,
uamuzi mwingi wa binadamu utawaliwa na woga/mashaka kuliko kutawaliwa na
kujiamini na matumaini mema. Na kama akili yako isipoona ama kutafakari yale
unayoyataka ni vigumu sana kupata matokeo unayoyataka. Kwa maana hiyo siri
ninayokuachia leo hii ni kuhakikisha muda wote unawaza yale unayoyataka yatokee
katika mazingira chanya na hivyo utokeaji wake uweze kukufanya upige hatua moja
kwenda mbele katika kutimiza ndoto zako za kuwa tajiri.
Imeandaliwa
na Ndg.
Augustine M. Bilondwa
Karibu
kwenye fikra za kitajiri tubadilishane
mawazo kupitia mawasiliano yafuatayo:-
Namba
ya Simu ya Mkononi 0786
– 881155/0763 – 745451
Blog
fikrazakitajiri.blogspot.com
1 comments:
Choose to be rich by unleashing your brain with what the richest do